KUFUNGIWA NIRA PAMOJA NA KRISTO/ USHIRIKA NA KRISTO (Sehemu ya Kwanza)


Bro Jackobo


Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu?? Karibu tujifunze kidogo neno la Mungu juu kufungiwa Nira pamoja na Kristo.

Utakuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

Maana ya Nira
Nira ni mti ambao unawaunganisha kwa pamoja ng'ombe (Maksai) wawili wanapokuwa wanalima.

Kwahiyo kufungiwa nira pamoja na Kristo ni hali ya kujijenga kimahusiano au kiushirika baina ya mwanadamu/Mwamini na Mungu wake kupitia Kristo Yesu.

2 Wakorintho 6:14
"Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?"

Ukisoma vizuri maandiko hapo juu utaona ya kwamba mtumishi wa Mungu Paulo alipokuwa anazungumza na wakorintho anazungumzia suala la kufungiwa nira na wasio amini kwa namna isiyo sahihi, kumbe Katika kufanya ushirika Kuna masharti na vigezo vya ushirika.

Hakuna ushirika wowote usio kuwa na vigezo na masharti lazima viwepo vitu ambavyo ndio kipimo cha kuweza kushirikiana baina ya watu hawa wakiwa kwenye kuhusiana. Kwahiyo Tunapokuja kuzungumzia suala la Kufungiwa nira pamoja na Kristo lazima viwepo vigezo vinavyotakiwa kuwepo ili huyu mwamini aweze kushirikiana na Mungu wake katika Utumishi ambao kaitiwa na Sio kwenda pasipo kuwa na utaratibu.

Sasa ukiangalia mwanzilishi wa kwanza wa Ushirika alikuwa ni Mungu mwenyewe ambaye yeye ndiye alitaka kuwa na uhusiano na mwanadamu ndio maana baada ya anguko la mwanadamu pale Bustani ya Edeni Mungu yeye ndiye alikuwa wa kwanza kutangaza kutaka ushirikaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Mwanzo 3:21 (KJV)
"Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika."

Kitendo cha Mungu kuwafanyia Adamu na eva mavazi ilikuwa ni kurudisha uhusiano waliokuwa wameshauharibu kwa kukosa utii kwenye maisha yao. Mavavi huwa ni Sitara na tena aliwatengenezea mavazi ya ngozi ikimaanisha kwamba kuna mnyama ambaye aliuawa ili yeye azichukue dhambi za Adamu na Eva, kwahiyo hatia ya makosa ya Adamu na Eva ilikuwa juu ya mnyama aliye uawa ili watengenezewe mavazi hawa watu. Huu ni upendo wa Ajabu sana Ambao Mungu ana muonyesha mwanadamu kwamba licha ya kuwa kakosea ila bado anatamani huyu mwanadamu awe na mahusiano na yeye, Hii ndio maana halisi ya kwamba Mungu katupenda kwa upendo wa mileleπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Yeremia 31:3 (KJV)
"Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu."

ukiangalia maandiko hapo utaona Mungu anamuambia Yeremia ili asije akajidharau bali ajichukulie katika heshima ambayo Mungu amempatia. Ndivyo ambavyo Mungu ametupenda na sisi na anataka tuishi na kujiona ni wenye thamani ili tusije tusikajidharau na ndio maana ametuita kwa fadhili zake ili tuweze kuwa karibu na yeye.

Sasa Mungu alikuwa ameona kikwazo kilichopo ambacho huwa kinawafarakanisha wanadamu na Mungu ambapo ni maovu au dhambi tunazozifanya. Maana Mungu huwa hawezi kuwa na Ushirika na mtu ambaye anazo Dhambi maana huwa dhambi zina mtenga mtu na Mungu wakeπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Isaya 59:1-4 (KJV)
"Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong'ona ubaya. Hapana adaiye kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu."

Sasa baada ya kuona hilo kuwa mwanadamu akiwa na Dhambi hawezi kushirikiana na yeye ili mlazimu amtume mwanawe Yesu kristo aje kuwa ondoleo la dhambi zetu tulizokuwa nazo wakati huoπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Yohana 3:16 (KJV)
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

kwasababu ya Upendo wake Mungu aliona ni vyema sasa akamtoa Mwanawake yeye azichukue dhambi zetu pale kalivari ili aweze kushirikiana na Sisi

Yohana 1:29 (KJV)
"Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!"

Waebrania 9:26 (KJV)
"kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake."

1 Timotheo 1:15 (KJV)
"Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi."

Ukisoma vifungu vyote hapo juu utaona Yesu kumbe ndiye alikuwa ondoleo la Dhambi kwa mwanadamu kwahiyo mimi ili niweze kushirikiana na Mungu lazima nikubali kazi ya msalaba ambapo yeye alizibeba Dhambi zetu pale kalivari.

Isaya 53:12 (KJV)
" Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji"

Isaya alipewa maono juu ya Yesu kuchukua dhambi zetu ndio maana hata pale msalabani Yesu alikuwa akilia Kwamba Mungu mbona kamuacha kwakuwa dhambi za ulimwengu zilikuwa juu yake na Mungu haambatani na dhambi hata siku mojaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Mathayo 27:46 (KJV) 
"Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?."

Kwahiyo kwasababu hiyo lazima sisi kama waamini tuwe na ushirika na Yesu Kristo wakati wote maana bila yeye hatuwezi kuwa na mahusiano mazuri na Mungu.

KAZI YA YESU KWENYE USHIRIKA WAKE NA MWAMINI ANAVYOIFANYA
Kuna mambo mengi Yesu huwa anayafanya kwenye maisha yetu ili tuweze kuwa na ushirika naye embu tuangalieπŸ‘‡πŸ‘‡

Mathayo 11: 20-30 (28-30) (KJV)
"Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi."

✍️✍️ Yesu alifanya miujiza lengo kuwafanya watu wa miji hiyo wamuamini kwa ajili ya kazi alizokuwa anazifanya
✍️✍️ Tena miujiza huwa inadhihirisha utendaji wa Mungu katika eneo japo hapa lazima kuwa makini maana hata shetani huwa anafanya miujiza ili aweze kuwateka watu waweze kumuendea yeye kwenye maisha yao.
N.B: Huo utendaji na udhihirisho wa Mungu kamili unatosha kabisa kumfanya huyu mtu aweze kuamini na kuingia kwenye pendo la Mungu yaani katika NIRA.
✍️✍️Yesu sasa anawaita watu wote wenye mizigo/Dhambi waje kwake ili aweze kuwatua hapo ndipo tunapo pata nafasi ya kuwa na ushirika na Yeye.

Mathayo 8:4 (KJV)  
" Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao."

Marko 1:44 (KJV)  
"akamwambia, Angalia, usimwambie mtu neno lolote, ila enenda zako ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe alivyoamuru Musa kwa kutakasika kwako, iwe ushuhuda kwao."

✍️✍️✍️ Yesu alimuambia mtu yule mwenye ukoma akajionyeshe kwa makuhani kama sehemu ya kuwafanya na wao waelewe na  waamini kazi ya Mungu ili na wao pia waingie kwenye ushirika wake wakati wote.

Embu turudi kwenye andiko letu la msingi la kwanzaπŸ‘‡πŸ‘‡

2 Wakorintho 6:14-18 (KJV)   
"Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.  Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,"

Paulo alikuwa anazungumza na watu wakorintho kujiepusha na mambo yafuatayo
1. Ibada ya sanamu
2. Kulichafua hekalu la Mungu
3. Kufanya uasi yaani kwenda kinyume na sheria ya Mungu
 4. Kuacha kumtazama Yesu kama mwanadamu yaani asiringanishwe.

Sasa ikiwa tunayaishi hayo hapo juu ndio kufungiwa Nira pamoja na wasio amini maana hayo ndiyo asili yao kwenye mambo kama hayo. Kwahiyo lazima kujitenga na kila namna inayoleta shida kwenye ushirika na Mungu wetu maana tunapo yaepuka hayo ndipo yeye anakuwa Baba kwetu nasi tunakuwa wana (Shirika au uhusiano au Nira inawekwa baina yetu na Baba).

hii ndiyo maana yesu alipokuwa akiwafundisha wanafunzi wake aliwajenga zaidi katika mahusiano mazuri zaidi na Mungu (Mathayo 6:9-15).

