Utakuwa nami mpendwa katika kristo Yesu
Name: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com
Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu?? Ninakusalimu kwa jina la Yesu kristo aliye haiπππ
"Hata kesho ipo" imekuwa ni kauli ya kawaida sana kwa waamini katika kanisa siku za leo katika utendaji wa kazi ya Mungu pamoja na kuyaishi maisha matakatifu katika ukristo... karibu tuione jinsi hii kauli "hata kesho ipo" ilivyokuwa na matokeo yake ndani ya Muamini kwa habari ya UTENDAJI WA KAZI YA MUNGU pamoja na KUYAISHI MAISHA MATAKATIFU...
Mithali 27:1
"Usijisifu kwa ajili ya kesho;
Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja."
Biblia inajaribu kuweka wazi kwamba hautakiwi kufika hatua ukajisifia kuhusu kesho maana siku za mtu zimefungwa katika mamlaka ya Mungu na yeye ndiye anajua jambo gani litakuwepo na litatokea. Sio andiko hilo tu pia unaweza ukaona katika fungu lifuataloπππ
Yakobo 4:13-15
"Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka. Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi."
Usiitegemee faida ijayo hata siku moja nje ya kusudi, mpango na tumaini la Mungu maana yeye ajua yote yanayokuja. Embu tuone sasa ni kwa namna gani kanisa limeutumia huu usemi "Hata kesho ipo"
1. KUYAISHI MAISHA MATAKATIFU.
Mambo ya Walawi 11:45
"Kwa kuwa mimi ni BWANA niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu."
1 Petro 1:16
"kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu."
Ukiyasoma hayo mafungu mawili utaona mpango wa Mungu kwa mwamini ni kuyaishi maisha matakatifu siku zote na wakati wote.
Katika kanisa na kizazi cha leo sio kitu cha kushangaza mtu kumuona yuko kanisani lakini maisha anayoyaishi ni tofauti sana na neno la la Mungu kisa kwamba anajua hata kesho ipo na anaweza akatubu...
Mbona kujipalia moto wa adhabu mwenyewe kwa kuyadharau maneno ya Mungu?? Unafikiri YESU alipokuokoa alitazamie uishi maisha ya dhambi?? Kwanini unaingia kwa nyumba ya Mungu na Bado mambo unayoyafanya yanafanana na watu wa mataifa??
Watu mmefika kuitumia neema ya Mungu vibaya sana aise.. ni kweli kabisa Mungu anasamehe lakini kwanini uruhusu kufanya dhambi kwa sababu utatubu?? Kumbuka paulo alivyosemaππππ
Warumi 6:15
"Ni nini basi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali chini ya neema? Hasha!"
Paulo alifika wakati akaona kanisa la Rumi linaitumia vibaya neema ya Mungu kwa kuendelea kuishi katika dhambi kwasababu wanajua kuna nafasi ya kutubu. Ndivyo ilivyo kanisa la leo mana limekuwa linaitumia kauli "Hata kesho ipo" kuishi namna watakavyo maana watatubu eti..
Hasira ya Bwana iko juu yako wewe ambaye unafanya dhambi kwa makusudi ukisema utatubu, hivi wewe ushawahi kuelewa hili fungu???ππ
Mathayo 5:13
"Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu."
Hili andiko hapa juu linatuambia kwamba mwamini ni chumvi na ikiwa ameharibika hafai tena. Sasa ukikaa chini ukajiuliza vizuri utaelewa. Wewe umeokolewa ili uwafae wengine kwa ajili ya kazi yake na utumishi wake kwa hiyo ukishatambua hivyo lazima utunze kila kitu ambacho Mungu amekupa mwana wa Mungu. Jitahidi sana uishi utakatifu utakuwa na usalama. Usiwe na maisha ya sirini ya Michanganyo ili Mungu ajivunie wewe✍️✍️
Note: UTAKATIFU WA MTU unapimwa kwa maisha yako ya sirini na sio ambavyo unajionyesha kwa watu maana mtu wa kwanza kuyashuhudia maisha yako ya utakatifu ni wewe na Mungu pekee.
ACHA KUIFURAHIA DHAMBI UKISEMA UTATUBU KWA SIKU NYINGINE.ππ
Mithali 27:12
"Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha;
Bali wajinga huendelea mbele wakaumia."
Tafuta kuwa Miongoni mwa watu wenye busara ukayaache mabaya yako yote ya sirini na umtumikie Mungu kwa moyo mnyoofu.
2.UTENDAJI WA KAZI YA MUNGU.
Pia watumishi wa Mungu wengi wamefika hatua ya kuchukulia ni kitu cha kawaida kuamua kufanya kazi ya Mungu pale wanapopata nafasi.
Yakobo4:17
"Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi."
Biblia inakuambia ukiwa unajua kufanya mambo mema usiyafanye ni dhambi. Unajua kwamba wewe unatakiwa kumtumikia Mungu katika eneo fulani usifanye kwako ni dhambi.
Wapo waimbaji, walimu, wainjilisti n.k ambao wanaipuuzia sana nafasi ambayo Mungu amewapa ya utumishi na kufanya huduma wanavyojisikia wakijifariji na kusema kwamba watafanya hata siku nyingine kitu ambacho ni machukizo mbele za Mungu.
Yeremia 20:9
"Nami nikisema, Sitamtaja, wala sitasema tena kwa jina lake; basi, ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia."
Moja ya kitu ambacho nilijifunza hapa kwa nabii Yeremia ni hiki richa ya upinzani na ugumu ambao alikutana nao kwenye huduma yake alipojaribu kuacha ule wito ndani ulimpa kutokutulia sasa wewe Mungu kakupa huduma ya kufanya unawezaje kutulia ukasema nitafanya siku nyingine wakati unao muda wa kufanya. Hicho ni moja ya kipimo cha wewe kwamba umepungua kiroho na una hatihati ya kufa na kupotea katika msitari wa Mungu.
Zaburi 86:12
"Nitakusifu Wewe, Bwana, Mungu wangu,
Kwa moyo wangu wote,
Nitalitukuza jina lako milele."
Daudi alidhamiria toka ndani kumtumikia Mungu katika eneo la Sifa kwa moyo wake wote na sio nusu nusu kwamba leo kidogo na kesho itakuwepo nitafanya. Mungu anatamani umtumikie kana kwamba hautatumika tena. Pale unapopata nafasi jifunze kufanya kama hutafanya tena achana na mawazo ya kwamba kesho ipo.
Mungu akubariki kwa kuambatana nami katika hili somo fupi
Ulikuwa nami mpendwa katika kristo Yesu
Name: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com
No comments:
Post a Comment