KWENDA MPAKA MWISHO PAMOJA NA MUNGU {SEHEMU YA PILI}


Bro Jackobo

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu?? 
Namshukuru Mungu kipekee kwa ajili ya nafasi nyingine hii ambayo ametupa leo kuendelea na somo letu sehemu ya pili.

Utakuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email; jackobombwaga@gmail.com 

Baada ya kuona sehemu ya kwanza katika maana pamoja na kujua kwanini tunatakiwa kwenda pamoja na Mungu kama waamini mpaka mwisho. Sasa leo tutaenda kuangalia kwanini watumishi wa leo imekuwa ni changamoto sana kuweza kumaliza safari pamoja na Mungu. Kama hujapata kusoma sehemu ya kwanza bonyeza hapa➡️➡️ SEHEMU YA KWANZA

 Wagalatia 1:6 
"Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine."

Ni jambo la kushangaza sana kuona muamini anarudi nyuma na ndio maana Paulo alibaki kuwashangaa watu wa galatia kwamba ni kwanini wanamuacha Mungu kwa haraka๐Ÿค”๐Ÿค” ndio hivyo ambavyo hata kristo Yesu anavyolitazama kanisa  na kushangaa.

Kwanini unamuacha kristo kwa haraka mpendwa๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ
 
Wagalatia 3:3 
" Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?"
Paulo anaumia moyo na kuwaambia wagalatia ni nani aliye waloga nyie maana mlianza katika Roho lakini mnataka kumaliza katika mwili. Tumeanza kwa Roho lazima tumalize kwa Roho maana sisi asili Yetu ni Roho.

 KWANINI WAKRISTO WENGI WAMEKUWA WANASHINDWA KUMALIZA SAFARI VIZURI??.

Tutaenda kujifunza sababu kuu mbili za kwanini kanisa la leo wengi wanamaliza vibaya. Ambapo ni hizi sababu kuu  mbili
1⃣ ROHO YA MAZOEA
2⃣KUIPENDA DUNIA

 1⃣. ROHO YA MAZOEA
hii ni hali ya kufanya jambo pasina kuangalia msingi mkuu halisi wa Mungu kwa wewe kufanya hilo jambo. Roho ya mazoea huwa inatokea mara kwa mara baada ya mtu kuwa alishawahi kufanya jambo fulani kwa mafanikio kwahiyo anafanya akiangalia yale mafanikio yake ya mwanzo pasina kuangalia au kusikiliza Mungu anachotaka akifanye. 
Maandiko ya msingi kwenye kipengele hiki yamejikita kwenye kitabu hiki๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

 WAAMUZI 16:1-20 (20)
Basi naomba tuanzie hapa๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
 Waamuzi 16:20 
 "Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa BWANA amemwacha."

sasa ukisoma hiyo sura nzima utagundua namna ambavyo Samsoni alikuwa amefanya makosa lakini msitari wa 20 ndio ambapo inabeba maana ya Roho ya mazoea. Samsoni kwakuwa Mungu alikuwa anajidhihirisha kwake basi alijua hata wakati huo bado Mungu alikuwa naye kumbe Mungu ameshamuacha. Maana licha ya kwamba alikuwa ameingia kwa kahaba ila bado Mungu alikuwa pamoja naye kwasababu ile ishara ya mapatano bado ilikuwa ipo yaani vile vishungi vya nywele na alipotoa siri na vikaondolewa hakuelewa kama tayari ameshaondolewa vishungi alipoambiwa wafilisti wanakujia alisema nitainuka kama ilivyo kawaida Yangu ila asitambue kwamba Mungu amemuacha.
Kanisa la leo wengi wameachwa na Mungu ila hawajielewi na hata kama wanajielewa wengi wao wanakaza shingo na kusema wako pamoja na Mungu wakati Roho zao zinawa shuhudia kwamba hawako pamoja na Mungu.