Paulo anawaambia watu wa Korintho kuweka mbali kila namna ya Uovu kwenye maisha yao akitamani Dhambi isitamkwe kwao yaani maisha yawe ya ushuda wa kristo maana kuishi maisha ya ushuhuda huwafanya wengine ambao walikuwa hawaamini kuvutwa kuja kwa kristo Yesu. Kwahiyo kama kanisa lazima tuishi kwa ushuhuda  mzuri ili tuwe na ushirika na Mungu ili hata wengine wavutwe kwenye huu ushirika na Mungu.

Mungu akubariki kwa kuambatana na mimi tangu tumeanza sehemu hii ya kwanza ya somo tutaendelea sehemu ya pili pale Mungu atatupa kibali. Unaweza ukamshirikisha na mwenzako juu ya neno hili ambalo Kristo ameliweka ndani yangu kwa ajili ya Kanisa lake la wakati huu


Ulikuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com


KIU YA KUMTAFUTA MUNGU (sehemu ya pili)


BRO JACKOBO

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu??
Utakuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com


Kutokana na baadhi ya maswali na michango nimekuwa nikiipokea nimeona ni vema niongezee kipengele cha pili kwenye somo juu ya KIU YA KUMTAFUTA MUNGU kwa upande wa Umuhimu wake

Kama haujasoma sehemu ya kwenza unaweza kubonyeza hapaπŸ‘‰πŸ‘‰SEHEMU YA KWANZA

Basi Nikianzia na maana niliyokuwa nimetoa mwanzoniπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 KIU hii ni hali ya ndani anayokuwa nayo mtu ili aweze kupata au kufanikisha jambo fulani alilokuwa na uhitaji nalo. 

 Kiu ya kumtafuta Mungu hiii ni hali ya ndani inayojengeka kwenye Nafsi ya mwamini kuhitaji ushirika na Mungu katika nyanja zote za maisha yake yani kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiroho.


UMUHIMU WA KUWA NA KIU YA KUMTAFUTA MUNGU KWA MWAMINI 
Sasa umuhimu wa kuwa na kiu uko hivi πŸ‘‡πŸ‘‡

1. Kumruhusu Mungu achukue hatamu ya maisha kwa kila jambo ambalo utakuwa unalifanya

 1 Wakorintho 10:31
 "Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu."

Ukisoma hilo Fungu unaona Paulo ana wausia watu wa Korintho kwamba kila kitu kinapofanyika kwa mwamini inatakiwa kufanyika kwa utukufu wa Mungu. Kwahiyo ukiwa na kiu utafanya mambo yako yote chini ya maongozi ya Mungu na papo hapo itakuwa Mungu anatukuzwa kwa kuwa mambo au mafanikio yako yatakuwa yamejengwa kwa Mungu mwenyewe πŸ™ŒπŸ™Œ


2. Inasaidia kujijengea heshima ya kibinafsi juu ya mambo yako [SELF DISCIPLINE]

πŸ‘‰πŸ‘‰Kwakuwa ndani ya nafsi yako imejengeka hali ya kumuhitaji Mungu hautafanya mambo kwa pupa maana nafsi yako itakuwa iko kwenye hitaji la kumtukuza Mungu kwahiyo maamuzi yako yatakuwa sahihi yaliyokuwa balanced..

Pia inabidi ujue kuwa kwenye nafsi ndiko kuliko UTASHI, UELEWA, MAAMUZI, AKILI NA MOYO(HIFADHI/KUMBUKUMBU).  Kwahiyo ukiwa na Kiu mambo yako na maamuzi yako yatajikiti kwenye kuhakikisha unampendeza Mungu si utajizuia kwa mambo mengi.

N.B hapo kwenye NAFSI ni somo linajitegemea ambapo inahitaji pia mda wa kutosha kuelewa ila kama Mungu atatupa kibali nitaliweka pia kwenye hii website yangu.

Ndio maana Suleiman anasema kwamba πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 Mithali 29:18
 "Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria."

Nia pia inakuonyesha jambo la kufanya ndio maana hukupa ile self discipline for anything you will be intending and interesting to do in future.

3. Kumfanya mtu awe na ushirika {FELLOWSHIP} bora na Mungu.

πŸ‘‰πŸ‘‰ Maisha ya ukristo sio tu kwenda kanisani bali ni uhusiano binafsi wa mtu na Mungu wake katika mazingira na nyanja mbalimbali za maisha. Kwahiyo mtu mwenye kiu huwa inamfanya atamani sana kukaa na Mungu kwa karibu kitu kinachomjengea msingi mkuu wa ushirika wake na Mungu.

 1 Petro 2:2
 "Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;"

Unapokuwa na kiu utakuwa mtu wa kujifunza maneno ya Mungu na kujikuta unaukulia wokovu ambako huko hufanya kuimarisha ushirika na Mungu wako.

4. Kuondoa hali ya mazoea kwenye utumishi wako 

πŸ‘‰πŸ‘‰Watu wengi wanafanya mambo kwa mazoea yaani bila kufwata maelekezo ya Mungu anavyotaka kwakuwa ndani ya maisha yao haiko Shauku au Kiu ya kumtaka Mungu bali wanafanya kama taratibu za kila siku.

Huduma yeyote ambayo umepewa na Mungu unahitaji unyenyekevu wa hali ya juu na sio kwakuwa unaweza au ulimuona mtu fulani anafanya basi na wewe unafanya. Embu ona hawa watuπŸ‘‡πŸ‘‡

Matendo ya Mitume 19:13-16
 "Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa."

Hawa wapunga pepo kwakuwa kiu yao ilikuwa kujipatia faida na sio kuwa na Yesu walijikuta wanaingia pabaya na kutendewa yasiyo faa na yule pepo mchafu.

Kwahiyo ukiwa na kiu hutafanya kwa mazoea kama hawa watu walivyofanya ili wajipatie heshima mbele za watu wa mji ule. Sasa wewe kwenye utumishi wako utatenda ili Mungu atukuzwe ndani yako na kukufanya hali ya mazoea kuto kuwepo ndani yako.


5. Kuruhusu Tunda la Roho kuleta matokeo ndani yako.

πŸ‘‰πŸ‘‰Mtu anapokuwa ameokoka huwa Roho mtakatifu anakuja ndani yake ila madhihirisho ya kujazwa na Nguvu au uwezo wa Roho mtakatifu hufuatia baadaye pale anapokuwa anaendelea  kuukulia wokovu japo kuna wengine pia hupata madhihirisho wakati huohuo baada ya kumuamini Yesu na kazi yake ya msalaba na umuhimu wake. (πŸ‘‰πŸ‘‰Mfano wanafunzi wa Yesu walipata madhihirisho baada ya Yesu kuondoka.. Soma Matendo 2:1-4 wakati wengine ka Kornelio walipokea papo hapo pindi anaipata injili.. soma Matendo 10:44-46 ila soma sura nzima ya 10 hiyo)

Sasa Roho mtakatifu huwa analeta yale matunda ya Roho kwenye MATENDO 5:22-24  Kuwa dhahiri kwa mwa mwamini. Kwahiyo kwa mtu aliyekuwa na kiu ndani ndio huruhusu hayo mambo kufanyika kwake na hii ndio huja kuleta utofauti baina ya mwamini na mwamini mwingine.

6. UNYENYEKEVU kuwa ni sehemu ya maisha yako.

Mtu ambaye bado hajajikita kumtaka Mungu ni rahisi sana kutaka yeye aonekane kwenye jambo lolote na sio Mungu. Ila huyu mtu akiwa na kiu anakuwa na hali ya uhitaji kiasi kwamba anakuwa ana unyenyekevu na kuwekelea mbali kila namna ya kiburi ndani yake kitu ambacho humfanya apate kibali mbele za Bwana. Embu ona watu hawaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 Mwanzo 11:3-4
 "Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote."

Ukiwaangalia hawa watu utagundua walitamani wajipatie sifa na kuacha kufuata agizo la Mungu la kutakiwa kutawanyika juu ya uso wa nchi yote kama alivyosemaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 Mwanzo 1:28
 "Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi."

Hapo unaona kiburi kiliinuka lakini kama wangekuwa wanamtaka Mungu basi wangefuata maelekezo yake ambayo ingeleta unyenyekevu ndani yao.

Pia siku zote mtu anayemtaka Mungu lazima awe na unyenyekevu ndani yake maana Kwake maelekezo ya Mungu kwake ni Lulu na uhai maana sisi katika kristo huwaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Matendo ya Mitume 17:28
"Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake."

