KUSIMAMA IMARA NDANI YA YESU KRISTO (sehemu ya kwanza)


Bro Jackobo

Utakuwa nami mtumishi katika kristo Yesu 
Jina: Bro Jackobo
Namba: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu?? Natumaini hali yako iko salama basi kama hauko salama nakuombea kwa jina la Yesu ukapate usalama kwa kadri ya uhitaji wako ndani ya nafsi yako.


Karibu tujifunze somo hili ambalo Mungu amenipa ndani yangu ili nishirikishane na kanisa lake la kizazi hiki cha leo. Somo letu litakuwa katika Vipengele vifuatavyo hapa chiniπŸ‘‡πŸ‘‡

1. Utangulizi 
2. Maandiko ya msingi yanayobeba somo letu.
3. Namna ya kuingia ndani ya Yesu kristo
4. Maana ya kusimama imara ndani ya Yesu kristo/Mungu
5. Kwanini mwamini anapaswa kusimama Imara ndani ya Kristo Yesu
6. Mambo yanayoweza kunifanya nikasimama Imara ndani ya Yesu kristo
7. Uhusiano wako wa karibu na Mungu (Intimacy with the father) utakao kufanya uweze kusimama imara ndani ya Yesu kristo.

1. UTANGULIZI 
■ Mungu amemuumba mwanadamu tofauti sana na viumbe vingine alivyoviumba kwakuwa kwanza kamuumba kwa mfano wake huku mambo yanayomfanya mwanadamu awe mfano wa Mungu ni Utashi na Utakatifu

Mwanzo 1:26 "Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi."

■ kwa habari ya Utashi huu ni uwezo wa mwanadamu kuweza kuamua jambo fulani pasina kuingiliwa na Mungu katika maamuzi yake. Huu utashi ni moja vitu vya hatari na vya thamani kwakuwa mwanadamu anao uhuru wa kimaamuzi.

■ Utashi unaweza kuwa hatari kwakuwa huyu mtu anaweza kuamua kinyume na namna Mungu ambavyo anataka tena huu utashi ni kitu cha thamani sana kwakuwa  mtu anaweza kuishi na kuamua kama Mungu pasipokuingiliwa huku akiuthibitisha uungu ambao Mungu ameuweka ndani yake.

■ Sasa suala la kusimama Imara ndani ya Yesu kristo ni la mtu binafsi ambapo yeye mwenyewe kwa kutumia utashi wake mwenyewe pasipo kuingiliwa na Mungu kwenye uamuzi wake ila Mungu yeye atafanya kazi ya kukushauri namna gani ambavyo unapaswa kuamua.

Kumbukumbu la Torati 30:19 "Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;"

■ Pale ambapo mwanadamu anapoamua kusimama imara ndipo Mungu anakuja sasa kumuimarisha yeye mwenyewe maana kuamua kwako hakutoshi peke yake kukufanya kuwa imara kama Mungu hajahusika ukakaa Imara kwenye maisha yako ya kila siku.

Warumi 1:11 "Kwa maana ninatamani sana kuwaona, nipate kuwapa karama ya rohoni, ili mfanywe imara;"
Warumi 16:25 "Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele," 

Sasa ukiyasoma hayo maandiko mawili hapo juuu utagundua kwamba kumbe ili uimarike bado lazima Mungu ahusike mwenyewe lasivyo itakuwa Ngumu sana kuweza kustahimili kukaa katika Yesu kristo.

2. Maandiko ya msingi katika Somo 

Hapa ni jumla ya maandiko ambayo Somo letu tutakalo kuwa nalo limejikita au limejengwa kupitia Maandiko haya ya msingi.

2 Wathesalonike 2:15 "Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu."

■Ukisoma hapo unaona Paulo anawaambia watu wa thesalonike wasimame Imara kwa kuyashika mambo ambayo walifundishwa ambapo sasa mtu anaweza kuamua kutosimama Imara au awe imara kwa kuzingatia utashi wake namna utakavyo mpa mwelekeo.
■ Mwanadamu anapokuwa ameokolewa inakuwa sio mwisho bali ndio mwanzo wa tabia zinazomjenga yeye na sifa za kuweza kukaa ndani ya ufalme wa Mungu kama mwana wa ufalme.
■ Kwahiyo pale unaposimama Imara unatengeneza sifa yako yakuweza kuendelea kukaa kwenye ufalme wa Mungu licha ya kuwa umeokolewa hapo mwanzo. Tabia ya kusimama Imara inahitajika kwa mtu yeyote anayetaka kukaa kwenye pendo la Mungu na katika tabia za kifalme

Wafilipi 4:1 "Basi, ndugu zangu, wapendwa wangu, ninaowaonea shauku, furaha yangu, na taji yangu, hivyo simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu."

Tunamuona tena mtumishi wa Mungu paulo anasema na watu wa efeso akiwa anawafurahia na huku furaha yake inaonyesha kuweza kutimilizwa kupitia wao kukaa imara ndani ya Bwana wetu Yesu kristo. Kwahiyo kusimama Imara ni kitu cha msingi sana kwa mwamini yeyote anayetaka kukaa katika tabia za kifalme. Ambapo bado msingi unabaki kuwa ni uleule ya kwamba kusimama kwao kumejikita kwa maamuzi ya mtu mmoja binafsi pasipo kulazimishwa kwenye maamuzi yao.

1 Wakorintho 16:13-14 "Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari. Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo."

Andiko letu lingine la msingi tunaona Paulo anasisitiza watu kuwa imara katika Imani akiwataka wawe hodari yaani shupavu/wasiteteleke katika kumuamini Yesu kristo lakini anakuja kutupa msingi mmoja kwamba katika jambo lolote unalolifanya lazima lifanyike kwa Upendo maana huo ndio msingi wa maamuzi ya mtu ambaye ameokoka. Hautakiwi kufanywa kwa kulazimishwa kuwa imara ndani ya Yesu kristo bali lile pendo la ki Mungu lililotufunza namna ya kupenda basi liwe ni kigezo kikubwa cha maamuzi yetu ya kila siku.

Waefeso 3:16-18 "awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani. Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina;"

Paulo bado anaonyesha kila wakati alikuwa akiwaombea watu wa Efeso kwamba Mungu awafanye imara katika imani lakini anabaki kuweka msingi na shina la yote liwe ni Upendo baada ya yote. Na ndio maana upendo ni kifungo cha ukamilifu maana hakuna unachoweza kukifanya kwa mafanikio makubwa pasipo Upendo. Unataka kuwa Imara lazima ujijenge katika Upendo lasivyo utafanya vitu vingi kwa kuigiza kitu ambacho hakitampendeza Mungu hata kidogo. Hii unaweza ukaona hapa πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Wakolosai 3:14 "Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu."


3. Namna ya kuingia ndani ya Yesu kristo
■ Haiwezekani kuweza kuelewa kiundani zaidi juu ya kukaa imara ndani ya Yesu kristo kama hutajua kwanza namna gani mtu anaweza kuwa ndani ya Yesu kristo. Hili somo ni kwa mtu yeyote ambaye amempokea Yesu kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake ndio litamfaa tena litamjenga.
■ Njia pekee ambayo mwanadamu anaweza kukaa ndani ya Yesu kristo ni WOKOVU PEKE YAKE

Yohana 1:12 "Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;"

Sasa hapa tunamuona Yohana akizungumza na kanisa juu ya uwana au kitendo cha kuchukua mwana asiyekuwa wako kuwa wako kwa minajili ya kumkubali yeye. Sasa kwa mtu yeyote ambaye anamkubali Yesu kristo kwa kumuamini moja kwa moja anakuwa mtoto wa Mungu huku watu wasioamini wanabaki kuwa Wana wa Mungu pekee maana yeye ndiye aliye waumba wote. Sasa huku kuamini huja kwa msingi huuπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Warumi 10:9-10 "Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu."

Sasa huu wokovu ambao mwanadamu anakuwa ameshaupata ndio ambao sasa unamfanya huyu mtu aweze kukaa ndani ya Yesu kristo. Pia kwasababu hiyo ndio maana hata paulo anaeleza ya kwamba πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Warumi 1:16 "Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia."

Katika kujifunza ujio wa Yesu kristo kwenye maisha yetu lazima tujue ya kwamba alikuja kuleta ufalme wa Mungu kwenye maisha yetu na ndio maana hata yohana mbatizaji aliwaambia watu kwa habari ya Toba ili waweze kuupokea huo ufalmeπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Mathayo 3:1-2 "Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia." 

Huu ufalme wa Mungu ulioletwa na Yesu ulileta mamlaka na utawala wa Ki Mungu Duniani ambapo na sisi kama watu tulio amini tuna haki ya kiurithi katika ufalme kama wana wa ufalme. Sasa ninapokuwa na Yesu ninapewa tabia za kifalme na yeye ambazo zinanifanya niendelee kuwa na haki ya kiurithi na Endapo sita zifuata hizo haki zangu naweza kuzipoteza. Hii ni sawa na Esau alivyouza haki yake ya uzaliwa wa kwanza kwa yakobo kwasababu ya kutokujielewa kwake.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Mwanzo 25:29-34 "Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja kutoka nyikani, naye alikuwa amechoka sana. Esau akamwambia Yakobo, Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo walimwita jina lake Edomu. Yakobo akamwambia, Kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza. Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu kufa, itanifaa nini haki hii ya uzazi? Yakobo akamwambia, Uniapie kwanza. Naye akamwapia, akamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza. Yakobo akampa Esau mkate na chakula cha dengu, naye akala, akanywa, kisha akaondoka, akaenda zake. Hivyo Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza."

Kupitia kiapo cha Esau alichokifanya kilimfanya apoteze ila haki yake ya uzaliwa wa kwanza pamoja na urithi ambao alipaswa kuwa nao kama mtoto wa kwanza. Sasa ukiangalia sio Esau tu hata waamini wengi wamepoteza haki zao kama wato wa kifalme kwa namna ya matendo yao wanayoishiπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Waefeso 2:1-3 "Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine."

