KUITOA MIILI YETU KUWA DHABIHU MBELE ZA BWANA (SEHEMU YA TATU- FINAL)

KUITOA MIILI YETU KUWA DHABIHU MBELE ZA BWANA (SEHEMU YA TATU-FINAL)
BRO JACKOBO
Mwal: Jackobo Abely Mbwaga (Bro jackobo)
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441 and +255621036471

BWANA YESU asifiwe mtumishi??? Tumekwisha kuona sehemu ya kwanza ya somo letu juu ya maana ya Dhabihu na tukaona sehemu ya pili juu ya maana Ya mwili, Dhabihu za mwili na tukaangalia Sifa za mtu aliyejitoa dhabihu mbele za bwana anakuwaje pamoja  namna ya kuitoa miili Yetu kwa kuangalia kazi ya mwili ya kupokea ambapo tuliegemea katika Milango ya Fahamu.... Sasa embu tumalizie na kazi zingine za mwili na namna ya kujitoa kuwa wakifu mbele za Bwana..

2. KUHIFADHI/ KUTUNZA

Kikawaida mwili huwa unatumika kutunza mambo Mengi sana lakini ngoja tuende moja kwa moja kiroho kwanini tunasema mwili huwz unafanya kazi ya kutunza/ kuhifadhi

1 WAKORINTHO 6:19-20
"Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu."

Biblia Imeweka wazi kabisa juu ya kwamba mwili ni hekalu la Roho mtakatifu yaani ni mahali ambapo Roho hufanya makazi sasa je mwili wako wewe huwa unatumika kufanya nini??? Je unamtukuza Mungu kupitia mwili wako? Je unauweza mwili wako katika usafi na utaua?? Jichunguze hata kama upo unaingia kanisani maana unaweza ukawa unaingia kanisani lakini bado humtukuzi Mungu.


MAMBO YA KUKUONYESHA UNAMTUKUZA MUNGU KWENYE MWILI WAKO

a). Mavazi yako

Kimekuwa ni kipengele ambacho kimeleta utata sana ndani ya kanisa la leo sana watu wanavaa mavazi ambayo ni ya aibu hata wewe usiyeyavaa huwezi kumuangalia mara mbili unaona fedheha kumtazama lakini yeye yuko huru kabisa.

1TIMOTHEO 2:9
"Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani"

Hapo biblia iko wazi kabisa inawataka wanawake wavae mavazi ya kusitiri (Kuhifadhi/ kutunza) mwili wake. Sasa mwanamke umevaa vimini unadai eti Mungu eti haangalii mavazi na hapo umejisitiri wewe si umevaa nusu u hi kabisa Mungu akurehemu.
Mwingine kavaa kisuruali kimembana makalio hata maeneo yake ya siri yanajichora alafu anadai Roho mtakatifu amemwambia avae hivyo au eti mchungaji wake kamwambia haina shida jamani tusimtukane Mungu kwa namna tunavyovaa.
"HIVI WEWE NA KAHABA/ MALAYA TUNAWATOFAUTISHA VIPI" ??? maana uvaaji wenu uko sawa hauna tofauti alafu unasema Mungu anaangalia Moyo!!!
Sikushangai ni kwasababu umepata mafundisho katika mukitadha usio sahihi mana biblia inasema

1TIMOTHEO 4:12
"Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika use zeemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.

Kuwa kielelezo ni kuwa mfano yani wengine wakuchukulie kama Reference njema sasa wewe umevaa kimini au Suruali imekubana maungio yako yote yanaonekana hata yale ya siri unafikili kuna mtu atataka wanawe wakuige??? Acha na mavazi yasiyo stahiki mheshimu Mungu.

b) Usemi na Maneno yako kiujumla

Watu wako kanisani lakini kwa matusi ndio wanaongoza alafu wanasema kwamba wamejitoa wakifu mbele za Bwana hapo ni kwamba wewe Mungu hayupo kwako ila unajifariji tu ni wakati wa kugeuka na kuacha yote ndiyo maana paulo alimtaka Timotheo  awe kieelelezo kwenye usemi wake. Mungu atusaidie tuwe na rijamu kwenye Maisha yetu.

AMOSI 6:5
"ninyi mnaoimba nyimbo za upuzi pamoja na sauti ya vinanda, na kujifanyizia vinanda vya namna nyingi, kama vile Daudi" 

Kuna watu wanaimba nyimbo ambazo hazimtukuzi Mungu hata kidogo yani zimejaa matusi alafu wanajifariji wao ni wana wa mfalme!! Lahasha ninyi mnajifariji na hamjajitoa kikamilifu mbele za Mungu isipokuwa mnajifariji tu. Amosi alipewa kuwaambia wana wa Israeli Kwamba Ole wao na wewe kama unafanya Hivyo Ole wako na Mungu akuhurumie kabisa.

3.KUJIPENDA.

Kila mwanadamu amepewa kujipenda na kuwapenda wengine kama nafsi yake. Sijawahi kuona mtu asiyejipenda ingawa wapo wasiojipenda na hao huwa mara nyingi wanakuwa na matatizo ya kiakili (Psychiatric disorders). Mwili wa mwanadamu hujipenda kwa kuvaa vizuri, kujihurumia, kupata favour au upendeleo au kibali.
Mungu alipoona ya kwamba mwili huwa unatabia hiyo ndio maana akatupa moja ya amri hii

MATHAYO 19:19
"Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako."