Mungu akubariki kwa kusoma sehemu hii ya pili. Unaweza kuwashirikisha na wengine pia

Ulikuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Phone; +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

KIU YA KUMTAFUTA MUNGU (Sehemu ya kwanza)


Bro Jackobo


Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu? Karibu tujifunze kwa pamoja hili somo ambalo Mungu amenipa

Utakuwa nami mtumishi katika Bwana wetu Yesu kristo
Name: Bro Jackobo
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441


KIU hii ni hali ya ndani anayokuwa nayo mtu ili aweze kupata au kufanikisha jambo fulani alilokuwa na uhitaji nalo.

Kiu ya kumtafuta Mungu hiii ni hali ya ndani inayojengeka kwenye Nafsi ya mwamini kuhitaji ushirika na Mungu katika nyanja zote za maisha yake yani kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiroho.

Zaburi 42:1-2
"Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? "

Daudi anajaribu kuonyesha uhitaji wake wa ndani kwenye nafsi yake namna ambavyo anatamani kuwa na ushirika na Mungu, anaonyesha kuwa na njaa kwenye nafsi yake ili aweze kufanya maamuzi sahihi ya kuweza kuamua vyema kwenye maisha yake ya kila siku. Daudi alihisi kama vile Mungu yuko mbali na yeye kwahiyo alitamani sana awe karibu na Mungu kwenye ushirika.

Daudi alipopita nyakati za Giza aliona kama machozi yake yamekuwa ndio chakula chake (Utoshelevu wake) lakini yeye akaona Utoshelevu zaidi ni kuwa na Ushirika na Mungu ndio maana akawa anahitaji nafsi yake ishikamane na Mungu.

NB: Mwanadamu kaumbwa na vitu vikuu vitatu yaani Mwili, Roho na Nafsi, Ambapo nafsi ndio kama daraja lililopo kati ya mwili na Roho lenye kubeba maamuzi ndani ya mtu.

Mungu alipomuumba mwanadamu alimfanya awe chombo cha mahusiano (Relational being) na ndio maana kila wakati aliwatembelea kipindi cha jioni katika ile bustani ya Edeni.

Mwanzo 3:8
"Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone."

Kwahiyo Mungu anatamani kuona ushirika mzuri baina ya mwanadamu na yeye wakati wote na ndio maana baada ya uhusiano na mwanadamu kuharibika pale bustani ya edeni alimleta Bwana Yesu ili afanye uimara wa ushirika huu.

Mwamini anayo kila sababu ya yeye kujenga uhitaji mkuu wa ndani mwenyewe kutaka kukaa na Mungu kwa karibu kimazungumzo zaidi.

MAMBO YANAYO DHOHOFISHA KIU YA KUMTAFUTA MUNGU.

1. Dhambi/Uovu
Mtu afanyapo maovu au Dhambi Upendo ndani yake huwa unashuka kiasi kwamba anashindwa kuona uzuri wa Mungu kwenye maisha yake na kumfanya asiwe na uhitaji wa kuwa na ushirika naye. Hii ndiyo maana yesu alisema maneno yafuatayo πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Mathayo 24:12
"Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa."

Pia Dhambi ina tabia ya kumfukuzisha mtu kuwa karibu na Mungu, kwahiyo huyu mtu anakuwa na haja ya kutoka na kukaa mbali na Mungu. Mfano Adamu na Eva baada ya kula Tunda waliamua kwenda kujificha maana ile Dhambi yao iliwaondolea ujasiri wa kukaa kwenye utukufu wa Mungu kiasi kwamba hawakuweza kustahimili kusikia sauti yake.

Mwanzo 3:10
"Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha."

Pia uovu wa mwanadamu una tabia ya kumfanya yeye akae mbali na Mungu maana huleta faraka baina ya huyu mwamini na Mungu wake.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Isaya 59:2
"lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia."

Kwahiyo kama utaruhusu dhambi na Maovu kuwa sehemu ya maisha yako yatakuwa yanakufanya wewe usimpende Mungu, pia kukufanya uwe na faraka na Mungu na pia kumruhusu Shetani akupige upofu katika macho ya moyo wako hali ambayo huleta ugumu wa wewe kuwa na shauku ya kuwa na ushirika na Mungu.


2. Roho ya Mazoea
hii ni hali ambayo huwapata watu waliokuwa na ushirika mzuri na Mungu pale wanapoacha kuisikiliza sauti ya Mungu na kuishi kwa namna wanataka bila ushirika wa mzee wa siku mwenyewe.

Mungu anataka kila jambo tulifanyalo tulifanye kwa utukufu wake na chini ya maongozi yake.

Waamuzi 16:20
"Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa Bwana amemwacha."

Samsoni alijizoeza kwamba yeye ni mwenye nguvu wakati wote hakujua kwamba ili yeye awe na nguvu lazima patano la agano liwepo yaani vishungi saba vya nywele na ndio maana baada ya kuviondoa aliishiwa Nguvu.

N.B Lazima ukae na kujua kila Agano linalofanyika huwa linakuwa na vigezo na masharti pindi vigezo na masharti yanapopuuzwa basi uhalali wa agano huwa unaondoka kabisa kwenye maisha ya mtu.

Hali ya mazoea huwa inafanya mtu asiwe na haja ya kuhitaji kuwa na maelekezo kutoka kwa Mungu kitu ambacho hupelekea yeye huyo mtu asiwe na shauku ya kuwa na ushirika na Mungu wake kwakuwa anakuwa ana hali ya kujiona yeye ana utoshelevu wake mwenyewe.

3. Roho ya Kiburi

Kiburi ni hamu isiyoratibiwa ya kujipatia ukuu dhidi ya wengine pengine hata dhidi ya Mungu.

Au

Kiburi ni hisia na fikra zilizopotoka kuhusu ukweli na uhalisia wa mambo namna yanapaswa kuwa .

Mwanadamu ukifika hatua anatamani kujitengenezea nafasi kubwa mbele za watu humfanya yeye asiwe mtu wa kujishusha. Embu tuangalie hiki kisaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Mwanzo 11:3-4
"Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote."

Sasa ukisoma hicho kisa utaona namna ambavyo watu walipotaka wao wajitengenezee jina na sifa nyingi na sio kumpa Mungu utukufu.
Hao watu wa kwanza baada ya ile gharika walikuwa na lugha na usemi mmoja kiasi kwamba wakakubaliana kufanya jambo kwa ajili ya wao wajipatie utukufu.

Watu hawa waliutamani ukubwa kiasi kwamba wakaacha mpango wa Mungu aliokuwa amewaagiza kuijaza nchi wao wakataka kukaa sehemu moja kwa matakwa yao binafsi. Ona hapaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Mwanzo 1:27-28
"Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi."

Ukisoma hapo Mungu alipokuwa amekwisha kuwaumba adamu na Eva basi lengo lake ilikuwa ni kuwa waijaza dunia yote lakini Kiburi cha hawa watu kikawafanya watu hawa wapingane na mpango wa Mungu.

Kwahiyo kiburi kitakufanya ukatae mpango na utaratibu ambao Mungu amekuwekea uufatwe kitu ambacho kitakufanya usitake ushirika kuwa na Mungu.

Sasa tumeona namna ambavyo baadhi ya vitu hudhohofisha watu kuwa na ushirika na Mungu basi ngoja tuone namna gani tunafanya ili tuweze kuwa na kiu ya ushirika pamoja na Mungu.

MAMBO YA MSINGI ILI MTU AWE NA KIU YA KUMTAFUTA MUNGU

1. Kuacha kuishi maisha Ya Dhambi
hili ndilo jambo la kwanza kwa mwamini ambapo yeye kama yeye hawezi kuacha dhambi ila kuacha kwake dhambi ni kupitia kumuamini Kristo Yesu ndiye atampa uwezo wa kuishinda dhambi.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Mathayo 11:28-30
" Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi."

Kwahiyo kwa Yesu huwa hatuendi angali tumekuwa watakatifu bali yeye hutuondoa mizigo ya Dhambi zetu na ndio maana hata kama mtu kakosea hatakiwi kumkimbia Mungu bali amuendee ili yeye amtue zile shehena za Dhambi.

Pia kama mtu atakosea lazima akumbuke kutubu mbele za Mungu kwa kosa lolote ambalo kalifanya maana Mungu wetu ni mwaminifu huwa anasameheπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Ufunuo wa Yohana 2:5
"Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu."

Kwahiyo kupitia kuacha dhambi kutasaidia wewe kumuhitaji sana Mungu pia upendo wako kwa Mungu utaimarika sana maana Dhambi hudhohofisha upendo (hii tumekwisha kuiona mapema).

