ROHO MTAKATIFU NDANI YA MWAMINI


Bro Jackobo {JAM295}


Nini maana ya kujazwa Roho mtakatifu?

Kabla sijaendelea naomba nianze na utangulizi kidogo juu ya Roho  mtakatifu kabla sijaeleza kujazwa Roho mtakatifu ni nini

ROHOMTAKATIFU NI NANI??? 
NOTE. Kwanza jua ya kwamba huwezi kumtenganisha ROHO MTAKATIFU pekee yake akawa anajitosheleza palipo yeye lazima hata mwana na Baba wote wapo na hapa si watatu bali ni mmoja 

1.ROHO MTAKATIFU NI MUNGU Hizi ni sifa zake zinazoonyesha uungu wake
✓Anajua yote
1 Wakorintho 2:14
"Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni."

✓Yupo mahali pote
Zaburi 139:7-9
"Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko. Ningezitwaa mbawa za asubuhi, 
Na kukaa pande za mwisho za bahari;"

✓Ana nguvu zote
 Matendo ya Mitume 1:8
"Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi."

Ni wa milele yote
Waebrania 9:14
"basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?"

✓Ana uwezo wa kufufua 
Warumi 8:11
"Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu."

2.ROHO MTAKATIFUNI NAFSI YA TATU YA MUNGU 
sifa zake kama nafsi 
Roho mtakatifu anasema
 MDO10:19-20 
Roho mtakatifu anakataza
 Matendo ya Mitume 16:6-7
"Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa"

Kwanini tujawe na Roho mtakatifu?

kujawa Roho mtakatifu ni kukipokea kipawa cha Mungu alichokiahidi{Matendo 1:8} 

Huu ujazo wa Roho mtakatifu huwa unadhihirika kwa ishara ya kunena kwa Lugha na mambo mengne mengi yaliyo elezwa katika utendaji wa kazi ya Mungu  pamoja na mwamini

Matendo ya Mitume 2:1-4
"Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka."

Kujazwa ROHOMTAKATIFU sio swala la siku moja ni la kila siku kwa kila Mwamini. 

Note: kuna uwezekano mkubwa mtu akawa ameokoka lakini bado hajajazwa ROHOMTAKATIFU bali anaye ROHOMTAKATIFU 

tofauti kati ya mtu aliyejazwa na ambaye ana Roho Mtakatifu iko hapaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡ 

1️⃣Mtu aliyejazwa anaye ROHO MTAKATIFU pamoja na nguvu za Mungu na huyu mtu anaweza kusimama kama mwakilishi wa MUNGU {Matendo 1:8}  wakati aliye na Roho mtakatifu pekee hana ile nguvu na hawezi kuwa mwakilishi wa Mungu vizuri na hata kama akiwa mwakilishi atakuwa mtu wa kuanguka na kusima siku zote. Hii ina maana kwambaπŸ‘‡πŸ‘‡
Huyo aliyejazwa Roho mtakatifu anaweza akasimama akawashahidi wa MUNGU lakini huyu aliye na Roho wa Mungu lakini hajajaa hawezi akasimama kama shahidi maana hataweza kusimama kwa ujasiri kueleza siri za MUNGU na huyu yuko hatiani sana kuanguka wakati wowote

Kumbuka petro kabla hajajazwa Roho mtakatifu alimkana yesu lakini baada yakujaa alieleza siri za MUNGU kwa ujasiri Mbele ya kadamnasi bila woga Soma {Matendo 2:14-42} 

2️⃣Pia mtu ambaye amejazwa Roho mtakatifu huwa anashuhudiwa ndani yake kwamba yeye ni mwana wa Mungu na Mungu anafanya kazi pamoja naye lakini mtu ambaye hajajazwa huwa hana wa kumshuhudia pia ni ngumu kujitambua nafasi yake vizuri kama kweli kaokoka au bado na ndio maana anakuwa mtu wa kuanguka ovyoovyo.

Warumi 8:16-17
"Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye."


KWANINI KUJAZWA ROHO MTAKATIFU NI MUHIMU KWA MWAMINI

Note: Kila aliye mwami Yesu ni lazima ajazwe na ROHO MTAKATIFU 

Kujazwa na Roho mtakatifu ni agizo la Yesu kwa wafuasi wake
MDO1:2-4; YOH15:16 

✓Ahadi yetu kutoka kwa baba
LUKA24:49; MDO2:38-39 

kwasababu ya wajibu/majukumu tuliopewa na Baba
tumepewa wajibu/Majukumu  muhim sana kama yafuatayo 
Kujengana ndani ya kanisa, kumwabudu Mungu yoh 4:23-24, math15:8
•kuufikiaulimwengu Rumi8:1 

Mpendwa katika Kristo Yesu imekupasa kupokea nguvu ya Roho mtakatifu ili kuwa na usalama wa safari yako ya mbinguni. 

Kwa hiyo ni lazima ujae na kunena kwa Lugha mpya, kuweka mikono juu ya wagonjwa waka pata afya japo hiyo sio tiketi ya kwamba umejawa na yeye maana yeye huwa anajisimamia mwenyewe katika utendaji wa kaziyake kwahiyo lazima uhakikishwe na yeye mwenyewe kwamba wewe ni wake kabisa.

 NJIA ZA KUJILIWA/KUJAZWA NA ROHO MTAKATIFU 

✓ Kusikia neno laMUNGU MDO10:44-46 
✓ Kusifu na kabudu katika utakatifu 
LUKA24:50-53 MDO16:24 
✓ Kumuomba MUNGU juu ya ujazowa NGUVUzake LUKA11:13 
✓ Kuwekewa mikono na watumishi wa Mungu
MDO 8:14-17 MDO 19:6-7 

SIFAZAMTU MWENYEKUJILIWA NA ROHOMTAKATIFU 

1.lazima awe AMEOKOKA
MDO2:37-39 MATH5:8 
2.Lazima huyuMTU awe na kiu ya Kumpokea ROHO MTAKATIFU yoh7:37-39 MATH5:6 
3.Lazima awe na imani ya kumpokea Roho wa Mungu EBR11:6 

MATOKEOYA KUJILIWANAROHO MTAKATIFU 
1.Kunena kwa LUGHA MPYA MDO2:4 
2.kupoke nguvu Za Mungu MDO 1:8 na mengine mengisana 

Ulikuwa nami mpendwa katika kristo Yesu 
Bro Jackobo
jackobombwag@gmai.com 
jackobombwaga.blogspot.com
+255766944441 +255621036471 

JE UNAYO NAFASI YA KRISTO YESU NDANI YA MOYO WAKO?


Bro Jackobo

Utakuwa namimi mpendwa wako katika kristo Yesu

Name:Bro Jackobo email: jackobombwaga@gmail.com 
Phone; +255766944441

Bwana Yesu apewe sifa Wana wa Mungu? napenda tushirikiane jambo hili kidogo

Kanisa la Leo limekuwa ni waaminifu sana kuhudhuria Ibada na vikundi mbalimbali vilivyo ndani ya kanisa lakini nafasi ya Yesu ndani ya maisha yao imekuwa ni shida sana tena sana mpaka inaleta huruma kuona watu hawana msimamo kamili wa Ki-Mungu ila wanaishi kimazoea tu kama walivyoishi Jana.

Ndipo nakumbuka kuna wakati Yesu aliwahi kuzungumza neno lifuatalo

 MATHAYO 15:8-9
 "Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami Nao waniabudu bure Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu."

Wakuu wa dini walikuwa wakiishi kwa  mapokeo lakini waliacha msingi wa kweli wa kumfanyia Mungu Ibada ya kweli kwahiyo katika vinywa vyao walikuwa wakitamka kumpenda Mungu lakini kiuhalisi hawakuwa na Mungu ndani yao na hili ndilo kanisa ambalo tuko nalo kizazi cha leo watu wanaeleza wema wa Mungu lakini hawawahi kupata Raha iliyoko ndani ya kristo. Ni kawaida Ukaona mtu anafundisha Ubatizo wa Roho mtakatifu lakini hajawahi kushuhudia Radha ya Roho mtakatifu hata siku moja..

Nampenda sana paulo maana alitamani kanisa liishi kwa mfano pia hata wake. Embu ona hayo mafunguπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 1 WAKORINTHO 11:1
 "Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo."

 WAFILIPI 3:17
 "Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi."

Mafungu yote hapo juu yanaonyesha namna paulo alivyojiweka kipaumbele mwenyewe ili kwamba watu waige mfano wao lakini kanisa la leo halina watu wanao weza kunena kwa ujasiri kwamba mnifuate mimi kama nilivyo mfuata kristo Yesu kwasababu maisha yao hayana ushuhuda hata kidogo maana wamejichanganya kupita kiasi tena kiasi. Mungu akukumbuke ndugu yangu badilika.

 LUKA9:57
"Yesu akamwambia, Mbweha wana pango,na ndege wa angani wanaviota, lakini Mwana wa Adamu hana pa kujilaza kichwa chake."

Ukianza kusoma mistari ya nyuma utaona huyu mtu alitaka kumfuata lakini Yesu anakuja kumpa majibu magumu sana yule mtu kwamba hana nafasi ya kuweza kukaa kwake. 

Yule mtu alikuwa na nia yakumfuata kristo lakini ndani yake alikuwa hajampa kristo nafasi hata kidogo maana Imani bila matendo imekufa πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 YAKOBO 2:17
 "Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake."

Wengi wetu tuna nia ya kumfuata kristo lakini hatujaambatanisha nia zetu pamoja na matendo yetu. Na ndio maana biblia inasisitiza kujikana mwenyewe lasivyo utakuwa unaingia kwenye nyumba ya Mungu lakini hutakuwa una nafasi ya Yesu kristo.

 MATHAYO 16:24 
 "Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate." 

Nikuulize swali na wewe je umempa nafasi gani kristo Yesu kwenye maisha yako?
 
Au umekuwa na wewe unaingia kwenye nyumba ya Mungu huku umemuweka mbali sana Yesu kristo?  

Au umekuwa ni mtu unaye mfuata Yesu wakati wa kustarehe na ukifika wakati wa magumu ulekuwa ukimuacha?
πŸ‘‰lazima uwe mtu wa kuvumilia kutenda mema siku zote ndipo utapata nafasi ya kuurithi ufalme wa MUNGU lasivyo unajidanganya.

 MATHAYO 24:13 
"Lakinimwenye kuvumiliahata mwisho, ndiyeatakayeokoka."

Mwisho wa safari yako ya hapa duniani ndiyo taswira kamili ya kile unachotakiwa kukipata baada ya yote hayo maana baada ya kifo ni hukumu.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 WAEBRANIA 9:27
 "Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;"

Kuna mafundisho yapo ambayo yanawaambia watu kwamba eti mtu anaweza kuombewa baada ya kufa akaenda peponi hayo ni mafundisho potofu yenye lengo la kuwafanya watu wasiogope kufanya dhambi wakiamini wataombewa na Mungu atawasamehe {wajidanganya bure} basi haikuwa na maana ya kuwaambia watu waishi maisha ya kumfuata Yesu na pia kwamba Ajikane mwenyewe basi Yesu angeseme mtu asiponifuata na ndugu zake watamuolbea akifa aende kwenye haki. Kwahiyo ukifa ni hukumu tu hakuna cha nafasi tena ya toba yani matendo yako yataambatana nawe.

Nikuambie tu ukweli kwamba kama umebadili mwili wako na moyo wako kuwa sehemuya uovu jua hukumu inakungoja haijarishi unaingia kanisani au hauingii

 MATHAYO 21;12
 "Yesu akaingiandani yahekalu,akawafukuzawote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni,akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwawakiuza njiwa"

kristo hataki michanganyo hata siku moja ndio maana alipoona wamegeuza sehemu ya ibada kuwa kama gulio ilimkasirisha sana YESU. ndivyo vivyohivyo anavyochukia pale unapoacha njia ya MUNGU na kufanya Mambo unayoyataka yaliyo tofauti na neno lake. 
Tambua ya kwamba wewe ni hekalu tena u sehemu ya ibada ya MUNGU ndani ya moyo wako. 
maana siku ile Mwana wa Mungu atakapokuwa kwenye kiti cha enzi atawabagua kama Mbuzi na kondoo kwa kadri ya mtu na matendo yake. (soma Mathayo 25:31-46)

usikae kwa hasara Mahali ulipo maana hukumu inakuja wala usije kuwa una mheshimu Mungu kwa kinywa tu bali na matendo yako yaambatane na namna kinywa chako kinavyozungumza.

nipende kukusihi ndugu yangu badirisha njia zako na kama bado hujatengeneza na MUNGU Yeyeb ado anatoa mwito yoyote aliye na mzigo wa aina yeyote yeye atakupumzisha.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 MATHAYO 11:28 
 "Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha."