 SIFA ZA MTU AMBAYE ANAENENDA KWA ROHO YA MAZOEA 

 ✍️✍️Huyu mtu anakuwa hana hofu ya Mungu au hofu ya Mungu hupungua ndani.

Ukimuangalia Samsoni alikuwa tayari ameenda tofauti na Mungu ila hakuwa na ile hali ya kuogopa kwamba Mungu anachukizwa na ninachokifanya kwahiyo akawa anafanya kwasababu Mungu alijitukuza kwake kwa wakati uliopita.
Kanisa la leo halimuogopi Mungu hata kidogo yaani mtu anaweza akadanganya, akadhurumu au akafanya uasherati lakini anaingia kanisani akiwa huru kabisa na wala hajuti moyoni mwake wala kuhisi hatia. Ni jambo la kutisha na hili ndilo balaa ambalo limelikuta kanisa la kizazi hiki cha leo.
 Soma Matendo ya mitume 5:1-11(8-9) 

Angalia mfano wa kanisa au mwamini aliyekuwa na mazoea ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
 Matendo ya Mitume 5:8-9 
" Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo. Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe."
 
Habari za anania na safira zinatisha watu hawa hawakuogopa hata kidogo kumdanya Roho wa Mungu kwasababu walijua ni kitu cha kawaida wala hakuna kibaya kitawakuta lakini kilichowakuta kilikuwa cha kutisha.
Kanisa la leo lime bweteka kwakuwa mtu hata kama akifanya dhambi huwa hawapatwi na mauti kama ilivyo kwa Anania na Safira wanasahau macho yao yanatiwa giza kiasi kwamba hawawezi kuona wema wa Mungu kwenye maisha yao.
Jichunguze vema huwa unafanyaje pale unapokosea.

 ✍️✍️Mtu huyu hujihesabia sana haki kwamba yuko sahihi kwa kila kitu.
Kujihesabia haki kunawakuta wengi wao ndio maana leo sio jambo geni kusikia mtumishi anajitangaza kwamba yeye ni mtakatifu sana kuliko wengine, kujiona anafanya huduma vizuri kuliko wengine huku akisahau kwamba Mungu kampa karama/kipawa ili kanisa liweze kufaidiana. Lazima ujifunze kwa Yesu mwenyewe unyenyekevu maana yeye licha ya kuwa alikuwa Mungu ila alinyenyekea mpaka mauti ili tuwe na usalama. Ukiwa unajiona wewe umekamilika basi uwe na uhakika uko karibu na kuanguka.  Samsoni yeye alikuwa tayari alishajimilikisha kwamba yeye ni wa kuwa na nguvu tu akasahau kuwa kuna wakati nguvu zitamtoka ikiwa atafanya tofauti na namna Mungu anataka.

 ✍️✍️ Huyu mtu anakuwa ni mtu wa kujiinua na kujisifu sana
Sasa ukimuangalia samsoni alipoambiwa wafilisti wanakujia alijibu nitainuka kama ilivyokawaida yangu hiyo ni ishara kwamba huyu mtu alikuwa tayari ameshajiona yeye ndio yeye na hakuna wa kumfanya kitu chochote. Ndiyo ilivyo kwa kanisa la Leo Mungu akukumbuke mtumishi wa Mungu. Nimekwisha kukuambia sehemu ya kwanza kwamba Utumishi wako sio sababu ya kukufanya kuurithi ufalme wa Mungu wala usije jaribu kuupima uhusiano wako na Mungu kwa kuangalia huduma yako.  

✍️✍️.Mtu huyu huwa Roho ya Toba inaondoka kwakwe
Mtu aliyezoelea Wokovu ,ndani yake Ile Roho ya Toba inaondoka kabisa na hatari huwa anaishi katika dhambi anasali na kuhudumu .
Toba hapa ni juhudi ya kuitubia dhambi yako ,kujutia na kufanya maamuzi ya kuacha kabisa na kugeuka kama Moyo wa Daudi namna ambavyo alifanya.
Unaweza ukasoma hapa ukaona๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
 (ZABURI 51:1-4)
Pia ile Hali ya kumrudia Mungu kwa kumaanisha kabisa ,kama Mwana mpotevu inakuwa halna kabisa kwa huyu aliyekuwa na Roho ya mazoea  (LUKA 15:21.)