Paulo anaonyesha ya kwamba watu wanakuwa wafu kwasababu ya kuenenda kwa namna Dunia inavyofanya ambapo hapo sasa anakuwa anafuata tamaa za mwili na mambo yote machafu, kwahiyo kupitia hayo matendo mabaya yasiyompendeza Mungu unakosa haki ya uhai wako kama mwana wa ufalme na zile haki zako za urithi kama mwana zinapotea na ndio maana imetupasa sisi kuyaishi matendo ya Mungu ili tuwe haiπŸ‘‡πŸ‘‡

Matendo ya Mitume 17:28 "Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake."

Mwana wa Mungu usikubali kuipoteza haki yako kwa kutenda mambo ya mwili bali jitunze ili Mungu ajitwalie utukufu kupitia wewe. Lazima ifike hatua ubadilishwe utu wako wa ndani kabisa ili usiende kama watu wa ulimwengu waendavyo huku haki yako ya kifalme kama mwana ikiwa bado imekaa kwako.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Warumi 12:1-2 "Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu."

Mungu akubariki kwa kuwa nami mpaka hapa toka tulipoanza. Nimeona ni vyema kufupisha somo ili tuende nalo taratibu. Tutaendelea sehemu ya pili panapo neema ya Mungu tutaenda kiundani kuangalia sasa nini maana halisi ya kuwa ndani ya kristo Yesu na mengineyo Mengi.

Ukiwa una swali au jambo waweza kuniuliza kupitia simu yangu ya mkononi 

Ulikuwa nami mtumishi katika kristo Yesu 
Jina: Bro Jackobo
Namba: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

KUUTUNZA WOKOVU (Sehemu ya Tatu-Final)


Bro Jackobo


Utakuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo 
Jackobombwaga@gmail.com 
+255766944441

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu?? Ni neema ya Mungu kwamba hatuangamii maana Rehema zake ni mpya kila inapoitwa leo na neema yake inatujazia Pendo linalotuhakikishia huruma zake kwenye maisha yetu kila inapoitwa leo.

Karibu tumalizie sehemu hii ya mwisho ya somo letu juu ya kuutunza wokovu na kama hukupata au kubahatika kusoma sehemu ya kwanza na sehemu ya pili. Naomba nikupe link hapo chini.


Bonyeza hapa SEHEMU YA KWANZA na SEHEMU YA PILI kama haukusoma sehemu ya mwanzo ili twende kwa pamoja.

Vipengele muhimu vya somo vilikuwa kama ifuatavyo
1. Utangulizi wa Somo
2. Maana ya wokovu katika mitazamo mbalimbali namna biblia imeeleza
3. Mambo ya msingi katika kupata wokovu
4. Kujibu dhana ya mwanadamu kuweza kuokoka akiwa bado yupo Duniani na sio baada ya kufa
5. Kweli kuu juu ya uhusiano wa matendo na wokovu
6. Mambo yanayo imarisha wokovu
7. Mambo yanayo dhohofisha wokovu

Sehemu ya kwanza na ya pili imechukua kipengele cha kwanza mpaka cha nne. Naomba tuendelee sasa na vipengele hivi vitatu vilivyobaki

5. KWELI KUU JUU YA UHUSIANO WA MATENDO NA WOKOVU.
Kumekuwa na Imani zinazoendelea kusambaa zinazo amini juu ya kuokoka huku wakiiweka mbali nafasi ya matendo kwenye maisha yao wakizani kwamba kuokoka hakuna athari katika matendo ya mwamini. Naomba ambatana nami tena

Matendo ni jumla ya mambo yote ambayo mwanadamu anakuwa anayafanya pindi anapokuwa yuko hai. Sasa ikiwa unapozungumzia swala la ujumla wa mambo yote mwanadamu anayafanya hapo unakuwa unazungumzia mfumo wa maisha wa mtu wa kila siku pindi anapoendelea kuwepo hapa Duniani.

Sasa zifuatazo ni baadhi ya kweli kuu zinazohusisha matendo pamoja na wokovu

Kweli ya kwanza: HAKUNA MWANADAMU AMBAYE ANAWEZA KUOKOKA KWASABABU YA MATENDO YAKE MWENYEWE.

Waefeso 2:8-10 (KJV) Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
 Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.

Kwahiyo matendo yako hayawezi kukufanya ukaokoka maana anayeleta wokovu ni Yesu kristo kwasababu ya Upendo wake maana sisi toka asili pale lilipotokea anguko mwanadamu alipoteza utukufu wa Mungu kwa kuwa tayari ametenda dhambi

Warumi 3:23-25 (KJV) kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;
 ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake,ili aonyeshe haki yake ,kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilzotangulia kufanywa.

Kwahiyo pale ambapo mtu anaanza kuipata neema ya wokovu sio kwasababu kafanya kitu ila Mungu pendo lake tu kwetu.

Kweli ya pili: MATENDO YAKO HAYAWEZI KUKUOKOA ILA YANA UWEZO WA KUKUFANYA UKASTAWI AU KUDIDIMIZA WOKOVU WAKO PINDI UNAPOKUWA UNAENDELEA KUISHI
Tumeona hapo mwanzo kwamba matendo yako hayana nafasi ya kukufanya wewe ukaokoka ila baada ya kuokoka unaweza ukastawishwa au kudidimizwa kwenye wokovu wako unapokuwa uko chini ya Mbingu hapa Duniani. Kwahiyo unapookolewa kuna tabia ya matendo ya kiungu ambayo lazima yazaliwe kwako kiufupi kwamba lazima Tunda la Roho mtakatifu lazima lijizihirishe kwako.

Kweli ya Tatu: MWANADAMU ALIUMBWA TANGU ASILI AISHI MATENDO MEMA SIKU ZOTE
Kama Mungu alituumba tuweze kuishi matendo mema kwenye maisha yetu (Waefeso 2:8-10) kwahiyo huo ndio mfumo wa maisha ambao tunapaswa kuishi (Matendo) kwahiyo matendo mema ndio tunatakiwa kuwa nayo. Kwahiyo aliyeokoka lazima matendo mema yawe sehemu ya maisha yake.

Kweli ya nne:  MATENDO MABAYA HUWA YANAFARAKANISHA UHUSIANO MZURI WA MWANADAMU AU MWAMINI NA MUNGU WAKE.

Isaya 59:1-2 (KJV) Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;
 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.

Zaburi 51:11 (KJV) Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.

Ukisoma Fungu la Isaya unaona moja kwa moja kwamba pale unafanya mambo mabaya unapoteza uhusiano wako na Mungu na kumfanya Mungu aufiche uso wake na ndio maana hata Daudi alipokuwa amefanya dhambi akakumbuka kwamba makosa yake yatamfanya Mungu ajitenge naye na hii pia ndio maana hata Yesu pale msalabani aliomba akisema Baba mbona umeniacha, hii ilikuja kwakuwa amebeba dhambi za mwanadamu ndio maana Mungu alikuwa yuko mbali kageuza uso wake. Kwahiyo ukiokoka kweli huwezi enda kwa matendo maovu na kama unaenda hapo kuna haja ya wewe kukaa zaidi kwa neno ili uhuishwe nafsi yako.

Kweli ya Tano: IMANI HUKAMILISHWA KWA MATENDO IJAPOKUWA HAIANZI KWA MATENDO YA MTU AWAYE YEYOTE.

Mathayo 11:28-30 (KJV) Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.

Ukisoma hapo unaona Yesu anatoa mwaliko wa watu kuja kwao wakiwa na mizigo (Tabia/matendo yasiyo haki) anasema kwamba atawapumnzisha yaani atawaondolea na baadaye atawapa tabia njema ndani yao( Mzigo wake ni mwepesi yaani tabia au matendo yake ni mepesi kwa kuwa hakuna atakaye kushutumu kwa kuyafanya hayo). Ukiwa uko makini utagundua kumbe unapoondolewa tabia unapewa tabia nyingine kwahiyo hakuna uwezo wa kuondoka tabia pasina kuwepo na tabia nyingine iliyoingia ndani ya mtu.

Yakobo 2:14-17 (KJV) Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa?
 Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki,
 na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini?
 Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.
(Soma Yakobo 2:14-26)

Ukisoma hapo maandiko yanasema wazi kabisa kwamba Imani na matendo huwezi kutenganisha na kama Kuupata wokovu lazima uwe na Imani kwahiyo wokovu pamoja na matendo havitengani hata kidogo kwahiyo utapokea bila matendo ila utakamilisha kwa njia ya matendo kwenye maisha yako ya kila siku. 

Kweli ya Sita: Ikiwa Imani pasina matendo imekufa basi KUAMINI PASIPO KUYAAMINI MATENDO YA KUAMINI KWAKO NI KAZI BURE.
Haijalishi wewe ni nani lakini matendo ya kuamini kwako sio sehemu ya maisha yako kiufupi bado kuna eneo unatakiwa kuhuishwa ili utengenezewe maisha ya Kiungu yaliyo kamili kwenye maisha yako. Ndio maaana hata kumpenda Mungu kumefungwa kwenye kuyaishi mapenzi ya Mungu na sio katika kunena mambo ya Mungu peke yake.

1 Yohana 5:3 (KJV) Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.
 
Kwahiyo: Hakuna ukamilifu wa wokovu tunaoweza kuuishi tulio upokea kwa njiaa ya Imani pasina kumaliza kumuishia Mungu kwenye maisha yetu.


6. MAMBO AMBAYO HUIMARISHA WOKOVU WA MWAMINI NA KUUFANYA UWE HAI
Tunaokolewa kwa neema kabisa lakini kama hatuta fuata yale Mungu anataka thamani ya wokovu wetu hainakuwa na maana yeyote kwenye maisha yetu.

