Utakuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
+255766944441
jackobombwaga@gmail.com
Vipengele muhimu vya somo vitakuwa kama ifuatavyo
1. Utangulizi wa Somo
2. Maana ya wokovu katika mitazamo mbalimbali namna biblia imeeleza
3. Mambo ya msingi katika kupata wokovu
4. Kujibu dhana ya mwanadamu kuweza kuokoka akiwa bado yupo Duniani na sio baada ya kufa
5. Kweli kuu juu ya uhusiano wa matendo na wokovu
6. Mambo yanayo imarisha wokovu
7. Mambo yanayo dhohofisha wokovu
1. UTANGULIZI
Ashukuriwe Mungu ambaye siku zote anatufanyia mambo mengi kwenye maisha hata kama hatukusitahili ila anatustahilisha kuwa nayo na kuwa na uhalali kamili wa kuyamiliki hayo.
Mungu alipo muumba mwanadamu alimuweka bustani ya edeni kwa kupenda mwenyewe lakini hakuacha mwanadamu aweze kukaa peke yake bali alimpa na kampa aitunze kitu ambacho kinatupa ufunguo kwamba lolote Mungu anakupa kuna sehemu ya wewe kufanya hata kama umepewa bure.
Mwanzo 2:15
"BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza."
Pia ukiangalia hata maisha na uhai wetu Mungu ametupa hatuna sehemu ya kujiongezea uhai wetu ila Mungu ametupa maarifa ya namna nzuri ya kuhakikisha tunatunza afya zetu ndio maana kawapa wengine neema ya kuwa madakitari, wauguzi, wataalamu wa maabara n.k ili kuhakikisha kwamba afya zetu zinakuwa imara. Pia katoa baadhi ya mambo mtu anaweza akafanya ili asijikute afya yake ikawa inatahayarika mfano kufanya mazoezi, kula mlo kamili n.k. lakini mambo yote haya lazima yafanyike huku Mungu anakuongoza na kukutangulia maana kwa akili zako wewe huwezi ndio maana maandiko yanasema..
Zaburi 127:1
"BWANA asipoijenga nyumba waijengao wafanya kazi bure Bwana asipoulinda mji yeye aulindaye akesha bure"
Pia ukisoma hapa
Yuda 1:3
"Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu."
Ukisoma andiko la hapo Juu utaona Yuda alivyoandika waraka wake maana aliona kwamba wamepewa wokovu bure lakini haina maana kwamba ndio wakae hivi hivi akaamua kuwaandikia waweze kuelewa kwamba imewapasa kuishindania imani maana hata wokovu ni Tendo linalo kuja kwa imani. Pia aliandika hivyo kwasababu alijua kuwa kuna mafundisho mabaya ya kuwaharibu kama hawatasimama imara kuishindania imani. Kwahiyo hapo anatuonyesha umuhimu wa kutunza kile ambacho umepewa na Mungu.
Nimeandika haya yote kwasababu kuna watu wanao amini ya kwamba mtu akisha kuokoka hana jambo la kufanya kwakuwa Yesu kristo amekwisha kumaliza yote wanasahau kwamba Mungu anasema hivi..
Mathayo 11:28-30
"[28]Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. [29]Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; [30]kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi."
Yesu anaeleza kuwatua watu mizigo (Kuondoa tabia zisizostahiki kwa kumpa uwezo wa kuacha), tena anatoa wito wa mtu kwa utayari wake kujifunza kwake mwenyewe na sio kumlazimisha mtu (Hapa inaonyesha wazi kuna jambo la mwitikio kwa mwamini juu ya mambo ambayo Mungu anataka kukupea wewe kama mwamini, tena anamaliza kwamba kuna kazi ya kuubeba mzigo wake ulio mwepesi(Hapa anaonyesha tabia za haki ambazo mwamini anatakiwa kuwa nazo ambazo zinabaki katika uwezo wa mwanadamu yeye mwenyewe kuamua kumfuata au kuishi wema pasipo kulazimishwa). Kwahiyo Mungu anapofanya kwako kuna sehemu ya wewe kulinda kile Mungu amekupa.
