SOMO: KIJUMBA CHA UFICHO
Mwandishi:MBWAGA JACKOBO
Email. Jackobombwaga@gmail.com
Phone:+255766944441 and +255621036471
UTANGULIZI
Watu wengi sana makanisani wapo wanaendelea kuingia kanisani lakini maisha yao bado yako kama watu ambao bado wako nje ya kanisa. Tunakosa kukaa kwenye viwango vya MUNGU anavyovikusudia tukae katika hivyo
MANA YA SOMO LENYEWE
KIJUMBA CHA UFICHO ni hali ya kujitengenezea mazingira ambayo mtu anakuwa anaingia kanisani lakini bado ana matendo maovu ambayo kiuhalisia yanakuwa hayampendezi MUNGU hata kidogo
UFUNUO3;1-2Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.
MSINGI MKUU WA SOMO
MWANZO3:1-10
Baada ya Adamu na Eva kufanya Dhambi waliamua kwenda kujificha ili kwamba MUNGU asiwaone mahali walipokuwa amewaweka. Je unafikiri kwamba MUNGU alikuwa hamuoni Adamu??? Hapana MUNGU alikuwa anamuona adamu lakini hakukaa katika sehemu ambayo MUNGU alitaka akae..
Je ndugu yangu unafikiri kwamba maisha yako unayoyaishi ni yale ambayo kristo anataka uyaishi???
Je umekuwa mtu wa kuingia kanisani lakini umeacha matendo yako mema ambayo MUNGU alikusudia uishi katika hayo???
MATENDO 5:1-11
Anania na Safira walikuwa wameazimia mioyoni mwao kwamba wazuie sehemu ya kiwanja walicho kiuza kwa ajili ya kazi ya MUNGU.
Watu wengi sana wameingia kwenye kijumba cha uficho ni kwa sababu ya UONGO.
MATENDO5;3 Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?
Kwa hiyo kama kanisa lazma uingie kwa kichwa na miguu yako yote kwa KRISTO YESU ili aweze kukufanikisha uweze kufika kwenye lengo la MUNGU anania na safira walifanya hivyo ni kwa sababu walikuwa hawajaamua kwelikweli ndani ya mioyo yao kwamba watayoa sehemu ya mali yao kwa ajili ya kazi ya MUNGU.
MAMBO YA KUYAFANYA ILI UWEZE KUONDOKA AU KUTO KUINGIA KWENYE KIJUMBA CHA UFICHO KWENYE MAISHA YAKO
1. Kuutafuta UTAKATIFU
UTAKATIFU ni kufanya kwa adili kama vile MUNGU anataka uwe
MAMBO YA WALAWI 20:26;
MAMBO YA WALAWI 20:6-8
Jitakaseni basi, iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.
Kwa unayayetaka kumuona MUNGU lazima uachane na Dhambi omba toba na rehema mbele zake ili akutakase maisha ya utakatifu yatakufanya uwe na usalama katika maisha yako ya kila siku na hautoingia kwenye dhambi
2. Lazima uwe MTIIFU katika kila jambo jema
1SAMWELI15:22Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.
Sauli hakusikiliza namna ambavyo MUNGU alimuamulu afanye akafanya mateka ya vitu ambavyo hakuamuliwa maana aliambiwa ateketeze kila kitu ila yeye aliona hakuna umuhimu wa kuifuta na kuisikiliza sauti ya MUNGU sasa mpendwa ukitii utakuwa na nafasi kubwa mbele za MUNGU lakini kama usipotii utakuwa kwenye kijumba cha uficho
3. Lazima uwe mtu wa MAOMBI
MAOMBI ni mawasiliano ya mtu na MUNGU wake
Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.
MATHAYO7;7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
Lazima uwe mtu wa maombi ndipo utaweza kuishi maisha ya kumpendeza MUNGU lasivyo utakuwa unajidanganya
4. LAZIMA UPIGE TATHMINI YA MAISHA YAKO YA WOKOVU
UFUNUO3:3 NA UFUNUO2:2-4
Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.
Ukiwa unakaa chini na kupiga tathimini ya ulikotoka na unakoelekea utaweza kuumaliza mwendo wako vizuri katika safari yako
LAZIMA UOKOKE ILI UWEZE KUMUONA MUNGU NAKUSHAURI MPENDWA KWAMBA USIKUBALI KUPOTEZA MDA WAKO KWENYE NYUMBA YA MUNGU WAKATI MAISHA YAKO HAYANA USALAMA TENGENEZA KWANZA NYUMBA YAKO NA ROHO YAKO KABLA YA YOTE
MUNGU AKUBARIKI KWA KUSOMA UJUMBE HUU SHARE NA WENGINE TUSHIRIKI BARAKA HIZI KWA PAMOJA
KIJUMBA CHA UFICHO
BADO NEEMA YA WOKOVU IPO HAKUNA HAJA YA KUOGOPA WEWE TUBU DHAMBI ZAKO UTASAMEHEWA NAWE UTAOKOKA
(MATHAYO 11:28)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
KUSIMAMA IMARA NDANI YA YESU KRISTO (sehemu ya Pili_Final)
Bro Jackobo Utakuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu Jina: Bro Jackobo Number: +255766944441 Email: jackobombwaga@gmail.com Blog website: ja...
-
Bro Jackobo Utakuwa nami mtumishi katika kristo Yesu Jina: Bro Jackobo Namba: +255766944441 Email: jackobombwaga@gmail.com Bwana Yesu asifi...
-
Bro Jackobo Utakuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu Jina: Bro Jackobo Number: +255766944441 Email: jackobombwaga@gmail.com Blog website: ja...
No comments:
Post a Comment