2. Kuacha kuishi kwa mazoea
Hii itakufanya uwe mnyenyekevu sana mbele za Mungu na kujikuta wakati wote unamsikiliza Mungu na nafsi yako inajengeka katika ibada ya kuhitaji ushirika na yeye

Wafilipi 2:5-8
" Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; "

Lazima ujifunze kuwa na hali ya unyenyekevu kama Kristo Yesu namna alivyo kuwa mnnyenyekevu ndipo utaweza kuimarika ndani na kujikuta hali yako ya ndani inahitaji kuwasiliana na Mungu wakati wote.

Hali ya unyenyekevu ilimfanya Yesu kuwa mtu wa kumfanyia Mungu Baba Ibada na hii ikiwepo kwetu tutajikuta ni watu tunaopondeka na kuwa watu tutakao kumfanyia Mungu Ibada.

3. Kuwa na Roho Mtakatifu pamoja na kujazwa
Roho mtakatifu ni nguvu yaani uwezesho wa mwamini katika kutenda kazi ya Mungu. Sasa mtu anakuwa na Huyu Roho mtakatifu anakuwa anatiwamoyo wa kuendelea kumtafuta Mungu na kujikuta ile hamu ya kuwa na Mungu inakuwa kubwa.

Matendo Ya Mitume 1:8
"Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi."

4. Kuwa na Neno la Mungu ndani yako
Neno la Mungu huwa linatuonyesha namna maisha yetu yalivyo mbele za Mungu kiasi kwamba unaweza kujitambua wewe uko vipi mahusiano yako na Mungu pia linakuonyesha kinachokupasa kukifanya kwa wakati.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡


Zaburi 119:105
"Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu."

Hii ndio maana Paulo pia alisema kwamba neno lake Kristo Likae kwa wingi katika mioyo yenu

Wakolosai 3:16  
"Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu."

Pale neno la Mungu linapokuwa limeujaza moyo wako basi huwa linakufanya ujitambue wewe ni nani na jambo gani unatakiwa kuwa nalo. Kwahiyo linakuongoza unakotakiwa kwenda.

Hii itakufanya wewe ujitambue wewe ni kiumbe umeumbwa kuwa kiumbe cha mahusiano (Relational being)  na Mungu ko utajikuta kila wakati unatamani kushirikiana na Mungu wako.

5. Kuwa mtu wa maombi
Maombi ni mawasiliano baina ya pande mbili yani Mungu na mwamini yaliyojengeka katika mfumo wa mahusiano na sio swala la kupeleka tu shida zako mbele za Mungu.

Watu wengi hawapati matokeo ya kile wanachokiomba kwakuwa wameyafanya maombi ni sehemu ya kupeleka tu shida zao mbele za Mungu pasina kujua kwamba kuwa ni sehemu ya kimahusiano na Mungu wako. Hii ndio maana uliambiwa hiviπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

1Wathesalonike 5:17
"ombeni bila kukoma"

Ingekuwa suala kuomba ni wakati wa shida basi isingekuwa kuomba bila kukoma. (Kama Mungu atatupa neema nitaandaa somi juu ya Maombi kiundani zaidi).

Sasa unapokuwa kwenye maombi huwa watu wanatiwa Moyo pia wanapokea nguvu ya uwezesho kuendelea kukaa kwenye ushirika na Mungu kitu ambacho hukusaidia wewe kuwa na hamu na furaha ya kuendelea kuwa na ushirika na Mungu.

Mungu akubariki kwa kufuatana nami kwenye somi hili unaweza ukawa shirikisha na wengine piaπŸ™πŸ™πŸ™


Unaweza kusoma sehemu ya pili πŸ‘‰πŸ‘‰πŸ‘‰SEHEMU YA PILI hii nimei update baada ya wengi kuhitaji kujua umuhimu wake

Ulikuwa nami mtumishi katika Bwana wetu Yesu kristo 
Name: Bro Jackobo
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441

KIPI KITUMIKE KATIKA KUOA AU KUOLEWA??? LOVE♥️♥️


Bro Jackobo


Bwana Yesu asifiwe mtu wa Mungu???
Nilikutana na hili swali na mimi nikawa na jibu lake... Karibu tulione

Swali: Je inakaaje hapa maana tunasikia kwambaπŸ‘‡πŸ‘‡

"Mwanaume unatakiwa kuoa mwanamke anayekupenda sana kuliko wewe unavyompenda au Mwanamke unatakiwa kuelewa na Mwanaume anayekupenda sana kuliko wewe unavyompenda"

Utakuwa nami mchambuzi wako
Name: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

anajibuπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡...

Tunashukuru Mungu kwakuwa tunapata changamoto na mawazo mbalimbali yanayotupa akili na ufahamu wa kutafuta kujua kweli.πŸ™πŸ™πŸ™


Tatizo sio hiyo statement ila hiyo statement iko na a lot of pains behind...

Niliwahi kusikia wakisema "There is unspoken truth within the song that someone loves the most"
sasaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

People have faced with a lot of "Psychological tortures and disappointments" following true love they had before, sasa baada ya kuumia wameshikwa na kitu kinaitwaπŸ‘‡πŸ‘‡ "Post Traumatic stress Disorder {PTSD}" sasa hii inawagharimu maana wanahisi wakiwa na mtu wanampenda sana wanaweza kuumizwa tena mara ya Pili. Sasa ego zao ndio zinawafanya wawe na little faith kwamba watampata mtu ambaye ni mwaminifu siku zote ili kuepuka kuumia mara ya piliπŸ™ŒπŸ™Œ.

So watu wanakuwa na Denial kwenye kuwa na mtu anayempenda maana kiuhalisia hakuna ambaye hataki kuoa au kuole na mtu ampendaye sana. Kuna mengi ya kusema but acha niishie hapo hope utakuwa umenipata kidogo......

labda kimsingi inatakiwa iwe namna gani kimsingi??πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

What will make people bounded together firmly is True love only kwahiyo lazima umpende mtu unayetaka kumuoa au kuolewa naye.

Mwingine atasema mwanamke anaheshimu ila Mwanaume anapendaπŸ˜‚πŸ˜‚ sawa sikukatalii ngoja nikuonyeshe kitu hapa ndugu yanguπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Waefeso 5:24-25 (KJV)
"Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;"

Msingi wa Ndoa ni Yesu Kristo na kanisa. Mwanaume akitaka kuoa lazima ajipime kwa kigezo cha Kristo Yesu katika kumpenda mtu huyo anataka kumuoa ukiona huwezi kuwa kama Yesu alivyo na anavyolipenda kanisa basi wewe hutakiwi kumuoa huyo mtu maana kuna wakati mambo yanaweza yakaenda kombo na itatakiwa hiviπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

πŸ‘‰Ujitoe sadaka kwa ajili yake na uwe radhi hata kufa kwa ajili ya mkeo_
πŸ‘‰uwe tayari kumsamehe katika kila kosa atakalokufanyia ndio maana biblia inazungumza masuala ya kutokuwa na uchungu na wake zenu_
πŸ‘‰Kuwa tayari kudharilishwa kwa ajili ya huyo mke wako au mtu wako ili apate heshima mf Soma Hosea kwa Gomeri ilikuwaje {kitabu cha Hosea} pia Yesu mwenyewe kwa ajili yetu sisi. N.k

Hapo nimekuonyesha nafasi kidogo ya namna mwanaume anatakiwa kumpenda mkewe. Sasa ukiona kwa namna hiyo huwezi kumpenda mkeo au mtu huyo uko naye kwa mpango wa ndoa basi wewe hauko tayari kwenda na huyo..........

Sasa twende kwa upande wa mwanamkeπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Tumekwisha kuona msingi wa Ndoa ni Yesu Kristo na KanisaπŸ™ŒπŸ™Œ

Yaani YESU=Mume na KANISA=MKE. Ukitaka kuelewa kwanini wanasema mwanamke amtii mume basi jifunze kwa kanisaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Yohana 15:16 (KJV)
"Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni."

