KUJIKANA NDANI YA KRISTO


Bro Jackobo
Utakuwa nami mpendwa katika kristo yesu
Name: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email; jackobombwaga@gmail.com

Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu??

Karibu tujifunze kwa pamoja somo hili "kujikana ndani ya kristo Yesu"

Maana:
Kujikana katika kristo ni hali ya kuacha mambo yako yaliyokuwa na heshima, ufahari na kukupatia faida kwa ajili ya kufanya mapenzi ya  Mungu kristo/ Bwana wako.

Luka 9:23-24
"Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha."

Ukiangalia hapo Yesu alipokuwa akisema na wanafunzi wake alikuwa anawaandaa katika hali ya kumuishia Mungu katika mantiki ya kwamba wayahesabu mambo yao sio ya maana bali waone kwamba mambo ya Kristo Yesu ndio ya maana zaidi.

Hii ilimfanya ufike wakati sasa awaambie wajikatae/kujikana ili kwamba wamfuate Yesu na huku wamebeba mizigo/msalaba/mateso yao.

Hapa alikuwa akiwaonyesha kwamba katika kristo sio kwamba watapata kufurahi tu bali hata mateso yangewakuta.

Nani alikuwa mwanzilishi wa kujikana??
Note: Mwanzilishi mkuuu wa kujikana alikuwa ni Yesu mwenyewe kwa namna ambavyo aliacha Enzi na utukufu wake akaja kutuokoa sisi. Na aliona kwamba ile heshima na utukufu wa ki-Mungu sio kitu cha maana ila kukamilisha ule wito au kule kukubali kwake kujitoa kwa ajili ya maisha yetu hata ukafika hatua akawa yuko tayari kunyenyekea hata mauti ili aweze kutupata sisi ambao tulikuwa tumepotea.

Wafilipi 2:5-7
"Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;"

Pia Yesu aliweza kutuchagua sisi licha ya kwamba tulikuwa na dhambi ili kwamba atufanye sisi tuwe wana wa Pendo lake na sio sisi tuliomchagua yeye. Sasa huku kwa yeye kutuchagua kunaonyesha kujikana kwake mbele ya Mungu baba ambako pia ndio mfano tunatakiwa kuufuata.

Yohana 15:16
"Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni."

Katika kujitoa/kujikana kwa Yesu kristo ndiko ambako mwamini inatakiwa afuate mfano wake na sio mfano wa mwanadamu awaye yeyote. Hii ilimfanya mpaka atupe uhakika wa kuweza kufanya mambo ambayo ameyafanya na zaidi ya yale aliyokuwa ameyafanya. Ona hapa ambapo alituthibitishia ili kwamba tukiwa na hekima na maarifa ya Ki-Mungu tuweze kufuata njia yakeπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Yohana 14:12
"Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba."

MAENEO MUHIMU AMBAYO MWAMINI ANATAKIWA KUJIKANA NDANI YA KRISTO
1. Utumishi
2. Maisha ya utakatifu na utauwa.

1. UTUMISHI
hii ni hali ya kuwa na utayari wa ndani na kutekeleza majukumu/maagizo ambayo Bwana wako amekupa  ili uweze kuyatekeleza.

Wafilipi 3:7-8
"Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;"

Paulo kwa ajili ya kristo aliamua kupata hasara ili aweze kumpendeza kristo ambaye alimuita ili aweze kumtumikia yeye na huku ndiko kujikana ambapo Kristo alitamani wanafunzi wake wawe kama namna ambavyo paulo alikuwa tayari kuingia gharama. Paulo aliacha mshahara na marupurupu mbalimbali kutoka kwenye dini ya kiyahudi ili aweze kumpendeza Mungu.

Kuna wakati kama mwamini lazima ufike hatua uwe tayari kuacha yote ili uweze kuitimiza ile kazi ambayo Mungu amekupa wewe kuifanya kama vile ambavyo paulo alifanya.
Ndio maana Yesu alipokuwa anaondoka aliwaambia wanafunzi juu ya utumishi katika kuieneza injili yake na sio vinginevyo. Na alitamani wanafunzi wake wawe hivyo onaπŸ‘‡πŸ‘‡
Marko 16:15
"Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe."

Sasa wewe uliye tayari kuwa na Mungu lazima ukubari kuihubiri injili kwa mazingira yawayo yoyote ili kuonyesha utayari wako kumtumikia Mungu katika eneo ambalo amekupa uweze kutumika.

Usikubali kukaa tu ndani ya nyumba ya Mungu pasina kuwa na kazi yeyote lazima uwe tayari kuifanya ile huduma ambayo Mungu amekupa wewe.

Watu wamejikuta wanakumbana na vikwazo vingi sana vinavyowafanya washindi kujidhabihu vizuri katika eneo la utumishi. Tutaviangalia hivyo vizuizi kiufupi sana ambapo nimevuweka katika makundi makuu mawili.

