Jina: Bro Jackobo (JAM295)
Phone: +255766944441 na +255621036471
Email: jackobombwaga@gmail.com
UTANGULIZI WA KUELEWA JANGWA KWA MWAMINI
Maana ya Jangwa
JANGWA ni mahali pa ukame ambapo hakuna mvua ya kutosha na kupelekea mazao pamoja na wanyama kuwa na mazingira magumu katika ukuaji.
JANGWA kwa mwamini inaweza kuwa
✍️✍️Kukosa msaada katika mazingira ya ROHONI na MWILINI
A. MAZINGIRA YA KIMWILI
•kutelekezwa
• kuumizwa,
• kutukanwa
•kudharaulika hata kushushwa chini kuliko vile ulikuwa unategemea kuwaiwe kulinganisha na namna ulivyo
•Jaribu katika maisha yako ya kila siku n.k
B. MAZINGIRA YA ROHONI
✓unakosa msaada wa kiroho yaani namna ya kuweza kukutana na Mungu
•Hapa unakuwa umekosa mtu wa kukusaidia au mazingira yanakuzuia kuweza kumtafuta Mungu wako
•kutembea katika wakati ambapo huoni bubujiko la Roho mtakatifu ndani yako wakati hakuna dhambi ambayo umeifanya
• Kupigwa vita katika Huduma
UFUNUO WA YOHANA 1:9-11
"Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu, ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiat ira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia."
Yohana alikuwa katika Mazingira ambayo kiuhalisia ilikuwa changamoto sana maana alitengwa katika kisiwa cha patimo na hakuwepo mtu wa kumkumbusha namna gani amtazamie Bwana katika maisha yake alipokuwa mahali pale ila Maisha yake yalimfanya Mungu aonekane kwake nakumpa ufunuo. Pia mazingira yale aliyokuwa yupo yalikuwa ni mazingira yasiyokuwa na usalama pia hapakuwa na faraja yeyote ya mwanadamu mahari pale. Ukiangalia hapo utajua kwamba kweli ilikuwa ni wakati mgumu kwake sana maana alikuwa ametengwa na haoni msaada wowote wa kumpa tumaini la usalama pale kisiwa cha PATIMO. Inawezekana na wewe upo kwenye wakati ambapo hakuna mtu hata mmoja anaye kutia Moyo kila ukitazama unaona hakuna mlango wa Kupita lakini usiogope hata kidogo endelea nami kunalo tumaini.
Yohana hakuyahesabu mazingira yale kuwa kikwazo cha yeye kuwasiliana na Mungu. Ila ilikuwa ni kipindi cha Jangwa kwake maana
✍️Hapakuwa na faraja ya mwanadamu
✍️Hapakuwa na mazingira mazuri yakumfanya awe na usalama maana alikuwa sehemu yenye uwezekano wa samaki hatarishi kama nyangumi n.k
✍️hakuhimizwa kumtafuta Mungu
MWANZO 37:23-28
"Ikawa Yusufu alipofika kwa ndugu zake, wakamvua Yusufu kanzu yake, kanzu ile ndefu aliyoivaa, wakamtwaa wakamtupa katika birika; na hiyo birika ilikuwa tupu, hamna maji. Nao wakakaa kitako kula chakula; wakainua macho yao, wakaona, msafara wa Waishmaeli wanakuja wakitoka Gileadi na ngamia zao, wakichukua ubani na zeri na manemane, wakisafiri kuvichukua mpaka Misri. Yuda akawaambia ndugu zake, Kwafaa nini kumwua ndugu yetu, na kuificha damu yake? Haya, na tumwuze kwa hawa Waishmaeli, wala mikono yetu isimdhuru, maana yeye ni ndugu yetu, na damu yetu. Ndugu zake wakakubali. Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika birika, wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri."
Kwahiyo pia hata ukimuangalia Yusufu utagundua kwamba wale watu waliokuwa ni ndugu zake ndio waliomtendea hiana kwenye maisha yake maana walikuja kumtoa kuwa kama bidhaa ya kuuza na kununuliwa. Kwahiyo hiyo ilikuwa jangwa kwa namna ifuatayo
✍️Ndugu zake ilitakiwa wampe ulinzi lakini waliondoa ulinzi kwake.
✍️Ndugu zake walikuwa wakimuwazia mabaya maana walikuwa wanatamani hata kumuua..
✍️Yusuph alitupwa kwenye birika(shimo) ambapo mle hakuwa na msaada wowote
Kwa mazingira kama hayo unaweza ukagundua namna Jangwa linakuwa kwa mwanadamu awaye yeyote haijarishi kwamba ni ndugu au ni watu toka mbali wanamfanya awe katika hilo jangwa
Tutaendelea sehemu ya pili kwa wakati Mwingine kama MUNGU atatupa kibali cha kuendelea naamini umepata jambo hapo namna mwamini anavyoweza kuwa anapita wakati wa Jangwa.
Mungu akubariki kwa kusoma kipengele hiki cha kwanza cha UTANGULIZI juu ya Namna ya kuishi wakati wa jangwa kwa mwamini
Ulikuwa nami mpendwa katika kristo YESU
Jina: Bro Jackobo (JAM295)
Phone: +255766944441 na +255621036471
Email: jackobombwaga@gmail.com
Nimehudumiwa......ubarikiwe sana mwana wa Mungu.
ReplyDeleteAmen my brother
DeleteAmen neno la Mungu ni neno jema ndilo litupalo wokovu tulifurahie na kulishangilia🙏
ReplyDeleteGod blees you i have get some thing here
ReplyDeleteAmen
DeleteMungu akubariki Brother,
ReplyDeleteAsante kwa fundisho hili, maana huwa twapitia ugumu katika nyakati fulani na kudhani kuwa Mungu ayupo, kumbe huwa yupo pale pale kama kwa yohana kule patmo au Yusuph kule misri....
Asante sana Mtumishi wa Bwana
Stay blessed in Jesus name
Amen mtumishi
DeleteAmeen
ReplyDeleteAmina Jacobo
ReplyDeleteBarikiwa Bro Jacob🙌🙌
ReplyDeleteBarikiwa Bro Jacob🙌🙌
ReplyDeleteBarikiwa Bro Jacob🙌🙌
ReplyDeleteBarikiwa Bro Jacob🙌🙌
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteAmen mtumishi
DeleteUbarikiwe mtumish wa Mungu kwa kutoa neno la kweli lisiko goshiwa
ReplyDeleteAmina mtumishi wa Mungu
DeleteUbarikiwe mtumish wa Mungu kwa kaz yako njema
ReplyDeleteAmen
Delete