Phone: +255766944441 and +255621036471
Email: jackobombwaga@gmail.com
Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu? naomba tushirikishane kidogo kuhusu hili somo maana imekuwa changamoto kubwa sana kwamba kwanini watu wanakula nyama ya nguruwe wakati biblia inazungumza kwamba ni mnyama najisi.
lakini ili tuelewe kwanini tunakula nyama ya nguruwe tutajadili hili somo katika misingi na mfululizo ufuatao
👉Mwanzo Mungu alipoumba ulimwengu aliweka watu wale vitu gani?
👉Vipindi mbalimbali vya maongozi ya Mungu katika biblia pamoja na utaratibu wake
👉Kwanini nyama ya nguruwe inaliwa katika kipindi hiki cha neema?
1. MWANZO MUNGU ALIPOUMBA
Baada ya Mungu kuumba ulimwengu huu na vyote vilivyomo, alifanya kwamba mwanadamu pamoja na mnyama yeyote walikuwa wanakula nyasi tu hapakuwepo Simba wala Chui wala mwanadamu aliyekuwa akila nyama
Mwanzo 1:29-30
“Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu; na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.”
Zaburi 104:14
“Huyameesha majani kwa makundi, Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu; Ili atoe chakula katika nchi,”
Hayo maandiko yanaonyesha wazi kwamba katika mwanzo wa yote Mungu aliweka wazi kwamba watu wote pamoja na wanyama wale majani pamoja na matunda kuwa sehemu ya chakula chao cha kila siku.
kuna maswali Mengi sana kwamba kama ndio hivyo kwanini sasa Simba, chui n.k wanakula nyama siku za leo, Hapo tunahitajika kukaa sana na Mungu vizuri ili atufundishe. naomba nisiende mbali sana naomba nirudi kwenye mtirriko niliouorodhesha pale juu kwamba tutaenda nao.
2. VIPINDI MBALIMBALI VYA MAONGOZI YA MUNGU KATIKA BIBLIA PAMOJA NA UTARATIBU WAKE.
Vipindi au Nyakati za Maongozi ya Mungu kibiblia Zimegawanyika katika Maeneo makuu saba ambapo kila kipindi kilikuwa na utaratibu wake uliokuwepo. Katika vipindi hivi vyoote Mungu aliweka sheria mbalimbali za kuongoza vipindi hivyo,Mtu asipofahamu vizuri anaweza kuchanganya mambo katika vipindi hivyo Mungu aliweka au kubadili sheria zake kulingana na nyakati hizo na makusudi yake aliyoyakusudia kwa wakati huo.
✍️INNOCENCE PERIOD
Hiki kilikuwa ni Kipindi toka uumbaji mpaka anguko la Adamu. katika kipindi hiki tukiangalia katika habari ya vyakula Mungu aliweka sheria kubwa moja ambayo ilikuwa kwamba ale majanj pamoja na matunda ya miti pekee (Mwanzo 1:29) huku akiwapa katazo la kutokula Tunda la ujuzi wa mema na mabaya (Mwanzo 2:17) na hazikuwepo sheria kwamba usiue, usizine n.k simply ni kwasababu walikuwa wawili tu.
👉CONCIENCE PERIOD-KIPINDI CHA DHAMIRI
Hiki kilikuwa ni kipindi cha kutoka anguko mpaka wakati wa Gharika. katika kipindi hiki Mungu alikuwa akitenbea nao wanadamu katika utaratibu aliokuwa nao toka kipindi cha uumbaji mpaka anguko lakini anakuja kuongeza jambo baada ya gharika kwamba wale na nyama isipokuwa uhai yaani Damu
Mwanzo 9:3-4
“Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote.Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.”
Sasa kama utakuwa makini utaona hapo kwamba kila chenye uhai, sasa tujiulize hivi Nguruwe ana uhai(damu)? bila shaka utagundua ni ndio anao uhai. kumbe hata nguruwe alikuwa mmoja wa waliokuwa wakiliwa kipindi hicho baada ya gharika ile.
✍️HUMAN GOVERNMENT PERIOD
Hiki kilikuwa ni kipindi ambacho kilikuwa cha kujitawala mpaka wakati wa ibrahimu. Hapa hakuna specification maalumu ambayo Mungu kaweka kuhusu vyakula kwahiyo walitembea sawa na kipindi cha kutoka gharika
✍️PATRIARCH/ PROMISE PERIOD
hiki ni kipindi ambacho kimeanza wakati wa ibrahimu yaani mababa wa imani mpaka Musa. hapa pia ni kama kipindi cha hapo juu tu. Ukiangalia utakutana na ahadi nyingi Mungu anauwekea Ibrahimu, Isaka, Yakobo na Yusuph.