Usiridhike na kuingia kwako ibadani tu ridhika ikiwa unashuhudiwa na Roho mtakatifu kwamba umekaa sawa.

 WARUMI 10;10 
 "Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu."

kazi yako ni kuamini na kumpa kristo maisha yako na sio kwenda kanisani tu na huku unafanyavitu visivyofaa

Saa ya hukumu iko karibu badili njia zako ndugu yangu.

Mungu alibariki kwa kuusoma ujumbe huu na Mungu akupe hatua ya kutoka katika kifungo chako kinachokutesa kinachokufanya unakuwa na maisha ya kifafa.
Unaweza ukapata masomo yanu mengine ukatafuta kwenye browser yako kwa kuandika
(Jackobombwaga.blogspot.com)

 Ulikuwa nami mpendwa katika kristo Yesu
Name:Bro Jackobo
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441

JIFUNZE KUWA MWAMINIFU MPAKA MWISHO HATA KAMA UNAONA UGUMU


Bro Jackobo {JAM295}

Utakuwa nami mpendwa katika kristo Yesu.
Name: Bro Jackobo
Phone; +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu?? Karibu tushiriki pamoja neno hili kwa kifupi sana katika siku hii ya leo.

Kumekuwa na ugumu sana wa watu kuutunza uaminifu pindi pale mazingira kwao yanapokuwa magumu na mazingira ya kweli yao yanawaumiza wao wenyewe.

Mwanzo 39:9-12
"Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?
Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye. Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani; huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje."

Yusufu alipita wakati mgumu ambao huo wakati ulikuwa mgumu maana yake alipata nafasi kabisa ya kuweza kulala na mke wa potifa lakini yeye aligoma kabisa kulala na mke wa potifa maana alikuwa akitafuta kuwa mwaminifu mbele za MUNGU hakujali hata kukimbia na kuacha mavazi yake ambayo aliona kwamba yangemletea shida hata kwa baadae kwenye maisha yake.

Jiulize mara ngapi wewe umeacha sheria ya MUNGU kwa sababu ya magumu yaliyokuzunguka?? Ni mara ngapi umevunja uaminifu wako kwa sababu ya vitisho kwenye maisha yako ya kila siku??

Mathayo 15:8-9
"Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure,
Wakifundisha mafundisho
Yaliyo maagizo ya wanadamu."

Mbona umekuwa ni Mtu wa kumuheshimu Mungu tu kwenye maisha yako kwa kinywa lakini matendo yako yamekuwa yakimkana Mungu siku zote.

Au hujui ya kwamba kuna laana ipo pale ambapo mtu akifanya mambo ya ajabu lakini asiwe tayari kuishi katika kweli ya Mungu? πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Mithali 28:13
"Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema."
Ukiwa mtu wa kumheshimu MUNGU kwa kinywa tu na matendo yako yanamkana MUNGU inamaanisha huwa unauficha ubaya wako wa kila siku baada ya kwamba uutubie huo ubaya wako wewe unaendelea kujificha jua ya kwamba unajiletea laana mbele za Mungu kwenye maisha yako.

Ndio maana nakushauri ndugu yangu kwamba uamue kuwa mwaminifu siku zote za maisha yako hata kama unaona magumu kwenye maisha yako.

Ndio maana YESU anakushauri hivi
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Ufunuo wa Yohana 3:15
"Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto."

Katika maandiko hayo hapo juu yako wazi kabisa na yanakutaka uamue kuchagua upande mmoja wa kuwa mwaminifu ukiamua kuwa wa kristo basi uishi kama Kristo na kama ni kwa shetani uishi kama kwa shetani tu. Usiwe mtu wa kumega huku na kule.

MAENEO AMBAYO YAMEKUWA NA KUKOSEKANA KWA UAMINIFU NDANI YA KANISA
Kuna maeneo mbalimbali na mengi sana ambayo yamekuwa na changamoto kuwa na uaminifu lakini nitakuelezea maeneo machache tu
{A} Mahusiano, uchumba na ndoa
{B} Biashara
{C}Ibada na maombi
{D} Matoleo pamoja na ahadi

{A} MAHUSIANO, UCHUMBA NA NDOA
mahusiano na uchumba
Vijana wengi wamekuwa wanaingia kwenye mahusiano na uchumba kwa siri na hata kufanya mambo yasiyotakiwa kwa siri(kukosa uaminifu) huku wanafanya ibada kila inapoitwa leo
Mbona umekuwa unafanya tendo la ndoa, unafanya Romance wakati hauko kwenye ndoa ndugu yangu? Mungu akupe neema utoke huko kwa jina la Yesu kristo.
Kuna watu wanadai kwamba miili inawasukuma kufanya hivyo lakini nawaambia kuna mambo mawili hapa ya msingi ukiyajua yatakusaidiaπŸ‘‡πŸ‘‡

πŸ‘‰πŸ‘‰Moja: Mwili kuhitaji tendo la ndoa kwa mwanadamu ambaye yuko vizuri kibiolojia ni kitu cha kawaida lakini umepewa namna ya kuweza kushinda


Wagalatia 5:16
"Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili."

Hapo juu biblia inakuambia uenende kwa Roho ili usitimize tamaa za mwili kiufupi ni kwamba tamaa za mwili zitakuja isipokuwa ili usizitimize/usiziishi lazima uwe katika Roho yaani ukubali kuwa chini ya maongozi ya Roho mtakatifu lasivyo utakuwa unajidanganya tu. Wengi wanajikuta kuingia kutenda dhambi ni kwasababu hawajakaa katika Roho mtakatifu.

1 Wathesalonike 4:3-5
"Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu."
Maandiko hapo juu yanakukukataza uasherati lakini yanakuambia ujue kuuweza mwili wako katika utakatifu na heshima kwahiyo hata kama ikitokea wewe nenda mbele za Mungu kwa moyo wa Toba na yeye atakusamehe na kukusafisha kabisa.
Mwingine anaweza sema nawaambia watu waendelee katika tamaa lakini sio hivyo ila hiyo inatokea na ndio maana paulo alisema

1 Wakorintho 7:1-2
"Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke.
Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe."
Hapo anaeleza habari ya zinaa ndio inamfanya mtu basi awe na ile ya kumgusa na kuwa na mke au mume ambapo zinaa ni matokeo ya tamaa. Kwahiyo usiogope ikitokea hivyo ila mtafute Mungu atakusaidia.

Note: mtu asije akakudanganya kwamba eti ukiwa katika kristo kama ni kijana uliye okoka kushituka hakupo. Kushituka kupo ila Mungu anatutunza na kutupa uwezo wa kustahimili. Aliposema kila mtu ajue kuuweza mwili inamaana mwili kuna namna utahitaji hakusema mkiwa katika kristo mwili utakuwa hauna chochote. Na anaposema kwamba hatutatimiza tamaa za mwili maana yake yapo matamanio ya mwili ila tukiwa katika Roho hatutayaishi.

πŸ‘‰πŸ‘‰Pili, Tendo la ndoa sio dhambi kabisa ila likifanyika kwa wakati sahihi na kwa watu sahihi

Kwahiyo ukiona huwezi kukaa bila tendo la ndoa basi jitahidi kuoa au kuolewa na kuepukana na hatia ya dhambi itakayokuwa kwako kwa kuqhindwa kujizuia kwako.

Ndoa
Pia hapa kuna changamoto kubwa sana ndani ya kanisa unaweza kukuta mwalimu wa kwaya au kiongozi yeyote anatembea na mshirika ndani ya kanisa mahali palepale kitu ambacho kinaleta shida kubwa sana ndani ya kanisa.

Mpendwa usiendelee kujifariji tu kwamba uko na Mungu kumbe Mungu amekuacha  tubu dhambi yako biblia imejieleza kabisa katika
Kutoka 20:14 "Usizini." Jitahidi utoke huko bado Mungu anakupenda.

{B} BIASHARA
Katika eneo hili Mungu atusaidie kanisa tutoke hapo maana wafanyao biashara wamekuwa ni watu wa kuwaibia wale watu wanaowauzia wakitaka kupata faida kubwa katika vile vitu wanavyovuza mfano
πŸ‘‰Watu hutengeneza vifaa vya kuuzia vidogo chini ya kipimo sahihi na namna inatakiwa n1 kujikuta wakifanya mambo yasiyofaa na kuangukia katika Dhambi

Mambo ya Walawi 19:35
"Msifanye yasiyo haki katika hukumu, wala katika kupima, wala katika mizani, wala katika cheo."
Mithali 11:1
"Mizani  ya hadaa ni chukizo kwa BWANA; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza."
Ezekieli 45:10
"Mtakuwa  na mizani ya haki, na efa ya haki, na bathi ya haki."
Maandiko hayo yamejieleza kufanya katika mizani ya haki kwahiyo jitahidi kuwa mwaminifu katika eneo hilo 
πŸ‘‰pia watu walioajiliwa huwa wanaiba katika faida zile wanapata na kupeleka pungufu kwa waajiri wao.
Kwahiyo Mungu akusaidie ufanye kama inavyotakiwa usiwe mtu wa kuvunja uaminifu bado Mungu anakupenda.

{C} IBADA NA MAOMBI
Watu wengi wamekosa kuwa waaminifu kwenye maisha yao binafsi maana wamekuwa ni watu kufanya ibada ili waonekane lakini unakuta ndani yao hakuna ibada ya kweli jifunze kuwa mtu wa ibada ya kweli inayoanzia ndani mwako hata unapokusanyika na wenzio basi iwe kama hitimisho la ibada na Mungu atakufanikisha sana na utanawili sana kwenye maisha yako ya kila siku.
Katika eneo la maombi inakubidi kufanya kama maandiko yanavyotaka kufanyika basi Mungu akupe neema nmejaribu kukuelezea kifupi tu ili upate mwanga.
 
Kwahiyo jitahidi kuwa mwaminifu katika eneo lolote ambalo utakuwa umekaa na ndio maana na ndio maana huwa nina msemo mmoja huuπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡ 

UKIWA MWAMINIFU TU MBELE ZA WATU WAKATI UKIWA MWENYEWE HUWEZI KUUTUNZA UAMINIFU BASI UJUE WEWE SIO MWAMINIFU BALI NI MIONGONI MWA WANAFIKI WALIOPO

Nina Mengi ya kusema katika hili lakini naomba nieleze tu hiyo kifupi maana kuna baadhi ya mambo hapo unaweza ongezea mfano
πŸ‘‰Mambo yatakayoniwezesha kuwa na uaminifu
πŸ‘‰Namna gani baadhi ya watumishi waliomfano wa maaandiko walivyotunza uaminifu wao kila siku
πŸ‘‰Faida za uaminifu 
πŸ‘‰Madhara yatokanayo na kukosa uaminifu

Yote hayo ningeyazungumzia lakini kwakuwa nimepewa kwa leo kuandika hayo naomba niishie hapo ila kama itatokea neema nitaandika sehemu ya pili ya hili

Ulikuwa nami mpendwa katika kristo Yesu.
Name: Bro Jackobo
Phone; +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

SAFARI YA JANGWA KWA MWAMINI {sehemu ya pili Final}


Bro Jackobo

Utakuwa nami mpendwa wako katika kristo Yesu
Name: Bro Jackobo {JAM295}
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu? Na tumaini utakuwa unaendelea vizuri na kama hauko vizuri basi Mungu akutokee kwa jina la Yesu kristo. Naomba nimalizie kipengele cha pili kwenye somo letu hili na kama hukufanikiwa kusoma sehemu ya kwanza ningekuomba ukipitia ili tuende pamoja. Kama hukuona basi bonyeza hapaπŸ‘‰SEHEMU YA KWANZA kuisoma


BAADHI YA MAENEO AMBAYO MTU ANAWEZA AKAPITA WAKATI WA JANGWA 
Kuna maeneo mengi sana watu wanapita katika jangwa lakini nitayaorodhesha machache tu na wewe utatafakari utaelewa.
1. Mahusiano na ndoa
Katika eneo hili watu hupitia magumu kama yafuatayo
A)Ndoa
   ✓Kukosekana kwa amani baina ya wanandoa
   ✓Kukosa watoto katika ndoa
   ✓ Usaliti katika ndoa yaani kuchepuka kwa mwezi wako
   ✓kuvunjika kwa ndoa baina ya wanandoa
{Soma 1samweli 1:1-16}

B) Mahusiano
   ✓ Kukataliwa na watu pindi unapotaka kuanza safari ya ndoa
   ✓Kuvunjika kwa uchumba pasipokuwa na sababu ya msingi
   ✓kusalitiana wakati bado mko kwa mahusiano 

2. Uchumi
Katika eneo hili watu hupitia magumu kama yafuatayo
   ✓Kukosa mafanikio wakati unafanya kazi kwa bidii
   ✓kupotea kwa mali zako pasina kuelewa huku unafuata sheria zote za Mungu
   ✓kuwa na madeni ambayo mda mwingine inakuwa ngumu kuyaeleza
 {Soma 2wafalme 4:1-2}

3. Elimu
Katika eneo hili watu hupitia magumu kama yafuatayo
     ✓ Kuwa na matokeo mabaya wakati unafanya bidii katika kusoma kwako
     ✓kukosa vufaa vya kukuwezesha kuweza kupata elimu mfano Ada n.k
     ✓Kukosa watu watakao kutia moyo katika kusoma kwako

Pia yapo maeneo mbalimbali unaweza ukapita katika jangwa lakini natamani tuende moja kwa moja katika msingi mkuu wa somoo tunalo jifunza. Nakuombea upate neema ya kuelewa vizuri mahali hapa na Roho mtakatifu akufunulie upate kujua siri hii kwa jina la Yesu kristo mnazareti.