 ✍️✍️ Huyu mtu huwa anasikia neno la Mungu bila kulitii . 
Waamini waliozoelea Wokovu husikia sana neno la Mungu tena kwa ufasaha kabisa na kuguswa , isipokuwa hawezi kulitii wala kulitendea kazi tena .
Nguvu ya utii wa matendo ya rohoni inakuwa imeondoka na hata akijitahidi hawezi kwenda mbali.
Ndio maana , hawezi kuomba ,kusoma neno ,kufunga , kuja Ibadan au mkeshani bado hawana sababu yoyote . Hatari yao ule Utiisho wa Roho Mtakatifu juu ya matendo ya rohoni imeondoka na wanaona kawaida hata wasipofanya hivyo. Ukijiona hivyo fanya juu chini kutafuta msaada hii ni hatari sana mwana wa Mungu.

2⃣. KUIPENDA DUNIA
Jambo la pili ambalo limekuwa likilitesa kanisa ni kuipenda Dunia. Mwingine anasema sasa inawezekanaje kwa mwamini kuwa akawa anaipenda Dunia๐Ÿค” naomba tuende pamoja nami ndipo tutaelewana vizuri na ni kwa nini sasa nasema moja ya vitu vinawafanya watumishi wa Mungu washindwe kufika mwisho wa Safari huku wakiwa pamoja na Mungu kwenye maisha yao ya kila siku.
Andiko la msingi kwenye kipengele hiki ni kwenye ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
 1 Yohana 2:15-16
 "Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia."

Ukianza kuisoma Sura hiyo ya pili utaona Yohana kaandika jumbe kwa watu wa rika zote baadae ndipo anakuja kuwapa huu ujumbe wa pamoja kwa watu wote. Kwamba wasije wakaipenda Dunia na mambo yote yaliyoko ndani yake.

Mtumishi wa Mungu katika kuishi kwake katika ulimwengu huu anakuja kuona mambo makuu matatu ambayo yanayowafanya watu waonekane wanaipenda Dunia.

 MAMBO YALIYOKO DUNIANI YANAYOONYESHA KWAMBA MTU ANAUPENDA ULIMWENGU/DUNIA
1. Tamaa ya mwili
2. Tamaa ya macho
3. Kiburi cha uzima

Katika hayo mambo matatu ndipo watumishi wengi wanaangukia sehemu moja wapo ya hizo ndio maana hawawezi kufika sehemu Mungu anataka waweze kufika wanajikuta walianza vizuri lakini wanamaliza vibaya.

 1. TAMAA YA MWILI
Hapa kwenye tamaa ya mwili mtu anakuwa anafanya yale mambo ambayo mwili unataka ayafanye kama tunavyojua ya kwamba matendo ya mwili huwa yako dhahiri kabisa unaweza ukasoma๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

 Wagalatia 5:19-21
 "Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu."

Hayo mambo hapo juu ndiyo ambayo unakuta mwili unamshurutisha huyu mwamini kuweza kuyaisha na huyu mtu kwakuwa hajajaa nguvu za Mungu basi anajikuta anayaishi hayo mambo hata kama yupo kanisani na hata kama huwa anafundisha au kuhudumu kwa namna yeyote ambapo ni lazima awe tayari kuyaacha hayo ndio atakuwa na usalama lasivyo anajidanganya.

 Warumi 3:13-15 
 "Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira i chini ya midomo yao. Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu. Miguu yao ina mbio kumwaga damu."

