Mwl; Jackobo Abely Mbwaga
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441 and +255621036471
UTANGULIZI
Bwana YESU asifiwe mwana wa Mungu baada ya kuona sehemu ya kwanza ya utangulizi juu ya somo lenye kichwa "Kuitoa miili yetu kuwa Dhbihu mbele za Bwana" karibu tuendelee kuangalia Kiini kamili cha somo lenyewe. Na kama haujabahatika kusoma sehemu ya Kwanza ningependa kukushauri ukaisome kwanza hiyo sehemu ili kuweza kupata mtiririko mzuri wa Somo. Unaweza ukasoma kwanza kupitia hii link juu ya Utangulizi wa somo letu hili bonyeza hiyo sehemu nyekundu itakulelekezaa moja kwa moja kwenye Somo SEHEMU YA KWANZA
KIINI CHA SOMO LETU
Ni vyema tuanze kuelewa tunapozungumzia mwili na Dhabihu ya mwili ni kitu gani
Mwili ni nini???
Kwanza mtu ambaye yuko hai ameumbwa na vitu vikuu vitatu (Nafsi, Roho na Mwili) yani katika hivyo tunakuwa kamili pasina kimoja hakunaga ukamilifu hata siku moja ni sawa na ukazungumzia Mungu baba pekee{Mungu huwa anakamilishwa kwa utatu wake mtakatifu- Mungu baba, Mungu mwana na Roho mtakatifu(MUNGU)}
1 Wathesalonike 5:23
"nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.”
Waebrania 4:12
“ Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanyanafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.”
Katika maandiko tuliyoyasoma hapo juu yanaonyesha moja kwa moja kwamba Kuna Katika mwanadalu kuna vitu vitatu ambapo ukiangalia Fungu la kwanza paulo anawaambia watu wa Korintho kufanikiwa katika nyanja zote tatu. Hata hili andiko la waebrania linaonyesha kuna tofauti kati ya nafsi mwili na Roho. Hapa Pana somo linajitegemea kama Mungu atatupa kibali basi tutafundishana juu ya mwili, Nafsi pamoja na Roho.
Neno“ mwili ” katika lugha ya Kiyunani ni “ Soma” humaanisha “ gamba la nje,au mavumbi ya ardhi yaliyofunika pumzi ya Mungu”. Kwahiyo mwili ni nini??
Mwili ni hili gamba la nje la mwanadamu lionekanalo.
Tumekwisha kuona maana ya mwili basi twende tulione andiko letu la msingi linalo beba somo letu.
Neno la Msingi linalobeba somo letu hili ni kutoka kitabu cha
WARUMI 12:1
"Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana."
Maana ya DHABIHU YA MWILI
Dhabihu ya mwili ni Sadaka ya kujiachilia kwa Bwana ili Mungu ashike hatamu katika mfumo mzima wa miili yetu yani katika hali ya utendaji wa kazi ya kila namna.
Hapa viungo vyako vyote vinakuwa tayari kwa ajili ya kazi ya Mungu haijarishi uko vipi katika hali yako yaani uko kipindi cha uzuni, kipindi cha Furaha, kipindi cha maumivu au kipindi kufarijika.
Mfano kuna muimbaji wa nyimbo za injiri kaimba nitaimba haleluya asubuhi, mchana na hata jioni pia akasema wakati wa furaha na wakati wa huzuni yeye ataimba.
Kwahiyo: mtu ambaye amejitoa dhabihu ni yule ambaye anaweza kumtukuza Mungu kwa wokovu aliopewa na Mungu pasina kuangalia sababu za nje zinazokumba mwili wake, tena huyu mtu hayuko tayari kurudi nyuma kwa namna yeyote.
SIFA KUU AMBAZO ANAKUWA NAZO MTU ALIYEJITOA KIWA DHABIHU MBELE ZA MUNGU
1. Utakatifu kwake ni kipaumbele katika yote
1Thesalonike 4:4
"kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima"
Mtu huyu ambaye amejidhabihu mbele za Mungu anatenda mambo yake kwenye usafi wote kama vile Mungu alivyosema mtakuwa watakatifu kwakuwa Mimi Mungu ni mtakatifu
2korintho 7:1
"Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu."
Paulo anazungumza na kanisa la Korintho kwamba waendelee kujitakasa yani waendelee kuishi maisha ya kumpendeza Mungu kwenye maisha yao ambayo hiyo inaonyesha wazi kwamba Alitamani kanisa lijitoe dhabihu kwa ajili ya Mungu liachane na kila namna ya uchafu wa kidunia.
