KUITOA MIILI YETU KUWA DHABIHU MBELE ZA BWANA
SEHEMU YA KWANZA
Mwl: JACKOBO ABELY MBWAGA
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441 and +255621036471
1.UTANGULIZI
Bwana YESU asifiwe mwana wa Mungu karibu sana tushiriki kwa pamoja katika somo ambalo Mungu kanipa neema ya kuweza kusema na kanisa la wakati huu kwa watu wote popote walipo kwa yeyote atakaye weza kuupata ujumbe huu ambao Mungu ameuweka ndani yangu.
Tutajifunza juu ya namna ya kujitoa miili yetu kuwa dhabihu mbele za Mungu yaani tukiangalia maana ya dhabihu, maana ya mwili na dhabihu ya mwili.
Pia tutaangalia Dhabihu ya mwili huwa inahusisha vitu gani na ni kwanini baadhi ya watu wanaingia kanisani lakini bado hawajajitoa miili yao kuwa Dhabihu mbele za Bwana na utaweza kujielewa na nitaweza kujielewa kama nimejitoa mbele za Mungu au Bado naingia kanisani wakati bado sijajitoa kikamilifu mbele za Mungu.
Kwa Neema ya Mungu Somo hili litagawanyika katika sehemu kuu tatu au nne katika mfululizo wa kuwapa waamini mtiririko mzuri na kuwarahisishia watu waweze kupata muda wa Kusoma na kutafakari mbele za Mungu ili asiwepo hata mmoja wa kushindwa kuelewa.... Naomba tuende pamoja katika hili somo.
2. MAANA YA DHABIHU
DHABIHU ni matoleo ya hiari ambayo hufanywa na mwanadamu kwa Mungu wake katika kweli na utaua wote chini ya maongozi ya Mungu mwenyewe...
Matoleo haya huwa ni msingi mkubwa wa Imani iwayo yeyote haijarishi ni imani ya kweli au sio ya kweli na ndiyo maana hata shetani anapotaka kumfanikisha mtu yeyote lazima ampe mtihani wa kutoa sadaka haijarishi itakuwa vipi yaani namaanisha KAFARA. Hii ni mbinu ambayo shetani ameichukua kwa Mungu maana asili ya yote ni MUNGU pekee na shetani hakuhusika katika uumbaji uwao wowote na ndio maana huwa anaiga vitu vyake toka kwa Mungu(muumbaji wa vyote hapa umimwenguni)
Matoleo haya huwa yanatolewa kama sehemu moja wapo ya kuonyesha shukurani mbele za Mungu kwa matendo makuu ambayo ameyafanya kwenye maisha ya Mtu....
Kutoka 3:18
"Nao watakusikia sauti yako; nawe utakwenda, wewe na wazee wa Israeli kwa mfalme wa Misri, na kumwambia, Bwana Mungu wa Waebrania, amekutana nasi; basi sasa twakuomba, tupe ruhusa twende mwendo siku tatu jangwani, ili tumtolee dhabihu Bwana Mungu wetu."
Sababu kubwa iliyowafanya wana wa israeli waende kumtolea Mungu Dhabihu ni kwasababu Mungu alikuwa pamoja nao na alionekana kwao kupitia mtumishi wa Mungu Musa ili awatoe katika ardhi ya utumwa....
Je wewe Mungu akionekana kwako huwa unafanya nini na huo unachukua hatua gani katika maisha yako unapokuwa unaishi hapa ulimwenguni???
Kutoka18:12
"Yethro mkwewe Musa akamletea Mungu sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; na Haruni akaja, na wazee wote wa Israeli, wale chakula pamoja na mkwewe Musa mbele za Mungu."
Licha ya kwamba Yethro alikuwa ni mtu wa mataifa lakini bado alikuwa anaelewa umuhimu wa kutoa dhabihu mbele za Mungu. Baada ya Mungu kumtetea Musa alipokuwa anawatoa wana wa israeli nchi ya utumwa Yethro aliona amtukuze Mungu kwa namna ambavyo alikuwa amewaokoa akina Musa pamoja na wana wa israeli na mikono ya farao..
