JIFUNZE KUWA MWAMINIFU MPAKA MWISHO HATA KAMA UNAONA UGUMU


Bro Jackobo {JAM295}

Utakuwa nami mpendwa katika kristo Yesu.
Name: Bro Jackobo
Phone; +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu?? Karibu tushiriki pamoja neno hili kwa kifupi sana katika siku hii ya leo.

Kumekuwa na ugumu sana wa watu kuutunza uaminifu pindi pale mazingira kwao yanapokuwa magumu na mazingira ya kweli yao yanawaumiza wao wenyewe.

Mwanzo 39:9-12
"Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?
Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye. Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani; huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje."

Yusufu alipita wakati mgumu ambao huo wakati ulikuwa mgumu maana yake alipata nafasi kabisa ya kuweza kulala na mke wa potifa lakini yeye aligoma kabisa kulala na mke wa potifa maana alikuwa akitafuta kuwa mwaminifu mbele za MUNGU hakujali hata kukimbia na kuacha mavazi yake ambayo aliona kwamba yangemletea shida hata kwa baadae kwenye maisha yake.

Jiulize mara ngapi wewe umeacha sheria ya MUNGU kwa sababu ya magumu yaliyokuzunguka?? Ni mara ngapi umevunja uaminifu wako kwa sababu ya vitisho kwenye maisha yako ya kila siku??

Mathayo 15:8-9
"Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure,
Wakifundisha mafundisho
Yaliyo maagizo ya wanadamu."

Mbona umekuwa ni Mtu wa kumuheshimu Mungu tu kwenye maisha yako kwa kinywa lakini matendo yako yamekuwa yakimkana Mungu siku zote.

Au hujui ya kwamba kuna laana ipo pale ambapo mtu akifanya mambo ya ajabu lakini asiwe tayari kuishi katika kweli ya Mungu? ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Mithali 28:13
"Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema."
Ukiwa mtu wa kumheshimu MUNGU kwa kinywa tu na matendo yako yanamkana MUNGU inamaanisha huwa unauficha ubaya wako wa kila siku baada ya kwamba uutubie huo ubaya wako wewe unaendelea kujificha jua ya kwamba unajiletea laana mbele za Mungu kwenye maisha yako.

Ndio maana nakushauri ndugu yangu kwamba uamue kuwa mwaminifu siku zote za maisha yako hata kama unaona magumu kwenye maisha yako.

Ndio maana YESU anakushauri hivi
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Ufunuo wa Yohana 3:15
"Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto."

Katika maandiko hayo hapo juu yako wazi kabisa na yanakutaka uamue kuchagua upande mmoja wa kuwa mwaminifu ukiamua kuwa wa kristo basi uishi kama Kristo na kama ni kwa shetani uishi kama kwa shetani tu. Usiwe mtu wa kumega huku na kule.

MAENEO AMBAYO YAMEKUWA NA KUKOSEKANA KWA UAMINIFU NDANI YA KANISA
Kuna maeneo mbalimbali na mengi sana ambayo yamekuwa na changamoto kuwa na uaminifu lakini nitakuelezea maeneo machache tu
{A} Mahusiano, uchumba na ndoa
{B} Biashara
{C}Ibada na maombi
{D} Matoleo pamoja na ahadi

{A} MAHUSIANO, UCHUMBA NA NDOA
mahusiano na uchumba
Vijana wengi wamekuwa wanaingia kwenye mahusiano na uchumba kwa siri na hata kufanya mambo yasiyotakiwa kwa siri(kukosa uaminifu) huku wanafanya ibada kila inapoitwa leo
Mbona umekuwa unafanya tendo la ndoa, unafanya Romance wakati hauko kwenye ndoa ndugu yangu? Mungu akupe neema utoke huko kwa jina la Yesu kristo.
Kuna watu wanadai kwamba miili inawasukuma kufanya hivyo lakini nawaambia kuna mambo mawili hapa ya msingi ukiyajua yatakusaidia๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰Moja: Mwili kuhitaji tendo la ndoa kwa mwanadamu ambaye yuko vizuri kibiolojia ni kitu cha kawaida lakini umepewa namna ya kuweza kushinda


Wagalatia 5:16
"Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili."

Hapo juu biblia inakuambia uenende kwa Roho ili usitimize tamaa za mwili kiufupi ni kwamba tamaa za mwili zitakuja isipokuwa ili usizitimize/usiziishi lazima uwe katika Roho yaani ukubali kuwa chini ya maongozi ya Roho mtakatifu lasivyo utakuwa unajidanganya tu. Wengi wanajikuta kuingia kutenda dhambi ni kwasababu hawajakaa katika Roho mtakatifu.

1 Wathesalonike 4:3-5
"Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu."
Maandiko hapo juu yanakukukataza uasherati lakini yanakuambia ujue kuuweza mwili wako katika utakatifu na heshima kwahiyo hata kama ikitokea wewe nenda mbele za Mungu kwa moyo wa Toba na yeye atakusamehe na kukusafisha kabisa.
Mwingine anaweza sema nawaambia watu waendelee katika tamaa lakini sio hivyo ila hiyo inatokea na ndio maana paulo alisema

1 Wakorintho 7:1-2
"Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke.
Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe."
Hapo anaeleza habari ya zinaa ndio inamfanya mtu basi awe na ile ya kumgusa na kuwa na mke au mume ambapo zinaa ni matokeo ya tamaa. Kwahiyo usiogope ikitokea hivyo ila mtafute Mungu atakusaidia.

