Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu?? Karibu tumalizie sehemu ya tatu na ya mwisho ya somo Letu.
Utakuwa nami mpendwa katika Kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Phone: j255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com
Baada Ya kuona sehemu ya kwanza juu ya maana ya kwenda mpaka mwisho pamoja na Mungu na kuangalia kwanini watumishi wengi wamekuwa wakianza vema lakini wakiishia njiani.
Sasa tutaenda kuangalia mambo yanayoweza kufanyika kumsaidia huyu mwaminini kuweza kufika mwisho pamoja na Mungu.
Kama haujaona sehemu ya kwanza unaweza bonyeza hapa➡️SEHEMU YA KWANZA. Pia unaweza angalia sehemeya pili hapa➡️SEHEMU YA PILI
MAMBO YA KUFANYA ILI KUMUWEZESHA MTU KUWEZA KUFIKA MPAKA MWISHO PAMOJA NA MUNGU.
1⃣. KUMJUA MUNGU
Mwamini anapaswa kumjua Mungu kwa kila nyanja ya maisha mfano kiuchumi, kijamiii n.k ili apate kujua ule utendaji wa ki-Mungu namna ulivyo kwa kila sehemu ambayo atakuwa yupo.
Kiukweli kufika hatua ukasema unamjua Mungu ni ngumu maana hauwezi kumchunguza Mungu lakini inatakiwa ujibidishe umuelewe MUNGU na ndio maana Ayubu anazungumza kwamba inakupasa umjue Mungu ili uwe nayo Amani.
AYUBU 22:21
"Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia."
Kwahiyo kupitia kumjua Mungu itakuepusha na WOKOVU WA KIFAFA (yaani maisha ya kuanguka na kusimama) kwahiyo utakuwa ni mtu ambaye hauwezi kutikiswa na jambo lolote kwenye maisha yako ya kila siku kwahiyo utaweza kutembea na Mungu kwenye nyakati zote ambazo ziko kwenye maisha yako ya kila siku hata kama zinakupa huzuni.
Sasa ni kwa namna gani mtu anaweza akamjua Mungu??
a) Kuwa watu wa Kumfanyia Mungu Ibada
Unapozungumzia swala la ibada unaweza ukachukulia ni kitu cha kawaida lakini ili tuseme kwanza kunayo ibada lazima kuwe na vitu vikuu vitatu MTOA IBADA (mwanadamu), MTOLEWA IBADA (MUNGU) pamoja na MADHABAHU (Sehemu ya kumfanyia Mungu ibada ambayo huwa inaambatana pamoja na utoaji wa Sadaka na Dhabihu mbalimbali) unaweza ukasoma habari za ELIYA katika kitabu cha 1WAFALME 18 sura yote utaelewa.
Kwahiyo kutoa kwetu ibada kutatufanya tuachane na maisha ya kuanguka na kusimama kila siku bali yatatupa kukaa na Mungu mda wote ambao tutakuwa tu wazima.
WAEBRANIA 10:25
"wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia."
Kwahiyo kukusanyika kwetu katika ibada kila siku kutatusaidia sana kuweza kuelekezana mambo mbalimbali juu ya kweli ya Mungu na namna ya kuweza kuishi maisha ya utaua/ utakatifu. Kuna baadhi ya watu ambao huamini kwamba hata wasipokusanyika kwenye nyumba za ibada wako salama lakini kiuhalisia hawako salama hiyo ni kanuni ya kiMungu ambayo kaiweka mwenyewe sasa kwanini uachane na utaratibu wake??
Mungu atusaidie sana tuwe watu wa ibada. Lazima utafute kuwa na Ibada za pamoja lakini kama ukikosa pia kuwa na Ibada za binafsi ujue bado kuna vitu utavikosa sana kwenye maisha yako. Mungu akufungue sana kama unafanya ibada za pamoja tu na haufanyi ibada ya kwako binafsi uelewe umuhimu wake.
b) Kuwa watu wa Maombi
Maombi ni mawasiliano baina ya muhitaji na mtoa majawabu ya mahitaji. Kwahiyo Maombi ni mawasiliano kati ya mwanadamu (ambao hawa ndio wahitaji) pamoja na Mungu( mtoa majibu ambaye huyu huwa anajitosheleza).
Kwahiyo lazima tuwe waombaji ili tuwe karibu na Mungu na itatusaidia kwa kiwango kikubwa kutokata tamaa na safari yetu ya wokovu tuliyo nayo
LUKA 10:22
"Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni."