A). Maisha ya Ibada
Kabla sijaelezea hii pointi naomba nitoe maana ya Ibada.
Neno "Ibada" limetokana na neno la kigiriki "Proskuneo" lenye maana ya "Kuanguka mpaka chini mbele za Mungu au kitu chenye thamani ya hali ya juu kuliko vyote" . Kwahiyo kwenye eneo hili lazima uwe mtu na ile hali ya ndani kabisa ya kushuka na kunyenyekea mbele za Mungu wako na sio katika mwili na hii ndio maana hasa kwa Dini ya Kiislamu huwa Ibada yao imekaa katika mfumo wa kushuka chini kwa kupiga goti na kusujudu mbele ya Mungu wao ambapo hata kwetu inatakiwa kuwa hivyo ikiwa kwanza imeanza Rohoni na kutoka nje kwa mwitikio wa mwili ambapo unaweza kujidhihirisha kwa kupiga magoti, kusujudu, kuinua mikono mbele zake, kutokwa machozi, kulala chini n.k pasina kuangalia heshima yako uliyo nayo kwa jamii inayokuzunguka katika mazingiara unayoishi. Kwahiyo unaweza ukaelezea Ibada kama

Ibada ni tendo la heshima ya hali ya juu litolewalo na mtu mbele ya Mungu wake au kwa kitu kinacho hesabiwa kuwa kama Mungu siku zote za maisha yake.

Yohana 4:23-24 (KJV) Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

Ukisoma hapo juu unaona kwamba Yesu anaeleza umuhimu wa yule mwanamke kuabudu katika Roho na kweli maana hicho ndicho kina cha Ibada na sio katika mlima ambapo yule mwanamke alijua na alisimuliwa na wazazi wake kwamba wanapaswa kuabudu huko. Sasa maisha ha Ibada lazima yatokee ndani kabisa ili huyu mtu aweze kumpa Mungu heshima ya hali ya juu sana kuliko kitu chochote. Hii ndio maana kila siku tunahimizana kukutana kwa pamoja kila inapoitwa leo kwenye maisha yetu ya kila siku.

Waebrania 10:25 (KJV)   wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.

Kwahiyo mtu anapokuwa mtu wa Ibada anakuwa yuko karibu na Mungu kiasi kwamba thamani yake katika wokovu inakuwa ina maana na sio  tu kwa kunena. Hii inapaswa kuwa tabia ya kila siku ya mtu pindi anapokuwa anaishi hapa Duniani na sio swala la siku moja yani uwe mfumo wake wa maisha ya kila siku.


B). Kulishika neno na kulitafakari kila siku

Yoshua 1:8 (KJV) Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.

Mungu alisema na Yoshua ili aweze kustawi lazima aishi kwa kulijua au kuijua sheria ya Mungu na kupata nafasi ya kutafakari kwnye maisha yake ya kila siku. Ndivyo ambavyo na sisi tutaweza kustawi ikiwa tutakuwa watu ambao tunakaa kwenye neno la Mungu na kuwa na mda wa kulitafakari wakati wote wa maisha yetu na hii inapaswa iwe tabia yetu ya kila siku kila inapoitwa leo kwa usalama wa Roho zetu.

C). Maisha ya maombi
Kwa mwanadamu yeyote lazima awe mtu wa maombi kwakuwa "Maombi" ni "Mawasiliano ya moja kwa moja kati ya mwanadamu na Mungu".  Na hii ni muhimu sana kwakuwa ili kuutunza wokovu uliopewa lazima upewe maelekezo na Mungu mwenyewe ndio maana kuna ufunuo ambao huwa kila mtu ambaye ameokoka anatakiwa kuupata ili aende kwa ujasiri kwenye maisha yake. Mfano Mungu alijifunua kwa Musa kama "NIKO" lakini sio kwa wote alijifunua hivyo wengine kajifunua kama ELOHIMU, wengine ADONAI n.k. ndio maana lazima uwe mtu wa kuwasiliana na Mungu ndio maana maandiko yanasema kwamba.

1 Wathesalonike 5:17 (KJV) "ombeni bila kukoma;"
Mathayo 17:21 (KJV)   [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]

D). Kujazwa na Roho mtakatifu
 Kwa mwamini yeyote lazima ajazwe na Roho mtakatifu kwa kuwa kupitia Roho mtakatifu huwa tunapewa Nguvu za kuweza kustahimili kwenye wokovu pamoja na kuwa mashahidi wake katika maeneo mbalimbali katika ulimwengu huu.

Matendo ya Mitume 1:8 (KJV) Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

Pia huwa Roho mtakatifu ni msaidizi wa mambo mengi hata kuweza kuomba ambako kuna muelekea Mungu maana sisi tunaweza kuomba lakini hatujui namna ya kuomba namna ambavyo inatakiwa tuombe ila Roho mtakatifu ndiye anajua namna tunapaswa kuomba kwenye maisha yetu.

Warumi 8:26 (KJV) Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

E). Toba ya kweli
Toba ni neno lenye maana ya "Kugeuka kunako ambatana na kubadilisha mawazo au mtazamo wako". Kwahiyo mtu anapokuwa amakubali kuupokea wokovu lazima awe amebadili mtazamo wake amuelekee Mungu katika kweli yote toka ndani ya moyo wake na sio tu kwa kinywa chake.

Matendo ya Mitume 3:19 (KJV) Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;

Mathayo 3:8-9 (KJV)   Basi zaeni matunda yapasayo toba; wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto.

Mathayo 4:17 (KJV) Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.

Ukisoma maandiko ya hapo juu unaona yaneleza kuwataka watu wabadilishe mtazamo ili waweze kusamehewa dhambi zao kwenye maisha yao ya kila siku maana msamaha kwanza huanza na kubadilika kwa mtazamo wa mtu unaopatikana kupitia neno la Mungu kwenye maisha yake ya kila siku.


7. MAMBO YANAYO DHOOFISHA WOKOVU KWA MWAMINI MBELE ZA MUNGU 
Kuna mwenendo na Tabia ambazo mwamini anapokuwa yuko nazo kwenye maisha yake hufanya aweze kufarakanisha mahusiano yake na Mungu ambayo hayo ina paswa huyu mwamini kuweza kuyaepuka siku zote za maisha ya kila siku.

A). Kuruhusu Dhambi itawale Maisha Yake
DHAMBI imetokana na neno la kigiriki "Hamartia" ambalo lina maana ya " kukosea katika kulenga shabaha" ambapo mtu anakuwa anafanya jambo pasipokuwa na usahihi wa aina yeyote kulingana na namna ambavyo ilipaswa kufanyika kwa kiwango stahiki. 
Pia ukisoma Biblia inakuonyesha kwamba 
1 Yohana 3:4 (KJV) Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.
Kwahiyo pale ambapo unakataa kufuata maelekezo ya Mungu unakuwa unafanya uasi kwahiyo kiufupi unatenda dhambi hii ndiyo inatutengenezea namna ya kwenda sawasawa na neno la Mungu kwenye maisha yetu ya kila siku.

Kama ambavyo tumeona kwenye Isaya 59:1-3 kwamba dhambi ina tabia ya kuleta faraka kwenye maisha kwahiyo lazima tuepukane nayo kwa namna yeyote kwa kujinyenyekeza mbele za Mungu siku zote ili 

B). Kufuata mafundisho potofu
Watu wengi wamekuwa wanafuata mafundisho yanayo danganya ambayo ni kama yamejikita kwa neno la Mungu lakini yanakana uhalisia wa Mungu pamoja na neema yake ambayo amekwisha kuiacha.

1 Timotheo 4:1-4 (KJV) Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.
 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;

Ikiwa nyakati za mwisho zitakuwa za hatari watu watakuwa wakidanganywa basi ili wewe usidanganywe lazima katika maisha yako uwe na neno la Mungu pia Uwe tayari kuongozwa na neno la Mungu siku zote wala usiogope.

Zaburi 119:9-11, 105 (KJV) Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.
 Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako.
 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.
 Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.

C). Kuanguka kwa sababu ya majaribu na shughuli mbalimbali za maisha
Changamoto za maisha  pamoja na majaribu huwa wengine vinawafanya watu  wengi wakatoka nje ya msitari wa Mungu kwa kutokufuata maelekezo ua Mungu maana mioyo jao inakuwa ni migumu kiasi kwamba haiwezi kustahimili kuutunza ule wokovu wa Mungu ambao amepewa kwenye maisha yake ya kila siku.

Luka 8:11, 14 (KJV) Na huo mfano, maana yake ni hii; Mbegu ni neno la Mungu.
 Na zilizoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lo lote.

Sasa hapo mtu anaweza kulisikia neno la Mungu na kuamini akaupokea wokovu kwenye maisha yake ya kila siku lakini ikiwa huyu mtu shughuli za maisha zikamzidia basi huwa anaweza kupoteza kile ambacho Mungu amempatia kwa maisha yake. Hii ndio msingi ambapo Mungu anazungumzia suala la kushika sana ulicho nacho maana kama hautakishika vizuri yupo ambaye anaweza kukiiba kwenye maisha yako.

Ufunuo wa Yohana 3:10-11 (KJV) Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.
 Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.

Katika misongo yote ya maisha haijalishi ni majaribu yanayokuja kwako, hayo yote yasikufanye wewe ukamuacha Mungu kwa maisha yako maana hayo yote wewe unayaweza maana Mungu huruhusu majaribu yaje ambayo yako katika Imani maana Mjngu hawezi kuruhusu jaribu linalo kuzidi kwahiyo jua hata hilo una uwezo wa kulibeba kabisa. Usimuache Mungu wako hata tone yako ya mwisho ya Damu ikutoke. 

1 Wakorintho 10:13 (KJV) Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.

Kwahiyo hata hilo unaliweza ndio maana Mungu ameliacha lije kwako yeye anajua namna ya kukuokoa katika hilo ndio maana usalama wako ni katika kumjishia Mungu kwa maisha yako. 

