Utakuwa ndugu mpendwa
Bro Jackobo (JAM295)
Phone: +255766944441 and +255621036471
Email: jackobombwaga@gmail.com
Naomba twende wote kwa pamoja
Mara nyingi tumekuwa tukichukulia kawaida suala la Mahusiano ya kirafiki na kiuchumba na kuona ni kama kipindi cha Kujiachia,au cha Kujaribu jaribu kama kuna bahati yako au la, kumbe nikipindi Muhimu ambacho ni msingi wa ndoa ya mtu.
Ndoa nyingi zina machafuko yasiyokoma,ambayo masuluhisho mengi ya kwa wazazi, wasimamizi,wachungaji,mpaka na mahakama yamegonga mwamba hakuna kutulia, Machafuko yametokea kwasababu mbalimbali lakini nitazungumza juu ya jambo moja tu ambalo ni kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa au Msingi Mbovu wa Mahusiano unaoambatana na Tendo la Ndoa.
Miongoni mwa vitu ambavyo wengi wa wanaofunga ndoa upuuzia nakuona ni kitu kidogo,ni Ni wao kuanguka katika zinaa(Kushiriki ngono)kabla ya ndoa halafu wakaoana wakiamini wanaendeleza Upendo,kumbe ndo wamefuta upendo.
ππLabda nikupe siri hii ya Kisaikolojia na kiroho sex ina pande mbili za shilingi ni TAMU na INAUNGANISHA NAFSI ZA WATU na kuwafanya wawe na Sura moja (Kama imefanyika katika muda muafaka kwa watu sahihi bila hatia)ππ
1 SAMWELI 1:19
"Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za Bwana, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye Bwana akamkumbuka."
ππSex ikifanyika kwa watu waliosahihi yaani mke na mme ina MKONO WA BWANA WA BARAKA.
πPili SEX inakawida ya Kuwaachanisha watu nafsi, kufuta upendo, Amani, furaha kati ya watu Walioifanya Kinyume, nje ya muda na si watu sahihiππ
2SAMWELI 13:10-17
" Amnoni akamwambia Tamari, Kilete chakula chumbani, nipate kula mkononi mwako. Basi Tamari akaitwaa mikate aliyoifanyiza, akamletea Amnoni nduguye mle chumbani. Naye alipokwisha kuileta karibu naye, ili ale, Amnoni akamkamata, akamwambia, Njoo ulale nami, ndugu yangu. Naye akamjibu, La, sivyo, ndugu yangu, usinitenze nguvu; kwani haifai kutendeka hivi katika Israeli; usitende upumbavu huu. Nami nichukue wapi aibu yangu? Wewe nawe utakuwa kama mmoja wa wapumbavu wa Israeli. Basi, sasa, nakusihi, useme na mfalme; kwa maana hatakukataza kunioa.
Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye. akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako. Naye akamwambia, Sivyo, kwa kuwa mabaya haya ya kunitoa ni makuu kuliko yale uliyonitendea. Lakini alikataa kumsikiliza. Ndipo akamwita mtumishi wake aliyemtumikia, akasema, Mtoe sasa mwanamke huyu kwangu, ukafunge mlango nyuma yake."
ππ Wakati sex isiyo halali inakuwa ina vutia na inapofusha macho nikama unajituliza ila matokeo yake baadaye INAFUTA KILA AINA YA FURAHA NA AMANI KATIKA NAFSI ZA WAWILI
MADHARA YA TENDO LA NDOA KABLA YA NDOA
Naandika haya sio kukupa hofu bali kukufanya uweze kutambua madhara na matokeo ya jambo utakalo kulifanya
1. Madhara ya kiujumla wa maisha ya mtu
2. Madhara wakati mkiwa kwenye mahusiano
3. Madhara mkishaingia kwenye ndoa
1. MADHARA YA KIUJUMLA YA MAISHA YA MTU
ππ DHAMBI
Kiasili toka mwanzo tendo la ndoa sio dhambi kabisa ila likifanyika kwa wanandoa tu na kama wanandoa wakiwa pamoja basi hata Roho wa MUNGU anakuwepo akiwafurahia na ndio maana toka asili alimuumba mtu mume na mke (MWANZO 1;27) lakini kwa wasiokuwa wanandoa ni dhambi.
Hapa sipendi nipazungumzie sana ila inafahamika kwamba afanyaye tendo la ndoa kabla ya ndoa huyo kwake ni dhambi
ππ KUVAMIWA NA MAROHO MACHAFU.