2 Huyu mtu hana maisha ya kifafa i.e huyu mtu ana maisha ya unyoofu kiroho (SPIRITUAL CONSISTENCY LIFE)
Mtu mwenye kifafa huyu huwa anakuwa na maisha ya kuanguka na kuinuka yaani hana mwendelezo( Consistency) ya kuuishi uhalisia wa Mungu
Isaya 26:7
"Njia yake mwenye haki ni unyofu; Wewe uliye mnyofu wainyosha njia ya mwenye haki."
Kama nilivyokwisha tangulia kusema huyu mtu anakuwa anaenda katika unyoofu wa Mungu. Biblia imezungumzia haki ikimaanisha kutembea kwenye sheria za Mungu alizoziweka mwenyewe
Ukisoma kitabu hiki huwa kina watatiza Wengi wetu
Mithali 24:16
"Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya."
Hapa biblia haijakupa ticketi ya wewe basi kutenda dhambi kwasababu utainuka bali inazungumzia kuinuka tena kozi kunavitu vinaweza vikawa vinakusonga upesi ukajikuta unakosea ila una nafasi ya kusimama tena.
Kumbuka neno la waebrania
Waebrania 6:4-6
"Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri."
Watu wanachukulia toba ni kama kitu cha kawaida lakini kiuharisia TOBA ya kweli ina gharama hata kama watakufariji kwa maneno kwamba MUNGU ni wa rehema, sawa, sijakataa lakini kumbuka pia kwamba Mungu ni mkali sana yeye ndiye aliwachoma SODOMA NA GOMORA KWA MOTO, sasa kama Mungu ni mkali kwanini tusifike hatua tuamue Kuishi maisha ya unyoofu??
Kama wewe wokovu wako ni wa kifafa yani unaanguka na kuinuka jua ya kwamba wewe bado haujajiweka wakifu mbele za Bwana yani haukujitoa dhabihu mbele zake Bwana.
3. Watu hawa huwa wanaitazama mbele ya katika upande chanya
Ayubu 19:25-26
"Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu:
Ayubu hakuwahi kuona kwamba safari yake ya kumuona Mungu haiwezekani licha ya kwamba walimvunja moyo na alipoteza thamani nyingi alizokuwa nazo. Hata ukafika hatua hata mke wake anamuambia mkufuru Mungu ufe lakini bado yeye alisimama pamoja na Mungu katika yote.
Jichunguze maisha yako wewe ni kwa namna gani umekuwa mwepesi wa kukata tamaa hata hutaki kuendelea na imani yako ya kumtafuta Mungu???
Wengine kuachwa na wachumba wao wamevunjika moyo wanasema kwamba basi waachane na Imani ya YESU kristo
Acha mawazo mafupi utakuja kujuta na maamuzi yako hayo tafadhari tembea na Mungu atakusaidia. Kama utajiona uko mtu wa kukata tamaa kaa ukijua ya kwamba wewe bado hauja fika hatua ya kuuweka mwili wako uwe dhabihu mbele za Mungu maana tayari mwili wako umekukoseha tayari yaani umekupinga kufanya maauzi ya kiroho ambayo ni ya kimungu mwenyewe.
Ili tuweze kuelewa ni kwa namna gani tunaweza kuitoa miili yetu kuwa Dhabihu ya kupendeza na takatifu mbele za Mungu embu tuangalie kazi za mwili huku tukiweka Muunganiko na namna ya kuitoa miili yetu kuwa dhabihu takatifu mbele za Mungu
KAZI ZA MWILI
1. KUPOKEA NA KUTOA
Hapa ni nazungumzia moja kwa moja Kazi ya milango mitano ya fahamu ( Kuona, kunusa, kuonja, kusikia, na kuhisi)
Watu wengi tuko kanisani lakini bado hatujafika hatua ya kuelewa namna ya matumizi mazuri ya milango ya Fahamu yetu ambayo Mungu ametupa ili iwe kwa utukufu wa jina lake.
A) Kuona
Kazi ya kuona hufanywa na Macho sasa embu tuangalie namna gani sasa tunaweza jitoa miili yetu kuwa dhabihu kupitia kuona.
Zaburi 103:3
"Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami."
Hapa Mungu atuokoe kanisa sana maana watu umefika wakati wanaangalia mambo ya kishetani mfano kuangalia videos za ngono (Pornography) alafu bado wako katika nyumba ya Mungu alafu wanasema ya kwamba eti wamekwisha kutengwa Yani kwamba eti wamejitoa miili yao kuwa dhabihu mbele za Bwana iliyo takatifu... Embu acha huoo ujinga unajiangamiza nafsi yako mwenyewe. Wengine wanadai eti wanataka kupata utoshelevu wa kihisia za kimapenzi kwa namna hiyo (SEXUAL SATISFACTION) huku wakidai ya kwamba hawataki kufanya uasherati
Embu usijidanganye kama ni kijana jua miamko ya kihisia lazima itakuja kwako kwahiyo utakuwa ushazini tayari isipokuwa bado tu haujafanya moja kwa moja soma kitabu cha (Mathayo 5:28) sasa wewe endelea kujifariji kwamba umeuweka mwili wako kwa ajili ya kristo wakati tayari ushakuwa miliki ya shetani.