Biblia inaonyesha umpende Jirani yako kama nafsi yako sasa kumpenda jirani yako kama nafsi yako yani uwe na uwezo wa kufanyia jirani yako kwa namna ambavyo wewe unataka na Unapenda Kupata. Japo kuna watu wanafikiri kwamba ni jambo Rahisi sana eti kumpenda jirani yako kama Nafsi yako 
Pasipokuwa na Unafiki wowote utaungana nami kwamba mwili huwa unatabia ya kutaka kupokea wenyewe kwanza wenyewe na sio wengine na ndio maana tukifika hapo tunajikuta tabia za uchoyo zinaingia kwa mtu. Sasa ni wakati wa kujichunguza kwenye maisha yako je wewe hauna tabia za kiuchoyo na kama zipo basi jua ya kwamba kuna namna haujajitoa kikamilifu mbele za Mungu.
Kuna watu anaweza akawa anamiliki vitu vingi sana kiasi kwamba havina hata matumizi kwake lakini kuvitoa akawape wengine Moyo wake unamuuma na yuko kwenye Nyumba ya Mungu na anajiona ya kwamba amekwisha kujitoa kuwa dhabihu mbele za Bwana, lakini uhalisia ni kwamba bado amefungwa katika maarifa ya eneo hilo na anamuhitaji MUNGU ili amtoe hapo wewe ingia chumba chako cha ndani mtafute Mungu akujenge Upya usiwe na wakati wa kupoteza nafasi yako mbele za Mungu.
Ndugu yangu kitu kidogo ukifanyachokinatosha kabisa kukupotezea mahusiano yako na Mungu yani kosa Dogo tu linatosha kukuondoa kwenye lengo la Mungu. Embu angalia hapo chini

1 WAKORINTHO 5:6

"Kujisifu kwenu si kuzuri. Hamjui kwamba chachu kidogo hulichachusha donge zima?" 

Ukiangalia Paulo anajaribu kuwaonyesha ya kwamba maisha yao yanaweza yakaharibiwa na kitu kidogo kwahiyo kuwa makini sana Mpendwa katika Kristo Yesu juu ya Mambo madogo madogo unayoyafanya yasije yakakutoa kwenye kusudi na Mpango wa Mungu.
Tumekwisha kuona namna gani mtu anaweza kujiotoa kuwa wakifu Mbele za Bwana Na bila shaka kama umekwisha kusoma masomo yetu naamini umeshapata neema tayari ya kujielewa kiasi kama umeshajitoa mwili wako kuwa dhabihu mbele za Mungu au La. Sasa nifanye nini ili niweze kujitoa wakifu mbele za Bwana??


NAMNA KUJITOA MIILI YETU KUWA WAKIFU MBELE ZA BWANA

1. TOBA
Kitu cha kwanza ni kuingia katika toba yaani kuomba msamaha kwanza mbele za Mungu kwa yote ambayo umekuwa ukiyafanya hata kama umekuwa ukiingia kanisani ndiyo maana ukisoma sala ya Bwana ambayo YESU aliwafundisha wanafunzi wake, Yesu aliwaambia kwamba kila wanaposali wamuombe kwamba awasamehe makosa yao kama wanavyowasamehe wale waliowakosea 

MATHAYO 6:12
"Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu." 

Kwahiyo kuomba msamaha itakupelekea kuwa ni mwenye Sifa ya UTAKATIFU ambayo ni sifa kuu ya mtu aliye jitoa mwili wake kuwa Dhabihu takatifu mbele za Mungu. (Rudi ukaone sehemu ya pili ya Somo utaona)

2.KUTAFUTA  KUMJUA MUNGU
Kiukweli kufika hatua ukasema unamjua Mungu ni ngumu maana hauwezi kumchunguza Mungu lakini inatakiwa ujibidishe umuelewe MUNGU na ndio maana Ayubu anazungumza kwamba inakupasa umjue Mungu ili uwe nayo Amani.
AYUBU 22:21
"Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia."
Kwahiyo kupitia kumjua Mungu itakuepusha na WOKOVU WA KIFAFA (ona sehemu ya Pili ya Somo)

NAMNA YA KUWEZA KUMJUA MUNGU

a)  Kuwa watu wa Kumfanyia Mungu Ibada

Unapozungumzia swala la ibada unaweza ukachukulia ni kitu cha kawaida lakini ili tuseme kwanza kunayo ibada lazima kuwe na vitu vikuu vitatu MTOA IBADA (mwanadamu), MTOLEWA IBADA (MUNGU) pamoja na MADHABAHU (Sehemu ya kumfanyia Mungu ibada ambayo huwa inaambatana pamoja na utoaji wa Sadaka na Dhabihu mbalimbali) unaweza ukasoma habari za ELIYA katika kitabu cha 1WAFALME 18 sura yote utaelewa.

Kwahiyo kutoa kwetu ibada kutatufanya tuachane na WOKOVU WA KIFAFA na tutamtukuza Sana MUNGU kwenye maisha Yetu.

WAEBRANIA 10:25
"wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia."

Kwahiyo kukusanyika kwetu katika ibada kila kutatusaidia sana kuweza kuelekezana mambo mbalimbali juu ya kweli ya Mungu na namna ya kuweza kuishi maisha ya utaua/ utakatifu. Kuna baadhi ya watu ambao huamini kwamba hata wasipokusanyika kwenye nyumba za ibada wako salama lakini kiuhalisia hawako salama hiyo ni principle ya kiMungu ambayo kaiweka mwenyewe sasa kwanini uachane na utaratibu wake??