✍️LAW DISPENSATION PERIOD- KIPINDI CHA SHERIA
Hapa ndipo pana himbuko la mambo Mengi sana ambapo ndipo kilikuwa kipindi cha sheria za Musa ambacho kimeanza kwa Musa mpaka wakati wa Yesu kristo. ambapo Mungu aliwaamuru wale baadhi ya vyakula na vingine waviache wasile. Yani kukawa na mwanzo wa vyakula najisi na visivyo najisi. Hii ilikuwa ni kwa sababu za kiafya na kutafuta utii wa Israel, baadhi ya vitu vilivyokatazwa ni pamoja na Ngamia, Sungura, Nguruwe, Kambale, Taa, Pweza, Ngisi, n.k. Mungu aliwakataza WAYAHUDI peke yao wasile baadhi ya wanyama na samaki wote wasio na Magamba na wanyama wasio na kwato zilizopasuliwa kati, au wenye kwato zilizopasuliwa kati lakini hawacheui soma (WALAWI 11;1-47).
Pia maandiko Mengine mfano
Kumbukumbu la torati 14:8
“na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.”
ISAYA 66: 17
“Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani, nyuma yake aliye katikati; wakila nyama ya nguruwe, na machukizo, na panya; watakoma pamoja, asema Bwana”
Hapa ndipo unaweza ukajikuta unachukuliwa na Upepo wa kila namna yaani ukikutana na msabato atakupa changamoto pia ukikutana na muislamu atakupa changamoto.
Lakini usiogope tutaona kwanini sasa imefika hatua tunakula nguruwe wakati biblia imeonyesha wazi kwamba msile…. ENDELEA NAMI..
✍️DISPENSATION OF GRACE-KIPINDI CHA NEEMA (KIPINDI CHA WAKATI WA MATAIFA)
Hiki ni kipindi cha kuanzia Yesu kristo mpaka wakati huu tulio nao wakati huu ukiwa unasoma ujumbe huu. Wakati wa neema ndio wakati huu wa agano jipya ambapo tunaruhusiwa kula kila kitu bila kujali wala kuulizauliza. Naomba kipengele hiki nitarudi mbele kidogo na ndio nitakujibu kwanini tunakula kila kitu isipokuwa bado uhai hatutakiwi kula. ngoja nimalizie kipindi cha mwishokatika biblia
✍️ESCATOLOGICAL TIMES
Hiki ni kipindi cha wakati unaokuja yaani mmbo yajayo( dhiki kuu, hukumu ya mataifa, utawala wa miaka 1000, ziwa la moto, vita ya gogu na magogu, mbingu mpya na nchi mpya n.k
3. KWANINI NYAMA YA NGURUWE INALIWA KATIKA KIPINDI HIKI CHA NEEMA?
Tumekwisha kuona vipindi mbalimbali katika biblia na namna ilivyokuwa na tumekwisha kuelewa tuko katika kipindi kipi ( tuko kipindi cha neema). Wakati huu Mungu aliamuru kuliwa kwa vitu vyote isipokuwa damu ambayo kibiblia imekatazwa milele.
unaweza ukajiuliza maswali yafuatayo
👉kwanini nasema kwamba wakati huu tumeruhusiwa kula
👉Je, kuna aya yeyote ile katika Agano Jipya inayo mkataza Mkristo kula nyama ya Nguruwe?
👉Je, kuna sheria yeyote ile kwenye Agano Jipya inayo kataza kula nyama ya Nguruwe?
👉Je, Yesu alisema au waamrisha Wafuasi wake wasile Nyama ya Nguruwe?
Theolojia inatueleza kwamba vizazi vya ulimwengu huu vimetokana na wana watatu wa Nuhu ambao ni Shemu, Hamu, na Yafethi sasa katika historia ya chanzo cha mataifa mbalimbali kama inavyoelezwa kwamba wanadamu yaani mataifa yote yaliotokana na watoto wa Nuhu walikuwa wakiishi pamoja na walikuwa na lugha moja na usemi mmoja na waliishi pamoja, wanadamu hawa ikumbukwe kwamba hawakupewa sheria yoyote inayohusiana na wanyama wapasao kuliwa na wasiopaswa. hawakupewa na hapa tunaelezwa ndio chanzo cha mataifa mbalimbali maana baada ya Mungu kuwachafulia lugha walisambaa kila mmoja mahali pake (Mwanzo 11:1-9}
msitari wa tisa(9) “Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote.”
Sasa swali la kujiuliza je wanadamu hawa waliondoka na ufahamu upi kuhusiana na vyakula, kwamba Nguruwe haramu ama?
Maana ifahamike kuwa kwao walipewa wanyama wote kuwa chakula kwa sababu hawakuwa na sheria inayohusiana na vyakula safi na visivyo safi kwao wanyama wote ni safi tu waliondoka na imani hiyo kama walivyopokea huu ndio ukawa mwanzo wa mpishano wa vyakula baina ya watu walioitwa wa mataifa na wayahudi baada ya wao kupewa sheria iliyohusiana na wanyama walio safi na wasiokuwa safi.