YESU alipokuwa anawaambia wasijewakiingia majaribuni sio kwamba alimaanisha wasingekutana na majaribu ila ni kwamba hawatayatii yale majaribu ya shetani kwenye maisha yao yani wakaenda kwa namna majaribu yanataka wawe.
1 WAKORINTHO 5:17.
"ombeni bila kukoma".
Kwahiyo inatupasa siku zote tuwe watu wa kutaka kuwa na Maombi na kumtafuta Mungu ndipo tutapata usalama lasivyo tunajipotezea nafasi mbele za Mungu
2⃣.KUONGEZA SHAUKU YA KIU YA HAKI
Shauku ni nia ya ndani ya kufanya jambo fulani kwa viwango vikubwa.
Endapo mwamini ataluwa anahitaji kwa kiwango kikubwa kuwa na haki mbele za Mungu itamfanya Mungu amjibu matamanio yake ambayo yuko nayo.. ona hapa πππ
Mathayo 5:6
"Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa."
Ukiangalia hapo Yesu alikuwa akizungumza na wanafunzi wake kwamba yeye ambaye akiwa na njaa na kiu ya haki yeye atashibishwa na Bwana, kwahiyo endapo kama ukiwa na shauku ya haki itakufanya ukawa unaishi maisha ya kumpendeza Mungu wakati mwingi maana wakati wote utakuwa ukitaka kumfanyia Mungu yale yanayompendeza na kujikuta unaishi maishi ya kuwa karibu na Mungu. Hii itakupa uwezo wa mda wote kuwa karibu na Mungu.
3⃣. KUENENDA KATIKA ROHO MTAKATIFU
Hii ni hali ya mwamini kuweza kuenda au kuishi kulingana na maelekezo ya Roho mtakatifu.
Maelekezo ya Roho mtakatifu huwa yanamfanya mwamini kuishi maisha ambayo yanamtukuza Munguππ
Wagalatia 5:16-17
"Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka."
Ukisoma hapo utaona paulo alivyokuwa akiwaambia wagalatia ambao walikuwa wameanza kwa Roho lakini baadae wakaanza kuishi kwa namna mwili unataka na sio kama Mungu alivyokuwa anataka maana matendo maovu yalikuwa sehemu yao.
Sasa mpendwa kama ukikubali kuwa chini ya maongozi ya Roho mtakatifu utaweza kabisa kuwa na nguvu za kuishi utakatifu mpaka pale utakuwa ukiondoka Duniani.
Kwanini sasa kama mwamini unatakiwa kuongozwa na Roho mtakatifu??
✍️ Kuongozwa na Roho mtakatifu utaweza kujulishwa mambo yale yaliyopo, yaliyopita na yanayokuja
✍️ Roho mtakatifu tukiongozwa naye ataondoa kwetu Roho ya mazoea maana yeye ndiye atakuwa anatuongoza
✍️Roho mtakatifu ni Mungu mwenye nguvu ya uwezesho katika nafsi ya tatu ya Mungu. Kwa hiyo bila yeye hata ujitahidi vipi huwezi kufanya lolote.
✍️Roho mtakatifu atakuwa anatufundisha namna ya kuishi kwa utakatifu wote
✍️ Kukubali kuongozwa na Roho ni sehemu mojawapo ya kuonyesha itiifu wako mbele za Mungu.
4⃣. KUICHUKIA DUNIA
Hii ni hali ya kukataa kuyaishi mambo ya kidunia ambayo yanakufarakanisha na Mungu. Kwenye sehemu ya pili kuna mambo tuliyaona ukiyafanya hayo anakuwa anaupenda ulimwengu. Sasa katika kuichukia Dunia lazima uyakatae hayo mambo makuu matatu
A. Kukataa tamaa ya macho
Lazima kama mwamini ajue namna ya kuushinda huo ubaya utokanao na macho lasivyo utakuwa unaishi lakini kiroho umekufa lazima macho yako yatiwe Nuru ya Kristo ili uweze kumpendeza Mungu wakati wote.
B. Kuishi nje ya tamaa ya mwili
Kama tulivyoona matendo dhahiri ya mwili yalivyo kwenye wagalatia sura ya tano. Sasa kama mwamini lazima ujue kuuweza mwili wako lasivyo utakuwa unajidanya hata kama unafanya huduma na kuhubiri kwenye maisha yako ya kila siku.πππ
1 Wathesalonike 4:3-5
"Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu."
