Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu??
Utakuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com
Kutokana na baadhi ya maswali na michango nimekuwa nikiipokea nimeona ni vema niongezee kipengele cha pili kwenye somo juu ya KIU YA KUMTAFUTA MUNGU kwa upande wa Umuhimu wake
Kama haujasoma sehemu ya kwenza unaweza kubonyeza hapaππSEHEMU YA KWANZA
Basi Nikianzia na maana niliyokuwa nimetoa mwanzoniππππ
KIU hii ni hali ya ndani anayokuwa nayo mtu ili aweze kupata au kufanikisha jambo fulani alilokuwa na uhitaji nalo.
Kiu ya kumtafuta Mungu hiii ni hali ya ndani inayojengeka kwenye Nafsi ya mwamini kuhitaji ushirika na Mungu katika nyanja zote za maisha yake yani kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiroho.
UMUHIMU WA KUWA NA KIU YA KUMTAFUTA MUNGU KWA MWAMINI
Sasa umuhimu wa kuwa na kiu uko hivi ππ
1. Kumruhusu Mungu achukue hatamu ya maisha kwa kila jambo ambalo utakuwa unalifanya
1 Wakorintho 10:31
"Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu."
Ukisoma hilo Fungu unaona Paulo ana wausia watu wa Korintho kwamba kila kitu kinapofanyika kwa mwamini inatakiwa kufanyika kwa utukufu wa Mungu. Kwahiyo ukiwa na kiu utafanya mambo yako yote chini ya maongozi ya Mungu na papo hapo itakuwa Mungu anatukuzwa kwa kuwa mambo au mafanikio yako yatakuwa yamejengwa kwa Mungu mwenyewe ππ
2. Inasaidia kujijengea heshima ya kibinafsi juu ya mambo yako [SELF DISCIPLINE]
ππKwakuwa ndani ya nafsi yako imejengeka hali ya kumuhitaji Mungu hautafanya mambo kwa pupa maana nafsi yako itakuwa iko kwenye hitaji la kumtukuza Mungu kwahiyo maamuzi yako yatakuwa sahihi yaliyokuwa balanced..
Pia inabidi ujue kuwa kwenye nafsi ndiko kuliko UTASHI, UELEWA, MAAMUZI, AKILI NA MOYO(HIFADHI/KUMBUKUMBU). Kwahiyo ukiwa na Kiu mambo yako na maamuzi yako yatajikiti kwenye kuhakikisha unampendeza Mungu si utajizuia kwa mambo mengi.
N.B hapo kwenye NAFSI ni somo linajitegemea ambapo inahitaji pia mda wa kutosha kuelewa ila kama Mungu atatupa kibali nitaliweka pia kwenye hii website yangu.
Ndio maana Suleiman anasema kwamba πππ
Mithali 29:18
"Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria."
Nia pia inakuonyesha jambo la kufanya ndio maana hukupa ile self discipline for anything you will be intending and interesting to do in future.
3. Kumfanya mtu awe na ushirika {FELLOWSHIP} bora na Mungu.
ππ Maisha ya ukristo sio tu kwenda kanisani bali ni uhusiano binafsi wa mtu na Mungu wake katika mazingira na nyanja mbalimbali za maisha. Kwahiyo mtu mwenye kiu huwa inamfanya atamani sana kukaa na Mungu kwa karibu kitu kinachomjengea msingi mkuu wa ushirika wake na Mungu.
1 Petro 2:2
"Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;"
Unapokuwa na kiu utakuwa mtu wa kujifunza maneno ya Mungu na kujikuta unaukulia wokovu ambako huko hufanya kuimarisha ushirika na Mungu wako.
4. Kuondoa hali ya mazoea kwenye utumishi wako
ππWatu wengi wanafanya mambo kwa mazoea yaani bila kufwata maelekezo ya Mungu anavyotaka kwakuwa ndani ya maisha yao haiko Shauku au Kiu ya kumtaka Mungu bali wanafanya kama taratibu za kila siku.
Huduma yeyote ambayo umepewa na Mungu unahitaji unyenyekevu wa hali ya juu na sio kwakuwa unaweza au ulimuona mtu fulani anafanya basi na wewe unafanya. Embu ona hawa watuππ
Matendo ya Mitume 19:13-16
"Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa."