MAMBO YA KUKUSAIDIA KUISHI KIPINDI CHA JANGWA KAMA MWAMINI

✍️ KUMJUA MUNGU KIUNDANI
Ayubu 22:21
"Mjue sana Mungu, ili uwe na amani Ndivyo mema yatakavyokujia."

Katika kumjua Mungu ndio kutakuletea amani kwenye maisha yako kwahiyo msingi wa kuona amani kwa maisha ya mwamini ni kumjua Mungu maana panapo jangwa hakuna amani wala kutulia bali ni machafuko tu.

NAMNA GANI NAWEZA KUMJUA MUNGU WANGU
N.B Suala la kumjua Mungu ni la kila siku sio suala la siku moja wala wiki moja na ndio maana inahitajika jitihada sana ili uweze kumjua Mungu

πŸ‘‰πŸ‘‰Kuwa na neno la Mungu ndani yako
Ayubu 32:18
"Kwa kuwa nimejaa maneno; 
Roho iliyo ndani yangu hunihimiza"
Yohana 6:63
"Roho  ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima"
Wakolosai 3:16
"Neno  la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu."

Maandiko ya hapo juu yanatuhitaji kwamba tuwe na nzno la  Mungu ndani yetu tena yanatuambia kabisa juu ya umuhimu wa kuwa na neno la Mungu ndani yetu maana linatufunulia kwamba kukiwepo na neno kuna uwezo wa kuimizwa n1 unapokuwa unahimizwa ndio unamuelewa Mungu anataka kitu gani kwenye maisha yako. Tena biblia iko wazi kabisa kwamba maneno ni Roho kwahiyo kama ni R'oho ukiwa na Neno la Mungu ndani yako ujue utakuwa na uwezo wa kuwa na Roho wa Mungu ndani yako ambaye huyo atakufariji na kukupa namna ya kuendelea mbele hata kama mambo yako vibaya kwenye maisha yako.

Sasa kwanini tuhitaji neno la Mungu ndani Yetu wakati wa jangwa??
      ✓Neno la Mungu linatuhimiza katika mambo mema
Kwahiyo utaweza kuhimizwa zaidi kuendelea kusimama na Mungu wako hata kama mambo ni magumu ndio maana unasisitizwa kuwa na neno la Mungu ndani yako.
     ✓Neno la Mungu humfunua Mungu katika uhalisia wake.
Kinachotokea katika kanisa la leo ni kwamba Watu wengi Mungu hajajifunua kwao na ndio maana ni rahisi sana mtu akawa mtu wa kusimama n1 kuanguka lakini ukiwa na neno lake Mungu atajifunua dhahiri kwako utajua juu ya nguvu za Mungu, utendaji wake ulivyo, mamlaka yake ilivyo, namna Mungu anaruhusu baadhi ya mambo kuja kwetu huku akiwa bado ana mawazo mema na sisi katika yote tunayapitia. Katika gumu sasa linapokupata utakuwa una uelewa kamili namna Mungu anafanya kwahiyo utaweza kuvumilia ukijua yeye bado yupo na atakuwepo.
        ✓Neno ni mwanga katika maisha ya mwanadamu
Mwanga huwa unaondoa giza mahali kwahiyo kupitia nzno la Mungu unakuwa una taa ndani yako ambayo kwahiyo unaweza kupata muelekeo mzuri wa jinsi ya kuenda pindi uko katika wakati mgumu yaani hata kama unapigwa vita katika huduma bado Mungu atakuwa anakupa maelekezo kwamba ufanye nini ili uweze kufika salama katika safari yako.
         ✓Neno la Mungu hutuongoza wokovuni
Tunapokuwa na uwezo wa kusimama katika wokovu ndipo tunapoweza kuendelea kumtumaini Mungu katika yote ambayo yanatukumba hata kama yanatuvunja moyo.

πŸ‘‰πŸ‘‰Kuwa mtu wa Maombi siku zote za maisha yako kila inapoitwa leo

Luka 22:40-42
"Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni. Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba, akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke."

Yesu alikuwa katika kipindi kigumu cha jangwa maana alikuwa anajua wale aliowafanyia mema wanaenda kumtenda hiana ndio maana aliingia kwa maombi.
Pia yule ambaye alikula naye meza moja anaenda kumsaliti (Luka 22:47-53)
Pia ndio maana unashauliwa usizimie wakati wa tabu zako (Mithali 24:10) 

  πŸ‘‰πŸ‘‰Kuwa watu wa Kumfanyia Mungu Ibada
Unapozungumzia suala la ibada unaweza ukachukulia ni kitu cha kawaida lakini ili tuseme kwanza kunayo ibada lazima kuwe na vitu vikuu vitatu MTOA IBADA (mwanadamu), MTOLEWA IBADA (MUNGU) pamoja na MADHABAHU (Sehemu ya kumfanyia Mungu ibada ambayo huwa inaambatana pamoja na utoaji wa Sadaka na Dhabihu mbalimbali) unaweza ukasoma habari za ELIYA katika kitabu cha 1wafalme 18 sura yote utaelewa

Waebrania10:25
"wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia."
Kwahiyo kukusanyika kwetu katika ibada kila siku kutatusaidia sana kuweza kuelekezana mambo mbalimbali juu ya kweli ya Mungu na namna ya kuweza kuishi maisha ya utaua(uchaji)/ utakatifu. Kuna baadhi ya watu ambao huamini kwamba hata wasipokusanyika kwenye nyumba za ibada wako salama lakini kiuhalisia hawako salama hiyo ni principle ya kiMungu ambayo kaiweka mwenyewe sasa kwanini uachane na utaratibu wake??
Mungu atusaidie sana tuwe watu wa ibada.
Pia kuwa na Ibada za pamoja ni jambo jema sana lakini kama ukikosa kuwa na Ibada za binafsi ujue bado kuna vitu utavikosa sana kwenye maisha yako. Mungu akufungue sana kama unafanya ibada za pamoja tu na haufanyi ibada ya kwako binafsi uelewe umuhimu wake.

Note: Kuna namna nyingi sana unaweza kumjua Mungu ila kikubwa sana ni kutaka kuelewa makusudi ya MUNGU. Naomba niendeleee na point ya pili ya namna ya kuweza kuishi kipindi cha Jangwa.

✍️UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU

Matendo ya Mitume 1:8
"Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi."
Nguvu ni uwezo wa kufanya kazi. Watu wengi wapo kanisani wana Roho wa Mungu lakini bado hawana Ujazo wa Roho mtakatifu na hao ni wana wa Mungu kabisa maana 
Warumi 8:14 
"Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu
Lakini hata kabla ya hapo Yesu aliwaambia wanafunzi wake majina yao yameandikwa mbinguni (Luka 10:17-20) na ilikuwa kabla ya kushuka katika ubatizo siku ya pentecoste kwahiyo walikuwa na Roho wa Mungu ila hawakuwa na ujazo ambayo ndio hutoa uwezo wa kushinda maana baada ya hapo ndio anapotoa kwamba mtakuwa mashahidi wangu n. K
Kwahiyo kupitia nguvu ya Roho mtakatifu utaweza kuwa mwaminifu mbele za Mungu katika moments/Nyakati mambo yanapokuwa magumu na wakati hakuna wa kukuambia kwamba mshike Mungu, Roho yeye atakukumbusha yote kwahiyo tafuta nguvu kwanza ndipo utaweza kuwa salama.

✍️ KUKUMBUKA NAMNA MUNGU AMEFANYA JUUU YAKO
MWANZO 39:8-11
"Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu. Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu? Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye. Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani;"

✓Yusuph aliingia wakati wa jangwa pindi pale ambapo mke wa yule potifa alimtaka kingono maana alitegemea asingeweza kumwambia hivyo ila ashukuriwe Mungu alikumbuka namna Mungu alivyokuwa naye kwahiyo ukikumbuka namna Mungu amekutendea hutayahesabu magumu yale kuwa kitu cha maana zaidi utaishi kwa kusudi la Mungu na sio kuishi kwa matatizo. 
✓Jifunze kuwa mtu wa tafakari siku zote usiwe mwepesi wa kuamua jambo lolote fikiri kwa kina ndipo uchukue uamuzi wa kufuata jambo fulani na kweli ya Mungu itakuongoza katika maamuzi.

✍️ KUAMINI JUU YA UTENDAJI WA MUNGU KWENYE MAISHA YAKO NA KUKUMBUKA ALIKOKUTOA MPAKA ULIPOFIKA.
1Wakorintho 10:10-12
"Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu. Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke."

Kuamini ni kuwa na uhakika kwamba Itatokea hata kama huoni namna ya kuweza kufanikiwa. Ukiona kuna namna ya kwamba nitafanikisha na unamazingira yote ya kukufanikisha hiyo sio Imani.
Wana wa Israeli walishindwa kuamini juu ya utendaji wa Mungu walipokuwa wanatolewa katika nchi ya utumwa wakawa wanamnung'unikia Mussa pamoja na Mungu na ndio maana waliangamizwa lakini wewe usiwe mtu wa kumnung'unikia Mungu hata kama mambo yamekuwa magumu wewe amini tu ya kwamba atafanya na utauona mkono wa Mungu kwenye maisha yako.

✍️KUYAHESABU MAMBO YALIYOKUWA FAIDA KUWA SI FAIDA TENA KWAKO
Wafilipi 1:12-14
"Lakini, ndugu zangu, nataka mjue ya kuwa mambo yote yaliyonipata yametokea zaidi kwa kuieneza Injili; hata vifungo vyangu vimekuwa dhahiri katika Kristo, miongoni mwa askari, na kwa wengine wote pia. Na wengi wa hao ndugu walio katika Bwana, hali wakapata kuthibitika kwa ajili ya kufungwa kwangu, wamezidi sana kuthubutu kunena neno la Mungu pasipo hofu."

Wafilipi 3:7-8
"Lakini  mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;"

Mafungu hayo yameonyesha namna paulo alikuwa katika wakati mgumu kwa ajili ya kristo hata kapata vifungo mbalimbali kwa ajili ya kristo lakini bado mbele anakuambia mengi aliyaona  kuwa mavi yaliyokuwa thamani kwake kwahiyo alikubali kuchukua mzigo utakao kuja kwake kwa ajili ya Kristo Yesu.
Kama ukiweka mambo yako chini kuna namna Mungu atakusaidia kuweza kushinda kwahiyo magumu, changamoto, pale ambapo hakuna mtu wa kukuambia acha dhambi, kukufariji katika huduma yeye atakusaidia na kukupa mwangaza wa mafanikio.
Kama kuna mambo yanakupa faida lakini yanakupelekea wakati mgumu kwenye utumishi wako inakupasa kuyahesabu kama sio kitu cha maana yahesabu hayoo mambo kuwa si kitu cha thamani bali kristo ndani yako ndiye wa thamani utapata neema ya kushinda.

