Utakuwa namimi mpendwa wako katika kristo Yesu
Name:Bro Jackobo email: jackobombwaga@gmail.com
Phone; +255766944441
Bwana Yesu apewe sifa Wana wa Mungu? napenda tushirikiane jambo hili kidogo
Kanisa la Leo limekuwa ni waaminifu sana kuhudhuria Ibada na vikundi mbalimbali vilivyo ndani ya kanisa lakini nafasi ya Yesu ndani ya maisha yao imekuwa ni shida sana tena sana mpaka inaleta huruma kuona watu hawana msimamo kamili wa Ki-Mungu ila wanaishi kimazoea tu kama walivyoishi Jana.
Ndipo nakumbuka kuna wakati Yesu aliwahi kuzungumza neno lifuatalo
MATHAYO 15:8-9
"Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami Nao waniabudu bure Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu."
Wakuu wa dini walikuwa wakiishi kwa mapokeo lakini waliacha msingi wa kweli wa kumfanyia Mungu Ibada ya kweli kwahiyo katika vinywa vyao walikuwa wakitamka kumpenda Mungu lakini kiuhalisi hawakuwa na Mungu ndani yao na hili ndilo kanisa ambalo tuko nalo kizazi cha leo watu wanaeleza wema wa Mungu lakini hawawahi kupata Raha iliyoko ndani ya kristo. Ni kawaida Ukaona mtu anafundisha Ubatizo wa Roho mtakatifu lakini hajawahi kushuhudia Radha ya Roho mtakatifu hata siku moja..
Nampenda sana paulo maana alitamani kanisa liishi kwa mfano pia hata wake. Embu ona hayo mafunguππππ
1 WAKORINTHO 11:1
"Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo."
WAFILIPI 3:17
"Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi."
Mafungu yote hapo juu yanaonyesha namna paulo alivyojiweka kipaumbele mwenyewe ili kwamba watu waige mfano wao lakini kanisa la leo halina watu wanao weza kunena kwa ujasiri kwamba mnifuate mimi kama nilivyo mfuata kristo Yesu kwasababu maisha yao hayana ushuhuda hata kidogo maana wamejichanganya kupita kiasi tena kiasi. Mungu akukumbuke ndugu yangu badilika.
LUKA9:57
"Yesu akamwambia, Mbweha wana pango,na ndege wa angani wanaviota, lakini Mwana wa Adamu hana pa kujilaza kichwa chake."
Ukianza kusoma mistari ya nyuma utaona huyu mtu alitaka kumfuata lakini Yesu anakuja kumpa majibu magumu sana yule mtu kwamba hana nafasi ya kuweza kukaa kwake.
Yule mtu alikuwa na nia yakumfuata kristo lakini ndani yake alikuwa hajampa kristo nafasi hata kidogo maana Imani bila matendo imekufa πππππ
YAKOBO 2:17
"Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake."
Wengi wetu tuna nia ya kumfuata kristo lakini hatujaambatanisha nia zetu pamoja na matendo yetu. Na ndio maana biblia inasisitiza kujikana mwenyewe lasivyo utakuwa unaingia kwenye nyumba ya Mungu lakini hutakuwa una nafasi ya Yesu kristo.
MATHAYO 16:24
"Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate."
Nikuulize swali na wewe je umempa nafasi gani kristo Yesu kwenye maisha yako?
Au umekuwa na wewe unaingia kwenye nyumba ya Mungu huku umemuweka mbali sana Yesu kristo?
Au umekuwa ni mtu unaye mfuata Yesu wakati wa kustarehe na ukifika wakati wa magumu ulekuwa ukimuacha?
πlazima uwe mtu wa kuvumilia kutenda mema siku zote ndipo utapata nafasi ya kuurithi ufalme wa MUNGU lasivyo unajidanganya.
MATHAYO 24:13
"Lakinimwenye kuvumiliahata mwisho, ndiyeatakayeokoka."
Mwisho wa safari yako ya hapa duniani ndiyo taswira kamili ya kile unachotakiwa kukipata baada ya yote hayo maana baada ya kifo ni hukumu.πππ
WAEBRANIA 9:27
"Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;"
Kuna mafundisho yapo ambayo yanawaambia watu kwamba eti mtu anaweza kuombewa baada ya kufa akaenda peponi hayo ni mafundisho potofu yenye lengo la kuwafanya watu wasiogope kufanya dhambi wakiamini wataombewa na Mungu atawasamehe {wajidanganya bure} basi haikuwa na maana ya kuwaambia watu waishi maisha ya kumfuata Yesu na pia kwamba Ajikane mwenyewe basi Yesu angeseme mtu asiponifuata na ndugu zake watamuolbea akifa aende kwenye haki. Kwahiyo ukifa ni hukumu tu hakuna cha nafasi tena ya toba yani matendo yako yataambatana nawe.
Nikuambie tu ukweli kwamba kama umebadili mwili wako na moyo wako kuwa sehemuya uovu jua hukumu inakungoja haijarishi unaingia kanisani au hauingii
MATHAYO 21;12
"Yesu akaingiandani yahekalu,akawafukuzawote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni,akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwawakiuza njiwa"
kristo hataki michanganyo hata siku moja ndio maana alipoona wamegeuza sehemu ya ibada kuwa kama gulio ilimkasirisha sana YESU. ndivyo vivyohivyo anavyochukia pale unapoacha njia ya MUNGU na kufanya Mambo unayoyataka yaliyo tofauti na neno lake.
Tambua ya kwamba wewe ni hekalu tena u sehemu ya ibada ya MUNGU ndani ya moyo wako.
maana siku ile Mwana wa Mungu atakapokuwa kwenye kiti cha enzi atawabagua kama Mbuzi na kondoo kwa kadri ya mtu na matendo yake. (soma Mathayo 25:31-46)
usikae kwa hasara Mahali ulipo maana hukumu inakuja wala usije kuwa una mheshimu Mungu kwa kinywa tu bali na matendo yako yaambatane na namna kinywa chako kinavyozungumza.
nipende kukusihi ndugu yangu badirisha njia zako na kama bado hujatengeneza na MUNGU Yeyeb ado anatoa mwito yoyote aliye na mzigo wa aina yeyote yeye atakupumzisha.πππ
MATHAYO 11:28
"Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha."
Usiridhike na kuingia kwako ibadani tu ridhika ikiwa unashuhudiwa na Roho mtakatifu kwamba umekaa sawa.
WARUMI 10;10
"Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu."
kazi yako ni kuamini na kumpa kristo maisha yako na sio kwenda kanisani tu na huku unafanyavitu visivyofaa
Saa ya hukumu iko karibu badili njia zako ndugu yangu.
Mungu alibariki kwa kuusoma ujumbe huu na Mungu akupe hatua ya kutoka katika kifungo chako kinachokutesa kinachokufanya unakuwa na maisha ya kifafa.
Unaweza ukapata masomo yanu mengine ukatafuta kwenye browser yako kwa kuandika
(Jackobombwaga.blogspot.com)
Ulikuwa nami mpendwa katika kristo Yesu
Name:Bro Jackobo
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441
Amina kubwa
ReplyDeleteHaleluya.....
ReplyDeleteAsante sana Brother na Mtumishi wa Mungu kwa neno hili jema, Mungu akubariki sana Ndugu.
Asante.....
Amen
Delete