Mungu atusaidie sana tuwe watu wa ibada na haba ni njema Sana kuwa na Ibada za pamoja lakini kama ukikosa kuwa na Ibada za binafsi ujue bado kuna vitu utavikosa sana kwenye maisha yako. Mungu akufungue sana kama unafanya ibada za pamoja tu na haufanyi ibada ya kwako binafsi uelewe umuhimu wake.

b) Kuwa watu wa Maombi

Maombi ni mawasiliano baina ya muhitaji na mtoa majawabu ya mahitaji. Kwahiyo Maombi ni mawasiliano kati ya mwanadamu (ambao hawa ndio wahitaji) pamoja na Mungu( mtoa majibu ambaye huyu huwa anajitosheleza).

Kwahiyo lazima tuwe waombaji ili tuwe karibu na Mungu na itatusaidia kwa kiwango kikubwa kutokata tamaa na safari yetu ya wokovu tuliyo nayo

LUKA 10:22
"Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni."

YESU alipokuwa anawaambia wasijewakiingia majaribuni sio kwamba alimaanisha wasingekutana na majaribu ila ni kwamba hawatayatii hale majaribu ya shetani kwenye maisha yao yani wakaenda kwa namna majaribu yanataka wawe.

1 WAKORINTHO 5:17. "ombeni bila kukoma". 
Kwahiyo inatupasa siku zote tuwe watu wa kutaka kuwa na Maombi na kumtafuta Mungu tupo tutapata usalama lasivyo tunajipotezea nafasi mbele za Mungu wetu.

HITIMISHO 
MUNGU akubariki sana kwa kuchukua nafasi ya kusoma Somo hili japo ni SOMO lefu. Naamini kama umefuatana nami kutoka tangu tumeanza basi bila shaka Umepata vitu vya Msingi au kitu cha Msingi cha kukusaidia kwenye haya waisha ya WOKOVU. 
Kwa Ushauri na maswali tunaweza kuwasiliana kwa njia ya Simu au kwa njia ya Email. Pia Kama unaoushauri wa namna ya kuifanya kazi hii ya Mungu unaweza kunipa kupitia hizo njia za mawasiliano.
Ni wako mwalimu wa neno la Mungu 
Jackobo Abely Mbwaga (Bro Jackobo)
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441 and +255621036471

KUITOA MIILI YETU KUWA DHABIHU MBELE ZA BWANA (SEHEMU YA PILI)

SEHEMU YA PILI

BRO JACKOBO

Mwl; Jackobo Abely Mbwaga
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441 and +255621036471


UTANGULIZI
Bwana YESU asifiwe mwana wa Mungu baada ya kuona sehemu ya kwanza ya utangulizi juu ya somo lenye kichwa "Kuitoa miili yetu kuwa Dhbihu mbele za Bwana" karibu tuendelee kuangalia Kiini kamili cha somo lenyewe. Na kama haujabahatika kusoma sehemu ya Kwanza ningependa kukushauri ukaisome kwanza hiyo sehemu ili kuweza kupata mtiririko mzuri wa Somo. Unaweza ukasoma kwanza kupitia hii link juu ya Utangulizi wa somo letu hili bonyeza hiyo sehemu nyekundu itakulelekezaa moja kwa moja kwenye Somo SEHEMU YA KWANZA


KIINI CHA SOMO LETU
Ni vyema tuanze kuelewa tunapozungumzia mwili na Dhabihu ya mwili ni kitu gani

Mwili ni nini???
Kwanza mtu ambaye yuko hai ameumbwa na vitu vikuu vitatu (Nafsi, Roho na Mwili) yani katika hivyo tunakuwa kamili pasina kimoja hakunaga ukamilifu hata siku moja ni sawa na ukazungumzia Mungu baba pekee{Mungu huwa anakamilishwa kwa utatu wake mtakatifu- Mungu baba, Mungu mwana na Roho mtakatifu(MUNGU)}

1 Wathesalonike 5:23
"nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.” 

Waebrania 4:12
“  Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanyanafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.” 

Katika maandiko tuliyoyasoma hapo juu yanaonyesha moja kwa moja kwamba Kuna Katika mwanadalu kuna vitu vitatu ambapo ukiangalia Fungu la kwanza paulo anawaambia watu wa Korintho kufanikiwa katika nyanja zote tatu. Hata hili andiko la waebrania linaonyesha kuna tofauti kati ya nafsi mwili na Roho. Hapa Pana somo linajitegemea kama Mungu atatupa kibali basi tutafundishana juu ya mwili, Nafsi pamoja na Roho.

Neno“ mwili ” katika lugha ya Kiyunani ni “ Soma” humaanisha “ gamba la nje,au mavumbi ya ardhi yaliyofunika pumzi ya Mungu”. Kwahiyo mwili ni nini??

Mwili ni hili gamba la nje la mwanadamu lionekanalo.

Tumekwisha kuona maana ya mwili basi twende tulione andiko letu la msingi linalo  beba somo letu.

Neno la Msingi linalobeba somo letu hili ni kutoka kitabu cha 
WARUMI 12:1 
"Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana."