Mungu akubariki kwa kuungana nami tangu mwanzo mpaka mwisho toka sehemu ya kwanza mpaka hii ya pili.
Unaweza ukawashirikisha na wengine pia mwana wa Mungu. 

Lakini katika yote nakuombea ufanikiwe katika magumu yako yote Mungu akufanyie mlango kwa jina la Yesu kristo Amen...

Ulikuwa nami mpendwa wako katika kristo Yesu
Name: Bro Jackobo {JAM295}
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

SAFARI YA JANGWA KWA MWAMINI{sehemu ya kwanza}.


BRO JACKOBO

Jina: Bro Jackobo (JAM295)
Phone: +255766944441 na +255621036471
Email: jackobombwaga@gmail.com

UTANGULIZI WA KUELEWA JANGWA KWA MWAMINI

Maana ya Jangwa

JANGWA ni mahali pa ukame ambapo hakuna mvua ya kutosha na kupelekea mazao pamoja na wanyama kuwa na mazingira magumu katika ukuaji.

JANGWA kwa mwamini inaweza kuwa
✍️✍️Kukosa msaada katika mazingira ya ROHONI na MWILINI

A. MAZINGIRA YA KIMWILI
•kutelekezwa
• kuumizwa,
• kutukanwa
•kudharaulika hata kushushwa chini kuliko vile ulikuwa unategemea kuwaiwe kulinganisha na namna ulivyo
•Jaribu katika maisha yako ya kila siku n.k

B. MAZINGIRA YA ROHONI
unakosa msaada wa kiroho yaani namna ya kuweza kukutana na Mungu
•Hapa unakuwa umekosa mtu wa kukusaidia au mazingira yanakuzuia kuweza kumtafuta Mungu wako
•kutembea katika wakati ambapo huoni bubujiko la Roho mtakatifu ndani yako wakati hakuna dhambi ambayo umeifanya
• Kupigwa vita katika Huduma

UFUNUO WA YOHANA 1:9-11
"Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu, ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiat ira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia."

Yohana alikuwa katika Mazingira ambayo kiuhalisia ilikuwa changamoto sana maana alitengwa katika kisiwa cha patimo na hakuwepo mtu wa kumkumbusha namna gani amtazamie Bwana katika maisha yake alipokuwa mahali pale ila Maisha yake yalimfanya Mungu aonekane kwake nakumpa ufunuo. Pia mazingira yale aliyokuwa yupo yalikuwa ni mazingira yasiyokuwa na usalama pia hapakuwa na faraja yeyote ya mwanadamu mahari pale. Ukiangalia hapo utajua kwamba kweli ilikuwa ni wakati mgumu kwake sana maana alikuwa ametengwa na haoni msaada wowote wa kumpa tumaini la usalama pale kisiwa cha PATIMO. Inawezekana na wewe upo kwenye wakati ambapo hakuna mtu hata mmoja anaye kutia Moyo kila ukitazama unaona hakuna mlango wa Kupita lakini usiogope hata kidogo endelea nami kunalo tumaini.

Yohana hakuyahesabu mazingira yale kuwa kikwazo cha yeye kuwasiliana na Mungu. Ila ilikuwa ni kipindi cha Jangwa kwake maana
✍️Hapakuwa na faraja ya mwanadamu
✍️Hapakuwa na mazingira mazuri yakumfanya awe na usalama maana alikuwa sehemu yenye uwezekano wa samaki hatarishi kama nyangumi n.k
✍️hakuhimizwa kumtafuta Mungu

MWANZO 37:23-28
"Ikawa Yusufu alipofika kwa ndugu zake, wakamvua Yusufu kanzu yake, kanzu ile ndefu aliyoivaa, wakamtwaa wakamtupa katika birika; na hiyo birika ilikuwa tupu, hamna maji. Nao wakakaa kitako kula chakula; wakainua macho yao, wakaona, msafara wa Waishmaeli wanakuja wakitoka Gileadi na ngamia zao, wakichukua ubani na zeri na manemane, wakisafiri kuvichukua mpaka Misri. Yuda akawaambia ndugu zake, Kwafaa nini kumwua ndugu yetu, na kuificha damu yake? Haya, na tumwuze kwa hawa Waishmaeli, wala mikono yetu isimdhuru, maana yeye ni ndugu yetu, na damu yetu. Ndugu zake wakakubali. Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika birika, wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri."

Kwahiyo pia hata ukimuangalia Yusufu utagundua kwamba wale watu waliokuwa ni ndugu zake ndio waliomtendea hiana kwenye maisha yake maana walikuja kumtoa kuwa kama bidhaa ya kuuza na kununuliwa. Kwahiyo hiyo ilikuwa jangwa kwa namna ifuatayo
✍️Ndugu zake ilitakiwa wampe ulinzi lakini waliondoa ulinzi kwake.
✍️Ndugu zake walikuwa wakimuwazia mabaya maana walikuwa wanatamani hata kumuua..
✍️Yusuph alitupwa kwenye birika(shimo) ambapo mle hakuwa na msaada wowote

Kwa mazingira kama hayo unaweza ukagundua namna Jangwa linakuwa kwa mwanadamu awaye yeyote haijarishi kwamba ni ndugu au ni watu toka mbali wanamfanya awe katika hilo jangwa

Tutaendelea sehemu ya pili kwa wakati Mwingine kama MUNGU atatupa kibali cha kuendelea naamini umepata jambo hapo namna mwamini anavyoweza kuwa anapita wakati wa Jangwa.

Mungu akubariki kwa kusoma kipengele hiki cha kwanza cha UTANGULIZI juu ya Namna ya kuishi wakati wa jangwa kwa mwamini

Ulikuwa nami mpendwa katika kristo YESU

Jina: Bro Jackobo (JAM295)
Phone: +255766944441 na +255621036471
Email: jackobombwaga@gmail.com

SIRI YA USHINDI WA KIJANA/MWAMINI KATIKA MAZINGIRA YA KIROHO(SEHEMU YA KWANZA)

 
BRO JACKOBO(JAM295)

Phone: +255766944441 na +255621036471
Email: jackobombwaga@gmail.com

UTANGULIZI
Maono... 
Mithali 29:18
"Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria."

Ushindi wowote huwa unaanza katika kuwa na maono(vision)

Maana ya MAONO(VISION)

Vision...is  An ideal or a goal toward which one aspires(dream or hope)
In swahiliπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 Maono ni wazo au lengo ambalo mtu anatumainia au ana ndoto nalo

Maono huwa yanaanza kwa imani.. yaani yanakuwa ni matarajio ambayo mtu anatazamia kuyafikia ingawa bado haoni au anaona mlango wa kufikia.
Kijana ambaye ameokoka lazima ajizatiti kwanza katika mambo makuu mawili yaani akiwa na mtazamo chanya katika maeneo makuu mawili ambayo ni KIROHO na KIMWILI kwa ajili ya mafanikio yake mwenyewe. Pasipokuwa na jambo unalitumainia katika ulimwengu wa Roho uwe na uhakika kwamba utaishia njiani kabisa.

KIINI CHA SOMO

MAFANIKIO KATIKA MAZINGIRA YA KIROHO
Hapa nazungumzia suala zima la kuwa na mahusiano mazuri na Mungu pamoja na kuweza kuufikia ule utimilifu wote wa Kimbingu yaani ije ifike wakati umekaa pamoja na watakatifu wake kule mbinguni.
Kijana siku zote amekuwa ni mtu ambaye kama akijielewa vizuri basi atakuwa na mahusiano vizuri na Mungu( 1Yohona2:13) japo Huwa katika ujana ndipo mambo mengi ya kidunia yanaibuka ndio maana Maandiko yanazungumza hivi

Zaburi 119;9
"Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako"

Hapa maandiko yanweka wazi kwamba mara nyingi njia za kijana huwa haziko safi sasa afanye nini ili aweze kuzisafisha basi inakuja kutoa majibu kwamba lazima awe mtu wa kutii na kufuata neno la Mungu.

Mwanzo 8:21
"Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya"

Baada ya Nuhu kumtolea Mungu sadaka baada ya kuwa wametoka katika ile safina aliamua kubadili mambo mengi aliyokuwa amekwisha yaweka mfano wa mambo hayo ilikuwa ni

πŸ‘‰πŸ‘‰πŸ‘‰ kuilaani ardhi ambapo aliilani baada ya Adamu kusikiliza sauti ya mkewe, Mungu anakuja kuifuta hiyo kwamba hatailani tena maana mawazo ya mwanadalu ni mabaya toka ujana wake. Unaweza soma hapo chini andiko linalothibitisha 

Mwanzo 3:17 
"Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako"

πŸ‘‰πŸ‘‰πŸ‘‰Kuiangamiza Dunia kwa maji(gharika). Baada ya wana wa Mungu kuwaingilia wana wa wanadamu ndipo Mungu aliamua kukiondoa kile kizazi na ndio maana akasema hatashindana na mwanadamu. Lakini baada ya hapo vitu vyote alisema hata vifanya tena maana alishagundua katika ujana kuna mawazo Mengi mabaya huwa yanaibuka kipindi cha ujana. Unaweza ukasoma katika
Mwanzo 6:1-13
Mawazo ya mwanadamu ni mabaya toka ujana wake... Kwahiyo katika ujana ndiko mambo mengi ya uharibifu yanaanza Sasa Kama kijana asipokuwa na mikakati mizuri ya namna ya kushinda katika ulimwengu wa Roho basi uwe na uhakika huyo mru atapoteza lengo lake la kukutana na Mungu.

BAADHI YA MAMBO YANAYOWEZA KUMSAIDIA KIJANA KATIKA MAFANIKIO YA KIROHO

1. KUSIMAMA KATIKA NAFASI MUNGU AMEKUPA.

Mwanzo 3:8-11
"Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha. Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?"

Ukisha tenda dhambi huwa siku zote watu wanakaa mbali na kukimbia pale Mungu amewapa kusimama na kutembea na ndio maana hata adamu baada ya kuona kwamba kashafanya tofauti kwanza aliamua kujificha asionekane mahali Mungu kamuweka... Ndio maana Mungu alipoitazama nafasi yake hakumuona katika nafasi ambayo Mungu alimpa akae akamuuliza uko wapi na haina maana kwamba Mungu alikuwa hajamuona adamu bali alimuona adamu isipokuwa katika nafasi Mungu alitatarajia adamu akae hakumuona adamu. Na siku zote Mungu anapomtazama mwamini huwa anachokifanya anaangalia nafasi ambayo amemuweka ili aweze kufanya kazi aliyokuwa amemuagiza.

HABAKUKI 2:1
"Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwangu"

Ukisoma Sura ya kwanza ya habakuki utamuona namna Habakuki alivyokuwa akilalamika lakini Mungu hakuonyesha majibu yeyote mpaka ulipofika hatua ya kwamba yeye atasimama kwa zamu yake(nafasi yake) ndipo Mungu anaanza kujidhihirisha kwake kwa hiyo ili Mungu aweze kukufanikisha katika mazingira lazima ujue nafasi yako katika ulimwengu wa roho usimame hapo ndipo utapata mafanikio.
Watu wengi tumeshindwa kutumia nafasi Mungu alizotupa ndio maana tumekuwa watu wa kushindwa kuendelea kiroho tumekuwa na kiroho cha kifafa kila siku kitu ambacho Mungu kiuhalisia hakubaliani nacho kwahiyo lazima utambue nafasi yako mwana wa Mungu pasipokujua nafasi yako utajikuta unamkosea Mungu kila inapoitwa leo.

MADHARA YA KUKAA KATIKA NAFASI AMBAYO MUNGU HAJAKUWEKA KUKAA

Waamuzi 16:1-25

✍️✍️✍️✍️ KUKOSA MACHO YA KIROHO

WAAMUZI 16: 1-24(21)
"Wafilisti wakamkamata, wakamng'oa macho; wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza."