Paulo anaandika kwa watu wa kanisa la Thesalonike kwamba wafanywe safi na waepukane na tamaa za mwili mfano uasherati. Pia paulo anawaambia watu wote waweza kuuweza mwili wao katika Utakatifu na heshima. Huku ndiko kutawafanya waepukana na tamaa za mwili. Hii itawafanya waishi na Mungu vizuri bila mawaa wakati wote mpaka kifo chake.
C. Lazima kuachana kiburi cha uzima ndipo pia utaweza kuwa na usalama mpaka unaiacha Dunia
MUNGU akubariki kwa kuwa pamoja nami sehemu hizi tatu za somo letu.
Lakini ngoja nikuongezee Swali moja niliulizwa na mtumishi wa Mungu yawezekana ukawa upo miongoni mwao ila unaogopa kuuliza.πππ
SWALI
A. Hivi Kama mtu ameshaanguka na kiukweli yuko hatua nyingi nyuma ya alivyokuwa mwanzo afanye nini?
B. Labda hata hawezi kuomba tena, hawezi kusoma Neno tena, hawezi kumsifu Mungu na kumuabudu Mungu tena katika Roho na kweli kama mwanzo, Hawezi hata kukemea Dhambi hata ile nguvu ya injili imeisha kabisa yani kiufupi amekata tamaa, Moyo wa toba umeisha afanyeje???.
JIBUππ
Ohhh ikiwa imemkuta nampa pole lakini bado tunalo tumaini katika kristo Yesu.....
Huyu mtu kwanza tatizo lake kuu liko katika "Ufahamu wa Pendo la kristo Yesu kwake" maana kama akielewa Upendo wa Kristo Yesu hawezi kufikia viwango vya kukata tamaa kiasi hicho.
Japo wengi wao ambao wanakumbwa na hali hiii wanakuwa walikuwa wamemshuhudia Mungu kwa viwango vikubwa kwenye maisha yao na baada hapo wanakuja kuanguka sasa hatia ya dhambi inakuwa inawatesa ndio maana wanafika hatua wanapoteza kila kitu yaani Shauku, nguvu ya kuomba na kila kitu.
Sasa haya ni baadhi ya mambo ambayo anatakiwa kuyafanya huyu mtu wa namna hiiiπππ
1. Jambo la kwanza kabisa auelewe Upendo wa Mungu
Upendo wa Mungu unajidhihirisha kwa namna tofautitofauti kwa mwamini yeyote. Sasa inabidi huyu mtu apate uelewa juu ya namna ambavyo Mungu anampenda ili kuweza kumpa mtu uwezo wa kusonga mbele .
Watu wengi wanapotea kabisa kwasababu ya mafundishoππ
Hosea 4:6a
"Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;"
Hapo unaona mtu akikosa uelewa tu ni rahis sana akafungwa ufahamu na adui kiasi kwamba akajikuta hawezi kusonga mbele zaidi hata hatua moja.
Kwenye pendo la Mungu akielewa haya yanaweza kumsaidiaππ
➡️ Mungu ametupenda sisi tukiwa na dhambi na sio kwa matendo yetu mema.
Yohana 3:16
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Mungu kitendo cha kumtuma mwanawe haikuwa kwasababu tulikuwa watakatifu bali wenye dhambi ili tupate uzima sasa ukifika hatua ukajua ulipendwa angali una dhambi basi hutakwama kuendelea mbele zaidi hata kidogo.
Warumi 3:23-24
"kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;"
Hili fungu nililielezea. Ukishajua ya kwamba watu wanakosea ila kupitia kristo yesu tunahesabiwa haki ko kazi yake sio kujikinai mwenyewe bali ajishushe kwa Yesu pekee.
➡️ Mungu anasamehe dhambi zote na alikuja kwa ajili ya hilo
Isaya 1:18
"Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu"
Hapo anaonyesha ukifanya dhambi ya namna gani bado Mungu anaweza akakusamehe haijarishi umefanya kosa gani.
1 Petro 2:24
Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.
Pia hapo juu unaona kwamba yeye ndiye aliyechukua dhambi zetu so ukiwa umekosea lazima uende kwake tu na ndio maana alisema kwambaππ
Mathayo 11:28
"Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha".