Ukisoma hapo ni kwamba Yesu ndiye anachagua halafu kanisa linatii wito ndipo imekuja hii concept broπŸ™ŒπŸ™Œ kwamba Mwanaume atamchagua mwanamke anayemtaka kwa maongozi ya Mungu mwenyewe then mwanamke atapima na kumkubali au kumkataa sasa ikiwa amemkubali inabidi afuate yale maagizo ya mumewe yaani atiiπŸ™Œ sijui umenipata concept ilipokuja kuanzia eehhπŸ€”πŸ€”πŸ€”

sasa kwanini nimesema lazima kuwe na True love between them from both side yani Kijana wa kiume na BintiπŸ‘‡πŸ‘‡

Ona hapo mtumishi
Yohana 14:15-16 (KJV)
"Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;"

Yesu anawaambia wanafunzi/Kanisa wakimpenda watashika amri zake ni sawa niseme hivi..πŸ‘‡πŸ‘‡

"Mke akimpenda mume atamtii yaani atashika sheria za mumewe"

Sasa kinachoweza kumfanya Mke aweze kumtii mumewe ni Yeye kumpenda mumewe bila kumpenda hawezi kumtii yaani mimi kanisa nisipompenda Yesu piga ua galagaza siwezi shika sheria zake.

Kwahiyo mke sio kwamba alipoambiwa amtii mumewe basi hatakiwi kupenda ila nikujaribu kuonyesha msisitizo wa kiuongozi ndani ya Familia na mgawanyiko wa kimajukumu ili kwamba kusije tokea migogoro isiyo ya lazimaπŸ™ŒπŸ™Œ

Kama ni binti lazima uwe na mtu ambaye unampenda.

Hilo wazo la kwamba "Umuoe mtu anayekupenda sana au uolewe na anayekupenda sana" litaleta shida kubwa katika ndoa kikubwa lazima kuwepo kwa upendo baina ya watu hao ndipo wataweza kuwa pamoja na Roho wa Mungu atawafunika katika kila kitu wakifanyacho. Huwa ninasema hivi siku zoteπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

"Love is life, out of Love there is no life"

So without Love no marriage that will exist.

So Mwanamke hajawa excluded kupenda.

Moja ya dhara kubwa ya kuishi ma mtu usiyempenda ni kwambaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

"Ukiwa na mtu usiyempenda huwezi kuwa committed kwake na kuna uwezekano mkubwa mkaachana maana bado haujampenda huyo mtu vizuri."

Yaani kuna watu wanafikiri kwamba zile sifa za upendo kwenye wakorinthoπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

1 Wakorintho 13:4-8(KJV)
"Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika."

Hufikiri kwamba hizi sifa hazitumiki katika ndoa kitu ambacho ni wazo potofu. Sasa huu upendo unatumika katika ndoa bila hivyo hamtaweza kudumu pamoja.

LET LOVE LEAD❤️❤️

Ulikuwa na mchambuzi wako
Name: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

KWENDA MPAKA MWISHO PAMOJA NA MUNGU {SEHEMU YA TATU_FINAL)


Bro Jackobo


Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu?? Karibu tumalizie sehemu ya tatu na ya mwisho ya somo Letu.

Utakuwa nami mpendwa katika Kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Phone: j255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

Baada Ya kuona sehemu ya kwanza juu ya maana ya kwenda mpaka mwisho pamoja na Mungu na kuangalia kwanini watumishi wengi wamekuwa wakianza vema lakini wakiishia njiani.

Sasa tutaenda kuangalia mambo yanayoweza kufanyika kumsaidia huyu mwaminini kuweza kufika mwisho pamoja na Mungu. 

Kama haujaona sehemu ya kwanza unaweza bonyeza hapa➡️SEHEMU YA KWANZA. Pia unaweza angalia sehemeya pili hapa➡️SEHEMU YA PILI

 MAMBO YA KUFANYA ILI KUMUWEZESHA MTU KUWEZA KUFIKA MPAKA MWISHO PAMOJA NA MUNGU.

 1⃣. KUMJUA MUNGU
Mwamini anapaswa kumjua Mungu kwa kila nyanja ya maisha mfano kiuchumi, kijamiii n.k ili apate kujua ule utendaji wa ki-Mungu namna ulivyo kwa kila sehemu ambayo atakuwa yupo. 

Kiukweli kufika hatua ukasema unamjua Mungu ni ngumu maana hauwezi kumchunguza Mungu lakini inatakiwa ujibidishe umuelewe MUNGU na ndio maana Ayubu anazungumza kwamba inakupasa umjue Mungu ili uwe nayo Amani.

 AYUBU 22:21
 "Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia."

Kwahiyo kupitia kumjua Mungu itakuepusha na WOKOVU WA KIFAFA (yaani maisha ya kuanguka na kusimama) kwahiyo utakuwa ni mtu ambaye hauwezi kutikiswa na jambo lolote kwenye maisha yako ya kila siku kwahiyo utaweza kutembea na Mungu kwenye nyakati zote ambazo ziko kwenye maisha yako ya kila siku hata kama zinakupa huzuni.

 Sasa ni kwa namna gani mtu anaweza akamjua Mungu??

 a)  Kuwa watu wa Kumfanyia Mungu Ibada
Unapozungumzia swala la ibada unaweza ukachukulia ni kitu cha kawaida lakini ili tuseme kwanza kunayo ibada lazima kuwe na vitu vikuu vitatu MTOA IBADA (mwanadamu), MTOLEWA IBADA (MUNGU) pamoja na MADHABAHU (Sehemu ya kumfanyia Mungu ibada ambayo huwa inaambatana pamoja na utoaji wa Sadaka na Dhabihu mbalimbali) unaweza ukasoma habari za ELIYA katika kitabu cha 1WAFALME 18 sura yote utaelewa.

Kwahiyo kutoa kwetu ibada kutatufanya tuachane na maisha ya kuanguka na kusimama kila siku bali yatatupa kukaa na Mungu mda wote ambao tutakuwa tu wazima.

 WAEBRANIA 10:25
"wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia."

Kwahiyo kukusanyika kwetu katika ibada kila siku kutatusaidia sana kuweza kuelekezana mambo mbalimbali juu ya kweli ya Mungu na namna ya kuweza kuishi maisha ya utaua/ utakatifu. Kuna baadhi ya watu ambao huamini kwamba hata wasipokusanyika kwenye nyumba za ibada wako salama lakini kiuhalisia hawako salama hiyo ni kanuni ya kiMungu ambayo kaiweka mwenyewe sasa kwanini uachane na utaratibu wake??

Mungu atusaidie sana tuwe watu wa ibada. Lazima utafute  kuwa na Ibada za pamoja lakini kama ukikosa pia kuwa na Ibada za binafsi ujue bado kuna vitu utavikosa sana kwenye maisha yako. Mungu akufungue sana kama unafanya ibada za pamoja tu na haufanyi ibada ya kwako binafsi uelewe umuhimu wake.

 b) Kuwa watu wa Maombi

Maombi ni mawasiliano baina ya muhitaji na mtoa majawabu ya mahitaji. Kwahiyo Maombi ni mawasiliano kati ya mwanadamu (ambao hawa ndio wahitaji) pamoja na Mungu( mtoa majibu ambaye huyu huwa anajitosheleza).

Kwahiyo lazima tuwe waombaji ili tuwe karibu na Mungu na itatusaidia kwa kiwango kikubwa kutokata tamaa na safari yetu ya wokovu tuliyo nayo

 LUKA 10:22
 "Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni."

YESU alipokuwa anawaambia wasijewakiingia majaribuni sio kwamba alimaanisha wasingekutana na majaribu ila ni kwamba hawatayatii yale majaribu ya shetani kwenye maisha yao yani wakaenda kwa namna majaribu yanataka wawe.

 1 WAKORINTHO 5:17.
 "ombeni bila kukoma".

Kwahiyo inatupasa siku zote tuwe watu wa kutaka kuwa na Maombi na kumtafuta Mungu ndipo tutapata usalama lasivyo tunajipotezea nafasi mbele za Mungu

2⃣.KUONGEZA SHAUKU YA KIU YA HAKI
Shauku ni nia ya ndani ya kufanya jambo fulani kwa viwango vikubwa.
Endapo mwamini ataluwa anahitaji kwa kiwango kikubwa kuwa na haki mbele za Mungu itamfanya Mungu amjibu matamanio yake ambayo yuko nayo.. ona hapa πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 Mathayo 5:6 
 "Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa."

Ukiangalia hapo Yesu alikuwa akizungumza na wanafunzi wake kwamba yeye ambaye akiwa na njaa na kiu ya haki yeye atashibishwa na Bwana, kwahiyo endapo kama ukiwa na shauku ya haki itakufanya ukawa unaishi maisha ya kumpendeza Mungu wakati mwingi maana wakati wote utakuwa ukitaka kumfanyia Mungu yale yanayompendeza na kujikuta unaishi maishi ya kuwa karibu na Mungu. Hii itakupa uwezo wa mda wote kuwa karibu na Mungu.