Maana ya DHABIHU YA MWILI
Dhabihu ya mwili ni Sadaka ya kujiachilia kwa Bwana ili Mungu ashike hatamu katika  mfumo mzima wa miili yetu yani katika hali ya utendaji wa kazi ya kila namna. 
Hapa viungo vyako vyote vinakuwa tayari kwa ajili ya kazi ya Mungu haijarishi uko vipi katika hali yako yaani uko kipindi cha uzuni,  kipindi cha Furaha, kipindi cha maumivu au kipindi kufarijika.
Mfano kuna muimbaji wa nyimbo za injiri kaimba nitaimba haleluya asubuhi, mchana na hata jioni pia akasema wakati wa furaha na wakati wa huzuni yeye ataimba.
Kwahiyo: mtu ambaye amejitoa dhabihu ni yule ambaye anaweza kumtukuza Mungu kwa wokovu aliopewa na Mungu pasina kuangalia sababu za nje zinazokumba mwili wake, tena huyu mtu hayuko tayari kurudi nyuma kwa namna yeyote.

SIFA KUU AMBAZO ANAKUWA NAZO MTU ALIYEJITOA KIWA DHABIHU MBELE ZA MUNGU

1. Utakatifu kwake ni kipaumbele katika yote
    
1Thesalonike 4:4 
"kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima"
Mtu huyu ambaye amejidhabihu mbele za Mungu anatenda mambo yake kwenye usafi wote kama vile Mungu alivyosema mtakuwa watakatifu kwakuwa Mimi Mungu ni mtakatifu

   2korintho 7:1
"Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu."

Paulo anazungumza na kanisa la Korintho kwamba waendelee kujitakasa yani waendelee kuishi maisha ya kumpendeza Mungu kwenye maisha yao ambayo hiyo inaonyesha wazi kwamba Alitamani kanisa lijitoe dhabihu kwa ajili ya Mungu liachane na kila namna ya uchafu wa kidunia.

2 Huyu mtu hana maisha ya kifafa i.e huyu mtu ana maisha ya unyoofu kiroho (SPIRITUAL CONSISTENCY LIFE)
Mtu mwenye kifafa huyu huwa anakuwa na maisha ya kuanguka na kuinuka yaani hana  mwendelezo( Consistency) ya kuuishi uhalisia wa Mungu

Isaya 26:7
"Njia yake mwenye haki ni unyofu; Wewe uliye mnyofu wainyosha njia ya mwenye haki."  

Kama nilivyokwisha tangulia kusema huyu mtu anakuwa anaenda katika unyoofu wa Mungu. Biblia imezungumzia haki ikimaanisha kutembea kwenye sheria za Mungu alizoziweka mwenyewe 
Ukisoma kitabu hiki huwa kina watatiza Wengi wetu

Mithali 24:16
"Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya."
Hapa biblia haijakupa ticketi ya wewe basi kutenda dhambi kwasababu utainuka bali inazungumzia kuinuka tena kozi kunavitu vinaweza vikawa vinakusonga upesi ukajikuta unakosea ila una nafasi ya kusimama tena.
Kumbuka neno la waebrania
Waebrania 6:4-6
"Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,  na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri."

Watu wanachukulia toba ni kama kitu cha kawaida lakini kiuharisia TOBA ya kweli ina gharama hata kama watakufariji kwa maneno kwamba MUNGU ni wa rehema, sawa, sijakataa lakini kumbuka pia kwamba Mungu ni mkali sana yeye ndiye aliwachoma SODOMA NA GOMORA KWA MOTO, sasa kama Mungu ni mkali kwanini tusifike hatua tuamue Kuishi maisha ya unyoofu??
Kama wewe wokovu wako ni wa kifafa yani unaanguka na kuinuka jua ya kwamba wewe bado haujajiweka wakifu mbele za Bwana yani haukujitoa dhabihu mbele zake Bwana.

3. Watu hawa huwa wanaitazama mbele ya katika upande chanya

Ayubu 19:25-26
"Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu:

Ayubu hakuwahi kuona kwamba safari yake ya kumuona Mungu haiwezekani licha ya kwamba walimvunja moyo na alipoteza thamani nyingi alizokuwa nazo. Hata ukafika hatua hata mke wake anamuambia mkufuru Mungu ufe lakini bado yeye alisimama pamoja na Mungu katika yote.

Jichunguze maisha yako wewe ni kwa namna gani umekuwa mwepesi wa kukata tamaa hata hutaki kuendelea na imani yako ya kumtafuta Mungu??? 

Wengine kuachwa na wachumba wao wamevunjika moyo wanasema kwamba basi waachane na Imani ya YESU kristo 
Acha mawazo mafupi utakuja kujuta na maamuzi yako hayo tafadhari tembea na Mungu atakusaidia. Kama utajiona uko mtu wa kukata tamaa kaa ukijua ya kwamba wewe bado hauja fika hatua ya kuuweka mwili wako uwe dhabihu mbele za Mungu maana tayari mwili wako umekukoseha tayari yaani umekupinga kufanya maauzi ya kiroho ambayo ni ya kimungu mwenyewe. 