Katika kufanya ngono, wengine wanaenda hadi kwa waganga wa kienyeji na wachawi na huko wengine wanapewa madawa ya ajabu ambayo yanapelekea kuwamiwa na mapepo ya ajabu, na wengine kwa kupenda ngono wamefanya ngono na majini bila wao kujua na tayari yamesha wamiliki na hawajui watatokaje kwenye kifungo hicho. Lakini Mungu wetu ni wa Rehema anao msaada kwako kupitia Yesu kristo yaani msamaha wa Dhambi kama ukikubali na kumuamini Yeye utapata ondoleo la dhambi na kuwekwa huru kabisa
ππ KUWAPA WENGINE MIAKA YAKO.
Uchunguzi unaonyesha kwa mtu anayependelea kufanya ngono mara kwa mara hasa anapoanza kabla ya ndoa mara nyingi hawezi kuishi kwa muda mrefu si hivyo tu lakini pia tumeona mara nyingi vijana wakijiua/wakiuana /wakifa kwa ajili ya mapenzi, wengine wanaugua hadi wanakufa wadogo na kupatwa na magonjwa mabaya, na hivyo muda waliostahili waishi hapa duniani na hivyo wanakuwa wamewapa wengine miaka yao.πππ
MITHALI 5:9
"Usije ukawapa wengine heshima yako na wakorofi miaka yako"
Ukitaka kuelewa vizuri fungu hili soma sura nzima ya mithali 5 utaelewa kwanini nimesema hivyo
2.MADHARA MKIWA KWENYE MAHUSIANO
Hapa tutaona mkiwa bado hamjaoana nini huwa kinatokea
ππ Kupoteza Uaminigu baina yenu
kisaikolojia watu wakikutana na kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa huwa inakuwa ngumu kuaminiiana maana kuna kuwa na hisia za kwamba atakuwa anafanya hivyohivyo kwa wengine so kuaminiana kunakuwa kugumu
ππKupungua au kufa kwa Upendo
ukisoma kwenye fungu la juu utaona namna ambavyo Amnoni baada ya kufanya tendo la ndoa na tamari alimchukia sana tena sana na ndivyo iko kwa watu ambao wanafanya hivyo kabla ya ndoa
Baada ya kufanya mapenzi mara nyingi upendo hupungua hasa kwa vijana wa kiume na kwa mabinti upendo huongezeka na hii imewafanya Mabinti wengi wamejikuta wakipoteza THAMANI yao baada ya kuruhusu ku'sex na vijana wa kiume wakidhani kuwa kwa kufanya hivyo upendo utaongezeka kwa mwanaume kumbe wanajitengenezea misiba yao wenyewe.
Note: Upendo wa mtu huwa haupimwi kwa njia ya sex kwahiyo uwe makini.
ππ kuwashibisha wengine nguvu zako.
Mithali 5:10
"Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni"
Tendo la ndoa ni tendo linalohitaji mtu atumie nguvu, hivyo kadri mtu (hasa mwanume) anapofanya mara kwa mara anajipotezea nguvu zake anawashibisha wengine nguvu zake na hivyo dhoruba itamkuta katika ndoa yake pindi atakapooa kwa sababu hatakua na nguvu tena kama awali.
ππ utavunjiwa heshima.
Siku zote yule unayefanya naye tendo la ndoa kwanza atakuona wewe ni mpumpavu kwa sababu anajua afanyaye tendo hilo hana akili kabisaππ
mithali 6:32
"Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake"
kwa hivyo atakudharau, zaidi atakutangaza kwa wengine na wewe mwenyewe pindi utapooa au kuolewa kwa kuwa nguvu zako uliwashibisha wengine basi utavunjiwa heshima na huyo mwenzi wako.
ππ Kufanya jambo liangamizalo nafsi yako
Mithali 6:32
"Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake."
Nafsi kwa kiyunani inaitwa Psuche, ndani yake kuna hisia, akili na maamuzi ya mtu. Hivyo kuiangamiza nafsi yako ni kuangamiza future yako na mipango yako uliyokuwa umejiwekea ya mbele na ndio maana mtu huyu akishazoea kufanya tendo la ndoa atajikuta mda mwingi akili yake inamsukuma akafanye tendo la ndoa maana nafsi yake haina uwezo wa kuamua vyema. Kuna mengi ya kueleza hapa lakini ngoja niweke tu kiufupi sana hivyo.