Ukisoma vizuri biblia ukianza sura ya 14 ya waamuzi utaona ulikuwa ni mpango wa Mungu kutaka Samsoni akaoe mfilisti lakini ilipofika hatua imeshindikana samsoni kwa matakwa yake mwenyewe alienda kwa Kahaba wa kifilisti(Sura ya 16) angali yeye ni mnadhiri wa Mungu sasa ukiitazama hiyo siyo nafasi ambayo Mungu alitazamia kwamba samsoni aweze kukaa ndio maana mpaka ukafika hatua anaondokewa macho yake. Samsoni kama mnadhiri wa Mungu anakubali kuingia kwa kahaba yaani mwanmke ambaye anajiuza(anafanya tendo la ndoa na wanaume mbalimbali ili alipwe) albapo hata ukifikiri mw3nyewe samsoni alienda katika upande usiokuwa unmstahili kabisa.
Kama ukiwa unakaa katika sehemu ambapo Mungu hataki ukae basi uwe na uhakika kuna viwango fulani katika roho vitakuwavinapungua na kuna uwezekanao mkubwa ukajikuta  unaanguka katika dhambi.
Tafuta kujua nafasi ambayo Mungu anataka ukae usipelekeshwe na watu kwamba wanataka ufanye jambo gani ndipo utaweza kuwa na mafanikio ya kiroho lwenye mazingira yako.

✍️✍️✍️KUKOSEKANA KWA THAMANI YAKO

Waamuzi 16:1-25(25)
"Ikawa mioyo yao iliposhangilia, wakasema, Mwiteni Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze mbele yao wakamweka katikati ya nguzo mbili."

Baada ya samsoni kukaa nje ya nafasi ya kuwa mnadhiri wa Mungu alijikuta akiingia katika kazi ya kuanza kusaga ngano mpaka ukafika hatua anakuwa kama chombo cha burudani mbele ya wafilisti. Endapo utakaa mbali na sehemu Mungu amekupa ile heshima albayo Mungu alikupa uwe nayo basi uwe na uhakika ile heshima itaondo'ewa kwako haijalishi wewe ni mtu wa namna gani. Samsoni aliyekuwa mnadhiri wa Mungu anajikuta anaingia katika kudharauliwa ile heshima yote ya kuwa mnadhiri wa Mungu miaka 20 inapotea. Ni jambo la kutisha.
Kazi unayoifanya nje ya nafasi Mungu amekupa ukae inakuwa haina thamani mbele za Mungu maana yeye alitazamia ufanye kazi ndipo akupe ujira.
 Lakini Ukiona Mungu anaonekana kwako basi uwe na uhakika kwamba Mungu amekupa thamani ambayo inakupasa kuitunza.
1Samweli 2.1-12(8)
"Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake."
Hana baada ya kutokewa na Mungu aliamua kumtukuza Mungu akisema kwamba yeye huwa anawainua wanyonge na kuwaketisha pamoja na wakuuu kwahiyo lazima uitunze heshima hiyo kwa kumpa utukufu Mungu kama hana alivyoweza kufanya. Itumie nafasi vizuri pale Mungu anakupa nafasi.

✍️✍️✍️KUANGUKA KATIKA DHAMBI.

2SAMWELI 11:1-26(4-5)
"Basi Daudi akapeleka wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye; (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake.Yule mwanamke akachukua mimba; basi akapeleka na kumwambia Daudi, akasema, Ni mja-mzito"

Kama kiongozi wa sehemu lazima ujitahidi kuwa mfano wa kuigwa sikuzote. Tukimuangalia Daudi albaye alikuwa mfalme ilimoasa aende kwa wakati ule Vitani lakini yeye alibaki nyumbani akaanza kuangalia fahari yake ambayo alikuwa nayo ndipo anajikuta anaingia katika kishawishi cha kutenda dhambi baada ya kumuingilia mke wa Uria.

Kama Daudi angeenda vitani basi yote hayo yasingeweza kutokea yaani alikaa sehemu tifauti na Mungu akae ndio maana akajikuta akatenda dhambi kwahiyo lazima ukae kwenye sehemu yako ili uweze kukutana na Mungu na kuepukana na kila namna ya uovu

Mungu akubariki sana kwa kusoma hii sehemu ya kwanza unaweza ukashirikisha na Wengine pia tuweze kutoka kwenda sehemu.

Ulikuwa nami mpendwa katika kristo Yesu
Bro Jackobo (JAM295)
Phone: +255766944441 na +255621036471
Email: jackobombwaga@gmail.com

MSIFANYE JAMBO LOLOTE NJE YA IMANI


BRO JACKOBO

Wako mpendwa katika kristo yesu 
BRO JACKOBO
Phone:+255766944441 and +255621036471
Email: jackobombwaga@gmail.com

UTANGULIZI
Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu?? Naamini unaendelea vizuri na kama hauko vizuri Mungu akutokee ukawe vizuri katika Jina la Yesu kristo.
Watu wengi sana tumekuwa tukifanya mambo Mengi sana tukiwa chini ya jua ambapo Mengi yamekuwa hayafanikiwi na mengine yamekuwa yanafanikiwa. Haimaanishi kwamba kutokufanikiwa kwetu basi kutaondoa uwezo wa Mungu bali Mungu atabaki kuwa Mungu tu.

Sasa naomba tuangalie juu ya somo hili "TUSIFANYE JAMBO LOLOTE NJE YA IMANI" ili tuweze kupata matokeo mazuri katika Mambo tuyafanyayo.

Msingi mkuu
WARUMI 14:23
"Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi."

Neno la Msingi ni IMANI ambayo ni "kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana". (WAEBRANIA 11:1)

Ninapozungumza kwamba usifanye jambo lolote nje ya Imani namaanisha kwamba "usifanye kitu chochote ukiwa na wasiwasi na matokeo ya jambo utakalolifanya haijarishi hilo jambo liko vipi"

Mfano unapotoa sadaka yako ukiona kwamba unapoteza pesa yako tu basi USITOE HIYO SADAKA, unapokuwa unaomba lakini hauamini ya kwamba Mungu atafanya basi usiombe, pia unapokula chakula ukiamini kitakudhuru basi usile hicho chakula maana kitakudhuru kwahiyo kitu chochote lazima uwe na uhakika nacho

WARUMI 14:14
"Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi."

Pia biblia inazungumza kwamba namna utakavyokuwa unajiona ndiyo ulivyo kwahiyo ukishajiona katika nafsi yako ya kwamba hili jambo siwezi kufanikiwa basi uwe na uhakika hautafanikiwa maana unakuwa unatengeneza uzio wa Mungu kufanya nawewe

Imani yetu tuliyo nayo inatoka kwa MUNGU mwenyewe kupitia Yesu kristo, Kwahiyo ili ifike jambo kwamba huyu mtu yuko na Imani ni kwamba awe na uhakika na mambo yasiyoonekana kwamba yatadhihirika. 

Katika kuwa na Imani lazima msingi wako ujengwe kwa Kristo Yesu mwenyewe maana yeye ndiye aliyemuanzilishi wa Imani yetu(uhakika wetu) maana pasipo yeye hatutaweza kukaa katika uhakika wa kufanikiwa ndio maana petro alipoonyesha kuwa na uhakika kwamba Yesu ni mwana Wa Mungu ndipo Yesu alisema kupitia Imani ya kuwa na uhakika na yeye basi atalijenga kanisa lake mbalo litakuwa imara.

MATHAYO 16:16-18
"Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda."

Kwahiyo kuna matokeo makubwa ya ushindi sana pale unafanya mambo yako kwa Imani maana Mungu anakuwa pamoja na wewe.

KWANINI TUFANYE MAMBO YETU KWA IMANI??

1.Ukifanya mambo yako kwa Imani kunakufanya uwe mbali na kuhesabiwa kuwa na hatia Mbele za Mungu(Dhambi)

Biblia imezungumza katika WARUMI 14:23 kuwa tendo lolote linalofanyika nje ya imani ni dhambi sasa ukifanya kitu chochote ukiwa umemtanguliza Mungu basi hayo mambo yako yatathibitika mbele za Bwana na utakuwa na haki

2. Utakuwa unaonyesha unyenyekevu pamoja na matumaini yako kuwa mbele za Bwana.

WAKOLOSI 3:12
"Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu"

Kuwa mteule wa Mungu hapo ni tendo la kiimani sio jambo la kimwili au ambalo unaweza kulichukulia kawaida na ndio maana paulo aliwataka watu wa namna hiyo waenende katika hali ya unyenyekevu sasa inakuwa vipi Mungu atakuona ni mnyenyekevu..

MITHALI 22:4
"Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha Bwana Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima."

Ukiwa ni Mtu wa kumuamini Mungu basi hautacha kumfanyia Mungu ibada sasa katika kumfanyia Mungu ibada ndiko kunaonyesha thawabu yako ya unyenyekevu kwahiyo Mungu atakuona unanyenyekea mbele zake na atakutokea katika mambo yako yote unayoyafanya maana umemuamini yeye aliyekuumba basi Katika yote usifanye jambo lolote ukiwa na wasiwasi

3. Kupitia kufanya kwa Imani kunampa nafasi Mungu ya kuhusika na Maisha yako ya kila siku maana unakuwa umeuvunja ule ukuta wa yeye kufanya kazi.

4. Kufanya mambo kwa Imani kutakufanya uondokane na msongo mkubwa sana wa Mawazo juu ya mambo ambayo yanakuzingira.

5. Kutakufanya uweze kuvumilia mpaka mpaka wakati jambo limekwisha kutendeka haijarishi utapita wakati gani haujajibiwa mambo yako.

6. Kufanya Mambo kwa Imani huonyesha ukomavu wa kiroho wa mtu (Ukiwa unafanya mambo yako kwa imani utaendelea sana kuongezeka kiroho maana yeye mwenyewe atakuonga viwango.

MIFANO YA MAENEO MBALIMBALI AMBAYO WAKRISTO WAMESHINDWA KUFANIKIWA KUENDA NA IMANI NA MATOKEO YAKE

1. BIASHARA NA KILIMO

 Biashara nyingi zinafanywa na wapendwa huku wakiwa hawaamini kufanikiwa kwao ndio maana wanaishia kutokufanikiwa japo wanafanya kazi kwa bidiii ndugu yangu ukifungua mlango mmoja kwenye maisha yako ujue huo mlango ndio utakuwa sababu ya wewe kushindwa kufanikiwa kwako sasa Weka imani katika biashara yako Mungu atakutendea

Vivyo hivyo hata katika kilimo watu bado wamekuwa wanategemea sana hali ya hewa kuliko kumtegemea Mungu mpaka inawaletea shida sana. Sijasema kwamba usiangalie majira ya kufanya kilimo bali natamani uwe na imani kama umefanya jambo kwa majira sahihi basi Mungu atakufanikisha Mungu alishaiondoa laana ya ardhi aliyokuwa amempa Adamu pale bustani ya Edeni baada ya Nuhu kutoka katika ile safina kwahiyo barak zipo na Mungu amesema atabariki kazi ya mikono yako (KUMBUKUMBU LA TOTATI 28:3) sasa kwanini uogope?? Wewe mtumaini bwana tu atakufanikisha

MWANZO 8:21
"Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya"

2. MAHUSIANO YA UCHUMBA NA NDOA

Vijana na mabinti wengi wamekuwa na kasumba moja kwamba hawawezi kuingia kwenye mahusiano ya ndoa huku wakiwa wanawaamini hao wapenzi au wenzi wao watarajiwa wakidai hayupo mtu wa kuaminiwa lakini nhoja nikupe kitu kimoja tu hapa.

MITHALI 19:14
"Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Bwana."

Kwanza jambo la kwanza Ukishatambua kwamba ni Mungu ndiye anayetoa mke aliye bora basi lazima utakuwa ltu wa kumtafuta sana Mungu ukiwa na Uhakika ya kwamba Mungu atakupa mke mwema na usianze safari ya mahusiano pasipo Mungu kuhusika na wewe katika mwanzo wa safari yako

1WAKORINTHO 10:31
"Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu."

Sasa unapotaka kuyaanza mahusiano yako basi uyaanze kwa ajili ya utukifu wa Mungu yani watu wamtukuze Mungu kupitia Mahusiano yako maana kuna baadhi ya watu wanapokuwa katika mahusiano yao basi inakuwa ni kumtukana tu Mungu maana mambo yanayofanyika ni ya aibu hata huwezi kufarahi kuyasikia wengine wanafanya Romance, wengine uasherati (Zinaa) kwakweli inatish sana Mungu akusaidie sana usije ukapotelea mwisho.

Kama utakuwa hauna uhakika na mtu ambaye unataka kuingia nae kwenye mahusiano tafadhari usiwe mwepesi wa kuzungumza au kukubali ombi la mtu ili kuepusha kuumiza/kuumizwa kisaikolojia ambapo kutakufanya wewe usiwe na heshima mbele ya huyo mtu uliyemfanyia unyama.