2 Petro 2:9 (KJV) basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu;

Mungu anajua namna gani anaweza kukuokoa kwenye jaribu lako hilo ambalo linakusumbua wewe usiache wokovu mshikilie tu Mungu atakupa neema ya kushinda hakika. Wala huna haja ya kuogopa kwenye maisha yako.

Mungu akubariki kwa kuambatana nami kwenye somo hili tangu tumeanza sehemu ya kwanza mpaka tunamalizia sehemu hii ya mwisho ya tatu. Unaweza ukawashirikisha wengine neema hii Mungu kaiachilia kwangu kwa ajili ya kanisa lake la kizazi hiki


Ulikuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo 
Jackobombwaga@gmail.com 
+255766944441

KUUTUNZA WOKOVU (SEHEMU YA PILI)


Bro Jackobo

Utakuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
+255766944441
jackobombwaga@gmail.com 

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu? Mungu akubariki kwa kuwa pamoja tena kwenye sehemu ya pili ya somo letu juu ya KUUTUNZA WOKOVU. 

Kama haukufanikiwa kuipata au kusoma sehemu ya kwanza unaweza kubonyeza hapa ukasoma SEHEMU YA KWANZA. Ukisoma hiyo sehemu ya kwanza itakurahisishia kuelewa mtiririko wa Somo namna linaenda.

Sehemu ya kwanza tuliona utangulizi wa Somo letu na kuangalia namna unavyoelezewa huu wokovu kwamba ni kitu gani kwa msingi wa maandiko. Kwa kadri ambapo kiufupi tuliona kwamba Wokovu unaletwa na Mungu mwenyewe pasina ushawishi wa mwanadamu na mwanadamu yeye anafanya kuupokea huu wokovu. Basi embu tuendelee kipengele cha Tatu cha mfululizo wa Somo letu.

3. MAMBO YA MSINGI KATIKA KUUPATA WOKOVU
Tunapoendelea kujifunza naomba turudi kwenye andiko hili kwanza hapa

Yohana 3:16-17 (KJV) Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.

Ukisoma hapo andiko linaonyesha kwamba Mungu kwasababu ya Upendo ndio aliamua kumtoa mtoto wake wa pekee ambapo sasa huyo mtoto wake wa pekee kazi yake ilikuwa ni kuuleta wokovu kwa kila anaye amini maana yeye ulikuwa ndio wokovu pekee maana Damu za kondoo na wanyama wengine hazikuweza kuondoa dhambi ya mwanadamu bali zilizifunika Dhambi ambapo kila mwaka ilimpasa kuhani kupaingia patakatifu pa patakatifu afukize uvumba ili kufunika dhambi za wana wa Israel.

Waebrania 10:1-4 (KJV) Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.
 Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi?
 Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka.
 Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.

Ukisoma hapo juu unaona ambavyo dhabihu zote zilikuwa bado zina kumbukumbu la dhambi ndio maana sasa Mungu kwa Upendo wake aliona kwamba sio vyema sasa huyu mtu abaki kuwa na kumbukumbu la dhambi akataka sasa kumfanya huyu mtu aweze kuwa huru mbali na dhambi zote akiwa na lengo la kumfanya mwanadamu kuwa mtakatifu asiyekuwa na mawaa ya aina yeyote kama ambavyo alikuwa amemuumba hapo mwanzo akiwa ni mtakatifj kamili kama ambavyo yuko Mungu mwenyewe.

Sasa ukiwa umeambatana na mimi toka sehemu ya kwanza mpaka hapa utaona ya kwamba kuna mambo makuu mawili yanayoleta wokovu na kuwa kamili kwa mwanadamu ambayo ni
  1. Neno la Mungu
  2. Imani
A. NENO LA MUNGU
Neno la Mungu ni mbegu ambayo hiyo hupandwa kwa mwamini na kumpatia ufahamu na uelewa juu ya kile ambacho Mungu anakuwa amekikusudia kwa ajili yake.

Luka 8:11 (KJV) Na huo mfano, maana yake ni hii; Mbegu ni neno la Mungu. (Soma kuanzia msitari wa 4-15) 

Ukiangalia huo mfano utaona namna Yesu anajaribu kuwaelekeza wanafunzi wake namna ya uwezo wa mbegu kuweza kuleta matokeo ambapo ili kuleta matokeo kunategemea na mpokeaji namna ambavyo yeye yuko ambapo nitaidadavua vizuri kwenye kipengele cha Imani. Kwamba mbegu inakuwa haina shida kuleta matokeo isipokuwa huyu mtu ambaye anatakiwa kupata mabadiliko ndio itabaki kwenye utashi wake kuweza kuamua kukubali mabadiliko au la.

Sasa ukisoma kiundani zaidi utaona unapolizungumzia Neno la Mungu unakuwa moja kwa moja unamzungumzia Yesu kristo.

Yohana 1:1-5 (KJV) 
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.


Yohana 1:14 (KJV) Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

Ukisoma vifungu hivyo viwili unaona mojaa kwa moja kwamba huyo neno alikuwa kwa Mungu na alikuwa Mungu na alifanyika mwili ambapo hapo unakuwa unamzungumzia Mungu katika nafsi mwana katika utendaji wake kwenye utatu mtakatifu wake. Sasa Huyu neno ndiye ambaye analeta Nuru au mwangaza kiasi kwamba huyu mwanadamu anaweza kujua uhalisia wa Mungu katika uzuri wake wote maana humfunua Mungu. Pale anapokuwa anafunuliwa Mungu tunakuja kuuona Upendo wa Baba namna anafanya kujitoa mwenyewe ili sisi tuweze sasa kuokolewa. Kama Mungu asingejitoa kwetu na tukaona namna ambavyo Neno la Mungu linaweza kuleta matokeo kwenye maisha Yetu ambapo tokeo kubwa ni kutupatia wokovu.

Sasa pasipokuwa na neno la Mungu (Yesu kristo) hakuna mtu yeyote anaweza kuokoka maana tena Jina la yesu ndilo ambalo sisi wanadamj tunapaswa kuokolewa kwalo na hakuna jina lingine lenye uwezo wa kutupatia wokovu.

Matendo ya Mitume 4:12 (KJV) Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.

Ukisoma toka msitari wa kwanza wa sura hii ya nne utaona namna ambavyo mafarisayo walikuwa wakilalamika kwamba wasieleze habari zozote kupitia jina la Yesu na baadaye Petro akiwa amejaa Roho mtakatifu anakuja kuwaambia kwamba hakuna wokovu unaweza kupatikana nje ya Yesu na hakuna Jjna zaidi ya Yesu ambalo mwanadamu anaweza kuokolewa kwalo. Kwahiyo pasina kuwa na neno la Mungu hakuna wokovu wa aina yeyote unaoweza kupatikana.


B. IMANI
Ukirejea andiko letu tuliloanza nalo kwenye kipengele hiki cha pili (Yohana 3:16) utaona kuna jambo linaelezewa kwamba  aaminiye ataokoka (Tendo hili ndilo linaleta IMANI). Kwahiyo moja wapo ya vitu vya msingi katika kuupata wokovu ni kupitia Imani ambayo hii inatoka kwa mwanadamu. Basi kabla hatujaenda mbali naomba tuangalie Imani ni kitu gani sasa.

Maana ya Imani kulingana na maandiko yanavyosema

■  IMANI ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana(Waebrania 11:1)

Ukisoma hilo fungu linakuletea moja kwa moja maana ya Imani ambayo hiyo tumekuwa tunaambiwa kila inapoitwa leo. Kwahiyo Imani lazima ijengwe katika uhakika ambapo mtu anakuwa haoni katika mazingira ya kawaida bali anajua hii itakuwa kama hivi. Kiufupi ni kuwa na taraja la uhakika. Kwahiyo mtu inatakiwa awe na uhakika kwamba pale anapomkiri Yesu anapata moja kwa moja wokovu pasipo hivyo haiwezekani kuwa na huo wokovu.

■ IMANI ni hali ya ndani kwenye eneo la nafsi ya mtu au mwamini kuweza kupokea kile ambacho Mungu amekileta kwa ajili ya usalama wa Roho yake.

Warumi 10:17 (KJV) Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

Kwahiyo Hakuna kuamini pasipokuwa na taarifa mwanzo ndio maana Sehemu ya akili kwenye Nafsi ya mtu lazima ipokee taarifa juu ya wokovu ambao huo unakuja kupitia neno la Mungu. 

Kwahiyo Imani huwa inakuwa ni mwitikio wa mwanadamu juu ya kile Mungu anataka kufanya kwenye maisha yake mwenyewe. Kwahiyo sisi lazima nafsi zetu ziitikie kuwa kuna jambo la kupewa wokovu pasina kulazimishwa na mtu yeyote. 

Hapa lazima utashi wa mwanadamu(Sehemu ya nafsi) uamue kukubaliana na taarifa za kukombolewa. Moja wapo ya kitu cha thamani na kitu hatari Mungu kampatia mwanadamu ni UTASHI. Ni kitu cha thamani kwakuwa kinampa mwanadamu kuamua atakavyo kama  Mungu anavyoweza kuamua lakini ni hatari kwakuwa pia unaweza kuamua kufuata mapenzi yako nje na mapenzi ya Mungu yaani unaweza kuamua kinyume na Mungu.

Kwahiyo Suala la kuamini ni suala liko kwenye uwezo wa mwanadamu kuweza kukubali au kukataa ila Roho mtakatifu anakuwa anatoa ushauri tu wa vitu unapaswa kufanya kwa wakati fulani. 

■ IMANI ni kuwa na tumaini kamili liletalo uaminifu na kujitolea


Tumaini ni taraja analokuwa nalo mtu juu ya jambo fulani kwamba litakuja kutokea. Sasa hili taraja lazima lisiwe na shaka ya aina yeyote ndipo linakuja kuwa imani ambalo hili linakuja kumjenga mtu katika kufanya kwa uadilifu kamili (Utakatifu usiokuwa na mawaa ya aina yeyote) na huyu mtu anakuwa yuko tayari kufanya kwa ajili ya Mungu (kujitoa).