3⃣. KUENENDA KATIKA ROHO MTAKATIFU

Hii ni hali ya mwamini kuweza kuenda au kuishi kulingana na maelekezo ya Roho mtakatifu.
Maelekezo ya Roho mtakatifu huwa yanamfanya mwamini kuishi maisha ambayo yanamtukuza MunguπŸ‘‡πŸ‘‡

 Wagalatia 5:16-17
 "Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka."

Ukisoma hapo utaona paulo alivyokuwa akiwaambia wagalatia ambao walikuwa wameanza kwa Roho lakini baadae wakaanza kuishi kwa namna mwili unataka na sio kama Mungu alivyokuwa anataka maana matendo maovu yalikuwa sehemu yao.
Sasa mpendwa kama ukikubali kuwa chini ya maongozi ya Roho mtakatifu utaweza kabisa kuwa na nguvu za kuishi utakatifu mpaka pale utakuwa ukiondoka Duniani.

 Kwanini sasa kama mwamini unatakiwa kuongozwa na Roho mtakatifu??
✍️ Kuongozwa na Roho mtakatifu utaweza kujulishwa mambo yale yaliyopo, yaliyopita na  yanayokuja
✍️ Roho mtakatifu tukiongozwa naye ataondoa kwetu Roho ya mazoea maana yeye ndiye atakuwa anatuongoza
✍️Roho mtakatifu ni Mungu mwenye nguvu ya uwezesho katika nafsi ya tatu ya Mungu. Kwa hiyo bila yeye hata ujitahidi vipi huwezi kufanya lolote.
✍️Roho mtakatifu atakuwa anatufundisha namna ya kuishi kwa utakatifu wote
✍️ Kukubali kuongozwa na Roho ni sehemu mojawapo ya kuonyesha itiifu wako mbele za Mungu.

4⃣. KUICHUKIA DUNIA
Hii ni hali ya kukataa kuyaishi mambo ya kidunia ambayo yanakufarakanisha na Mungu. Kwenye sehemu ya pili kuna mambo tuliyaona ukiyafanya hayo anakuwa anaupenda ulimwengu. Sasa katika kuichukia Dunia lazima uyakatae hayo mambo makuu matatu 

 A. Kukataa tamaa ya macho
Lazima kama mwamini ajue namna ya kuushinda huo ubaya utokanao na macho lasivyo utakuwa unaishi lakini kiroho umekufa lazima macho yako yatiwe Nuru ya Kristo ili uweze kumpendeza Mungu wakati wote.

 B. Kuishi nje ya tamaa ya mwili
Kama tulivyoona matendo dhahiri ya mwili yalivyo kwenye wagalatia sura ya tano. Sasa kama mwamini lazima ujue kuuweza mwili wako lasivyo utakuwa unajidanya hata kama unafanya huduma na kuhubiri kwenye maisha yako ya kila siku.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 1 Wathesalonike 4:3-5
 "Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu."

Paulo anaandika kwa  watu wa kanisa la Thesalonike kwamba wafanywe safi na waepukane na tamaa za mwili mfano uasherati. Pia paulo anawaambia watu wote waweza kuuweza mwili wao katika Utakatifu na heshima. Huku ndiko kutawafanya waepukana na tamaa za mwili. Hii itawafanya waishi na Mungu vizuri bila mawaa wakati wote mpaka kifo chake.

 C. Lazima kuachana kiburi cha uzima ndipo pia utaweza kuwa na usalama mpaka unaiacha Dunia

MUNGU akubariki kwa kuwa pamoja nami sehemu hizi tatu za somo letu. 

Lakini ngoja nikuongezee Swali moja niliulizwa na mtumishi wa Mungu yawezekana ukawa upo miongoni mwao ila unaogopa kuuliza.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

SWALI
  A. Hivi Kama mtu ameshaanguka na kiukweli yuko hatua nyingi nyuma ya alivyokuwa mwanzo afanye nini?  
B. Labda hata hawezi kuomba tena, hawezi kusoma Neno tena, hawezi kumsifu Mungu na kumuabudu Mungu tena katika Roho na kweli kama mwanzo, Hawezi hata kukemea Dhambi hata ile nguvu ya injili imeisha kabisa yani kiufupi amekata tamaa, Moyo wa toba umeisha afanyeje???. 

 JIBUπŸ‘‡πŸ‘‡

Ohhh ikiwa imemkuta nampa pole lakini bado tunalo tumaini katika kristo Yesu.....

Huyu mtu kwanza tatizo lake kuu liko katika "Ufahamu wa Pendo la kristo Yesu kwake" maana kama akielewa Upendo wa Kristo Yesu hawezi kufikia viwango vya kukata tamaa kiasi hicho. 

Japo wengi wao ambao wanakumbwa na hali hiii wanakuwa walikuwa wamemshuhudia Mungu kwa viwango vikubwa kwenye maisha yao na baada hapo wanakuja kuanguka sasa hatia ya dhambi inakuwa inawatesa ndio maana wanafika hatua wanapoteza kila kitu yaani Shauku, nguvu ya kuomba na kila kitu.

 Sasa haya ni baadhi ya mambo ambayo anatakiwa kuyafanya huyu mtu wa namna hiiiπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡ 

 1. Jambo la kwanza kabisa auelewe Upendo wa Mungu 
Upendo wa Mungu unajidhihirisha kwa namna tofautitofauti kwa mwamini yeyote. Sasa inabidi huyu mtu apate uelewa juu ya namna ambavyo Mungu  anampenda ili kuweza kumpa mtu uwezo wa kusonga mbele .
Watu wengi wanapotea kabisa kwasababu ya mafundishoπŸ‘‡πŸ‘‡
 Hosea 4:6a
 "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;"
Hapo unaona mtu akikosa uelewa tu ni rahis sana akafungwa ufahamu na adui kiasi kwamba akajikuta hawezi kusonga mbele zaidi hata hatua moja.

 Kwenye pendo la Mungu akielewa haya yanaweza kumsaidiaπŸ‘‡πŸ‘‡

 ➡️ Mungu ametupenda sisi tukiwa na dhambi na sio kwa matendo yetu mema.
 
Yohana 3:16 
 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Mungu kitendo cha kumtuma mwanawe haikuwa kwasababu tulikuwa watakatifu bali wenye dhambi ili tupate uzima sasa ukifika hatua ukajua ulipendwa angali una dhambi basi hutakwama kuendelea mbele zaidi hata kidogo.

 Warumi 3:23-24
"kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;"
Hili fungu nililielezea. Ukishajua ya kwamba watu wanakosea ila kupitia kristo yesu tunahesabiwa haki ko kazi yake sio kujikinai mwenyewe bali ajishushe kwa Yesu pekee.

 ➡️ Mungu anasamehe dhambi zote na alikuja kwa ajili ya hilo

Isaya 1:18
 "Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu"

Hapo anaonyesha ukifanya dhambi ya namna gani bado Mungu anaweza akakusamehe haijarishi umefanya kosa gani.

1 Petro 2:24
 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.

Pia hapo juu unaona kwamba yeye ndiye aliyechukua dhambi zetu so ukiwa umekosea lazima uende kwake tu na ndio maana alisema kwambaπŸ‘‡πŸ‘‡

 Mathayo 11:28 
 "Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha".

Ukisoma hapo Mungu anataka watu wamuendee na mizigo yani dhambi zao yeye ndiye atawapumnzisha na sio waache dhambi zao ndio wamfuate bali ukiwa na makosa umuendee yeye akupe haki.

Sasa kuna namna nyingi upendo wa Mungu unajidhihirisha kwa mtu ambako huko kuna mfanya mtu akikosea aweze kurudi kwake na kusamehewa.

Kwanini nimeelezea hiki kipengeleπŸ€”πŸ€” ni kwasababu watu wanafundishwa mafundisho yanayowafanya wajihisi kuwa na hatia wakati wote na sio upendo wa Mungu kwa kanisa kinachowafanya wengi sasa wakikosea kukumbana na hizi haliπŸ‘‡πŸ‘‡

✍️✍️Asione haja ya kwenda kwa ibada maana akienda anakuwa anahisi hatia tu ndani
✍️✍️ Anakosa ujasiri wa kuomba. Japo ukifanya dhambi usipoitu ia lazima ikutee hii hali
✍️✍️ Hawezi tena kusema Habari za Mungu kwa ujasiri.
N.k

Na hii ndio sababu nimekuelekeza kwamba lazima apate uelewa vizuri wa upendo wa Mungu kwenye maisha yake. Ndio hatua yake ya kwanza kuweza kutoka maana bila hapo atakuwa mtumwa tu kwenye fikira zake.