2. MAANA YA WOKOVU KATIKA NAMNA MBALIMBALI AMBAZO BILBLIA IMEELEZEA.
Kumekuwa na dhana na Imani ambazo haziamini kwamba kuna kuokoka hapa Duniani zikiamini hakuna mwanadamu anaweza kuokoka akiwa Yupo hapa Duniani mpaka atakapokufa lakini katika msingi wa maandiko haijakaa sawa kwasababu biblia inaeleza wazi kwamba kuna uwezekano wa mtu kuokoka hata anapokuwa hapa Duniani.
Naomba tuangalie maana mbalimbali zenye mlengo mmoja katika kuelezea wokovu ni nini.
- WOKOVU ni mpango wa Mungu kumtafuta mwanadamu ili kumrejesha huyu mwanadamu katika sehemu ambayo alikuwa amemuweka aweze kukaa katika asili yake.
Mwanzo 2:7-8
"[7]BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. [8]BWANA Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya."
Mungu alituumba tuweze kukaa bustani ya Edeni ambapo kulikuwa hakuna magonjwa wala tabu za aina yeyote yaani ilikuwa ni sehemu ya amani ya kujitosheleza. Sasa baada ya anguko la mwanadamu Mungu alimuondoa mahali pale kwakuwa tayari alikuwa ashaleta tabia ambazo hazikupaswa kuwepo pale.
Sasa Mungu alianza kumtafuta mwanadamu tangu pale alipoanguka ili amrejeshee utakatifu aliokuwa ameupoteza ns ndio maana huu mpango ulianza kwa kusurubisha Dhambi yaani kiufupi palipo na na dhambi kuna adhabu itokanayo na hiyo dhambi. Sasa Mungu kwa kumpenda mwanadamu ili amuokoe na ile adhabu aliamua kumuua mnyama ili ampe mwanadamu sitara yake kwakuwa alikuwa alishapoteza utukufu wa Mungu.
Mwanzo 3:21
["21]BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.
Hapa Mungu alifanya ili kumpa mwanadamu heshima kwasababu ya Upendo wake ambapo ni utabiri wa wokovu kwa mwanadamu na ndio maana aliwavisha mavazi ya ngozi ikiwa na maana kwamba kuna mnyama alikufa ili Adamu na Eva wapate sitara.
Waefeso 2:10 (KJV) Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
Mungu alimuumba mwanadamu aweze kuishi maisha yaliyo jaa matendo mema ambapo hapo Mungu alipomuweka Adamu Edeni alikuwa amemuelekeza kuishi maisha yaliyo mema peke yakena sio vinginevyo. Sasa huu mpango wa kumuokoa unamfanya mtu aweze kurudi katika lile kusudi la Mungu la asili kuishi katika matendo mema peke yake.
Sasa uwezo wa kuishi matendo mema ulipotea pale mwanadamu alipokosea pale edeni
Mwanzo 2:16-17 (KJV) Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,
walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Sasa ukiona hilo neno hakika utakufa ndio hilo linaonyesha kuvunjika kwa ushirika uliojaa uwezesho wa kuweza kufanya mapenzi ya Mungu ndio maana sasa Mungu alimtuma sasa Yesu kristo ili aweze kuturudishia huo uwezo wa kuweza kuishi tukiwa tuko hai yani tukiwa tunafanya mapenzi ya Mungu.
- Wokovu ni hali ya kuwekwa mbali na hatia na adhabu itokanayo na makosa ambayo mwanadamu ameyafanya na kupewa haki kwa kumuamini Yesu kristo.
Warumi 3:23-25 (KJV) kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;
ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake,ili aonyeshe haki yake ,kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilzotangulia kufanywa.
Ukiangalia andiko hapo juu linaonyesha kiuhalisia mwanadamu hana haki mbele za Mungu maana kafanya dhambi ila haiishii hapo inakuja kutoa maelekezo kwamba kuna kuhesabiwa haki kupitia kuamini ukombozi wake unaopatikana kupitia Yesu kristo maana yeye anatukomboa kutoka kwa shetani kwa kutupatanisha na Mungu kupitia Damu yake mwenyewe iliyo mwagika pale msalabani. Sasa pale ambapo wewe unapo kuja kuamini kazi ya msalaba ndipo sasa unakuwa una haki mbele zake ndio maana ukisoma hapa...
Warumi 10:9-10 (KJV) Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
Kwahiyo unaona kazI ya mwanadamu ni kumkiri Yesu, kumuamini Yesu ndipo anapata kuokolewa na hapo ndipo ambapo sasa moyo (Sub-Concious mind) huamini kiukweli kulinganisha na taarifa ambayo huyu mwanadamu anapaswa kuwa nayo kwanza na kukiri kwa kinywa chake na kuupata wokovu.