Hawa watumishi wa Mungu walio kwenye tamaa ya mwili unakuta hawawezi hata kuwa na uwezo wa kuyatunza maneno na ndio maaana unakuta wengine niwachonganishi kabisa ndani ya kanisa yani kazi yao ni kuleta virugu tu.
Mwingine huyu mtu anakuwa hana nia ya kuleta vurugu ila kila neno akilisema ndani ya kanisa linaleta shida. Sasa kama ukijua na ukajipima ukakuta kila ukisema unaleta machafuko kwa watu basi jua ya kwamba umekwisha kuvamiwa na tamaa ya mwili inakue desha pasipo wewe kujua. Na hii inawafanya watumishi wengi kutomaliza na Mungu sasa wakiwa wameenda hvyo ndio maana hawamalizi pamoja na Mungu kwenye maisha yao ya kila siku.

 2. TAMAA YA MACHO
Kwenye eneo hili la tamaa ya macho limekuwa likileta shida shida maana limekuwa likigusa vijana, mpaka viongozi wa kanisa kwa sababu ya kutokuvifisha viungo vyao katika kristo Yesu.

 Mwanzo 19:26 
 "Lakini mkewe Lutu akatazama nyuma yake, akawa nguzo ya chumvi."
Ukisoma habari nzima kwenye sura ya ya 19 utaona namna ambavyo Lutu na familia yake walivyoambiwa kwamba wasigeuke nyuma kuangalia Sodoma na gomora lakini mke wa Lutu aliweza kugeuka akiwa njiani kwasababu ya tamaa ya macho.
Fahari ya macho ni kutazama kitu chochote kile lakini biblia inatuambia kwamba lazima tuwe makini mfano kuna mambo yambo yanaweza yakawa halali lakini yasifae ndio maana lazima uwe mtu wa kuweza kumsikiliza Mungu kwa kila hatua unayoenda kuipiga ndipo utakuwa na usalama lasivyo utajikuta unakosea wakati wote. 
Mfano kwa vija sio kitu cha ajabu huyu mtu ni mtumishi lakini anaangalia picha za ngono, na kuwaka tamaa kila amtazamapo binti yeyote sasa hii ni changamoto kubwa na ndio maana biblia inasema๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

 Mathayo 5:27-28
 "Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake."

Hapa inaeleza kwamba ukimtazama kwa kumtamani  tayari umekwisha kuzini naye. Kwahiyo lazima uangalie vile ambavyo unaishi na unavyochagua kuvitazama kwenye maisha yako ya kila siku. Watumishi wengi wameishia njiani kwasababu ya tamaa ya macho.

 3. KIBURI CHA UZIMA 
Hapa ukizungumzia kiburi cha uzima unamaanisha jumla ya dhambi au makosa ambayo mtu anakuwa anayafanya kwasababu yeye ni mzima au amepewa kufanya vyema zaidi na Mungu.
Watumishi wengi wamekuwa mda mwingine wakikataa kufanya huduma kwasababu wao wanapofanya huduma wengi huwa wanabarikiwa kwahiyo wanajikuta wakihitaji wapewe fedha nyingi ndipo wahudumu na hicho ndio kiburi cha uzima chenyewe sasa.

Mfano kuna baadhi ya waimbaji huwa hawawezi kuja kwa mialiko mpaka wapewe fedha nyingi sasa hiyo ni sehemu moja wapo ya vitu vitakavyo wafanya washindwe kuurithi ufalme wa Mungu maana wanafanya mambo ambayo ni machukizo mbele za Mungu. Na kwa mfumo huo hawawezi kwenda pamoja na Mungu.

Mungu akubariki kwa kuwa pamoja nami tangu tumeanza mpaka hapa.
Tutamalizia kipengele cha mwisho kwa wakati mwingine 

Ulikuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu 
Jina: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

No comments:

Post a Comment

KUSIMAMA IMARA NDANI YA YESU KRISTO (sehemu ya Pili_Final)

Bro Jackobo Utakuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu Jina: Bro Jackobo Number: +255766944441 Email: jackobombwaga@gmail.com Blog website: ja...