Sasa kumekuwa na kuvunjika kwa chumba nyingi sanaa maana kila mtu anapoingia ana mentality ya kutokuamini ambapo sasa matokeo yanayokuja kutokea ni kukosa msimamo katika mahusiano na kuyumbishwayumbishwa nakila upepo unaokuja baada ya hapo ni kuvunjika kwa uchumba.

YAKOBO 1:8 
"Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote."
 
Kwahiyo ukiwa huna uhakika utakuwa unamuona kijana mwingine au binti mwingine yuko vizuri kuliko yule mtu wako ambaye unampenda ambapo hii kisaikolojia ni mbaya sana inaweza kupelekea ukawa unamchukulia poa au unamchukulia kawaida maana haujawa committed kwake na baada ya hapo ni kuachana. 
Sasa ukitaka kuingia kwenye mahusiano yeyote basi jihakikishe kwanza ndipo uingie kwenye mahusiano hayo lasivyo utakuwa ni mtu wa kutangatanga sana.

3. MAGONJWA

Hapa pia kumekuwa na changamoto kubwa sana kutokana na maendeleo ya sayansi na tekinolojia. Kuna magonjwa ambayo kiutalamu hayana tiba mfano UKIMWI, SARATANI N.K sasa haya yamekuwa yakileta wakati mgumu sana kwa kanisa kuelewa kwamba Mungu anaweza kufanya au la embu tuangalie kidogo hapa

ZABURI 33:19
"Yeye huwaponya nafsi zao na mauti, Na kuwahuisha wakati wa njaa."

Mungu ndiye mwenye uwezo wa kuwaponya watu na mauti ya KIROHO pamoja na KIMWILI kwahiyo yeye ni mponyaji. Sasa kwanini hatufiki wakati Mungu akafungua yale ambayo mwanadamu anayaona kwamba hayawezekani katika hali ya kawaida wakati amesema ya kwamba hakuna jambo ambalo yeye haliwezi (YEREMIA 32:27).

Watu inafika wakati hawafunguliwi ni kwasababu wanafanya mambo yao nje na imani sasa ukitaka Mungu afanye yale yasiyowezekana basi weka imani yako mbele za Mungu kwamba anaweza akafanya basi utauona mkono wa Bwana.
Kuna maeneo Mengi tu ambayo lazima uweke Imani yako mbele za Mungu ili uweze kufanikiwa lasivyo utakuwa unajidanganya tu.

FANYA MAMBO YAKO KWA IMANI
Ulikuwa nami mpendwa wako katika kristo Yesu na Mwokozi wetu
BRO JACKOBO
Phone: +255766944441 na +255621036471
Email: jackobombwaga@gmail.com
Blog link: jackobombwaga.blogspot.com

ULAJI WA NYAMA YA NGURUWE KWA WAKRISTO KATIKA KIPINDI HIKI CHA NEEMA


BRO JACKOBO

Phone: +255766944441 and +255621036471
Email: jackobombwaga@gmail.com

Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu? naomba tushirikishane kidogo kuhusu hili somo maana imekuwa changamoto kubwa sana kwamba kwanini watu wanakula nyama ya nguruwe wakati biblia inazungumza kwamba ni mnyama najisi.
lakini ili tuelewe kwanini tunakula nyama ya nguruwe tutajadili hili somo katika misingi na mfululizo ufuatao
πŸ‘‰Mwanzo Mungu alipoumba ulimwengu aliweka watu wale vitu gani?
πŸ‘‰Vipindi mbalimbali vya maongozi ya Mungu katika biblia pamoja na utaratibu wake
πŸ‘‰Kwanini nyama ya nguruwe inaliwa katika kipindi hiki cha neema?

1. MWANZO MUNGU ALIPOUMBA
Baada ya Mungu kuumba ulimwengu huu na vyote vilivyomo, alifanya kwamba mwanadamu pamoja na mnyama yeyote walikuwa wanakula nyasi tu hapakuwepo Simba wala Chui wala mwanadamu aliyekuwa akila nyama

Mwanzo 1:29-30

“Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu; na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.”

Zaburi 104:14
Huyameesha majani kwa makundi, Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu; Ili atoe chakula katika nchi,”

Hayo maandiko yanaonyesha wazi kwamba katika mwanzo wa yote Mungu aliweka wazi kwamba watu wote pamoja na wanyama wale majani pamoja na matunda kuwa sehemu ya chakula chao cha kila siku.
kuna maswali Mengi sana kwamba kama ndio hivyo kwanini sasa Simba, chui n.k wanakula nyama siku za leo, Hapo tunahitajika kukaa sana na Mungu vizuri ili atufundishe. naomba nisiende mbali sana naomba nirudi kwenye mtirriko niliouorodhesha pale juu kwamba tutaenda nao.

2. VIPINDI MBALIMBALI VYA MAONGOZI YA MUNGU KATIKA BIBLIA PAMOJA NA UTARATIBU WAKE.
Vipindi au Nyakati za Maongozi ya Mungu kibiblia Zimegawanyika katika Maeneo makuu saba ambapo kila kipindi kilikuwa na utaratibu wake uliokuwepo. Katika vipindi hivi vyoote Mungu aliweka sheria mbalimbali za kuongoza vipindi hivyo,Mtu asipofahamu vizuri anaweza kuchanganya  mambo katika vipindi hivyo Mungu aliweka au kubadili sheria zake kulingana na nyakati hizo na makusudi yake aliyoyakusudia kwa wakati huo.

✍️INNOCENCE PERIOD 
Hiki kilikuwa ni Kipindi toka uumbaji mpaka anguko la Adamu. katika kipindi hiki tukiangalia katika habari ya vyakula Mungu aliweka sheria kubwa moja ambayo ilikuwa kwamba ale majanj pamoja na matunda ya miti pekee (Mwanzo 1:29) huku akiwapa katazo la kutokula Tunda la ujuzi wa mema na mabaya (Mwanzo 2:17) na hazikuwepo sheria kwamba usiue, usizine n.k simply ni kwasababu walikuwa wawili tu.

πŸ‘‰CONCIENCE PERIOD-KIPINDI CHA DHAMIRI 
Hiki kilikuwa ni kipindi cha kutoka anguko mpaka wakati wa Gharika. katika kipindi hiki Mungu alikuwa akitenbea nao wanadamu katika utaratibu aliokuwa nao toka kipindi cha uumbaji mpaka anguko lakini anakuja kuongeza jambo baada ya gharika kwamba wale na nyama isipokuwa uhai yaani Damu

Mwanzo 9:3-4 
Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote.Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.”

Sasa kama utakuwa makini utaona hapo kwamba kila chenye uhai, sasa tujiulize hivi Nguruwe ana uhai(damu)? bila shaka utagundua ni ndio anao uhai. kumbe hata nguruwe alikuwa mmoja wa waliokuwa wakiliwa kipindi hicho baada ya gharika ile.

✍️HUMAN GOVERNMENT PERIOD
Hiki kilikuwa ni kipindi ambacho kilikuwa cha kujitawala mpaka wakati wa ibrahimu. Hapa hakuna specification maalumu ambayo Mungu kaweka kuhusu vyakula kwahiyo walitembea sawa na kipindi cha kutoka gharika

✍️PATRIARCH/ PROMISE PERIOD
hiki ni kipindi ambacho kimeanza wakati wa ibrahimu yaani mababa wa imani mpaka Musa. hapa pia ni kama kipindi cha hapo juu tu. Ukiangalia utakutana na ahadi nyingi Mungu anauwekea Ibrahimu, Isaka, Yakobo na Yusuph.

✍️LAW DISPENSATION PERIOD- KIPINDI CHA SHERIA
Hapa ndipo pana himbuko la mambo Mengi sana ambapo ndipo kilikuwa kipindi cha sheria za Musa ambacho kimeanza kwa Musa mpaka wakati wa Yesu kristo. ambapo Mungu aliwaamuru wale baadhi ya vyakula na vingine waviache wasile. Yani kukawa na mwanzo wa vyakula najisi na visivyo najisi. Hii ilikuwa ni kwa sababu za kiafya na kutafuta utii wa Israel, baadhi ya vitu vilivyokatazwa ni pamoja na Ngamia, Sungura, Nguruwe, Kambale, Taa, Pweza, Ngisi, n.k. Mungu aliwakataza WAYAHUDI peke yao wasile baadhi ya wanyama na samaki wote wasio na Magamba na wanyama wasio na kwato zilizopasuliwa kati, au wenye kwato zilizopasuliwa kati lakini hawacheui soma (WALAWI 11;1-47).

Pia maandiko Mengine mfano 
Kumbukumbu la torati 14:8
na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.”

ISAYA 66: 17
Watu wale wajitakasao, na kujisafisha katika bustani, nyuma yake aliye katikati; wakila nyama ya nguruwe, na machukizo, na panya; watakoma pamoja, asema Bwana”

Hapa ndipo unaweza ukajikuta unachukuliwa na Upepo wa kila namna yaani ukikutana na msabato atakupa changamoto pia ukikutana na muislamu atakupa changamoto.
Lakini usiogope tutaona kwanini sasa imefika hatua tunakula nguruwe wakati biblia imeonyesha wazi kwamba msile…. ENDELEA NAMI..

✍️DISPENSATION OF GRACE-KIPINDI CHA NEEMA (KIPINDI CHA WAKATI WA MATAIFA)
Hiki ni kipindi cha kuanzia Yesu kristo mpaka wakati huu tulio nao wakati huu ukiwa unasoma ujumbe huu. Wakati wa neema ndio wakati huu wa agano jipya ambapo tunaruhusiwa kula kila kitu bila kujali wala kuulizauliza. Naomba kipengele hiki nitarudi mbele kidogo na ndio nitakujibu kwanini tunakula kila kitu isipokuwa bado uhai hatutakiwi kula. ngoja nimalizie kipindi cha mwishokatika biblia

✍️ESCATOLOGICAL TIMES
Hiki ni kipindi cha wakati unaokuja yaani mmbo yajayo( dhiki kuu, hukumu ya mataifa, utawala wa miaka 1000, ziwa la moto, vita ya gogu na magogu, mbingu mpya na nchi mpya n.k

3. KWANINI NYAMA YA NGURUWE INALIWA KATIKA KIPINDI HIKI CHA NEEMA?
Tumekwisha kuona vipindi mbalimbali katika biblia na namna ilivyokuwa na tumekwisha kuelewa tuko katika kipindi kipi ( tuko kipindi cha neema). Wakati huu Mungu aliamuru kuliwa kwa vitu vyote isipokuwa damu ambayo kibiblia imekatazwa milele. 
unaweza ukajiuliza maswali yafuatayo
πŸ‘‰kwanini nasema kwamba wakati huu tumeruhusiwa kula
 πŸ‘‰Je, kuna aya yeyote ile katika Agano Jipya inayo mkataza Mkristo kula nyama ya Nguruwe?
πŸ‘‰Je, kuna sheria yeyote ile kwenye Agano Jipya inayo kataza kula nyama ya Nguruwe?
πŸ‘‰Je, Yesu alisema au waamrisha Wafuasi wake wasile Nyama ya Nguruwe?

Theolojia inatueleza kwamba vizazi vya ulimwengu huu vimetokana na wana watatu wa Nuhu ambao ni Shemu, Hamu, na Yafethi sasa katika historia ya chanzo cha mataifa mbalimbali kama inavyoelezwa kwamba wanadamu yaani mataifa yote yaliotokana na watoto wa Nuhu walikuwa wakiishi pamoja na walikuwa na lugha moja na usemi mmoja na waliishi pamoja, wanadamu hawa ikumbukwe kwamba hawakupewa sheria yoyote inayohusiana na wanyama wapasao kuliwa na wasiopaswa. hawakupewa na hapa tunaelezwa ndio chanzo cha mataifa mbalimbali maana baada ya Mungu kuwachafulia lugha walisambaa kila mmoja mahali pake (Mwanzo 11:1-9}

msitari wa tisa(9) “Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote.”