Habakuki 2:4 (KJV) Tazama, roho yake hujivuna, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake.

Waebrania 10:38-39 (KJV) Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.
 Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.


Habakuki alikuwa analia akiwa anaona maovu yanaongezeka na Mungu bado haonyeshi kufanya lolote na Mungu anakuja kumjibu kuwa mwenye haki anaishi kwa Imani hata kama haoni kwa nje maana akisitasuta Mungu anakuwa hana furaha naye tena.

 Pia ukiangalia mwandishi wa Waebrania (Inasemekana ni Paulo japo haijawa wazi moja kwa moja) anajaribu kuonyesha na kuongea na kanisa kwamba lilipokuwa limempokea kristo kwanza lilistahimili sana baadaye anaona kama kuna namna hawaendi kama wenye haki anakuja wakumbusha sasa kuwa wataishi kwa Taraja kamili sasa maana wao wako miongoni mwa walio na imani ya kuokolewa Roho zao. Ndivyo ambavyo iko kwamba huwezi kuokolewa pasina kuwa na Imani hata siku moja kwahiyo lazima sasa nawewe nafsi yako ikubaliana na wokovu unaoletewa na Mungu.

Kwahiyo NENO LA MUNGU huleta wokovu huku IMANI ni mkono wa kuupokelea huu wokovu ambao unaletewa na Mungu ambapo ukikiacha kimoja wapo kati ya hivi viwili haviwezi kuwa na ukamilifu wa aina yeyote kwahiyo na wewe uwe na utayari hata kama umepewa bure haina maana hakuna utayari unaotakiwa kuwa nao.

Note 1: Wokovu ni mkono wa Mungu wa kuleta usalama kwa mwanadamu ikiwa ni 
  1. Kusamehewa dhambi, 
  2. Kuhesabiwa haki na 
  3. kupewa utakatifu

Note 2: Imani huu ni mkono wa mwanadamu wa kupokelea mambo makuu matatu ya usalama kutoks kwa Mungu ambayo ni
  1. Kusamehewa Dhambi 
  2. Kuhesabiwa haki
  3.  Kupokea haki

4. MWANADAMU ANAWEZA KUOKOKA TU PINDI AKIWA YUKO HAI NA SIO BAADA YA KUFA.
Kumekuwa na dhana ambapo watu hawaamini kuwa kuna uwezo wa watu kuokoka akiwa yuko hapa Duniani wakiwa wanaamini tu kwamba mtu huwa anaongoka tu na anakuja kuokoka baada ya kufa.

Kabla ya yote labda tuangalie maana ya KUONGOKA na tutaangalia uhusiano wa KUONGOKA na KUOKOKA.

KUONGOKA hii ni hali ya mtu kugeuka kuelekea kwenye uthabiti kwenye Imani pasipo kupeperushwa na Upepo mbalimbali au mafundisho yanayokuja kwenye kipindi cha maisha.

Luka 22:31-32 (KJV) 
 Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano;
 lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako.
Ukisoma andiko hapo juu linajaribu kutupa mwongozo wa kuongoka ukoje ambapo sasa ukiangalia Yesu anamuambia petro kuwa atapitia nyakati ngumu lakini akisha kugeuka na kuwa kwenye Imani aliyowaachia basi awarejesha na wenzake. Kwahiyo kuongoka ni kugeuka katika uthabiti au uimara unaopaswa kuwa kama msingi wa neno.

Mathayo 18:3 (KJV) akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Yesu alikuwa anajaribu kuonyesha kwamba lazima mtu ageuke kama watoto maana hawa watoto wakiamua kukufuata huwa wanafanya katika kweli pasina kinyongo maana mioyo yao inakuwa haijatiwa sana na giza. Kwahiyo ukiongoka unakuwa umemgeukia Mungu wako.

1 Timotheo 3:6 (KJV) Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.
 Ukiangslia hapo Paulo anampa waraka Timotheo kuonyesha sifa za Askofu kwamba hapaswi kuwa mtu ambaye ameongoka hivi karibu yani hajageuka kuishi imani katika uthabiti akaja kunasa kwa mtego wa kujisifu maana bado atakuwa hajapata baadhi ya mambo ya msingi kuweza kuwa thabiti kwenye Imani.

Tumekwisha kuona sasa maana ya kuongoka ambapo hapo inakupa mwongozo kuwa ni suala la kuimarika katika uthabiti wa imani kwahiyo sisi tunaendelea kuongoka tukiwa katika Imani kwasababu kristo huwa anajifunua kwa kadri anavyotaka kiasi kwamba huwezi kujisifu kwamba nimeshakufika ndio maana hata paulo alisema kwamba

Wafilipi 3:12-14 (KJV) Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.
 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;
 nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.

Hili la kusema Duniani hakuna kuokoka huwa watu wanajenga msingi wao kwenye kifungu hiki hapa chini, ngoja tukichambue kidogo

Mathayo 10:22 (KJV) Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
(Soma pia Marko13:13, Mathayo 24:13)

Ukisoma hilo fungu hapo juu unaweza hitimisha kwamba kumbe wokovu au kuokoka ni pale mwisho wa safari ya mwanadamu lakini ukisoma kiundani utaweza kuelewa vizuri kabisa.

Hapo Yesu alikuwa akiwaambia wanafunzi wake juu ya nyakati ambazo zinawajia kwamba watapita katika moto lakini inawapasa kuvumilia isije ikatokea mtu kwasababu ya magumu anakuja kuikana Imani, hapa ndipo anakuja kueleza sasa matokeo ya kuikani Imani ndio hayo unakuwa umepoteza wokovu au usalama wako hapa ndipo pana msingi wa kwamba sasa hizi nyakati ukishakuwa thabiti (Ongoka) ndipo penye usalama wako. Sasa hili neno linazungumzia kuto kuikana Imani na kama wewe utaikana imani ni moja kwa moja wewe huwezi kumpendeza Mungu.

Waebrania 11:6 (KJV) Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

Sasa ukiona pasipokuwa na Imani haiwekani kumpendeza Mungu ina maana kwamba wewe una farakakanisha mahusiano yako wewe na Mungu wako

Kama ndiyo hivyo, kwanini sasa haiwezekani mtu kuokoka baada ya kufa??
Mtu anapokuwa amekufa kinachotokea ni kwamba Mwili na Roho vinatengana maana Roho inapomtoka mtu huwa inaondoka na Uzima wake ndio maana maandiko yanasema kwamba

Yohana 6:63 (KJV) Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
Kwahiyo pasina Roho hakuna uzima wa aina yeyote na kama hakuna uzima wa aina yeyote thamani ya mwanadamu inakuwa sasa haiko katika Mwili ule. Na mtu ili aweze kuokoka huanzia kwenye kuamini kwake pindi anapokuwa yuko katika mwili sasa akiwa amekufa atawezaje kuamini? Au atawezaje kulisikia neno la Mungu ili liweze kumbadilisha ingali hayupo katika mwili?? Sasa kama umefuatana nami vizuri utakuja kugundua kwamba huyu mtu aliyekufa anakuwa ameshapoteza sifa za kuweza kuokoka maana huyu mtu anakuwa hana hata uwezo wa kutubu. Ndio maana biblia inasema kwamba

Waebrania 9:27 (KJV) Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;

Ukisoma hapo unaona kwamba mtu anapokuwa ameshakufa kinachotokea mara moja ni kuhukumiwa na hapa kuhukumiwa ni kupewa haki yako kjlingana na namna ambavyo ulikuwa umeishi hapa duniani na sio vinginevyo  maana kila mtu atalipwa sawa sawa na matendo yake. Kwahiyo hakuna nafasi ya kuweza kutubu pindi mtu anapokuwa amekwisha kufa.

Pia hakuna mabadiliko yanaweza kutokea ikiwa hata mtu ataombewa Dua za kutosha ili Mungu amsamehe Dhambi zake alizofanya baada ya kufa. Mpendwa katika kristo Yesu usidanganyike kwamba eti mtu akifa anaweza kuombewa akabadilishiwa hatima ya kule alikokuwa anapaswa kwenda kwa kuombewa basi ingekuwa hivyo ilimpasa na kristo Yesu kuteswa mara mbili, mtu alishapewa msamaha wa dhambi tayari kazi yake ni kukubaliana na hilo pindi akiwa bado yu ngali ni mwenye uzima baada ya hapo utapewa kulinganisha na matendo yako.

Kwahiyo kuokoka ni hapahapa Duniani  na sio mbinguni kama wengine wanavyofikilia. Fanya uwezalo usikubali kufa kabla hujampokea Yesu kristo. Yesu yuko kazini bado anatafuta mtu aliyeko tayari aweze kumsamehe dhambi zake na kumpatia wokovu ulio jaa thamani isiyokuwa na mawaaa ya aina yeyote.

Note; Kwahiyo kuokoka ni suala la mwanzo kabisa ambalo mtu anapaswa kuwa nalo huku kila anapoendelea kuishi anaendelea kuongoka (kuwa thabiti katika Imani).

Neema ya wokovu bado imefunuliwa kwako kama hujampokea Yesu krusto kuwa Bwana na mwokozi wako wakati ni huu sasa wa kuweza kutengeneza maisha yako na Mungu ili aweze kukupatia usalama ulio jaa msamaha wa dhambi, kuhesabiwa haki pamoja na utakatifu. Unaweza kuwasiliana nami kwa njia ya mawasiliano yangu hapa chini kwa msaada na maswali na kujengana xaidi.

Naomba tukutane sehemu ya tatu ya mwendelezo wa somo letu pindi Mungu akitupatia kibali.

Ulikuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo 
+255766944441
jackobombwaga@gmail.com 


KUUTUNZA WOKOVU (SEHEMU YA KWANZA)


Bro Jackobo



Utakuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo 
+255766944441
jackobombwaga@gmail.com 

Bwana Yesu asifiwe watumishi wa Mungu?? Karibu tena katika Darasa ambalo Mungu kanipa neema ya kuweza kushiriki nanyi sehemu ya Mambo Mungu kanipa kuelewa kwa kiasi ili niweze kushiriki nanyi baraka hizi za Rohoni. Tutajifunza Juu ya kuutunza wokovu ambao Mungu ametupatia kupitia Yesu kristo.

Vipengele muhimu vya somo vitakuwa kama ifuatavyo
1. Utangulizi wa Somo
2. Maana ya wokovu katika mitazamo mbalimbali namna biblia imeeleza
3. Mambo ya msingi katika kupata wokovu
4. Kujibu dhana ya mwanadamu kuweza kuokoka akiwa bado yupo Duniani na sio baada ya kufa
5. Kweli kuu juu ya uhusiano wa matendo na wokovu
6. Mambo yanayo imarisha wokovu
7. Mambo yanayo dhohofisha wokovu

1. UTANGULIZI
Ashukuriwe Mungu ambaye siku zote anatufanyia mambo mengi kwenye maisha hata kama hatukusitahili ila anatustahilisha kuwa nayo na kuwa na uhalali kamili wa kuyamiliki hayo.
Mungu alipo muumba mwanadamu alimuweka bustani ya edeni kwa kupenda mwenyewe lakini hakuacha mwanadamu aweze kukaa peke yake bali alimpa na kampa aitunze kitu ambacho kinatupa ufunguo kwamba lolote Mungu anakupa kuna sehemu ya wewe kufanya hata kama umepewa bure.

Mwanzo 2:15
"BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza."

Pia ukiangalia hata maisha na uhai wetu Mungu ametupa hatuna sehemu ya kujiongezea uhai wetu ila Mungu ametupa maarifa ya namna nzuri ya kuhakikisha tunatunza afya zetu ndio maana kawapa wengine neema ya kuwa madakitari, wauguzi, wataalamu wa maabara n.k ili kuhakikisha kwamba afya zetu zinakuwa imara. Pia katoa baadhi ya mambo mtu anaweza akafanya ili asijikute afya yake ikawa inatahayarika mfano kufanya mazoezi, kula mlo kamili n.k. lakini mambo yote haya lazima yafanyike huku Mungu anakuongoza na kukutangulia maana kwa akili zako wewe huwezi ndio maana maandiko yanasema..

Zaburi 127:1
"BWANA asipoijenga nyumba waijengao wafanya kazi bure Bwana asipoulinda mji yeye aulindaye akesha bure"

Pia ukisoma hapa

Yuda 1:3
"Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu."

Ukisoma andiko la hapo Juu utaona Yuda alivyoandika waraka wake maana aliona kwamba wamepewa wokovu bure lakini haina maana kwamba ndio wakae hivi hivi akaamua kuwaandikia waweze kuelewa kwamba imewapasa kuishindania imani maana hata wokovu ni Tendo linalo kuja kwa imani. Pia aliandika hivyo kwasababu alijua kuwa kuna mafundisho mabaya ya kuwaharibu kama hawatasimama imara kuishindania imani. Kwahiyo hapo anatuonyesha umuhimu wa kutunza kile ambacho umepewa na Mungu.

Nimeandika haya yote kwasababu kuna watu wanao amini ya kwamba mtu akisha kuokoka hana jambo la kufanya kwakuwa Yesu kristo amekwisha kumaliza yote wanasahau kwamba Mungu anasema hivi..


Mathayo 11:28-30
"[28]Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. [29]Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; [30]kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi."

Yesu anaeleza kuwatua watu mizigo (Kuondoa tabia zisizostahiki kwa kumpa uwezo wa kuacha), tena anatoa wito wa mtu kwa utayari wake kujifunza kwake mwenyewe na sio kumlazimisha mtu (Hapa inaonyesha wazi kuna jambo la mwitikio kwa mwamini juu ya mambo ambayo Mungu anataka kukupea wewe kama mwamini, tena anamaliza kwamba kuna kazi ya kuubeba mzigo wake ulio mwepesi(Hapa anaonyesha tabia za haki ambazo mwamini anatakiwa kuwa nazo ambazo zinabaki katika uwezo wa mwanadamu yeye mwenyewe kuamua kumfuata au kuishi wema pasipo kulazimishwa). Kwahiyo Mungu anapofanya kwako kuna sehemu ya wewe kulinda kile Mungu amekupa.

2. MAANA YA WOKOVU KATIKA NAMNA MBALIMBALI AMBAZO BILBLIA IMEELEZEA.
Kumekuwa na dhana na Imani ambazo haziamini kwamba kuna kuokoka hapa Duniani zikiamini hakuna mwanadamu anaweza kuokoka akiwa Yupo hapa Duniani mpaka atakapokufa lakini katika msingi wa maandiko haijakaa sawa kwasababu biblia inaeleza wazi kwamba kuna uwezekano wa mtu kuokoka hata anapokuwa hapa Duniani.

Naomba tuangalie maana mbalimbali zenye mlengo mmoja katika kuelezea wokovu ni nini.

  • WOKOVU ni mpango wa Mungu kumtafuta mwanadamu ili kumrejesha huyu mwanadamu katika sehemu ambayo alikuwa amemuweka aweze kukaa katika asili yake.
Mwanzo 2:7-8
"[7]BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. [8]BWANA Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya."

Mungu alituumba tuweze kukaa bustani ya Edeni ambapo kulikuwa hakuna magonjwa wala tabu za aina yeyote yaani ilikuwa ni sehemu ya amani ya kujitosheleza. Sasa baada ya anguko la mwanadamu Mungu alimuondoa mahali pale kwakuwa tayari alikuwa ashaleta tabia ambazo hazikupaswa kuwepo pale.
Sasa Mungu alianza kumtafuta mwanadamu tangu pale alipoanguka ili amrejeshee utakatifu aliokuwa ameupoteza ns ndio maana huu mpango ulianza kwa kusurubisha Dhambi yaani kiufupi palipo na na dhambi kuna adhabu itokanayo na hiyo dhambi. Sasa Mungu kwa kumpenda mwanadamu ili amuokoe na ile adhabu aliamua kumuua mnyama ili ampe mwanadamu sitara yake kwakuwa alikuwa alishapoteza utukufu wa Mungu.

Mwanzo 3:21
["21]BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.

Hapa Mungu alifanya ili kumpa mwanadamu heshima kwasababu ya Upendo wake ambapo ni utabiri wa wokovu kwa mwanadamu na ndio maana aliwavisha mavazi ya ngozi ikiwa na maana kwamba kuna mnyama alikufa ili Adamu na Eva wapate sitara.

Waefeso 2:10 (KJV) Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.

Mungu alimuumba mwanadamu aweze kuishi maisha yaliyo jaa matendo mema ambapo hapo Mungu alipomuweka Adamu Edeni alikuwa amemuelekeza kuishi maisha yaliyo mema peke yakena sio vinginevyo. Sasa huu mpango wa kumuokoa unamfanya mtu aweze kurudi katika lile kusudi la Mungu la asili kuishi katika matendo mema peke yake.

Sasa uwezo wa kuishi matendo mema ulipotea pale mwanadamu alipokosea pale edeni

Mwanzo 2:16-17 (KJV) Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,
walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Sasa ukiona hilo neno hakika utakufa ndio hilo linaonyesha kuvunjika kwa ushirika uliojaa uwezesho wa kuweza kufanya mapenzi ya Mungu ndio maana sasa Mungu alimtuma sasa Yesu kristo ili aweze kuturudishia huo uwezo wa kuweza kuishi tukiwa tuko hai yani tukiwa tunafanya mapenzi ya Mungu.

  • Wokovu ni hali ya kuwekwa mbali na hatia na adhabu itokanayo na makosa ambayo mwanadamu ameyafanya na kupewa haki kwa kumuamini Yesu kristo.
Mahali popote panapokuwa na makosa lazima kuwepo na adhabu stahiki kwa kukosea  huko. Sasa ukija katika suala la wokovu ni kwamba Mungu anakuweka mbali kabisa na makosa  kwakuwa umemuamini Yesu kristo.

Warumi 3:23-25 (KJV) kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;
 ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake,ili aonyeshe haki yake ,kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilzotangulia kufanywa.

Ukiangalia andiko hapo juu linaonyesha kiuhalisia mwanadamu hana haki mbele za Mungu maana kafanya dhambi ila haiishii hapo inakuja kutoa maelekezo kwamba kuna kuhesabiwa haki kupitia kuamini ukombozi wake unaopatikana kupitia Yesu kristo maana yeye anatukomboa kutoka kwa shetani kwa kutupatanisha na Mungu kupitia Damu yake mwenyewe iliyo mwagika pale msalabani. Sasa pale ambapo wewe unapo kuja kuamini kazi ya msalaba ndipo sasa unakuwa una haki mbele zake ndio maana ukisoma hapa...

Warumi 10:9-10 (KJV) Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.

Kwahiyo unaona kazI ya mwanadamu ni kumkiri Yesu, kumuamini Yesu ndipo anapata kuokolewa na hapo ndipo ambapo sasa moyo (Sub-Concious mind) huamini kiukweli kulinganisha na taarifa ambayo huyu mwanadamu anapaswa kuwa nayo kwanza na kukiri kwa kinywa chake na kuupata wokovu. 


Warumi 8:1-2 (KJV) Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.

Ukisoma hapo pia juu unaona kwamba mtu aliye ndani ya kristo hakuna hukumu ya aina yeyote anayoweza kuipata maana yeye anaye Roho mtakatifu ambaye huyo humuweka na kumpa nguvu ya kuishi nje ya dhambi. Kwahiyo ile hukumu ilipaswa kupatikana kupitia dhambi Yesu aliishaiondoa na kutufunza sisi sasa kumuishia Yeye kwenye maisha Yetu ya kila Siku.