VIKWAZO KWENYE UTUMISHI
A). Upinzani wa ndani ya nyumba ya Mungu/kanisa
B).  Upinzani wa nje ya nyumba ya Mungu/kanisa

A. UPINZANI WA NDANI YA NYUMBA YA MUNGU/KANISA
Hivi vizuizi vinakuwa vinatokana na mazingira ya ndani kwenye nyumba ya Mungu ambayo yanamfanya huyu mtumishi wa Mungu ashindwe kuishi ule utayari wake wa kumtumikia Mungu ambapo ndio kujikana halisi kwa mwamini.

Mathayo 16:21-23
"Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu."

Ukiangalia hapo juu utaona Yesu alikuwa akikemewa na petro kwamba hata pitia mateso lakini Yesu hakumsikiliza Petro bali aliangalia mbele ili kutimiza kusudi lake lililomleta.

Tulitegemea kwamba Petro asiwe kikwazo au kumvunja moyo Yesu kutimiza kusudi japo kwa akili ya kibinadamu ilikuwa ni ngumu sana kuelewa ule utumishi ambao ilitakiwa Yesu kuupitia. Hii ndio inatufanya hata nasi kama waamini lazima uelewe vizuri ni kwa namna gani Mungu amekuita ile uweze kumtumikia na kama usipoelewa ndio unajikuta sasa unaishia kuvunjwa moyo na watu wako wa karibu au ndani ya nyumba ya Mungu.

Unaweza ukavunjwa moyo na watumishi wa Mungu mfano Mwalimu, mchungaji, mzee n.k lakini usiache kufanya kazi ya Mungu. Wewe hakikisha unamtazama kristo tu kama kielelezo chako katika kumtumikia Yeye.

Kwa namna gani upinzani wa ndani unaweza kuwafanya waamini wakate tamaa??
1. Kuzuiliwa katika huduma na kiongozi wako wa kiroho; usiaangalie ni kwa namna gani kiongozi wako kakuambia au kukukataza kutumika kikubwa jihakikishe  uhusiano wako na Mungu halafu uendelee kumuomba Mungu ili akupe namna ya kutumika.
2. Maisha ya dhambi kwa viongozi wa kiroho wanaosimama mbele ya madhabahu; watu wengi wanaosimama mbele ya madhabahu wamekuwa wakiwavunja moyo watumishi wengine kutumika kwa kuwa na maisha mabovu sana. Japo usimfanye mwanadamu akawa ni kielelezo chako kwenye kumtumikia Mungu maana wanadamu watakukatisha tamaa lakini wewe mtazame Yesu na umfuate na sio vinginevyo.

B). UPINZANI WA NJE YA NYUMBA YA MUNGU/KANISA

Yohana 16:1-3
"Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa. Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi."

Yesu aliamua kuwaambia wanafunzi wake juu ya changamoto na upinzani watakao upata kutoka kwa watu wa dini ya kiyaudi ili kwamba wasihe vunjika moyo hata siku moja. Na aliwaambia hivyo maana alijua wapo watakao fanya kama kuwaua kabisa wakijua ya kwamba wanamtumikia Mungu lakini kiuhalisia hawako kumtumikia Mungu bali wanafanya kazi ya shetani.
Pale ambapo ukikutana na watu wanakupiga vita juu ya kumtumikia Mungu huko nje usije ukaacha kumtumikia Mungu hata siku moja wewe fanya kazi ya Mungu tu hata kama mazingira ni magumu sana.

Watu wamekuwa na urafiki usiokuwa na mipaka kiasi kwamba hawawezi tena hata kuwaambia watu wengine juu ya utumishi wao walio nao. Kwahiyo watu wako wa nje na nyumba ya Mungu lazima uishi nao kwa kwa akili sana ili usije ukapoteza lengo la kuishi.
Hakikisha maisha yako mwenyewe ni ushuhuda tosha kwa ajili ya kukurahisisha kuweza kuwahudumia wale walioko nje waujilie ule upendo wa Kristo Yesu.

2. MAISHA YA UTAKATIFU NA UTAUWA
Hili ni eneo la pili la muhimu ambalo mwamini inampasa kuishi katika namna ya kujikana kama kukubali ule wito aliotupa yesu katika "Luka9:23-24" 

Neno "utakatifu" na neno "utauwa" ni maneno ambayo yamekuwa yakitumika kama neno lenye maana moja lakini yana utofauti kidogo ila yanafika kuwa na shabaha moja.

Maana ya "Utakatifu"
Utakatifu ni "hali ya usafi wa kiroho, nafsi na kimwili". 

Asili ya neno "utakatifu"
Neno "utakatifu" linaweza kuelezewa kutoka kwa maneno mawili, neno la kiebrania na neno la kigiriki
✍️Neno "utakatifu" limetokana na neno la kiebrania "Qadash"  likiwa na maana "kujitenga au kutengwa kwa usafi"
✍️Neno  "utakatifu"  linaweza elezewa na neno la kigiriki "Hagios" likimaanisha "kutokuwa na makosa au udhaifu au uchafu"

Mungu anatamani watu wote waliokubali kumuishia waishi maisha ya utakatifu haijarishi mazingira yake yako magumu vipi hata kama pia yanamshawishi yeye kuingia katika dhambi ila kwa ajili ya Mungu anatuyaka kuwa na maisha ya utakatifu na sio kitu kingine chochote.