Ukisoma hapo Mungu anataka watu wamuendee na mizigo yani dhambi zao yeye ndiye atawapumnzisha na sio waache dhambi zao ndio wamfuate bali ukiwa na makosa umuendee yeye akupe haki.
Sasa kuna namna nyingi upendo wa Mungu unajidhihirisha kwa mtu ambako huko kuna mfanya mtu akikosea aweze kurudi kwake na kusamehewa.
Kwanini nimeelezea hiki kipengeleπ€π€ ni kwasababu watu wanafundishwa mafundisho yanayowafanya wajihisi kuwa na hatia wakati wote na sio upendo wa Mungu kwa kanisa kinachowafanya wengi sasa wakikosea kukumbana na hizi haliππ
✍️✍️Asione haja ya kwenda kwa ibada maana akienda anakuwa anahisi hatia tu ndani
✍️✍️ Anakosa ujasiri wa kuomba. Japo ukifanya dhambi usipoitu ia lazima ikutee hii hali
✍️✍️ Hawezi tena kusema Habari za Mungu kwa ujasiri.
N.k
Na hii ndio sababu nimekuelekeza kwamba lazima apate uelewa vizuri wa upendo wa Mungu kwenye maisha yake. Ndio hatua yake ya kwanza kuweza kutoka maana bila hapo atakuwa mtumwa tu kwenye fikira zake.
Note: kuelewa kwamba Mungu anakupenda usije ukatenda dhambi kwasababu atakusamehe hata utakapokosea
2. UKISHAJUA UPENDO WA MUNGU HAYA MAMBO YANAWEZA KUKUSAIDIA SASA KUTOKA HAPO
A. Kuweka peupe kosa lililokufanya ukaanguka
Hapa inatakiwa mtu huyu amuelekeze kiongozi wake wa kiroho juu ya jambo hili alilolifanya lengo ni kulifanya lisiwe na nguvu ya hatia ndani yake.
Kufanya hivyo unakuwa unaiaibisha dhambi hiyo kwenye maisha yako na hapo sio kwamba unakuwa unaenda kutubu kwa mchungaji wako bali unakuwa unauaibisha ubaya ulioufanya hii itakupa ujasiri wa kuendelea kumtafuta Mungu. Lazima ulikiri kosa lako peupe.
B. Kuwa na watu watakaokufanya uendelee mbele zaidi
Lazima utafute mtu/watu ambaye anaweza kushirikiana naye katika maswala ya kiroho ili pale unakosa nguvu akutie joto la kuendelea mbeleππ
Mhubiri 4:9-11
"Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao. Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua! Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?"
C. Tafuta kwanza kuwa kwenye maombi ya ushirika sana kuliko wewe mwenyewe binafsi
D. Kumtaka bwana na Nguvu zake
yaani kuongeza shauku ya kuwa na nguvu za Roho mtakatifu maaana shauku ya kuabudu ni suala ambalo linakuja kulingana na ufahamu na hiyo nguvu ya Roho mtakatifu ndiyo itampa bubujiko na shauku kuu ndani ya ibadaππ
E. Lazima abadilishe vitu anavyoviangalia mara kwa mara ndipo ataweza kutoka huko.
Mfano mwingine unakuta mda wote anasikiliza nyimbo za bongo fleva, picha za ngono, na kufanya mambo mengi yafananayo na hayo huku anataka shauku ya ibada iongezeke kiasi kwamba anakuwa anajidanganya tu.
Hiyo inaweza kumsaidia huyo mtu kama atakuwa yuko tayari kutoka hapo alipo. Hatua ya kwanza siku zote ni kujua kwamba hauko sehemu sahihi na ukishajua ndipo unaweza kupiga hatua nyingine mbele. Zaidi itakayokufanya ufanye maamuzi sahihi.
Yuko kwenye wakati mzuri wa kuweza kutoka huko maana ameshatambua ya kwamba huko aliko sio salama na ndio maaana anataka aweze kutoka huko.
Mungu akubariki mtumishi kwa kuwa namimi tangu tumeanza mpaka hapa tulipofikia. Kulikuwa na mambo mengi ya kuweza kujadiliana lakini kwa sababu ya Muda nafikiri tuishie hapa. Ukiwa na swali maoni unaweza kuyaweka chini au kwa njia za mawasiliano hizo hapo.
Ulikuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Name: Bro Jackobo
Phone; +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com