ππ Kujitengenezea Majeraha na Fedheha
Sikiliza katika ngono unaweza ukapata kilema cha maisha, na magonjwa ya hatari kama vile kaswende, ukimwi n.k. Haya magonjwa yatapelekea nyama na mwili wako kuangamia utashindwa kufikia malengo uliyojipagia, utabakia kujuta tu na watu watakufanyia fedheha na wakati huo upo kitandani hujiwezi.
πππ
MITHALI 6:33
" atapata jeraha na kuvunjiwa heshima wala fedheha yake haitafutika"
3. MADHARA WAKATI WA NDOA
Sasa hapa tutaona matokeo yanayoweza kutokea kipindi mko katika ndoa.
ππ uaminifu kati yenu inakuwa changamoto
Kuna uwezekano mkubwa Hakuna atakaye kuja kumwamini mwenzake kwamba atakuwa mwaminifu kwasababu ulikuwa na Ujasiri wa kuvunja uaminifu wako mbele zake katika ujana wako.
kwa sasa ndo anaona huwezi shindwa vunja tena huo uaminigu wako. Yani kiufupi msingi wenu wa ndoa ulikuwa umeharibika maana mlianza vibaya na itakuchukua hatua nyingine kuujenga
Zaburi 11:3
Kama misingi ikiharibika,
Mwenye haki atafanya nini?
Mtaishi maisha ya kuwindana, kulaumiana sana. Kawaulize wote walioangukia Kona hii hata kama ni watumishi wa Madhabahuni, wengi wao wanalazimisha kuaminiana mdomoni ila Moyoni na Akilini wanashitukiana
ππ Kushuka kwa Heshima baina yenu wawili
Ukiona umevua au umevuliwa nguo kabla ya ndoa na huyo huyo mkaoana, Respect kati yenu inashuka chini ya nusu kwasababu Usiri wamiili yenu unabeba Heshima ya mioyo na utu wenu.
Mkisha vuana nguo Usitegemee, Baba mwenye nyumba kupata full respect,au mama kupendwa full love utakuwa na Partial.... Maana respect na love vilivuliwa moyoni mwako nje ya ndoa, hukuja navyo ndani ya ndoa.
ππ Kuna uwezekano mkubwa wa kuachana kimwili
kwanini hii hutokea?? Simply ni kwamba vitu muhimu vinavyo shikilia Ndoa hamkuingia navyo ndani mliviacha pale mlipovuana nguo ( Vitu kama, Usiri, Aibu, heshima, shahuku kwa mwenzako,) kwa hiyo mgogoro ukianza ndani Hauzimwi unatafuta Kuachana.
Huna haja ya kujiuliza sana yani fikilia tu kwamba mtu hamjaoana ila kila unachokita unakipata kwake yani unaweza kutimiza matakwa yako ya mwili (sex) hata unapotaka kumuoa huwezi kuwa na shauku kuu ya kumuhitaji maana wewe tayari kwake huna geni lolote.
Kilicho thamani huwa kinasitiriwa mpaka wakati ulio sahihi ufike ndugu yangu, please usijipotezee thamani mbele za Mungu na kwa mwenzi wako embu tunza utakatifu kwanza
ππ Fujo, magomvi Kunyimana tendo la ndoa haviwezi kukoma baina yenu.
(Maana moyo wa Upendo uliisha chukuliwa na adui) mtasuluhisha ila muafaka haupo,wanacho laumiana ni kidogo sana ila kinakuzwa na mbegu ya zinaa iliyofanyika. Mwaweza ishi ila si kwa Amani na upendo, mtakuwa na vipindi vifupi vya furaha na kipindi kirefu cha dhoruba.
HITIMISHO: KWA KIJANA AMBAYE BADO HAUJAOA AU BINTI AMBAYE HAUJAOLEWA USIKUBALI MTU AKAKUJUA MAPEMA KABLA YA NDOA KWA AJILI YA USALAMA WA MAISHA YAKO YA SASA NA YA BAADAYE NA KAMA ULISHAHARIBU KAZI BASI KUMBUKA KUINGIA KWA TOBA MBELE ZA MUNGU NA UWEZE KUSAIDIWA NAMNA YA KUWEZA KUTOKA HUKO
kuna watu wameshafika hatua wamepata addiction yani wanaona hawawezi kuishi bila kufanya tendo la Ndoa lakini nikuambie inawezekana na ukihitaji unaweza kutoka huko neema Ya Mungu imefunuliwa kwa ajili yako.
Ulikuwa nami mpendwa wako
Bro Jackobo
Phone: +255766944441 na +255621036471
Email:jackobombwaga@gmail.com
Ahsantee sana mtumishi MUNGU azidi kukuinua
ReplyDeleteshuklani sana
ReplyDelete