Ili tuweze kuelewa ni kwa namna gani tunaweza kuitoa miili yetu kuwa Dhabihu ya kupendeza na takatifu mbele za Mungu embu tuangalie kazi za mwili huku tukiweka Muunganiko na namna ya kuitoa miili yetu kuwa dhabihu takatifu mbele za Mungu 

KAZI ZA MWILI

1. KUPOKEA NA KUTOA 
 Hapa ni nazungumzia moja kwa moja Kazi ya milango mitano ya fahamu ( Kuona, kunusa, kuonja, kusikia, na kuhisi)
Watu wengi tuko kanisani lakini bado hatujafika hatua ya kuelewa namna ya matumizi mazuri ya milango ya Fahamu yetu ambayo Mungu ametupa ili iwe kwa utukufu wa jina lake.
A) Kuona
Kazi ya kuona hufanywa na Macho sasa embu tuangalie namna gani sasa tunaweza jitoa miili yetu kuwa dhabihu kupitia kuona.

Zaburi 103:3
"Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami."

Hapa Mungu atuokoe kanisa sana maana watu umefika wakati wanaangalia mambo ya kishetani mfano kuangalia videos za ngono (Pornography) alafu bado wako katika nyumba ya Mungu alafu wanasema ya kwamba eti wamekwisha kutengwa Yani kwamba eti wamejitoa miili yao kuwa dhabihu mbele za Bwana iliyo takatifu... Embu acha huoo ujinga unajiangamiza nafsi yako mwenyewe. Wengine wanadai eti wanataka kupata utoshelevu wa kihisia za kimapenzi kwa namna hiyo (SEXUAL SATISFACTION) huku wakidai ya kwamba hawataki kufanya uasherati
Embu usijidanganye kama ni kijana jua miamko ya kihisia lazima itakuja kwako kwahiyo utakuwa ushazini tayari isipokuwa bado tu haujafanya moja kwa moja soma kitabu cha  (Mathayo 5:28) sasa wewe  endelea kujifariji kwamba umeuweka mwili wako kwa ajili ya kristo wakati tayari ushakuwa miliki ya shetani.

Kwahiyo kuwa Dhabihu katika kipengele cha macho ni pamoja na kuweka mambo mema mbele ya macho yako achana na tabia za kuangalia picha za ngono, mapicha ya wadada ambao wanavaa nusu uchi (i.e wanavaa chupi na sindiria tu kwa mabinti). Kama utaona pasina kutegemea basi huwezi kuwa umeibeba dhambi lakini kama utakuwa una dhamiria kabisa na kuenda kutazama hizo picha kwa akili zako mwenyewe hiyo ni dhambi kabisa mbele za Bwana tena usijifariji hata kidogo
MATHAYO 15:11
"Sikilizeni, mfahamu; Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi."
Hili fungu linaonyesha utayari wa mtu kufanya kitu ndio unamtia unajisi sio vile vitu hana utayari navyo yaani wewe unakubaliana na akili yako unaanza kufungua websites zenye picha chafu alafu unataka kuwa dhabihu ya kumpendeza Mungu??  Haiwezekani Mungu sio wa udhalimu kiasi hicho yeye ni wa haki na utakatifu (utaua). Hapo moyoni mwako utakuwa umejaa picha chafu alafu zinakutoka na wewe unakubali wito wake.

Kuuweka mwili wako dhabihu lazima ujitenge kwanza na uovu wa macho lasivyo utaendelea kuingia kanisani wakati bado unao uovu ndani yako na unaendela hata mda mwingine kuhubiri injiri au kuimba ila kumbuka kuhudumu kwako hakutakupa nafasi ya kuuona ufalme wa Mungu (MATHAYO 7:21) kwahiyo usiendelee kujifariji ya kwamba utafika kwa namna hiyo lasivyo unapoteza mda wako kuingia kwenye Nyumba ya Mungu.....

B) KUSIKIA
Hii hufanywa na Masikio
Zaburi 1:1-2
"Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku."
Chanzo cha imani yeyote huwa ni kusikia na pasipo kusikia hakuna  imani yeyote inaweza kuumbika kwa mtu (warumi 10:17) kwahiyo pale tunapokuwa tunajisahau na kukaa sana sehemu za watu wenye mizaa kuna vitu vya KIROHO huwa vinapungua sana na kuna baadhi ya vitu vya kidunia vinaanza kuumbika taratibutaratibu.
Sasa kama wewe umeamua kwenda na YESU lazima ukae mbali na watu wenye mizaa na hata kama waishi hapo wanapokaa basi usiende kwenye njia yao(Yaani usiwe na wewe ni mtu wa mzaa) maana kutakuwa hakuna utofauti wowote wako wewe na hao watu wanaokuzunguka na huku ndiko kujitoa kuwa dhabihu maana Mungu ndiye katupa maelezo haya kwamba tusikae kwenye njia na maeneo yenye mizaha ya namna kama hiyo.
Pia mizaha huwa inapunguza sana nguvu ya Mungu sana na nimeona sana kwenye maisha yangu mwenyewe. Kuna wakati nimewahi penda sana kufanya mizaa sana hiki kitu kilinipa sana wakati mgumu sana wakuishi maisha matakatifu na ndio maana tuliokoka ni watu ambao tumetengwa na Mungu sasa inakuwaje unafika wakati tunataka kule ambako Mungu ametutoa??? Tunapoteza haki zetu mbele za Mungu na Mungu anatuacha tuende tunavyotaka kuenda.