Note: mtu asije akakudanganya kwamba eti ukiwa katika kristo kama ni kijana uliye okoka kushituka hakupo. Kushituka kupo ila Mungu anatutunza na kutupa uwezo wa kustahimili. Aliposema kila mtu ajue kuuweza mwili inamaana mwili kuna namna utahitaji hakusema mkiwa katika kristo mwili utakuwa hauna chochote. Na anaposema kwamba hatutatimiza tamaa za mwili maana yake yapo matamanio ya mwili ila tukiwa katika Roho hatutayaishi.

๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰Pili, Tendo la ndoa sio dhambi kabisa ila likifanyika kwa wakati sahihi na kwa watu sahihi

Kwahiyo ukiona huwezi kukaa bila tendo la ndoa basi jitahidi kuoa au kuolewa na kuepukana na hatia ya dhambi itakayokuwa kwako kwa kuqhindwa kujizuia kwako.

Ndoa
Pia hapa kuna changamoto kubwa sana ndani ya kanisa unaweza kukuta mwalimu wa kwaya au kiongozi yeyote anatembea na mshirika ndani ya kanisa mahali palepale kitu ambacho kinaleta shida kubwa sana ndani ya kanisa.

Mpendwa usiendelee kujifariji tu kwamba uko na Mungu kumbe Mungu amekuacha  tubu dhambi yako biblia imejieleza kabisa katika
Kutoka 20:14 "Usizini." Jitahidi utoke huko bado Mungu anakupenda.

{B} BIASHARA
Katika eneo hili Mungu atusaidie kanisa tutoke hapo maana wafanyao biashara wamekuwa ni watu wa kuwaibia wale watu wanaowauzia wakitaka kupata faida kubwa katika vile vitu wanavyovuza mfano
๐Ÿ‘‰Watu hutengeneza vifaa vya kuuzia vidogo chini ya kipimo sahihi na namna inatakiwa n1 kujikuta wakifanya mambo yasiyofaa na kuangukia katika Dhambi

Mambo ya Walawi 19:35
"Msifanye yasiyo haki katika hukumu, wala katika kupima, wala katika mizani, wala katika cheo."
Mithali 11:1
"Mizani  ya hadaa ni chukizo kwa BWANA; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza."
Ezekieli 45:10
"Mtakuwa  na mizani ya haki, na efa ya haki, na bathi ya haki."
Maandiko hayo yamejieleza kufanya katika mizani ya haki kwahiyo jitahidi kuwa mwaminifu katika eneo hilo 
๐Ÿ‘‰pia watu walioajiliwa huwa wanaiba katika faida zile wanapata na kupeleka pungufu kwa waajiri wao.
Kwahiyo Mungu akusaidie ufanye kama inavyotakiwa usiwe mtu wa kuvunja uaminifu bado Mungu anakupenda.

{C} IBADA NA MAOMBI
Watu wengi wamekosa kuwa waaminifu kwenye maisha yao binafsi maana wamekuwa ni watu kufanya ibada ili waonekane lakini unakuta ndani yao hakuna ibada ya kweli jifunze kuwa mtu wa ibada ya kweli inayoanzia ndani mwako hata unapokusanyika na wenzio basi iwe kama hitimisho la ibada na Mungu atakufanikisha sana na utanawili sana kwenye maisha yako ya kila siku.
Katika eneo la maombi inakubidi kufanya kama maandiko yanavyotaka kufanyika basi Mungu akupe neema nmejaribu kukuelezea kifupi tu ili upate mwanga.
 
Kwahiyo jitahidi kuwa mwaminifu katika eneo lolote ambalo utakuwa umekaa na ndio maana na ndio maana huwa nina msemo mmoja huu๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡ 

UKIWA MWAMINIFU TU MBELE ZA WATU WAKATI UKIWA MWENYEWE HUWEZI KUUTUNZA UAMINIFU BASI UJUE WEWE SIO MWAMINIFU BALI NI MIONGONI MWA WANAFIKI WALIOPO

Nina Mengi ya kusema katika hili lakini naomba nieleze tu hiyo kifupi maana kuna baadhi ya mambo hapo unaweza ongezea mfano
๐Ÿ‘‰Mambo yatakayoniwezesha kuwa na uaminifu
๐Ÿ‘‰Namna gani baadhi ya watumishi waliomfano wa maaandiko walivyotunza uaminifu wao kila siku
๐Ÿ‘‰Faida za uaminifu 
๐Ÿ‘‰Madhara yatokanayo na kukosa uaminifu

Yote hayo ningeyazungumzia lakini kwakuwa nimepewa kwa leo kuandika hayo naomba niishie hapo ila kama itatokea neema nitaandika sehemu ya pili ya hili

Ulikuwa nami mpendwa katika kristo Yesu.
Name: Bro Jackobo
Phone; +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

10 comments:

  1. Tunamushukuru Mungu kwa kutukanya na kutukumbusha njia iliyo sahihi ya kwendea.

    ReplyDelete
  2. Tunamushukuru Mungu kwa kutukanya na kutukumbusha njia iliyo sahihi ya kwendea

    ReplyDelete
  3. Hallelujah.....
    Mungu akubariki sana Ndugu, na pia anisaidie niwe mwaminifu mbele zake milele na daima yote,
    Amen

    ReplyDelete

KUSIMAMA IMARA NDANI YA YESU KRISTO (sehemu ya Pili_Final)

Bro Jackobo Utakuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu Jina: Bro Jackobo Number: +255766944441 Email: jackobombwaga@gmail.com Blog website: ja...