  • Wokovu ni kipawa cha Mungu ambacho kimefunuliwa kwa mwamini na kumpa uwezo wa kuishi mbali na dhambi
Waefeso 2:8 (KJV) Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;

Sasa huu wokovu ni zawadi ambayo Mungu amempatia mwanadamu ambayo yeye mwanadamu hana namna yeyote ya kufanya ili apate bali Mungu mwenyewe ndiye ameachilia kwa mwanadamu kwa kupenda kwake yeye mwenyewe.

Sasa hiki kipawa ndicho ambacho humpa mwamini kuweza kuishi sasa nje ya dhambi na ndio maana hakuna mtu anaweza sema nimeokoka akawa bado katika matendo yasiyo katika njia ya Mungu maana katika kufunuliwa kwa kipawa hiki ndiko ambako sasa kunaleta uwezo wa kuyaishi mapenzi ya Mungu maana hiki kipawa kinapofunuliwa kina mpa mwanadamu shule au Elimu ya namna ya kuishi akiwa yuko hapa Duniani.

Tito 2:11-12 (KJV) Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;

Kwahiyo unapopewa wokovu ni kwamba umepewa uwezo wa kuishinda dhambi kiufupi.

Hitimisho:  Kutokana na maana hizo hapo juu tumejifunza tunaweza kueleza kiufupi kwamba WOKOVU ni usalama ambao mwanadamu anakuwa anaupata pindi anapokuwa ameshamkubali, kumuamini na kuamua kufuatana naye kwenye maisha yake huyu mtu anakuwa amekwisha kuokoka na kuwa na haki zote za urithi kwakuwa mwana wa Mungu kwelikweli. Hii inaonyesha hapa

Yohana 1:12 (KJV) Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;

Mungu akubariki kwa kufuatana na mimi kwa sehemu hiii ya kwanza  ambapo ni kama msingi unaotupa kuelewa vizuri tunako elekea. Niombe basi ufuatilie sehemu ya pili itakuwa na package nyingine inayoendelea. Nkngeweza kuendelea lakini  ukiweka mambo mengi sana wengine hawawezi kusoma ndio maana nimejaribu kuligawa somo hili.

Lakini kama hujaokoka na unatamani kuingia kwenye ushirika huu wa Kuwa na Yesu kristo kristo kwenye maisha yako unaweza kuwasiliana nami kupitia mawasiliano hapo chini.

Ulikuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo 
+255766944441
jackobombwaga@gmail.com 

KUFUNGIWA NIRA PAMOJA NA KRISTO/ USHIRIKA NA KRISTO (Sehemu ya Kwanza)


Bro Jackobo


Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu?? Karibu tujifunze kidogo neno la Mungu juu kufungiwa Nira pamoja na Kristo.

Utakuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

Maana ya Nira
Nira ni mti ambao unawaunganisha kwa pamoja ng'ombe (Maksai) wawili wanapokuwa wanalima.

Kwahiyo kufungiwa nira pamoja na Kristo ni hali ya kujijenga kimahusiano au kiushirika baina ya mwanadamu/Mwamini na Mungu wake kupitia Kristo Yesu.

2 Wakorintho 6:14
"Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?"

Ukisoma vizuri maandiko hapo juu utaona ya kwamba mtumishi wa Mungu Paulo alipokuwa anazungumza na wakorintho anazungumzia suala la kufungiwa nira na wasio amini kwa namna isiyo sahihi, kumbe Katika kufanya ushirika Kuna masharti na vigezo vya ushirika.

Hakuna ushirika wowote usio kuwa na vigezo na masharti lazima viwepo vitu ambavyo ndio kipimo cha kuweza kushirikiana baina ya watu hawa wakiwa kwenye kuhusiana. Kwahiyo Tunapokuja kuzungumzia suala la Kufungiwa nira pamoja na Kristo lazima viwepo vigezo vinavyotakiwa kuwepo ili huyu mwamini aweze kushirikiana na Mungu wake katika Utumishi ambao kaitiwa na Sio kwenda pasipo kuwa na utaratibu.

Sasa ukiangalia mwanzilishi wa kwanza wa Ushirika alikuwa ni Mungu mwenyewe ambaye yeye ndiye alitaka kuwa na uhusiano na mwanadamu ndio maana baada ya anguko la mwanadamu pale Bustani ya Edeni Mungu yeye ndiye alikuwa wa kwanza kutangaza kutaka ushirikaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Mwanzo 3:21 (KJV)
"Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika."

Kitendo cha Mungu kuwafanyia Adamu na eva mavazi ilikuwa ni kurudisha uhusiano waliokuwa wameshauharibu kwa kukosa utii kwenye maisha yao. Mavavi huwa ni Sitara na tena aliwatengenezea mavazi ya ngozi ikimaanisha kwamba kuna mnyama ambaye aliuawa ili yeye azichukue dhambi za Adamu na Eva, kwahiyo hatia ya makosa ya Adamu na Eva ilikuwa juu ya mnyama aliye uawa ili watengenezewe mavazi hawa watu. Huu ni upendo wa Ajabu sana Ambao Mungu ana muonyesha mwanadamu kwamba licha ya kuwa kakosea ila bado anatamani huyu mwanadamu awe na mahusiano na yeye, Hii ndio maana halisi ya kwamba Mungu katupenda kwa upendo wa mileleπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Yeremia 31:3 (KJV)
"Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu."

ukiangalia maandiko hapo utaona Mungu anamuambia Yeremia ili asije akajidharau bali ajichukulie katika heshima ambayo Mungu amempatia. Ndivyo ambavyo Mungu ametupenda na sisi na anataka tuishi na kujiona ni wenye thamani ili tusije tusikajidharau na ndio maana ametuita kwa fadhili zake ili tuweze kuwa karibu na yeye.

Sasa Mungu alikuwa ameona kikwazo kilichopo ambacho huwa kinawafarakanisha wanadamu na Mungu ambapo ni maovu au dhambi tunazozifanya. Maana Mungu huwa hawezi kuwa na Ushirika na mtu ambaye anazo Dhambi maana huwa dhambi zina mtenga mtu na Mungu wakeπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Isaya 59:1-4 (KJV)
"Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong'ona ubaya. Hapana adaiye kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu."

Sasa baada ya kuona hilo kuwa mwanadamu akiwa na Dhambi hawezi kushirikiana na yeye ili mlazimu amtume mwanawe Yesu kristo aje kuwa ondoleo la dhambi zetu tulizokuwa nazo wakati huoπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Yohana 3:16 (KJV)
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

kwasababu ya Upendo wake Mungu aliona ni vyema sasa akamtoa Mwanawake yeye azichukue dhambi zetu pale kalivari ili aweze kushirikiana na Sisi

Yohana 1:29 (KJV)
"Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!"

Waebrania 9:26 (KJV)
"kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake."

1 Timotheo 1:15 (KJV)
"Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi."

Ukisoma vifungu vyote hapo juu utaona Yesu kumbe ndiye alikuwa ondoleo la Dhambi kwa mwanadamu kwahiyo mimi ili niweze kushirikiana na Mungu lazima nikubali kazi ya msalaba ambapo yeye alizibeba Dhambi zetu pale kalivari.

Isaya 53:12 (KJV)
" Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji"

Isaya alipewa maono juu ya Yesu kuchukua dhambi zetu ndio maana hata pale msalabani Yesu alikuwa akilia Kwamba Mungu mbona kamuacha kwakuwa dhambi za ulimwengu zilikuwa juu yake na Mungu haambatani na dhambi hata siku mojaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Mathayo 27:46 (KJV) 
"Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?."

Kwahiyo kwasababu hiyo lazima sisi kama waamini tuwe na ushirika na Yesu Kristo wakati wote maana bila yeye hatuwezi kuwa na mahusiano mazuri na Mungu.

KAZI YA YESU KWENYE USHIRIKA WAKE NA MWAMINI ANAVYOIFANYA
Kuna mambo mengi Yesu huwa anayafanya kwenye maisha yetu ili tuweze kuwa na ushirika naye embu tuangalieπŸ‘‡πŸ‘‡

Mathayo 11: 20-30 (28-30) (KJV)
"Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi."

✍️✍️ Yesu alifanya miujiza lengo kuwafanya watu wa miji hiyo wamuamini kwa ajili ya kazi alizokuwa anazifanya
✍️✍️ Tena miujiza huwa inadhihirisha utendaji wa Mungu katika eneo japo hapa lazima kuwa makini maana hata shetani huwa anafanya miujiza ili aweze kuwateka watu waweze kumuendea yeye kwenye maisha yao.
N.B: Huo utendaji na udhihirisho wa Mungu kamili unatosha kabisa kumfanya huyu mtu aweze kuamini na kuingia kwenye pendo la Mungu yaani katika NIRA.
✍️✍️Yesu sasa anawaita watu wote wenye mizigo/Dhambi waje kwake ili aweze kuwatua hapo ndipo tunapo pata nafasi ya kuwa na ushirika na Yeye.

Mathayo 8:4 (KJV)  
" Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao."

Marko 1:44 (KJV)  
"akamwambia, Angalia, usimwambie mtu neno lolote, ila enenda zako ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe alivyoamuru Musa kwa kutakasika kwako, iwe ushuhuda kwao."

✍️✍️✍️ Yesu alimuambia mtu yule mwenye ukoma akajionyeshe kwa makuhani kama sehemu ya kuwafanya na wao waelewe na  waamini kazi ya Mungu ili na wao pia waingie kwenye ushirika wake wakati wote.