Mambo ya Walawi 19:2
"Nena na mkutano wote wa wana wa Israeli, uwaambie, Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wenu, ni mtakatifu." 

Mungu alimwambia Musa awakumbushe wana wa Israel kwamba inatakiwa waishi maisha ya utakatifu maana yeye ni mtakatifu ndio vivyo hivyo hata kwetu kwamba tukijikana kwa ajili ya kristo Yesu basi tutakuwa tayari kuyaishi maisha ya utakatifu siku zote maana Yesu mwenyewe ni mtakatifu na sisi inatakiwa tuwe hivyo maana Yeye katika kuishi kwake hakufanya dhambi. Ona hapo chiniπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
1 Petro 2:22
"Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake."
Kama yeye hakufanya dhambi basi nasi lazima tuufuate mfano wake ili tuwe tumejikana kikamilifu na kumfuata namna ambavyo alikuwa amesema tumuishie.

✍️✍️✍️Usije ukajiachia hata siku moja maana utakatifu huwa unatafutwa na sio suala la dakika moja bali linaitaji kujengwa kuanzia msingi wa wewe kumjua na kumuelewa Mungu.
Waebrania 12:14
"Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;"
✍️✍️✍️ Lazima ujizoeze kuuishi utakatifu siku zote hata kama unaona mazingira yanakuwa magumu kwako huko ndiko kutakufanya kujikana kikamilifu wakati wote.
✍️✍️✍️Pia lazima ufike hatua ujue ya kwamba utakatifu unahusisha mwili, nafsi pamoja na Roho. Sasa kama wewe uko tayari kwenda na Mungu lazima ujue kuishi utakatifu  katika maeneo yote hayo matatu.
1 Wathesalonike 5:23
"Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo."
✍️✍️✍️ Jifunze kuwa mtu wa kusoma neno na kulitafakari neno la Mungu, kuwa mtu wa maombi n.k ndipo utaweza kuyaishi maisha ya utakatifu. Unaweza soma vifungu hivi (Yoshua1:9, Mithali4:20)

Maana ya UTAUWA
Utauwa ni hali ya kujitoa ki-Mungu ambayo huambatana na kuongezeka kwa uchaji mbele za Mungu.

1 Timotheo 3:16
"Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, 
Akahubiriwa katika mataifa, 
Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu."

Ukisoma maandiko hapo juu unaona namna Paulo anavyomwaambia Timotheo kwamba utauwa una siri kubwa halafu anaanza kueleza namna ambavyo Yesu alijitoa na kufanya kazi ambapo inatujengea msingi mkuu katika kuelewa kwamba Utauwa unaambatana na kujitoa katika kristo Yesu.

1 Timotheo 6:5
"na majadiliano ya watu walioharibika akili zao, walioikosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida."
 
Katika kujitoa ndiko kunawafanya watu waweze kupata faida, sasa ukimuangalia Paulo anazungumza na Timotheo kwamba watu ambao hawako vizuri na Mungu wanahisi kwamba utauwa unawapa wengine faida sasa hii pia inatupa maana ya namna kuuelewa Utauwa.

Katika hayo yote Yesu pia alitamani tuweze tuongezeke katika kumcha Mungu kwa kujitoa kwetu siku zote za Maisha yetu tunapokuwa chini ya Jua hapa.

Kaa chini angalia ni kwa namna gani ambavyo umejikana kwa ajili ya kristo na uishi kwa namna gani ili uwe sahihi mbele za Mungu.

Ulikuwa nami mpendwa wako katika kristo
Name: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email; jackobombwaga@gmail.com

3 comments:

  1. Asante Brother kwa neno hili jema kwangu, na nimezidi kujifunza zaidi *UTAUWA* Mungu ni mwema sana na asante kwa kuwa umeanza kunionesha ukuu wa siri hiyo ya UTAUWA

    BE BLESSED IN JESUS NAME

    ReplyDelete
  2. Ubarikiwe sana mtumishi wa Mungu aliye hai hakika umenena iliyo kweli yenye kujenga uhusiano mzuri na Mungu....uzidishwe kiu zaidi ya kufundisha na kuonya ikiwezekana mahali pa kukemea kemea ili kuendelea kumkumbusha bibi arusi ambaye anangojewa katika arusi ya mwanakondoo....

    ReplyDelete
  3. Neno jema na la kujengeka kiroho, Barikiwa dogo.

    ReplyDelete

KUSIMAMA IMARA NDANI YA YESU KRISTO (sehemu ya Pili_Final)

Bro Jackobo Utakuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu Jina: Bro Jackobo Number: +255766944441 Email: jackobombwaga@gmail.com Blog website: ja...