Bwana Yesu asifiwe kanisa??? Naomba tuangalie kidogo kuhusu uvaaji wa nguo kidogo katika VIMINI (NGUO FUPI NA IMPLICATION YAKE)
Kumekuwa na wimbi kubwa sana la kuwapoteza watu wakiwa wanadai kwamba eti kuvaa hakuna tatizo mbele za Mungu na wengine wanavaa vimini mpaka wakikaa wanatafuta vitambaa na kanga za kuficha maungio yao...
Sasa wewe umeokoka lakini unafanya hivyo je hilo ni tatizo au sio????
Naomba twende pamojaπ€²π€²π€²π€²
Tuanzie hapa tu jiraniππππ
MITHALI 12:16
Ghadhabu ya mpumbavu hujulika mara; Bali mtu mwerevu husitiri aibu
Note: Mtu aliye mwerevu huwa anasitiri aibu yake.
Naomba tujiulize ni kwanini sasa Binti unakuwa umevaa mavazi mafupi na madogo alafu unakuwa unapata shida unatamani kujifunika wakati mwenyewe ulichagua kuvaa vimini??
Hapo hutafuta asije akaaibika yaani mavazi yake mwenyewe yanamfanya awe na aibu
Sasa inakuwaje mtumishi wa Mungu eti unatuvalia vimini, vinguo vya kukubana mwili wako mpaka maungio ya mwili wako yanajulikana na kila mtu yaani mpaka unafika hatua kila mtu anajua namna maungio yako yalivyo pia kuna wakati hata nguo zako za ndani zinajichora alafu unasema umeficha aibu aiseee inatisha...
Embu tazama hapaππππ
1TIMOTHEO 2:9
Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani
Biblia iko wazi kabisa ikimtaka mwanamke avae mavazi yenye kusitiri( kuficha yale maungio yako i.e mapaja, nguo zake za ndani ambayo haya ilipaswa mume wake ndiyo ayaone)
Sasa wewe unavaa mavazi mafupi sana pamoja na kubana alafu unasema kwamba umesitiri mwili!!!!! Duuuhh ππππ na ndio maana unahangaika kutafuta kanga ili ujifiche maana umeiweka aibu yako peupe na unataka kuificha
Embu tazama maandiko hayaππ
MITHALI 7:10
Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo
Kuna mavazi ukivaa yanakutambulisha namna ulivyo sasa wewe umeokoka unavaa mavazi ya kikahaba (Vimini, nguo zenye kuchora maungio yako n.k) ambayo mtu yeyote akikutazama hamuoni Mungu bali anauona UASHERATI NA UZINZI ndani yako sasa unautofauti gani na mtu ambaye hajaokoka wewe???
Endelea nami utanielewaπππ
2WAKORINTHO 5:17
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya "
Kama ukiwa ndani ya kristo upekuwa kiumbe kipya mbona hatukuoni ukiwa tofauti na uvaaji wa makahaba?? Au unafikiri kwamba eti ni unakuwa kiumbe kipya katika Roho tu??? Hapana hata katika mwili wako lazima kuwe na utofauti
Embu tazama hiyoπππ
LUKA 6:45
Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake
Ukiwa mwema yanayotoka ni mema sasa inakuwa una Mungu ndani Yako lakini Bado mavazi yako hayana wema maana yako kama ya kahaba EMBU ACHANA NA MAVAZI YA AIBU NAMNA HIYO
Unafikiri kwanini YESU alisema amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye (MATHAYO5:28)
Mwanaume namna ameumbwa anaweza kupoteza dira kwa kumtazama mwanamke ndio maana haikuzungumzia amtazamaye mwanaume amekwisha kuzini nae (MUNGU AKUSAIDIE DADA KUELEWA) na ndio maana nimekwisha kukuambia kuna mavazi ya kikahaba
Hivi umewahi jiuliza kwanini makahaba huwa wanavaa vimini na nguo za kuwachoresha kila aina ya maungio yao???
Mavazi hayo huwa yanalenga kuwateka wanaume waingie katika tamaa ili wawatongoze hao wanawake wenye mavazi ya kikahaba ili ifuate anguko la aibu
Sasa dada wewe umeokoka kabisa na Bado unavaa mavazi ambayo yanaonyesha maungio yako hivi upya wako uko wapi na unatofauti gani na mtu asiyeokoka???
Yanayomtoka mtu ndiyo huwa yameujaza moyo wake haijarishi anajiita ameokoka.... Shetani haogopi kujiita kwako umeokoka anachotaka ni uwe chombo chake cha kuwarudisha watu nyuma....
Angalia umetumika kwa siri bila wewe hata kujua kuwa chombo cha shetani umewaangusha wengi katika dhambi kwa sababu ya kuvaaa kwako BADILIKA TUSIFARIJIANE MPENDWA SAFARI YA MBINGUNI NI KUJIKANA MWENYEWE
Nikikuona umevaa mavazi ya Aibu alafu unasema umeokoka unanipa wakati mgumu sana tena sana kukuelewa
Kuna wadada mna mtazamo kwamba UKIVAA NGUO FUPI UNAPENDEZA..... πππππ Pole zako
IMPLICATION YA KUAMBIWA UMEPENDEZA WAKATI UMEVAA NGUO FUPI
Haimaanishi umependeza isipokuwa wewe umevaa mavazi ambayo yanawafanya wanaume wawe kwenye msisimko wa kukutaka uingie kwenye zinaa yaani uasherati na Uzinzi
Mpendwa hata kama ni mtu ambaye uko nae kwa mahusiano anakuona umependeza ukiwa umevalia nguo za aibu (vimini) jua mtazamo wake umeharibika
EPUKA KUWA KIVUTIO CHA NGONO kwa watu
KWA AJILI YA UTUKUFU WA MUNGU NIKUSHAURI TU UACHE KUVAA MAVAZI YA AIBU UTAKUWA SALAMA PIA KUMBUKA MWANAMKE AJUAYE KUJISITIRI HUWA ANAPENDWA NA KILA MWANAUME NDUGU YANGU......
Muheshimu Mungu kwa mavazi yako
Wako mpendwa katika kristo Yesu
Bro Jackobo
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441 and +255621036471
No comments:
Post a Comment