Kumbuka sadaka hizi huwa zinatolewa kwa moyo wa kupenda (HIARI) ila lazima uwe makini Maana Mungu kakupa utashi kwa kuwa amekuumba kwa mfano wake (Mwanzo 1:27). Sasa kama umeumbwa kwa mfano wa Mungu je wewe unaishi kwa mfano wa Mungu yaani unatoa matunda kama ya Mungu ndani yako (UPENDO hilii ni tunda kuu ambalo Mungu ametuonyesha la kwanza kwenye maisha yetu tangu tulipokuwa tunaumba mpaka anapoamua kumtoa YESU kristo aje kwa ajili ya kutuokoa sisi...
Yohana3:16
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
usije ukajizalau ukajiona ya kwamba wewe sio kitu chochote.. nikukumbushe tu ya kuwa Mungu ametufanya sisi kuwa na tabia za kiuungu ndani yetu sasa unapojidharau nabaki kukushangaa sana
2petro1:4
"Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa"....
Sio tu agano la kale linazungumzia juu ya suala la Dhabihu embu tuangalie mifano midogo ambayo inaonyesha utoaji wa dhabihu
Matendo 14:8-18
Hapa utakutana na kiwete wa huko Listra ambaye Mungu alimfungua kupitia mikono ya Mtumishi wa Mungu paulo.. na baada ya kufunguliwa kwake watu walitaka kuonyesha shukurani zao kwa kumtolea dhabihu Paulo lakini Paulo aligoma kupokea hizo Dhabihu kwasababu alikuwa anajua ya kwamba anaye takiwa kutolewa Dhabihu ni Mungu.....
Sio tu hivyo Embu tazama huyu kuhani wa Zeu (The priest of Jupiter) ambaye hakuwa anamjua MUNGU wa kweli lakini bado alijua umuhimu wa utoaji Dhabihu sasa wewe unaingia kanisani lakini bado hajataka kumtolea Mungu dhabihu ya kweli juu ya mwili wako mwenyewe......
Siko kuzungumzia juu ya utoaji wa dhabihu kama seheme ya asilimia zako tisini(90%) baada ya kutoa zaka yako(10%) ambayo ni lazima kuitoa
Naomba tuelekee kwenye kiini kikuuu cha somo letu juu ya KUITOA MIILI YETU KUWA DHABIHU YA KUPENDEZA MBELE ZA BWANA...
Lakini kwa leo naomba nikuache na mtazamo huo wa maana ya Dhabihu. Lakini Chukua mda utafakari namna tulivyoona Dhabihu zilivyokuwa na zilivyotolewa kwa baadhi ya watu wengine..... Sogea sasa kama wewe utawezaje kujitoa kuwa dhabihu takatifu ya kumpendeza Mungu??? Naomba tukutane Sehemu ya Pili ya Somo hili.... Itaendelea
Kwa maswali pamoja na ushauri mbalimbali tunaweza kuwasiliana kwa njia zifuatazo
Wako
Mwl: Jackobo Abely Mbwaga
Phone;+255766944441 na +255621036471
Email: jackobombwaga@gmail.com
Www.jackobombwaga.blogspot.com
Thankyou
ReplyDeleteBe blessed bro
Amina
DeleteWaooh,
ReplyDeleteAsante sana Brother kwa upendo wako nami kushiriki baraka katika kujifunza katika mfululizo huu,
Bwana Yesu akutunze na kukuongeza mara dufu kwa ajili ya jina na ufalme wake hata milele
Amen mtumishi
Deleteubarikiwe mtumishi wa Mungu, hakika ni somo zuri, unitumie update kupitia email hii
ReplyDeleteNaomba niandikie kama email moja kwa moja maana nimeona sijabahatika kuiona maana haionyeshi Jina
DeleteNaomba niandikie kama email moja kwa moja maana nimeona sijabahatika kuiona maana haionyeshi Jina
DeleteAmina Mwl Jackobu
ReplyDelete