Tena unaweza kujiuliza sasa kama walipewa wayahudi sasa kwanini sisi tu akula nyama wakati yesu mwenyewe alikuwa myahudi? naomba twende pamoja
WAKOLOSAI 2:16
“Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato”
Hapo ukisoma utaona ya kwamba inakuambia kwamba mtu asije akakuhukumu kwa sababu ya vyakula kwahiyo unapata picha kwamba hakuna hukumu katika chakula. sasa ukiangalia unaweza fikiri kwamba kama kasema mtu je Mungu yeye itakuwaje?
Pia hapa utakutana na watu wanakuambia eti nguruwe sio chakula lakini wewe usiogope mrudishe kwanza asome MWANZO 9:3 kwamba kila chenye uhai kitakuwa chakula chenu sasa hapo tunapata picha kwamba nguruwe ni chakula.
1TIMOTHEO4:1-4
“Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli. Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;”
Paulo anatuweka wazi kabisa kwamba mafundisho ya kishetani yatakuwa yakiwaambia watu waachane na vyakula. Sasa kwani Mungu alipokuwa amewakataza wana wa Israeli alikuw ana ushetani ndani yake?
Hapana Mungu yeye ni mtakatifu (mambo ya walawi 11:4) na ni wa kuaminiwa wakati wote haijarishi ikoje
WARUMI 14:14
“Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi”
Mungu amekwisha kuvifanya vitu vyote kuwa vitakatifu maana tangu asili vilikuwa vitakatifu kwahiyo ukitaka kujua kwanini sasa aliwakataza utarudi nyuma uone kwenye kipengele cha “kipindi cha sheria” utaelewa
Biblia inafundisha kuwa kula au kutokula hakuongezi utakatifu wala hakuzuii tamaa za mwili (Kolosai 2;16-23) hivyo hatupaswi kujitia katika mambo ya kutunga tu ya mtu,au akilizake na maono ya wanao abudu malaika kumuabudu Mungu hakuji kwa kula au kutokula aina fulani ya vyakula bali katika moyo safi (Math 5;8)
Ukitaka kuelewa zaidi utaona kwamba wana wa Israeli walikuwa wanazuiliwa hata kugusa mizoga ya hao wanyama walio najisi lakini biblia inaonyesha wazi baada ya kuzaliwa kwa yohana mbatizaji alipokuwa kule nyikani alivaa mavazi ya ngamia ambaye alikuwa ni mnyma asiyeruhusiwa kuliwa.
MATHAYO 3;4
“Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu”
sasa hapo ndipo unaweza ukachanganyikiwa kwamba kwanini sasa aliyekuja kuandaa njia ya Kristo alivaa singa ambayo imetengenezwa kwa ngamia kwahiyo hapo unaweza kupata picha kwamba mambo yale yalikuwa katika kipindi cha sheria sasa ilikuwa tunaingia katika kipindi cha neema kwahiyo ilimpasa kwamba aandae mazingira ya kipindi cha neema kwahiyo ilitakiwa ianze hivyo.
Biblia inafundisha kuwa unajisi wa mtu hautoki nje bali ndani ya mtu pia Yesu alitakasa vyakula vyoote (Marko 7;14-16,17-19)
1KORITHO 6;13
“Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili”.
Paulo anajaribu kutupa mwanga tuweze kuelewa kazi kubwa ya vyakula kwamba ni kwa ajili ya mwili kwahiyo hata nguruwe ni kwa ajili ya mwili na sio mambo ya Rohoni sasa kama wewe unaenenda katika Roho kwanini upambane na mambo ya mwilini kwahiyo ukishajua hilo hwezi ogopa kula kitimoto maana kiko kwa ajili ya mwili.
1WAKORINTHO 10:25-28
" Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila ya kuuliza uliza kwa ajiri ya dhamiri ,maana ,dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo, mtu asiyeamini akiwaalika ninyi mnataka kwenda ,kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila ya kuuliza -uliza kwa ajili ya dhamiri"
Kwahiyo kitu chochote kinachouzwa unaweza ukakinunua na kukitumia ikiwepo hata nyama ya Nguruwe sasa ukipingana na maandiko ndio hapo unafika hatua unang’ang’ana na mambo ya mwilini na sio ya Rohoni.
kutokana na namna tulivyochambua tukianza na vipindi mbalimbali mpaka tukachambua kipindi hiki cha neema ikoje tumeona maandiko yako wazi dhahiri kwamba kula kitimoto sio Dhambi na hakuna tatizo lolote lakini kama ukaongozwa na Roho kwamba usile basi usile maana kuna mambo Mengine Mungu huwa anafanya kwa watu maalumu kwa sababu maalumu na ndio maana ukiangalia samsoni alizuiliwa kukata nywele kwasababu kulikuwa na unadhiri ndani yake ambao patano lake lilikuwa katika nywele zake.
Ulikuwa na wako mpendwa katika kristo Yesu
Bro Jackobo
+255766944441 and +255621036471
jackobombwaga@gmail.com
Safi sana, vipi kuhusu Sabato na amri za Mungu?
ReplyDeleteAsante Sana mtumishi naomba utuandalie pia somo linalohusu Sabato Na amri kumi za MUNGU
ReplyDelete