Embu turudi kwenye andiko letu la msingi la kwanzaπŸ‘‡πŸ‘‡

2 Wakorintho 6:14-18 (KJV)   
"Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.  Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,"

Paulo alikuwa anazungumza na watu wakorintho kujiepusha na mambo yafuatayo
1. Ibada ya sanamu
2. Kulichafua hekalu la Mungu
3. Kufanya uasi yaani kwenda kinyume na sheria ya Mungu
 4. Kuacha kumtazama Yesu kama mwanadamu yaani asiringanishwe.

Sasa ikiwa tunayaishi hayo hapo juu ndio kufungiwa Nira pamoja na wasio amini maana hayo ndiyo asili yao kwenye mambo kama hayo. Kwahiyo lazima kujitenga na kila namna inayoleta shida kwenye ushirika na Mungu wetu maana tunapo yaepuka hayo ndipo yeye anakuwa Baba kwetu nasi tunakuwa wana (Shirika au uhusiano au Nira inawekwa baina yetu na Baba).

hii ndiyo maana yesu alipokuwa akiwafundisha wanafunzi wake aliwajenga zaidi katika mahusiano mazuri zaidi na Mungu (Mathayo 6:9-15).

Paulo anawaambia watu wa Korintho kuweka mbali kila namna ya Uovu kwenye maisha yao akitamani Dhambi isitamkwe kwao yaani maisha yawe ya ushuda wa kristo maana kuishi maisha ya ushuhuda huwafanya wengine ambao walikuwa hawaamini kuvutwa kuja kwa kristo Yesu. Kwahiyo kama kanisa lazima tuishi kwa ushuhuda  mzuri ili tuwe na ushirika na Mungu ili hata wengine wavutwe kwenye huu ushirika na Mungu.

Mungu akubariki kwa kuambatana na mimi tangu tumeanza sehemu hii ya kwanza ya somo tutaendelea sehemu ya pili pale Mungu atatupa kibali. Unaweza ukamshirikisha na mwenzako juu ya neno hili ambalo Kristo ameliweka ndani yangu kwa ajili ya Kanisa lake la wakati huu


Ulikuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com


KIU YA KUMTAFUTA MUNGU (sehemu ya pili)


BRO JACKOBO

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu??
Utakuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com


Kutokana na baadhi ya maswali na michango nimekuwa nikiipokea nimeona ni vema niongezee kipengele cha pili kwenye somo juu ya KIU YA KUMTAFUTA MUNGU kwa upande wa Umuhimu wake

Kama haujasoma sehemu ya kwenza unaweza kubonyeza hapaπŸ‘‰πŸ‘‰SEHEMU YA KWANZA

Basi Nikianzia na maana niliyokuwa nimetoa mwanzoniπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 KIU hii ni hali ya ndani anayokuwa nayo mtu ili aweze kupata au kufanikisha jambo fulani alilokuwa na uhitaji nalo. 

 Kiu ya kumtafuta Mungu hiii ni hali ya ndani inayojengeka kwenye Nafsi ya mwamini kuhitaji ushirika na Mungu katika nyanja zote za maisha yake yani kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiroho.


UMUHIMU WA KUWA NA KIU YA KUMTAFUTA MUNGU KWA MWAMINI 
Sasa umuhimu wa kuwa na kiu uko hivi πŸ‘‡πŸ‘‡

1. Kumruhusu Mungu achukue hatamu ya maisha kwa kila jambo ambalo utakuwa unalifanya

 1 Wakorintho 10:31
 "Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu."

Ukisoma hilo Fungu unaona Paulo ana wausia watu wa Korintho kwamba kila kitu kinapofanyika kwa mwamini inatakiwa kufanyika kwa utukufu wa Mungu. Kwahiyo ukiwa na kiu utafanya mambo yako yote chini ya maongozi ya Mungu na papo hapo itakuwa Mungu anatukuzwa kwa kuwa mambo au mafanikio yako yatakuwa yamejengwa kwa Mungu mwenyewe πŸ™ŒπŸ™Œ


2. Inasaidia kujijengea heshima ya kibinafsi juu ya mambo yako [SELF DISCIPLINE]

πŸ‘‰πŸ‘‰Kwakuwa ndani ya nafsi yako imejengeka hali ya kumuhitaji Mungu hautafanya mambo kwa pupa maana nafsi yako itakuwa iko kwenye hitaji la kumtukuza Mungu kwahiyo maamuzi yako yatakuwa sahihi yaliyokuwa balanced..

Pia inabidi ujue kuwa kwenye nafsi ndiko kuliko UTASHI, UELEWA, MAAMUZI, AKILI NA MOYO(HIFADHI/KUMBUKUMBU).  Kwahiyo ukiwa na Kiu mambo yako na maamuzi yako yatajikiti kwenye kuhakikisha unampendeza Mungu si utajizuia kwa mambo mengi.

N.B hapo kwenye NAFSI ni somo linajitegemea ambapo inahitaji pia mda wa kutosha kuelewa ila kama Mungu atatupa kibali nitaliweka pia kwenye hii website yangu.

Ndio maana Suleiman anasema kwamba πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 Mithali 29:18
 "Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria."

Nia pia inakuonyesha jambo la kufanya ndio maana hukupa ile self discipline for anything you will be intending and interesting to do in future.

3. Kumfanya mtu awe na ushirika {FELLOWSHIP} bora na Mungu.

πŸ‘‰πŸ‘‰ Maisha ya ukristo sio tu kwenda kanisani bali ni uhusiano binafsi wa mtu na Mungu wake katika mazingira na nyanja mbalimbali za maisha. Kwahiyo mtu mwenye kiu huwa inamfanya atamani sana kukaa na Mungu kwa karibu kitu kinachomjengea msingi mkuu wa ushirika wake na Mungu.

 1 Petro 2:2
 "Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;"

Unapokuwa na kiu utakuwa mtu wa kujifunza maneno ya Mungu na kujikuta unaukulia wokovu ambako huko hufanya kuimarisha ushirika na Mungu wako.

4. Kuondoa hali ya mazoea kwenye utumishi wako 

πŸ‘‰πŸ‘‰Watu wengi wanafanya mambo kwa mazoea yaani bila kufwata maelekezo ya Mungu anavyotaka kwakuwa ndani ya maisha yao haiko Shauku au Kiu ya kumtaka Mungu bali wanafanya kama taratibu za kila siku.

Huduma yeyote ambayo umepewa na Mungu unahitaji unyenyekevu wa hali ya juu na sio kwakuwa unaweza au ulimuona mtu fulani anafanya basi na wewe unafanya. Embu ona hawa watuπŸ‘‡πŸ‘‡

Matendo ya Mitume 19:13-16
 "Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa."

Hawa wapunga pepo kwakuwa kiu yao ilikuwa kujipatia faida na sio kuwa na Yesu walijikuta wanaingia pabaya na kutendewa yasiyo faa na yule pepo mchafu.

Kwahiyo ukiwa na kiu hutafanya kwa mazoea kama hawa watu walivyofanya ili wajipatie heshima mbele za watu wa mji ule. Sasa wewe kwenye utumishi wako utatenda ili Mungu atukuzwe ndani yako na kukufanya hali ya mazoea kuto kuwepo ndani yako.


5. Kuruhusu Tunda la Roho kuleta matokeo ndani yako.

πŸ‘‰πŸ‘‰Mtu anapokuwa ameokoka huwa Roho mtakatifu anakuja ndani yake ila madhihirisho ya kujazwa na Nguvu au uwezo wa Roho mtakatifu hufuatia baadaye pale anapokuwa anaendelea  kuukulia wokovu japo kuna wengine pia hupata madhihirisho wakati huohuo baada ya kumuamini Yesu na kazi yake ya msalaba na umuhimu wake. (πŸ‘‰πŸ‘‰Mfano wanafunzi wa Yesu walipata madhihirisho baada ya Yesu kuondoka.. Soma Matendo 2:1-4 wakati wengine ka Kornelio walipokea papo hapo pindi anaipata injili.. soma Matendo 10:44-46 ila soma sura nzima ya 10 hiyo)

Sasa Roho mtakatifu huwa analeta yale matunda ya Roho kwenye MATENDO 5:22-24  Kuwa dhahiri kwa mwa mwamini. Kwahiyo kwa mtu aliyekuwa na kiu ndani ndio huruhusu hayo mambo kufanyika kwake na hii ndio huja kuleta utofauti baina ya mwamini na mwamini mwingine.

6. UNYENYEKEVU kuwa ni sehemu ya maisha yako.

Mtu ambaye bado hajajikita kumtaka Mungu ni rahisi sana kutaka yeye aonekane kwenye jambo lolote na sio Mungu. Ila huyu mtu akiwa na kiu anakuwa na hali ya uhitaji kiasi kwamba anakuwa ana unyenyekevu na kuwekelea mbali kila namna ya kiburi ndani yake kitu ambacho humfanya apate kibali mbele za Bwana. Embu ona watu hawaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 Mwanzo 11:3-4
 "Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote."

Ukiwaangalia hawa watu utagundua walitamani wajipatie sifa na kuacha kufuata agizo la Mungu la kutakiwa kutawanyika juu ya uso wa nchi yote kama alivyosemaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 Mwanzo 1:28
 "Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi."

Hapo unaona kiburi kiliinuka lakini kama wangekuwa wanamtaka Mungu basi wangefuata maelekezo yake ambayo ingeleta unyenyekevu ndani yao.

Pia siku zote mtu anayemtaka Mungu lazima awe na unyenyekevu ndani yake maana Kwake maelekezo ya Mungu kwake ni Lulu na uhai maana sisi katika kristo huwaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Matendo ya Mitume 17:28
"Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake."

Mungu akubariki kwa kusoma sehemu hii ya pili. Unaweza kuwashirikisha na wengine pia

Ulikuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Phone; +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

KUJIKANA NDANI YA KRISTO YESU (sehemu ya tatu- Final)

Bro Jackobo Utakuwa nami mpendwa katika kristo yesu Name: Bro Jackobo Phone: +255766944441 Email; jackobombwaga@gmail.com Bwana Yesu asifiwe...