Warumi 8:1-2 (KJV) Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.
Ukisoma hapo pia juu unaona kwamba mtu aliye ndani ya kristo hakuna hukumu ya aina yeyote anayoweza kuipata maana yeye anaye Roho mtakatifu ambaye huyo humuweka na kumpa nguvu ya kuishi nje ya dhambi. Kwahiyo ile hukumu ilipaswa kupatikana kupitia dhambi Yesu aliishaiondoa na kutufunza sisi sasa kumuishia Yeye kwenye maisha Yetu ya kila Siku.
- Wokovu ni kipawa cha Mungu ambacho kimefunuliwa kwa mwamini na kumpa uwezo wa kuishi mbali na dhambi
Waefeso 2:8 (KJV) Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
Sasa huu wokovu ni zawadi ambayo Mungu amempatia mwanadamu ambayo yeye mwanadamu hana namna yeyote ya kufanya ili apate bali Mungu mwenyewe ndiye ameachilia kwa mwanadamu kwa kupenda kwake yeye mwenyewe.
Sasa hiki kipawa ndicho ambacho humpa mwamini kuweza kuishi sasa nje ya dhambi na ndio maana hakuna mtu anaweza sema nimeokoka akawa bado katika matendo yasiyo katika njia ya Mungu maana katika kufunuliwa kwa kipawa hiki ndiko ambako sasa kunaleta uwezo wa kuyaishi mapenzi ya Mungu maana hiki kipawa kinapofunuliwa kina mpa mwanadamu shule au Elimu ya namna ya kuishi akiwa yuko hapa Duniani.
Tito 2:11-12 (KJV) Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;
Kwahiyo unapopewa wokovu ni kwamba umepewa uwezo wa kuishinda dhambi kiufupi.
Hitimisho: Kutokana na maana hizo hapo juu tumejifunza tunaweza kueleza kiufupi kwamba WOKOVU ni usalama ambao mwanadamu anakuwa anaupata pindi anapokuwa ameshamkubali, kumuamini na kuamua kufuatana naye kwenye maisha yake huyu mtu anakuwa amekwisha kuokoka na kuwa na haki zote za urithi kwakuwa mwana wa Mungu kwelikweli. Hii inaonyesha hapa
Yohana 1:12 (KJV) Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
Mungu akubariki kwa kufuatana na mimi kwa sehemu hiii ya kwanza ambapo ni kama msingi unaotupa kuelewa vizuri tunako elekea. Niombe basi ufuatilie sehemu ya pili itakuwa na package nyingine inayoendelea. Nkngeweza kuendelea lakini ukiweka mambo mengi sana wengine hawawezi kusoma ndio maana nimejaribu kuligawa somo hili.
Lakini kama hujaokoka na unatamani kuingia kwenye ushirika huu wa Kuwa na Yesu kristo kristo kwenye maisha yako unaweza kuwasiliana nami kupitia mawasiliano hapo chini.
Ulikuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
+255766944441
jackobombwaga@gmail.com
Mtumishi hongera sana Kwa kazi nzuri, hakika nimejifunza kitu kipya. Keep it up servant of God
ReplyDeleteBe blessed
ReplyDeleteUbarikiwe mzee, napata kujifunza, Bwana azidi kukufunulia mengi zaidi yazidi kutufaa
ReplyDeleteUbarikiwe mtumishi wa Mungu kwa huduma,nimejifunza kitu Mungu azidi kukutumua zaidi na zaidi
ReplyDeleteBarikiwa sana pastor Jacob
ReplyDeleteGlory to Jesus......
ReplyDeleteMtumishi wa Bwana, Mungu akupe neema zaidi maana u baraka kwetu, kimsingi kwangu kupitia neema hii katika neno la Mungu katika Kristo Yesu
Amen....
Amen
DeleteUbarikiwe sana mtumishi wa mungu kiukweli kuna kitu nimejifunza ko mungu aendelee kukuonyesha ili tuweze kujifunza zaidi
ReplyDeleteUbarikiwe sana Bro Jackobo🙏
ReplyDeletePOWERFUL 🙌🏾 For God's Glory
ReplyDelete