Mwl: Jackobo Abely Mbwaga
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441
Bwana Yesu apewe sifa Wana wa Mungu..... napenda tushirikiane jambo hili kidogo ambalo liko katika mfumo wa swali...
"Je ndani ya maisha yako yupo kristo kweli au umekuwa mtu wa kwenda kanisani kama utaratibu wa kawaida??????
LUKA9:57
"Yesu akamwambia, Mbweha wana pango,na ndege wa anganiwanaviota, lakiniMwanawaAdamu hana pa kujilaza kichwa chake".
Yule mtu alikuwa na nia ya kumfuata kristo lakini ndani yake alikuwa hajampa kristo nafasi hata kidogo na wewe je umempa nafasi gani kristo kwenye maisha yako????
lazima uwe mtu wa kuvumilia kutenda mema sikuzote ndipo utapata nafasi ya kuurithi ufalme waMUNGU lasivyo unajidanganya
MATHAYO 24:13
"Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
Maana kama umebadili mwiliwako na moyo wako kuwa sehemu ya uovu jua hukumu inakungoja haijarishi unaingia kanisani au hauingii
MATHAYO 21;12
Yesu akaingiandani yahekalu, akawafukuzawote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni,akazipinduameza zawabadili fedha, na viti vyao waliokuwawakiuza njiwa;
kristo hataki michanganyo hata siku moja ndio maaana alipoona wamegeuza sehemuya ibada kuwa kama gulio ilimkasirishasana YESU na ndivyo hivyo hivyo anavyochukia pale unapoachanjia ya MUNGU na kufanya Mambo unayoyataka yaliyo tofauti na neno lake.
wewe ni hekalu tena u sehemu ya ibada ya MUNGU ndani ya moyo wako.
maana siku ile Mwana waMungu atakapokuwa kwenye kiti cha enzi atawabagua kama Mbuzi na kondoo kwa kadri ya mtu na matendo yake
MATHAYO 25:31-46
usikae kwa hasara Maharii ulipo maana hukumu inakuja tena usije muheshimuMungu kwa kinywa tu bali na MATENDOyako ya ambatane na namna kinywa chako kinavyozungumza
MATHAYO 15:8-9
"Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami Nao waniabudu bure,Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizoya wanadamu."
Nipende kukusihi ndugu yangu badirisha njia zako kama bado hujatengeneza na MUNGU Yeyebado anatoa wito yeyote aliye na mzigo wa aina yeyote yeye atampumzisha (MATHAYO11:28 )
WARUMI10;10
"Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu".
kazi yako ni kuamini na kumpa kristo maisha yako na sio kwenda kanisani tu na kufanya vitu visivyofaaa
KUOKOKA NI LAZIMA SIO OMBI HUJACHELEWA NAFASI BADO IPO
MBONA KUJIONDOLEA MWENYEWE NAFASI YA YESU KRISTO NDANI YAKO...
TUNZA UTAKATIFU NA KAMA HAUNA FANYA KUUTAFUTA MAANA PASIPOKUWA NA HUO HAKUNA ATAKAYE MUONA MUNGU.
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441 and +255621036471
Www.jackobombwaga.blogspot.com
No comments:
Post a Comment