Kwahiyo kuwa Dhabihu katika kipengele cha macho ni pamoja na kuweka mambo mema mbele ya macho yako achana na tabia za kuangalia picha za ngono, mapicha ya wadada ambao wanavaa nusu uchi (i.e wanavaa chupi na sindiria tu kwa mabinti). Kama utaona pasina kutegemea basi huwezi kuwa umeibeba dhambi lakini kama utakuwa una dhamiria kabisa na kuenda kutazama hizo picha kwa akili zako mwenyewe hiyo ni dhambi kabisa mbele za Bwana tena usijifariji hata kidogo
MATHAYO 15:11
"Sikilizeni, mfahamu; Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi."
Hili fungu linaonyesha utayari wa mtu kufanya kitu ndio unamtia unajisi sio vile vitu hana utayari navyo yaani wewe unakubaliana na akili yako unaanza kufungua websites zenye picha chafu alafu unataka kuwa dhabihu ya kumpendeza Mungu?? Haiwezekani Mungu sio wa udhalimu kiasi hicho yeye ni wa haki na utakatifu (utaua). Hapo moyoni mwako utakuwa umejaa picha chafu alafu zinakutoka na wewe unakubali wito wake.
Kuuweka mwili wako dhabihu lazima ujitenge kwanza na uovu wa macho lasivyo utaendelea kuingia kanisani wakati bado unao uovu ndani yako na unaendela hata mda mwingine kuhubiri injiri au kuimba ila kumbuka kuhudumu kwako hakutakupa nafasi ya kuuona ufalme wa Mungu (MATHAYO 7:21) kwahiyo usiendelee kujifariji ya kwamba utafika kwa namna hiyo lasivyo unapoteza mda wako kuingia kwenye Nyumba ya Mungu.....
B) KUSIKIA
Hii hufanywa na Masikio
Zaburi 1:1-2
"Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku."
Chanzo cha imani yeyote huwa ni kusikia na pasipo kusikia hakuna imani yeyote inaweza kuumbika kwa mtu (warumi 10:17) kwahiyo pale tunapokuwa tunajisahau na kukaa sana sehemu za watu wenye mizaa kuna vitu vya KIROHO huwa vinapungua sana na kuna baadhi ya vitu vya kidunia vinaanza kuumbika taratibutaratibu.
Sasa kama wewe umeamua kwenda na YESU lazima ukae mbali na watu wenye mizaa na hata kama waishi hapo wanapokaa basi usiende kwenye njia yao(Yaani usiwe na wewe ni mtu wa mzaa) maana kutakuwa hakuna utofauti wowote wako wewe na hao watu wanaokuzunguka na huku ndiko kujitoa kuwa dhabihu maana Mungu ndiye katupa maelezo haya kwamba tusikae kwenye njia na maeneo yenye mizaha ya namna kama hiyo.
Pia mizaha huwa inapunguza sana nguvu ya Mungu sana na nimeona sana kwenye maisha yangu mwenyewe. Kuna wakati nimewahi penda sana kufanya mizaa sana hiki kitu kilinipa sana wakati mgumu sana wakuishi maisha matakatifu na ndio maana tuliokoka ni watu ambao tumetengwa na Mungu sasa inakuwaje unafika wakati tunataka kule ambako Mungu ametutoa??? Tunapoteza haki zetu mbele za Mungu na Mungu anatuacha tuende tunavyotaka kuenda.
C) KUHISI
Hapa nitaelezea hisia za kimwili ambazo mwanadamu anakuwa nazo (biological feelings) ukiringanisha na hisia za kiakili (mental feelings).
Mara nyingi hisia za kimwili tulizo nazo zinakuwa na uhusiano mkubwa na akili zetu hakuna hisia za kimwili zinaweza kuwepo pasipokuwepo na Akili
Sasa hapa kuna watu umefika hatua wanajirizisha miili yao kwa namna ambayo inaleta machukizo sana Mbele za Mungu... Embu tuangalie kitabu hikii
1WATHESALONIKE 4:4-5
"kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu"
Wapo watu ambao wana fanya USAGAJI, MASTERBATION, UZINZI NA UASHERATI lakini bado wanaingia kwenye nyumba za ibada na wanaona wamejitoa kwa ajili ya Mungu lakini Kiukweli wanajidanganya isipokuwa wamefungwa katika fahamu zao na wanaona ya kwamba ni kitu cha kawaida.