  C) KUHISI
Hapa nitaelezea hisia za kimwili ambazo mwanadamu anakuwa nazo (biological feelings) ukiringanisha na hisia za kiakili (mental feelings).
Mara nyingi hisia za kimwili tulizo nazo zinakuwa na uhusiano mkubwa na akili zetu hakuna hisia za kimwili zinaweza kuwepo pasipokuwepo na Akili
Sasa hapa kuna watu umefika hatua wanajirizisha miili yao kwa namna ambayo inaleta machukizo sana Mbele za Mungu... Embu tuangalie kitabu hikii

1WATHESALONIKE 4:4-5
"kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu"
Wapo watu ambao wana fanya USAGAJI, MASTERBATION, UZINZI NA UASHERATI lakini bado wanaingia kwenye nyumba za ibada na wanaona wamejitoa kwa ajili ya Mungu lakini Kiukweli wanajidanganya isipokuwa wamefungwa katika fahamu zao na wanaona ya kwamba ni kitu cha kawaida.
Kuna wakati nilitamani sana kuweza kujua juu ya maisha ya watumishi wengi sana wanavyokuwa wanaishi kwenye maisha yao. Kuna mtu mmoja wa mataifa aliniambia hao mnaowaita watumishi ndio watu ambao wanamambo ya ajabu sana wanajiendekeza sana kwenye maswala ya Ngono mno kiasi kwamba hata wao wanafika hatua wanaona ni bora kutokuokoka na mtumikia Mungu maana hao waliokatika utumishi ndio hao wanaongoza kwa kufanya Vitimbwi vya ajabu. 

Nilikuwa najiuliza sana ni kwanini watumishi wa Mungu wafike hatua wafanye mambo ya aibu kama hayo??? Lakini ashukuriwe Mungu nilikuja kufundishwa kwamba bado hawa watu wapo kwenye utumishi lakini Bado hawaji dhabihu mbele za Mungu hata siku Moja ila wapo tu wanaingia kwenye nyumba ya Mungu.

Pia kuna watu wapo kanisani (haswa vijana na mbainti wasio na ndoa) wamekuwa wakichezea hisia za jinsia tofauti alafu bado wanasema wamejidhabihu mbele za Mungu lakin kiuhalisia hakuna ukweli kabisa kama wamekwisha jidhabihu mbele za Mungu. Mungu akusaidie ndugu yangu utoke hapo ulipo kama unataka kumuona Mungu na unataka ujidhabihu mbele zake.

D) Kuonja 
Kuonja ni kazi moja wapo ambayo hufanywa na ulimi kwahiyo kwenye ulimi huwa kuna msingi mkubwa katika kujidhabihu mbele za Mungu 
Kwahiyo lazima ujue namna kuutumia vizuri ulimi wako. Ili tufike hatua ya kusema ya kwamba umejidhabihu ni lazima maneno yako yawe yanakolea Munyu yani yawe yanaleta ushuhuda mbele za Mungu na mbele za watu wanaokuzunguka.

 WAEFESO 4:29
"Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia."

Sasa napata wakati mgumu sana nikikuona mtumishi wa Mungu bado unatamka maneno maovu alafu unasema ya kwamba umejitoa kuwa dhabihu mbele za Bwana. Ndugu yangu Mungu akupe neema uwe na rijamu kwenye ulimi wako ili usije ukamkosea Mungu kwenye nyakati zako zote.
Mungu atusaidie sana kanisa maana tunaweza tukawa tunajifariji ya kwamba tuko pamoja na Mungu kumbe yeye ametuacha tutembee kama tunavyotaka siku zote sasa kuwa makini sana unachokifanya usije ukawa unaingia kumbe Mungu amekuacha Embu chukua nafasi mtake Bwana na nguvu zake akutoe hapo.

MITHALI 10:19
"Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili."

Usiwe mtu wa maneno Mengi sana kwenye maisha yako. Unapokuwa unaongea sana unaweza ukajikuta unatenda dhambi kiurahisi sana tena sana 
Nilikuwa najiulizaga sana hivi ni kwanini huwa inatokea kuna siku sipendi kabisa kuongea natamani kuwa mwenyewe nisizungumze nilikuwa kufunguliwa hapa kuna wakati Roho mtakatifu anakuwa anakuepesha na dhambi inayoweza ikawa inakunyemelea. Na suala hili kwa watu ambao wamewahi kuwa karibu na mimi wanaweza wakashuhudia kuna wakati huwa napenda kukaa peke yangu sitaki hata kuchangamana na watu.
Lakini sijakuambia uache kuongea na watu maana haohao watu ndio wengine wamebeba kusudi lako tena haohao watu ndio utakao takiwa kwenda kuwapa habari njema za kristo YESU.
Kwahiyo mtu aliyejitoa kuwa dhabihu mbele za Mungu anakuwa ni mtu aliyekuwa na control (Kujitawala) katika usemi wake.

MUNGU akubariki kwa kuchukua nafasi hii na kusoma SEHEMU YA PILI tutaendelea na kazi nyingine ya mwili pamoja na uhusiano wa namna ya kujitoa mbele za Mungu.

Kwa maswali au maoni unaweza ukawasiliana nami kwa njia zifuatazo

Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441 and +255621036471
www.jackobombwaga.blogspot.com

Wako Mwalimu wa neno la Mungu katika kristo Yesu 
Jackobo Abely Mbwaga (Bro Jackobo)

JE UNAYONAFASI YA KRISTO YESU NDANI YA MOYO WAKO???


Be faithful in ur ways

SOMO:JE UNAYONAFASI YA KRISTO YESUNDANIYA MOYOWAKO????? 