Sasa swali la kujiuliza je wanadamu hawa waliondoka na ufahamu upi kuhusiana na vyakula, kwamba Nguruwe haramu ama?
Maana ifahamike kuwa kwao walipewa wanyama wote kuwa chakula kwa sababu hawakuwa na sheria inayohusiana na vyakula safi na visivyo safi kwao wanyama wote ni safi tu waliondoka na imani hiyo kama walivyopokea huu ndio ukawa mwanzo wa mpishano wa vyakula baina ya watu walioitwa wa mataifa na wayahudi baada ya wao kupewa sheria iliyohusiana na wanyama walio safi na wasiokuwa safi.
Tena unaweza kujiuliza sasa kama walipewa wayahudi sasa kwanini sisi tu akula nyama wakati yesu mwenyewe alikuwa myahudi?  naomba twende pamoja

WAKOLOSAI 2:16
Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato”
Hapo ukisoma utaona ya kwamba inakuambia kwamba mtu asije akakuhukumu kwa sababu ya vyakula kwahiyo unapata picha kwamba hakuna hukumu katika chakula. sasa ukiangalia unaweza fikiri kwamba kama kasema mtu je Mungu yeye itakuwaje?
Pia hapa utakutana na watu wanakuambia eti nguruwe sio chakula lakini wewe usiogope mrudishe kwanza asome MWANZO 9:3 kwamba kila chenye uhai kitakuwa chakula chenu sasa hapo tunapata picha kwamba nguruwe ni chakula.

1TIMOTHEO4:1-4
Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli. Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;”

Paulo anatuweka wazi kabisa kwamba mafundisho ya kishetani yatakuwa yakiwaambia watu waachane na vyakula. Sasa kwani Mungu alipokuwa amewakataza wana wa Israeli alikuw ana ushetani ndani yake? 
Hapana Mungu yeye ni mtakatifu (mambo ya walawi 11:4) na ni wa kuaminiwa wakati wote haijarishi ikoje

WARUMI 14:14
“Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi
Mungu amekwisha kuvifanya vitu vyote kuwa vitakatifu maana tangu asili vilikuwa vitakatifu kwahiyo ukitaka kujua kwanini sasa aliwakataza utarudi nyuma uone kwenye kipengele cha “kipindi cha sheria” utaelewa
Biblia inafundisha kuwa kula au kutokula  hakuongezi utakatifu wala hakuzuii tamaa za mwili (Kolosai 2;16-23) hivyo hatupaswi kujitia katika mambo ya kutunga tu ya mtu,au akilizake na maono ya wanao abudu malaika kumuabudu Mungu hakuji kwa kula au kutokula aina fulani ya vyakula  bali katika moyo safi (Math 5;8)
Ukitaka kuelewa zaidi utaona kwamba wana wa Israeli walikuwa wanazuiliwa hata kugusa mizoga ya hao wanyama walio najisi lakini biblia inaonyesha wazi baada ya kuzaliwa kwa yohana mbatizaji alipokuwa kule nyikani alivaa mavazi ya ngamia ambaye alikuwa ni mnyma asiyeruhusiwa kuliwa.

MATHAYO 3;4
Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu”

sasa hapo ndipo unaweza ukachanganyikiwa kwamba kwanini sasa aliyekuja kuandaa njia ya Kristo alivaa singa ambayo imetengenezwa kwa ngamia kwahiyo hapo unaweza kupata picha kwamba mambo yale yalikuwa katika kipindi cha sheria sasa ilikuwa tunaingia katika kipindi cha neema kwahiyo ilimpasa kwamba aandae mazingira ya kipindi cha neema kwahiyo ilitakiwa ianze hivyo.
Biblia inafundisha kuwa unajisi wa mtu hautoki nje bali ndani ya mtu pia Yesu alitakasa vyakula vyoote (Marko 7;14-16,17-19)

 1KORITHO 6;13
Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili”.

Paulo anajaribu kutupa mwanga tuweze kuelewa kazi kubwa ya vyakula kwamba ni kwa ajili ya mwili kwahiyo hata nguruwe ni kwa ajili ya mwili na sio mambo ya Rohoni sasa kama wewe unaenenda katika Roho kwanini upambane na mambo ya mwilini kwahiyo ukishajua hilo hwezi ogopa kula kitimoto maana kiko kwa ajili ya mwili.

1WAKORINTHO 10:25-28
" Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila ya kuuliza uliza kwa ajiri ya dhamiri ,maana ,dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo, mtu asiyeamini akiwaalika ninyi mnataka kwenda ,kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila ya kuuliza -uliza kwa ajili ya dhamiri"
 
Kwahiyo kitu chochote kinachouzwa unaweza ukakinunua na kukitumia ikiwepo hata nyama ya Nguruwe sasa ukipingana na maandiko ndio hapo unafika hatua unang’ang’ana na mambo ya mwilini na sio ya Rohoni.
kutokana na namna tulivyochambua tukianza na vipindi mbalimbali mpaka tukachambua kipindi hiki cha neema ikoje tumeona maandiko yako wazi dhahiri kwamba kula kitimoto sio Dhambi na hakuna tatizo lolote lakini kama ukaongozwa na Roho kwamba usile basi usile maana kuna mambo Mengine Mungu huwa anafanya kwa watu maalumu kwa sababu maalumu na ndio maana ukiangalia samsoni alizuiliwa kukata nywele kwasababu kulikuwa na unadhiri ndani yake ambao patano lake lilikuwa katika nywele zake.


Ulikuwa na wako mpendwa katika kristo Yesu
Bro Jackobo
+255766944441 and +255621036471
jackobombwaga@gmail.com

BINTI ALIYEOKOKA NA UVAAJI WA VIMINI NA NGUO ZA AIBU


BRO JACKOBO

Bwana Yesu asifiwe kanisa??? Naomba tuangalie kidogo kuhusu uvaaji wa nguo kidogo katika VIMINI (NGUO FUPI NA IMPLICATION YAKE)

Kumekuwa na wimbi kubwa sana la kuwapoteza watu wakiwa wanadai kwamba eti kuvaa hakuna tatizo mbele za Mungu na wengine wanavaa vimini mpaka wakikaa wanatafuta vitambaa na kanga za kuficha maungio yao...

Sasa wewe umeokoka lakini unafanya hivyo je hilo ni tatizo au sio???? 

Naomba twende pamoja🀲🀲🀲🀲
Tuanzie hapa tu jiraniπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 MITHALI 12:16
 Ghadhabu ya mpumbavu hujulika mara; Bali mtu mwerevu husitiri aibu

 Note: Mtu aliye mwerevu huwa anasitiri aibu yake.

Naomba tujiulize ni kwanini sasa Binti unakuwa umevaa mavazi mafupi na madogo alafu unakuwa unapata shida unatamani kujifunika wakati mwenyewe ulichagua kuvaa vimini?? 

Hapo hutafuta asije akaaibika yaani mavazi yake mwenyewe yanamfanya awe na aibu
Sasa inakuwaje mtumishi wa Mungu eti unatuvalia vimini, vinguo vya kukubana mwili wako mpaka maungio ya mwili wako yanajulikana na kila mtu yaani mpaka unafika hatua kila mtu anajua namna maungio yako yalivyo pia kuna wakati hata nguo zako za ndani zinajichora alafu unasema umeficha aibu aiseee inatisha... 

Embu tazama hapaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

1TIMOTHEO 2:9
Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani

Biblia iko wazi kabisa ikimtaka mwanamke avae mavazi yenye kusitiri( kuficha yale maungio yako i.e mapaja, nguo zake za ndani ambayo haya ilipaswa mume wake ndiyo ayaone) 
Sasa wewe unavaa mavazi mafupi sana pamoja na kubana alafu unasema kwamba umesitiri mwili!!!!! Duuuhh 😭😭😭😭 na ndio maana unahangaika kutafuta kanga ili ujifiche maana umeiweka aibu yako peupe na unataka kuificha

Embu tazama maandiko hayaπŸ‘‡πŸ‘‡
MITHALI 7:10
Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo

Kuna mavazi ukivaa yanakutambulisha namna ulivyo sasa wewe umeokoka unavaa mavazi ya kikahaba (Vimini, nguo zenye kuchora maungio yako n.k) ambayo mtu yeyote akikutazama hamuoni Mungu bali anauona UASHERATI NA UZINZI ndani yako sasa unautofauti gani na mtu ambaye hajaokoka wewe???

Endelea nami utanielewaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
 2WAKORINTHO 5:17
 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya "
Kama ukiwa ndani ya kristo upekuwa kiumbe kipya mbona hatukuoni ukiwa tofauti na uvaaji wa makahaba?? Au unafikiri kwamba eti ni unakuwa kiumbe kipya katika Roho tu??? Hapana hata katika mwili wako lazima kuwe na utofauti 

Embu tazama hiyoπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
 LUKA 6:45
 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake

Ukiwa mwema yanayotoka ni mema sasa inakuwa una Mungu ndani Yako lakini Bado mavazi yako hayana wema maana yako kama ya kahaba EMBU ACHANA NA MAVAZI YA AIBU NAMNA HIYO

Unafikiri kwanini YESU alisema amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye (MATHAYO5:28)
Mwanaume namna ameumbwa anaweza kupoteza dira kwa kumtazama mwanamke ndio maana haikuzungumzia amtazamaye mwanaume amekwisha kuzini nae (MUNGU AKUSAIDIE DADA KUELEWA) na ndio maana nimekwisha kukuambia kuna mavazi ya kikahaba

Hivi umewahi jiuliza kwanini makahaba huwa wanavaa vimini na nguo za kuwachoresha kila aina ya maungio yao???
  
Mavazi hayo huwa yanalenga kuwateka wanaume waingie katika tamaa ili wawatongoze hao wanawake wenye mavazi ya kikahaba ili ifuate anguko la aibu

Sasa dada wewe umeokoka kabisa na Bado unavaa mavazi ambayo yanaonyesha maungio yako hivi upya wako uko wapi na unatofauti gani na mtu asiyeokoka???

Yanayomtoka mtu ndiyo huwa yameujaza moyo wake haijarishi anajiita ameokoka.... Shetani haogopi kujiita kwako umeokoka anachotaka ni uwe chombo chake cha kuwarudisha watu nyuma....
Angalia umetumika kwa siri bila wewe hata kujua kuwa chombo cha shetani umewaangusha wengi katika dhambi kwa sababu ya kuvaaa kwako BADILIKA TUSIFARIJIANE MPENDWA SAFARI YA MBINGUNI NI KUJIKANA MWENYEWE

Nikikuona umevaa mavazi ya Aibu alafu unasema umeokoka unanipa wakati mgumu sana tena sana kukuelewa


Kuna wadada mna mtazamo kwamba UKIVAA NGUO FUPI UNAPENDEZA..... 😭😭😭😭😭 Pole zako 

 IMPLICATION YA KUAMBIWA UMEPENDEZA WAKATI UMEVAA NGUO FUPI
Haimaanishi umependeza isipokuwa wewe umevaa mavazi ambayo yanawafanya wanaume wawe kwenye msisimko wa kukutaka uingie kwenye zinaa yaani uasherati na Uzinzi
Mpendwa hata kama ni mtu ambaye uko nae kwa mahusiano anakuona umependeza ukiwa umevalia  nguo za aibu (vimini) jua mtazamo wake umeharibika

EPUKA KUWA KIVUTIO CHA NGONO kwa watu 


KWA AJILI YA UTUKUFU WA MUNGU NIKUSHAURI TU UACHE KUVAA MAVAZI YA AIBU UTAKUWA SALAMA PIA KUMBUKA MWANAMKE AJUAYE KUJISITIRI HUWA ANAPENDWA NA KILA MWANAUME NDUGU YANGU......



Muheshimu Mungu kwa mavazi yako

Wako mpendwa katika kristo Yesu
Bro Jackobo
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441 and +255621036471

KUITOA MIILI YETU KUWA DHABIHU MBELE ZA BWANA (SEHEMU YA TATU- FINAL)

KUITOA MIILI YETU KUWA DHABIHU MBELE ZA BWANA (SEHEMU YA TATU-FINAL)
BRO JACKOBO
Mwal: Jackobo Abely Mbwaga (Bro jackobo)
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441 and +255621036471

BWANA YESU asifiwe mtumishi??? Tumekwisha kuona sehemu ya kwanza ya somo letu juu ya maana ya Dhabihu na tukaona sehemu ya pili juu ya maana Ya mwili, Dhabihu za mwili na tukaangalia Sifa za mtu aliyejitoa dhabihu mbele za bwana anakuwaje pamoja  namna ya kuitoa miili Yetu kwa kuangalia kazi ya mwili ya kupokea ambapo tuliegemea katika Milango ya Fahamu.... Sasa embu tumalizie na kazi zingine za mwili na namna ya kujitoa kuwa wakifu mbele za Bwana..