 Note: kuelewa kwamba Mungu anakupenda usije ukatenda dhambi kwasababu atakusamehe hata utakapokosea 

2. UKISHAJUA UPENDO WA MUNGU HAYA MAMBO YANAWEZA KUKUSAIDIA SASA KUTOKA HAPO
 A. Kuweka peupe kosa lililokufanya ukaanguka
Hapa inatakiwa mtu huyu amuelekeze kiongozi wake wa kiroho juu ya jambo hili alilolifanya lengo ni kulifanya lisiwe na nguvu ya hatia ndani yake.
Kufanya hivyo unakuwa unaiaibisha dhambi hiyo kwenye maisha yako na hapo sio kwamba unakuwa unaenda kutubu kwa mchungaji wako bali unakuwa unauaibisha ubaya ulioufanya hii itakupa ujasiri wa kuendelea kumtafuta Mungu. Lazima ulikiri kosa lako peupe.

B. Kuwa na watu watakaokufanya uendelee mbele zaidi
Lazima utafute mtu/watu ambaye anaweza kushirikiana naye katika maswala ya kiroho ili pale unakosa nguvu akutie joto la kuendelea mbeleπŸ‘‡πŸ‘‡

 Mhubiri 4:9-11
"Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao. Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua! Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?"

C. Tafuta kwanza kuwa kwenye maombi ya ushirika sana kuliko wewe mwenyewe binafsi

D. Kumtaka bwana na Nguvu zake

yaani kuongeza shauku ya kuwa na nguvu za Roho mtakatifu maaana shauku ya kuabudu ni suala ambalo linakuja kulingana na ufahamu na hiyo nguvu ya Roho mtakatifu ndiyo itampa bubujiko na shauku kuu ndani ya ibadaπŸ™ŒπŸ™Œ

E. Lazima abadilishe vitu anavyoviangalia mara kwa mara ndipo ataweza kutoka huko.

Mfano mwingine unakuta mda wote anasikiliza nyimbo za bongo fleva, picha za ngono, na kufanya mambo mengi yafananayo na hayo huku anataka shauku ya ibada iongezeke kiasi kwamba anakuwa anajidanganya tu.

Hiyo inaweza kumsaidia huyo mtu kama atakuwa yuko tayari kutoka hapo alipo. Hatua ya kwanza siku zote ni kujua kwamba hauko sehemu sahihi na ukishajua ndipo unaweza kupiga hatua nyingine mbele. Zaidi itakayokufanya ufanye maamuzi sahihi.

Yuko kwenye wakati mzuri wa kuweza kutoka huko maana ameshatambua ya kwamba huko aliko sio salama na ndio maaana anataka aweze kutoka huko.

Mungu akubariki mtumishi kwa kuwa namimi tangu tumeanza mpaka hapa tulipofikia. Kulikuwa na mambo mengi ya kuweza kujadiliana lakini kwa sababu ya Muda nafikiri tuishie hapa. Ukiwa na swali maoni unaweza kuyaweka chini au kwa njia za mawasiliano hizo hapo.

Ulikuwa nami mtumishi katika kristo Yesu 
Name: Bro Jackobo
Phone; +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

KWENDA MPAKA MWISHO PAMOJA NA MUNGU {SEHEMU YA PILI}


Bro Jackobo

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu?? 
Namshukuru Mungu kipekee kwa ajili ya nafasi nyingine hii ambayo ametupa leo kuendelea na somo letu sehemu ya pili.

Utakuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email; jackobombwaga@gmail.com 

Baada ya kuona sehemu ya kwanza katika maana pamoja na kujua kwanini tunatakiwa kwenda pamoja na Mungu kama waamini mpaka mwisho. Sasa leo tutaenda kuangalia kwanini watumishi wa leo imekuwa ni changamoto sana kuweza kumaliza safari pamoja na Mungu. Kama hujapata kusoma sehemu ya kwanza bonyeza hapa➡️➡️ SEHEMU YA KWANZA

 Wagalatia 1:6 
"Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine."

Ni jambo la kushangaza sana kuona muamini anarudi nyuma na ndio maana Paulo alibaki kuwashangaa watu wa galatia kwamba ni kwanini wanamuacha Mungu kwa harakaπŸ€”πŸ€” ndio hivyo ambavyo hata kristo Yesu anavyolitazama kanisa  na kushangaa.

Kwanini unamuacha kristo kwa haraka mpendwa😭😭
 
Wagalatia 3:3 
" Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?"
Paulo anaumia moyo na kuwaambia wagalatia ni nani aliye waloga nyie maana mlianza katika Roho lakini mnataka kumaliza katika mwili. Tumeanza kwa Roho lazima tumalize kwa Roho maana sisi asili Yetu ni Roho.

 KWANINI WAKRISTO WENGI WAMEKUWA WANASHINDWA KUMALIZA SAFARI VIZURI??.

Tutaenda kujifunza sababu kuu mbili za kwanini kanisa la leo wengi wanamaliza vibaya. Ambapo ni hizi sababu kuu  mbili
1⃣ ROHO YA MAZOEA
2⃣KUIPENDA DUNIA

 1⃣. ROHO YA MAZOEA
hii ni hali ya kufanya jambo pasina kuangalia msingi mkuu halisi wa Mungu kwa wewe kufanya hilo jambo. Roho ya mazoea huwa inatokea mara kwa mara baada ya mtu kuwa alishawahi kufanya jambo fulani kwa mafanikio kwahiyo anafanya akiangalia yale mafanikio yake ya mwanzo pasina kuangalia au kusikiliza Mungu anachotaka akifanye. 
Maandiko ya msingi kwenye kipengele hiki yamejikita kwenye kitabu hikiπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 WAAMUZI 16:1-20 (20)
Basi naomba tuanzie hapaπŸ‘‡πŸ‘‡
 Waamuzi 16:20 
 "Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa BWANA amemwacha."

sasa ukisoma hiyo sura nzima utagundua namna ambavyo Samsoni alikuwa amefanya makosa lakini msitari wa 20 ndio ambapo inabeba maana ya Roho ya mazoea. Samsoni kwakuwa Mungu alikuwa anajidhihirisha kwake basi alijua hata wakati huo bado Mungu alikuwa naye kumbe Mungu ameshamuacha. Maana licha ya kwamba alikuwa ameingia kwa kahaba ila bado Mungu alikuwa pamoja naye kwasababu ile ishara ya mapatano bado ilikuwa ipo yaani vile vishungi vya nywele na alipotoa siri na vikaondolewa hakuelewa kama tayari ameshaondolewa vishungi alipoambiwa wafilisti wanakujia alisema nitainuka kama ilivyo kawaida Yangu ila asitambue kwamba Mungu amemuacha.
Kanisa la leo wengi wameachwa na Mungu ila hawajielewi na hata kama wanajielewa wengi wao wanakaza shingo na kusema wako pamoja na Mungu wakati Roho zao zinawa shuhudia kwamba hawako pamoja na Mungu.

 SIFA ZA MTU AMBAYE ANAENENDA KWA ROHO YA MAZOEA 

 ✍️✍️Huyu mtu anakuwa hana hofu ya Mungu au hofu ya Mungu hupungua ndani.

Ukimuangalia Samsoni alikuwa tayari ameenda tofauti na Mungu ila hakuwa na ile hali ya kuogopa kwamba Mungu anachukizwa na ninachokifanya kwahiyo akawa anafanya kwasababu Mungu alijitukuza kwake kwa wakati uliopita.
Kanisa la leo halimuogopi Mungu hata kidogo yaani mtu anaweza akadanganya, akadhurumu au akafanya uasherati lakini anaingia kanisani akiwa huru kabisa na wala hajuti moyoni mwake wala kuhisi hatia. Ni jambo la kutisha na hili ndilo balaa ambalo limelikuta kanisa la kizazi hiki cha leo.
 Soma Matendo ya mitume 5:1-11(8-9) 

Angalia mfano wa kanisa au mwamini aliyekuwa na mazoea πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
 Matendo ya Mitume 5:8-9 
" Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo. Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe."
 