Mwl: Jackobo Abely Mbwaga
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441 

Bwana Yesu apewe sifa Wana wa Mungu..... napenda tushirikiane jambo hili kidogo ambalo liko katika mfumo wa swali...

"Je ndani ya maisha yako yupo kristo kweli au umekuwa mtu wa kwenda kanisani kama utaratibu wa kawaida?????? 

LUKA9:57 
"Yesu akamwambia, Mbweha wana pango,na ndege wa anganiwanaviota, lakiniMwanawaAdamu hana pa kujilaza kichwa chake"

Yule mtu alikuwa na nia ya kumfuata kristo lakini ndani yake alikuwa hajampa kristo nafasi hata kidogo na wewe je umempa nafasi gani kristo kwenye maisha yako???? 
lazima uwe mtu wa kuvumilia kutenda mema sikuzote ndipo utapata nafasi ya kuurithi ufalme waMUNGU lasivyo unajidanganya 

MATHAYO 24:13 
"Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. 

Maana kama umebadili mwiliwako na moyo wako kuwa sehemu ya uovu jua hukumu inakungoja haijarishi unaingia kanisani au hauingii 

MATHAYO 21;12
Yesu akaingiandani yahekalu, akawafukuzawote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni,akazipinduameza zawabadili fedha, na viti vyao waliokuwawakiuza njiwa

kristo hataki michanganyo hata siku moja ndio maaana alipoona wamegeuza sehemuya ibada kuwa kama gulio ilimkasirishasana YESU na ndivyo hivyo hivyo anavyochukia pale unapoachanjia ya MUNGU na kufanya Mambo unayoyataka yaliyo tofauti na neno lake.
wewe ni hekalu tena u sehemu ya ibada ya MUNGU ndani ya moyo wako. 
maana siku ile Mwana waMungu atakapokuwa kwenye kiti cha enzi atawabagua kama Mbuzi na kondoo kwa kadri ya mtu na matendo yake 

MATHAYO 25:31-46 
usikae kwa hasara Maharii ulipo maana hukumu inakuja tena usije muheshimuMungu kwa kinywa tu bali na MATENDOyako ya ambatane na namna kinywa chako kinavyozungumza 

MATHAYO 15:8-9 
"Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami Nao waniabudu bure,Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizoya wanadamu."

 Nipende kukusihi ndugu yangu badirisha njia zako kama bado hujatengeneza na MUNGU Yeyebado anatoa wito yeyote aliye na mzigo wa aina yeyote yeye atampumzisha (MATHAYO11:28 )

WARUMI10;10 
"Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu"

kazi yako ni kuamini na kumpa kristo maisha yako na sio kwenda kanisani tu na kufanya vitu visivyofaaa 

KUOKOKA NI LAZIMA SIO OMBI HUJACHELEWA NAFASI BADO IPO
MBONA KUJIONDOLEA MWENYEWE NAFASI YA YESU KRISTO NDANI YAKO...

TUNZA UTAKATIFU NA KAMA HAUNA FANYA KUUTAFUTA MAANA PASIPOKUWA NA HUO HAKUNA ATAKAYE MUONA MUNGU.

Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone:  +255766944441 and +255621036471
Www.jackobombwaga.blogspot.com

KUITOA MIILI YETU KUWA DHABIHU MBELE ZA BWANA (SEHEMU YA KWANZA)


Bro Jackobo

KUITOA MIILI YETU KUWA DHABIHU MBELE ZA BWANA

SEHEMU YA KWANZA

Mwl: JACKOBO ABELY MBWAGA
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441  and +255621036471

1.UTANGULIZI
Bwana YESU asifiwe mwana wa Mungu karibu sana tushiriki kwa pamoja katika somo ambalo Mungu kanipa neema ya kuweza kusema na kanisa la wakati huu kwa watu wote popote walipo kwa yeyote atakaye weza kuupata ujumbe huu ambao Mungu ameuweka ndani yangu.
Tutajifunza juu ya namna ya kujitoa miili yetu kuwa dhabihu mbele za Mungu yaani tukiangalia maana ya dhabihu, maana ya mwili na dhabihu ya mwili. 

Pia tutaangalia Dhabihu ya mwili huwa inahusisha vitu gani na ni kwanini baadhi ya watu wanaingia kanisani lakini bado hawajajitoa miili yao kuwa Dhabihu mbele za Bwana na utaweza kujielewa na nitaweza kujielewa kama nimejitoa mbele za Mungu au Bado naingia kanisani wakati bado sijajitoa kikamilifu mbele za Mungu.

Kwa Neema ya Mungu Somo hili litagawanyika katika sehemu kuu tatu au nne katika mfululizo wa kuwapa waamini mtiririko mzuri na kuwarahisishia watu waweze kupata muda wa Kusoma na kutafakari mbele za Mungu ili asiwepo hata mmoja wa kushindwa kuelewa.... Naomba tuende pamoja katika hili somo.

2. MAANA YA DHABIHU
DHABIHU ni matoleo ya hiari ambayo hufanywa na mwanadamu kwa Mungu wake katika kweli na utaua wote chini ya maongozi ya Mungu mwenyewe...