Hawa wapunga pepo kwakuwa kiu yao ilikuwa kujipatia faida na sio kuwa na Yesu walijikuta wanaingia pabaya na kutendewa yasiyo faa na yule pepo mchafu.
Kwahiyo ukiwa na kiu hutafanya kwa mazoea kama hawa watu walivyofanya ili wajipatie heshima mbele za watu wa mji ule. Sasa wewe kwenye utumishi wako utatenda ili Mungu atukuzwe ndani yako na kukufanya hali ya mazoea kuto kuwepo ndani yako.
5. Kuruhusu Tunda la Roho kuleta matokeo ndani yako.
ππMtu anapokuwa ameokoka huwa Roho mtakatifu anakuja ndani yake ila madhihirisho ya kujazwa na Nguvu au uwezo wa Roho mtakatifu hufuatia baadaye pale anapokuwa anaendelea kuukulia wokovu japo kuna wengine pia hupata madhihirisho wakati huohuo baada ya kumuamini Yesu na kazi yake ya msalaba na umuhimu wake. (ππMfano wanafunzi wa Yesu walipata madhihirisho baada ya Yesu kuondoka.. Soma Matendo 2:1-4 wakati wengine ka Kornelio walipokea papo hapo pindi anaipata injili.. soma Matendo 10:44-46 ila soma sura nzima ya 10 hiyo)
Sasa Roho mtakatifu huwa analeta yale matunda ya Roho kwenye MATENDO 5:22-24 Kuwa dhahiri kwa mwa mwamini. Kwahiyo kwa mtu aliyekuwa na kiu ndani ndio huruhusu hayo mambo kufanyika kwake na hii ndio huja kuleta utofauti baina ya mwamini na mwamini mwingine.
6. UNYENYEKEVU kuwa ni sehemu ya maisha yako.
Mtu ambaye bado hajajikita kumtaka Mungu ni rahisi sana kutaka yeye aonekane kwenye jambo lolote na sio Mungu. Ila huyu mtu akiwa na kiu anakuwa na hali ya uhitaji kiasi kwamba anakuwa ana unyenyekevu na kuwekelea mbali kila namna ya kiburi ndani yake kitu ambacho humfanya apate kibali mbele za Bwana. Embu ona watu hawaπππ
Mwanzo 11:3-4
"Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote."
Ukiwaangalia hawa watu utagundua walitamani wajipatie sifa na kuacha kufuata agizo la Mungu la kutakiwa kutawanyika juu ya uso wa nchi yote kama alivyosemaππππ
Mwanzo 1:28
"Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi."
Hapo unaona kiburi kiliinuka lakini kama wangekuwa wanamtaka Mungu basi wangefuata maelekezo yake ambayo ingeleta unyenyekevu ndani yao.
Pia siku zote mtu anayemtaka Mungu lazima awe na unyenyekevu ndani yake maana Kwake maelekezo ya Mungu kwake ni Lulu na uhai maana sisi katika kristo huwaπππ
Matendo ya Mitume 17:28
"Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake."
Mungu akubariki kwa kusoma sehemu hii ya pili. Unaweza kuwashirikisha na wengine pia
Ulikuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Phone; +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com
MUNGU AKUBARIKI KAKA NA AZIDI KUKUPA HEKIMA ZAIDI UZIDI KUTUFUNZA JUU YA NENO LAKE..
ReplyDeleteUbarikiwe Sana kaka kwa kuifanya kazi ya Mungu kwa bidii
ReplyDeleteUbarikiwe sana somo zuri sana
ReplyDeleteHaleluya.......
ReplyDeleteBlessed sana mwalimu wangu, kweli yapo mengi ya kujifunza kazi ni kwangu kutenda sawa na maelekezo hayo. Mungu atusaidie sana Masihi wa Bwana
Asante sana kwa neno hili jema kwangu
Asante mwalimu ni somo lenye matokeo sana
ReplyDeleteAmina kaka
ReplyDeleteNabarikiwa na somo
BARIKIWA SANA,
ReplyDeleteBINAFSI, NAKUOMBEA KWA MUNGU, AENDELEE KUKUPA MADINI YA NENO LA UZIMA NAMNA HII NA AKUPELEKE MPAKA MAHALI ALIPOKUSUDIA UFIKE!!
Be blessed mr and may God be your provider for his people for prospering their spiritual life
ReplyDeleteAmen