Kuna wakati nilitamani sana kuweza kujua juu ya maisha ya watumishi wengi sana wanavyokuwa wanaishi kwenye maisha yao. Kuna mtu mmoja wa mataifa aliniambia hao mnaowaita watumishi ndio watu ambao wanamambo ya ajabu sana wanajiendekeza sana kwenye maswala ya Ngono mno kiasi kwamba hata wao wanafika hatua wanaona ni bora kutokuokoka na mtumikia Mungu maana hao waliokatika utumishi ndio hao wanaongoza kwa kufanya Vitimbwi vya ajabu.
Nilikuwa najiuliza sana ni kwanini watumishi wa Mungu wafike hatua wafanye mambo ya aibu kama hayo??? Lakini ashukuriwe Mungu nilikuja kufundishwa kwamba bado hawa watu wapo kwenye utumishi lakini Bado hawaji dhabihu mbele za Mungu hata siku Moja ila wapo tu wanaingia kwenye nyumba ya Mungu.
Pia kuna watu wapo kanisani (haswa vijana na mbainti wasio na ndoa) wamekuwa wakichezea hisia za jinsia tofauti alafu bado wanasema wamejidhabihu mbele za Mungu lakin kiuhalisia hakuna ukweli kabisa kama wamekwisha jidhabihu mbele za Mungu. Mungu akusaidie ndugu yangu utoke hapo ulipo kama unataka kumuona Mungu na unataka ujidhabihu mbele zake.
D) Kuonja
Kuonja ni kazi moja wapo ambayo hufanywa na ulimi kwahiyo kwenye ulimi huwa kuna msingi mkubwa katika kujidhabihu mbele za Mungu
Kwahiyo lazima ujue namna kuutumia vizuri ulimi wako. Ili tufike hatua ya kusema ya kwamba umejidhabihu ni lazima maneno yako yawe yanakolea Munyu yani yawe yanaleta ushuhuda mbele za Mungu na mbele za watu wanaokuzunguka.
WAEFESO 4:29
"Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia."
Sasa napata wakati mgumu sana nikikuona mtumishi wa Mungu bado unatamka maneno maovu alafu unasema ya kwamba umejitoa kuwa dhabihu mbele za Bwana. Ndugu yangu Mungu akupe neema uwe na rijamu kwenye ulimi wako ili usije ukamkosea Mungu kwenye nyakati zako zote.
Mungu atusaidie sana kanisa maana tunaweza tukawa tunajifariji ya kwamba tuko pamoja na Mungu kumbe yeye ametuacha tutembee kama tunavyotaka siku zote sasa kuwa makini sana unachokifanya usije ukawa unaingia kumbe Mungu amekuacha Embu chukua nafasi mtake Bwana na nguvu zake akutoe hapo.
MITHALI 10:19
"Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili."
Usiwe mtu wa maneno Mengi sana kwenye maisha yako. Unapokuwa unaongea sana unaweza ukajikuta unatenda dhambi kiurahisi sana tena sana
Nilikuwa najiulizaga sana hivi ni kwanini huwa inatokea kuna siku sipendi kabisa kuongea natamani kuwa mwenyewe nisizungumze nilikuwa kufunguliwa hapa kuna wakati Roho mtakatifu anakuwa anakuepesha na dhambi inayoweza ikawa inakunyemelea. Na suala hili kwa watu ambao wamewahi kuwa karibu na mimi wanaweza wakashuhudia kuna wakati huwa napenda kukaa peke yangu sitaki hata kuchangamana na watu.
Lakini sijakuambia uache kuongea na watu maana haohao watu ndio wengine wamebeba kusudi lako tena haohao watu ndio utakao takiwa kwenda kuwapa habari njema za kristo YESU.
Kwahiyo mtu aliyejitoa kuwa dhabihu mbele za Mungu anakuwa ni mtu aliyekuwa na control (Kujitawala) katika usemi wake.
MUNGU akubariki kwa kuchukua nafasi hii na kusoma SEHEMU YA PILI tutaendelea na kazi nyingine ya mwili pamoja na uhusiano wa namna ya kujitoa mbele za Mungu.
Kwa maswali au maoni unaweza ukawasiliana nami kwa njia zifuatazo
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441 and +255621036471
www.jackobombwaga.blogspot.com
Wako Mwalimu wa neno la Mungu katika kristo Yesu
Jackobo Abely Mbwaga (Bro Jackobo)
Mungu akubariki kwa ujumbe mzuri AMEN
ReplyDeleteAmen
DeleteAmen mtumishi
ReplyDeleteMungu akubariki kwa kusoma
Delete