Matoleo haya huwa ni msingi mkubwa wa Imani iwayo yeyote haijarishi ni imani ya kweli au sio ya kweli na ndiyo maana hata shetani anapotaka kumfanikisha mtu yeyote lazima ampe mtihani wa kutoa sadaka haijarishi itakuwa vipi yaani namaanisha KAFARA. Hii ni mbinu ambayo shetani ameichukua kwa Mungu maana asili ya yote ni MUNGU pekee na shetani hakuhusika katika uumbaji uwao wowote na ndio maana huwa anaiga vitu vyake toka kwa Mungu(muumbaji wa vyote hapa umimwenguni) 

Matoleo haya huwa yanatolewa kama sehemu moja wapo ya kuonyesha shukurani mbele za Mungu kwa matendo makuu ambayo ameyafanya kwenye maisha ya Mtu....

Kutoka 3:18
"Nao watakusikia sauti yako; nawe utakwenda, wewe na wazee wa Israeli kwa mfalme wa Misri, na kumwambia, Bwana Mungu wa Waebrania, amekutana nasi; basi sasa twakuomba, tupe ruhusa twende mwendo siku tatu jangwani, ili tumtolee dhabihu Bwana Mungu wetu."
Sababu kubwa iliyowafanya wana wa israeli waende kumtolea Mungu Dhabihu ni kwasababu Mungu alikuwa pamoja nao na alionekana kwao kupitia mtumishi wa Mungu Musa ili awatoe katika ardhi ya utumwa....

Je wewe Mungu akionekana kwako huwa unafanya nini na huo unachukua hatua gani katika maisha yako unapokuwa unaishi hapa ulimwenguni???

Kutoka18:12 
"Yethro mkwewe Musa akamletea Mungu sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; na Haruni akaja, na wazee wote wa Israeli, wale chakula pamoja na mkwewe Musa mbele za Mungu."

Licha ya kwamba Yethro alikuwa ni mtu wa mataifa lakini bado alikuwa anaelewa umuhimu wa kutoa dhabihu mbele za Mungu. Baada ya Mungu kumtetea Musa alipokuwa anawatoa wana wa israeli nchi ya utumwa Yethro aliona amtukuze Mungu kwa namna ambavyo alikuwa amewaokoa akina Musa pamoja na wana wa israeli na mikono ya farao..

Kumbuka sadaka hizi huwa zinatolewa kwa moyo wa kupenda (HIARI) ila lazima uwe makini Maana Mungu kakupa utashi kwa kuwa amekuumba kwa mfano wake (Mwanzo 1:27). Sasa kama umeumbwa kwa mfano wa Mungu je wewe unaishi kwa mfano wa Mungu yaani unatoa matunda kama ya Mungu ndani yako (UPENDO hilii ni tunda  kuu ambalo Mungu ametuonyesha la kwanza kwenye maisha yetu tangu tulipokuwa tunaumba mpaka anapoamua kumtoa YESU kristo aje kwa ajili ya kutuokoa sisi...

Yohana3:16 
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

 usije ukajizalau ukajiona ya kwamba wewe sio kitu chochote..  nikukumbushe tu ya kuwa Mungu ametufanya sisi kuwa na tabia za kiuungu ndani yetu sasa unapojidharau nabaki kukushangaa sana
2petro1:4
"Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa"....

Sio tu agano la kale linazungumzia juu ya suala la Dhabihu embu tuangalie mifano midogo ambayo inaonyesha utoaji wa dhabihu

Matendo 14:8-18
Hapa utakutana na kiwete wa huko Listra ambaye Mungu alimfungua kupitia mikono ya Mtumishi wa Mungu paulo.. na baada ya kufunguliwa kwake watu walitaka kuonyesha shukurani zao kwa kumtolea dhabihu Paulo lakini Paulo aligoma kupokea hizo Dhabihu kwasababu alikuwa anajua ya kwamba anaye takiwa kutolewa Dhabihu ni Mungu.....
Sio tu hivyo Embu tazama huyu kuhani wa Zeu (The priest of Jupiter) ambaye hakuwa anamjua MUNGU wa kweli lakini bado alijua umuhimu wa utoaji Dhabihu sasa wewe unaingia kanisani lakini bado hajataka kumtolea Mungu dhabihu ya kweli juu ya mwili wako mwenyewe......

Siko kuzungumzia juu ya utoaji wa dhabihu kama seheme ya asilimia zako tisini(90%) baada ya kutoa zaka yako(10%) ambayo ni lazima kuitoa 
Naomba tuelekee kwenye kiini kikuuu cha somo letu juu ya  KUITOA MIILI YETU KUWA DHABIHU YA KUPENDEZA MBELE ZA BWANA...

Lakini kwa leo naomba nikuache na mtazamo huo wa maana ya Dhabihu. Lakini Chukua mda utafakari namna tulivyoona Dhabihu zilivyokuwa na zilivyotolewa kwa baadhi ya watu wengine..... Sogea sasa kama wewe utawezaje kujitoa kuwa dhabihu takatifu ya kumpendeza Mungu??? Naomba tukutane Sehemu ya Pili ya Somo hili.... Itaendelea

Kwa maswali pamoja na ushauri mbalimbali tunaweza kuwasiliana kwa njia zifuatazo

Wako
Mwl: Jackobo Abely Mbwaga
Phone;+255766944441 na +255621036471
Email: jackobombwaga@gmail.com
Www.jackobombwaga.blogspot.com

KUSIMAMA IMARA NDANI YA YESU KRISTO (sehemu ya Pili_Final)

Bro Jackobo Utakuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu Jina: Bro Jackobo Number: +255766944441 Email: jackobombwaga@gmail.com Blog website: ja...