2. KUHIFADHI/ KUTUNZA

Kikawaida mwili huwa unatumika kutunza mambo Mengi sana lakini ngoja tuende moja kwa moja kiroho kwanini tunasema mwili huwz unafanya kazi ya kutunza/ kuhifadhi

1 WAKORINTHO 6:19-20
"Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu."

Biblia Imeweka wazi kabisa juu ya kwamba mwili ni hekalu la Roho mtakatifu yaani ni mahali ambapo Roho hufanya makazi sasa je mwili wako wewe huwa unatumika kufanya nini??? Je unamtukuza Mungu kupitia mwili wako? Je unauweza mwili wako katika usafi na utaua?? Jichunguze hata kama upo unaingia kanisani maana unaweza ukawa unaingia kanisani lakini bado humtukuzi Mungu.


MAMBO YA KUKUONYESHA UNAMTUKUZA MUNGU KWENYE MWILI WAKO

a). Mavazi yako

Kimekuwa ni kipengele ambacho kimeleta utata sana ndani ya kanisa la leo sana watu wanavaa mavazi ambayo ni ya aibu hata wewe usiyeyavaa huwezi kumuangalia mara mbili unaona fedheha kumtazama lakini yeye yuko huru kabisa.

1TIMOTHEO 2:9
"Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani"

Hapo biblia iko wazi kabisa inawataka wanawake wavae mavazi ya kusitiri (Kuhifadhi/ kutunza) mwili wake. Sasa mwanamke umevaa vimini unadai eti Mungu eti haangalii mavazi na hapo umejisitiri wewe si umevaa nusu u hi kabisa Mungu akurehemu.
Mwingine kavaa kisuruali kimembana makalio hata maeneo yake ya siri yanajichora alafu anadai Roho mtakatifu amemwambia avae hivyo au eti mchungaji wake kamwambia haina shida jamani tusimtukane Mungu kwa namna tunavyovaa.
"HIVI WEWE NA KAHABA/ MALAYA TUNAWATOFAUTISHA VIPI" ??? maana uvaaji wenu uko sawa hauna tofauti alafu unasema Mungu anaangalia Moyo!!!
Sikushangai ni kwasababu umepata mafundisho katika mukitadha usio sahihi mana biblia inasema

1TIMOTHEO 4:12
"Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika use zeemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.

Kuwa kielelezo ni kuwa mfano yani wengine wakuchukulie kama Reference njema sasa wewe umevaa kimini au Suruali imekubana maungio yako yote yanaonekana hata yale ya siri unafikili kuna mtu atataka wanawe wakuige??? Acha na mavazi yasiyo stahiki mheshimu Mungu.

b) Usemi na Maneno yako kiujumla

Watu wako kanisani lakini kwa matusi ndio wanaongoza alafu wanasema kwamba wamejitoa wakifu mbele za Bwana hapo ni kwamba wewe Mungu hayupo kwako ila unajifariji tu ni wakati wa kugeuka na kuacha yote ndiyo maana paulo alimtaka Timotheo  awe kieelelezo kwenye usemi wake. Mungu atusaidie tuwe na rijamu kwenye Maisha yetu.

AMOSI 6:5
"ninyi mnaoimba nyimbo za upuzi pamoja na sauti ya vinanda, na kujifanyizia vinanda vya namna nyingi, kama vile Daudi" 

Kuna watu wanaimba nyimbo ambazo hazimtukuzi Mungu hata kidogo yani zimejaa matusi alafu wanajifariji wao ni wana wa mfalme!! Lahasha ninyi mnajifariji na hamjajitoa kikamilifu mbele za Mungu isipokuwa mnajifariji tu. Amosi alipewa kuwaambia wana wa Israeli Kwamba Ole wao na wewe kama unafanya Hivyo Ole wako na Mungu akuhurumie kabisa.

3.KUJIPENDA.

Kila mwanadamu amepewa kujipenda na kuwapenda wengine kama nafsi yake. Sijawahi kuona mtu asiyejipenda ingawa wapo wasiojipenda na hao huwa mara nyingi wanakuwa na matatizo ya kiakili (Psychiatric disorders). Mwili wa mwanadamu hujipenda kwa kuvaa vizuri, kujihurumia, kupata favour au upendeleo au kibali.
Mungu alipoona ya kwamba mwili huwa unatabia hiyo ndio maana akatupa moja ya amri hii

MATHAYO 19:19
"Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako."

Biblia inaonyesha umpende Jirani yako kama nafsi yako sasa kumpenda jirani yako kama nafsi yako yani uwe na uwezo wa kufanyia jirani yako kwa namna ambavyo wewe unataka na Unapenda Kupata. Japo kuna watu wanafikiri kwamba ni jambo Rahisi sana eti kumpenda jirani yako kama Nafsi yako 
Pasipokuwa na Unafiki wowote utaungana nami kwamba mwili huwa unatabia ya kutaka kupokea wenyewe kwanza wenyewe na sio wengine na ndio maana tukifika hapo tunajikuta tabia za uchoyo zinaingia kwa mtu. Sasa ni wakati wa kujichunguza kwenye maisha yako je wewe hauna tabia za kiuchoyo na kama zipo basi jua ya kwamba kuna namna haujajitoa kikamilifu mbele za Mungu.
Kuna watu anaweza akawa anamiliki vitu vingi sana kiasi kwamba havina hata matumizi kwake lakini kuvitoa akawape wengine Moyo wake unamuuma na yuko kwenye Nyumba ya Mungu na anajiona ya kwamba amekwisha kujitoa kuwa dhabihu mbele za Bwana, lakini uhalisia ni kwamba bado amefungwa katika maarifa ya eneo hilo na anamuhitaji MUNGU ili amtoe hapo wewe ingia chumba chako cha ndani mtafute Mungu akujenge Upya usiwe na wakati wa kupoteza nafasi yako mbele za Mungu.
Ndugu yangu kitu kidogo ukifanyachokinatosha kabisa kukupotezea mahusiano yako na Mungu yani kosa Dogo tu linatosha kukuondoa kwenye lengo la Mungu. Embu angalia hapo chini

1 WAKORINTHO 5:6

"Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima?" 

Ukiangalia Paulo anajaribu kuwaonyesha ya kwamba maisha yao yanaweza yakaharibiwa na kitu kidogo kwahiyo kuwa makini sana Mpendwa katika Kristo Yesu juu ya Mambo madogo madogo unayoyafanya yasije yakakutoa kwenye kusudi na Mpango wa Mungu.
Tumekwisha kuona namna gani mtu anaweza kujiotoa kuwa wakifu Mbele za Bwana Na bila shaka kama umekwisha kusoma masomo yetu naamini umeshapata neema tayari ya kujielewa kiasi kama umeshajitoa mwili wako kuwa dhabihu mbele za Mungu au La. Sasa nifanye nini ili niweze kujitoa wakifu mbele za Bwana??


NAMNA KUJITOA MIILI YETU KUWA WAKIFU MBELE ZA BWANA

1. TOBA
Kitu cha kwanza ni kuingia katika toba yaani kuomba msamaha kwanza mbele za Mungu kwa yote ambayo umekuwa ukiyafanya hata kama umekuwa ukiingia kanisani ndiyo maana ukisoma sala ya Bwana ambayo YESU aliwafundisha wanafunzi wake, Yesu aliwaambia kwamba kila wanaposali wamuombe kwamba awasamehe makosa yao kama wanavyowasamehe wale waliowakosea 

MATHAYO 6:12
"Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu." 

Kwahiyo kuomba msamaha itakupelekea kuwa ni mwenye Sifa ya UTAKATIFU ambayo ni sifa kuu ya mtu aliye jitoa mwili wake kuwa Dhabihu takatifu mbele za Mungu. (Rudi ukaone sehemu ya pili ya Somo utaona)

2.KUTAFUTA  KUMJUA MUNGU
Kiukweli kufika hatua ukasema unamjua Mungu ni ngumu maana hauwezi kumchunguza Mungu lakini inatakiwa ujibidishe umuelewe MUNGU na ndio maana Ayubu anazungumza kwamba inakupasa umjue Mungu ili uwe nayo Amani.
AYUBU 22:21
"Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia."
Kwahiyo kupitia kumjua Mungu itakuepusha na WOKOVU WA KIFAFA (ona sehemu ya Pili ya Somo)

NAMNA YA KUWEZA KUMJUA MUNGU

a)  Kuwa watu wa Kumfanyia Mungu Ibada

Unapozungumzia swala la ibada unaweza ukachukulia ni kitu cha kawaida lakini ili tuseme kwanza kunayo ibada lazima kuwe na vitu vikuu vitatu MTOA IBADA (mwanadamu), MTOLEWA IBADA (MUNGU) pamoja na MADHABAHU (Sehemu ya kumfanyia Mungu ibada ambayo huwa inaambatana pamoja na utoaji wa Sadaka na Dhabihu mbalimbali) unaweza ukasoma habari za ELIYA katika kitabu cha 1WAFALME 18 sura yote utaelewa.

Kwahiyo kutoa kwetu ibada kutatufanya tuachane na WOKOVU WA KIFAFA na tutamtukuza Sana MUNGU kwenye maisha Yetu.

WAEBRANIA 10:25
"wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia."

Kwahiyo kukusanyika kwetu katika ibada kila kutatusaidia sana kuweza kuelekezana mambo mbalimbali juu ya kweli ya Mungu na namna ya kuweza kuishi maisha ya utaua/ utakatifu. Kuna baadhi ya watu ambao huamini kwamba hata wasipokusanyika kwenye nyumba za ibada wako salama lakini kiuhalisia hawako salama hiyo ni principle ya kiMungu ambayo kaiweka mwenyewe sasa kwanini uachane na utaratibu wake??

Mungu atusaidie sana tuwe watu wa ibada na haba ni njema Sana kuwa na Ibada za pamoja lakini kama ukikosa kuwa na Ibada za binafsi ujue bado kuna vitu utavikosa sana kwenye maisha yako. Mungu akufungue sana kama unafanya ibada za pamoja tu na haufanyi ibada ya kwako binafsi uelewe umuhimu wake.

b) Kuwa watu wa Maombi

Maombi ni mawasiliano baina ya muhitaji na mtoa majawabu ya mahitaji. Kwahiyo Maombi ni mawasiliano kati ya mwanadamu (ambao hawa ndio wahitaji) pamoja na Mungu( mtoa majibu ambaye huyu huwa anajitosheleza).

Kwahiyo lazima tuwe waombaji ili tuwe karibu na Mungu na itatusaidia kwa kiwango kikubwa kutokata tamaa na safari yetu ya wokovu tuliyo nayo

LUKA 10:22
"Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni."

YESU alipokuwa anawaambia wasijewakiingia majaribuni sio kwamba alimaanisha wasingekutana na majaribu ila ni kwamba hawatayatii hale majaribu ya shetani kwenye maisha yao yani wakaenda kwa namna majaribu yanataka wawe.

1 WAKORINTHO 5:17. "ombeni bila kukoma". 
Kwahiyo inatupasa siku zote tuwe watu wa kutaka kuwa na Maombi na kumtafuta Mungu tupo tutapata usalama lasivyo tunajipotezea nafasi mbele za Mungu wetu.

HITIMISHO 
MUNGU akubariki sana kwa kuchukua nafasi ya kusoma Somo hili japo ni SOMO lefu. Naamini kama umefuatana nami kutoka tangu tumeanza basi bila shaka Umepata vitu vya Msingi au kitu cha Msingi cha kukusaidia kwenye haya waisha ya WOKOVU. 
Kwa Ushauri na maswali tunaweza kuwasiliana kwa njia ya Simu au kwa njia ya Email. Pia Kama unaoushauri wa namna ya kuifanya kazi hii ya Mungu unaweza kunipa kupitia hizo njia za mawasiliano.
Ni wako mwalimu wa neno la Mungu 
Jackobo Abely Mbwaga (Bro Jackobo)
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441 and +255621036471

KUJIKANA NDANI YA KRISTO YESU (sehemu ya tatu- Final)

Bro Jackobo Utakuwa nami mpendwa katika kristo yesu Name: Bro Jackobo Phone: +255766944441 Email; jackobombwaga@gmail.com Bwana Yesu asifiwe...