Habari za anania na safira zinatisha watu hawa hawakuogopa hata kidogo kumdanya Roho wa Mungu kwasababu walijua ni kitu cha kawaida wala hakuna kibaya kitawakuta lakini kilichowakuta kilikuwa cha kutisha.
Kanisa la leo lime bweteka kwakuwa mtu hata kama akifanya dhambi huwa hawapatwi na mauti kama ilivyo kwa Anania na Safira wanasahau macho yao yanatiwa giza kiasi kwamba hawawezi kuona wema wa Mungu kwenye maisha yao.
Jichunguze vema huwa unafanyaje pale unapokosea.

 ✍️✍️Mtu huyu hujihesabia sana haki kwamba yuko sahihi kwa kila kitu.
Kujihesabia haki kunawakuta wengi wao ndio maana leo sio jambo geni kusikia mtumishi anajitangaza kwamba yeye ni mtakatifu sana kuliko wengine, kujiona anafanya huduma vizuri kuliko wengine huku akisahau kwamba Mungu kampa karama/kipawa ili kanisa liweze kufaidiana. Lazima ujifunze kwa Yesu mwenyewe unyenyekevu maana yeye licha ya kuwa alikuwa Mungu ila alinyenyekea mpaka mauti ili tuwe na usalama. Ukiwa unajiona wewe umekamilika basi uwe na uhakika uko karibu na kuanguka.  Samsoni yeye alikuwa tayari alishajimilikisha kwamba yeye ni wa kuwa na nguvu tu akasahau kuwa kuna wakati nguvu zitamtoka ikiwa atafanya tofauti na namna Mungu anataka.

 ✍️✍️ Huyu mtu anakuwa ni mtu wa kujiinua na kujisifu sana
Sasa ukimuangalia samsoni alipoambiwa wafilisti wanakujia alijibu nitainuka kama ilivyokawaida yangu hiyo ni ishara kwamba huyu mtu alikuwa tayari ameshajiona yeye ndio yeye na hakuna wa kumfanya kitu chochote. Ndiyo ilivyo kwa kanisa la Leo Mungu akukumbuke mtumishi wa Mungu. Nimekwisha kukuambia sehemu ya kwanza kwamba Utumishi wako sio sababu ya kukufanya kuurithi ufalme wa Mungu wala usije jaribu kuupima uhusiano wako na Mungu kwa kuangalia huduma yako.  

✍️✍️.Mtu huyu huwa Roho ya Toba inaondoka kwakwe
Mtu aliyezoelea Wokovu ,ndani yake Ile Roho ya Toba inaondoka kabisa na hatari huwa anaishi katika dhambi anasali na kuhudumu .
Toba hapa ni juhudi ya kuitubia dhambi yako ,kujutia na kufanya maamuzi ya kuacha kabisa na kugeuka kama Moyo wa Daudi namna ambavyo alifanya.
Unaweza ukasoma hapa ukaonaπŸ‘‡πŸ‘‡
 (ZABURI 51:1-4)
Pia ile Hali ya kumrudia Mungu kwa kumaanisha kabisa ,kama Mwana mpotevu inakuwa halna kabisa kwa huyu aliyekuwa na Roho ya mazoea  (LUKA 15:21.)

 ✍️✍️ Huyu mtu huwa anasikia neno la Mungu bila kulitii . 
Waamini waliozoelea Wokovu husikia sana neno la Mungu tena kwa ufasaha kabisa na kuguswa , isipokuwa hawezi kulitii wala kulitendea kazi tena .
Nguvu ya utii wa matendo ya rohoni inakuwa imeondoka na hata akijitahidi hawezi kwenda mbali.
Ndio maana , hawezi kuomba ,kusoma neno ,kufunga , kuja Ibadan au mkeshani bado hawana sababu yoyote . Hatari yao ule Utiisho wa Roho Mtakatifu juu ya matendo ya rohoni imeondoka na wanaona kawaida hata wasipofanya hivyo. Ukijiona hivyo fanya juu chini kutafuta msaada hii ni hatari sana mwana wa Mungu.

2⃣. KUIPENDA DUNIA
Jambo la pili ambalo limekuwa likilitesa kanisa ni kuipenda Dunia. Mwingine anasema sasa inawezekanaje kwa mwamini kuwa akawa anaipenda DuniaπŸ€” naomba tuende pamoja nami ndipo tutaelewana vizuri na ni kwa nini sasa nasema moja ya vitu vinawafanya watumishi wa Mungu washindwe kufika mwisho wa Safari huku wakiwa pamoja na Mungu kwenye maisha yao ya kila siku.
Andiko la msingi kwenye kipengele hiki ni kwenye πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
 1 Yohana 2:15-16
 "Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia."

Ukianza kuisoma Sura hiyo ya pili utaona Yohana kaandika jumbe kwa watu wa rika zote baadae ndipo anakuja kuwapa huu ujumbe wa pamoja kwa watu wote. Kwamba wasije wakaipenda Dunia na mambo yote yaliyoko ndani yake.

Mtumishi wa Mungu katika kuishi kwake katika ulimwengu huu anakuja kuona mambo makuu matatu ambayo yanayowafanya watu waonekane wanaipenda Dunia.

 MAMBO YALIYOKO DUNIANI YANAYOONYESHA KWAMBA MTU ANAUPENDA ULIMWENGU/DUNIA
1. Tamaa ya mwili
2. Tamaa ya macho
3. Kiburi cha uzima

Katika hayo mambo matatu ndipo watumishi wengi wanaangukia sehemu moja wapo ya hizo ndio maana hawawezi kufika sehemu Mungu anataka waweze kufika wanajikuta walianza vizuri lakini wanamaliza vibaya.

 1. TAMAA YA MWILI
Hapa kwenye tamaa ya mwili mtu anakuwa anafanya yale mambo ambayo mwili unataka ayafanye kama tunavyojua ya kwamba matendo ya mwili huwa yako dhahiri kabisa unaweza ukasomaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 Wagalatia 5:19-21
 "Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu."

Hayo mambo hapo juu ndiyo ambayo unakuta mwili unamshurutisha huyu mwamini kuweza kuyaisha na huyu mtu kwakuwa hajajaa nguvu za Mungu basi anajikuta anayaishi hayo mambo hata kama yupo kanisani na hata kama huwa anafundisha au kuhudumu kwa namna yeyote ambapo ni lazima awe tayari kuyaacha hayo ndio atakuwa na usalama lasivyo anajidanganya.

 Warumi 3:13-15 
 "Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira i chini ya midomo yao. Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu. Miguu yao ina mbio kumwaga damu."

Hawa watumishi wa Mungu walio kwenye tamaa ya mwili unakuta hawawezi hata kuwa na uwezo wa kuyatunza maneno na ndio maaana unakuta wengine niwachonganishi kabisa ndani ya kanisa yani kazi yao ni kuleta virugu tu.
Mwingine huyu mtu anakuwa hana nia ya kuleta vurugu ila kila neno akilisema ndani ya kanisa linaleta shida. Sasa kama ukijua na ukajipima ukakuta kila ukisema unaleta machafuko kwa watu basi jua ya kwamba umekwisha kuvamiwa na tamaa ya mwili inakue desha pasipo wewe kujua. Na hii inawafanya watumishi wengi kutomaliza na Mungu sasa wakiwa wameenda hvyo ndio maana hawamalizi pamoja na Mungu kwenye maisha yao ya kila siku.

 2. TAMAA YA MACHO
Kwenye eneo hili la tamaa ya macho limekuwa likileta shida shida maana limekuwa likigusa vijana, mpaka viongozi wa kanisa kwa sababu ya kutokuvifisha viungo vyao katika kristo Yesu.

 Mwanzo 19:26 
 "Lakini mkewe Lutu akatazama nyuma yake, akawa nguzo ya chumvi."
Ukisoma habari nzima kwenye sura ya ya 19 utaona namna ambavyo Lutu na familia yake walivyoambiwa kwamba wasigeuke nyuma kuangalia Sodoma na gomora lakini mke wa Lutu aliweza kugeuka akiwa njiani kwasababu ya tamaa ya macho.
Fahari ya macho ni kutazama kitu chochote kile lakini biblia inatuambia kwamba lazima tuwe makini mfano kuna mambo yambo yanaweza yakawa halali lakini yasifae ndio maana lazima uwe mtu wa kuweza kumsikiliza Mungu kwa kila hatua unayoenda kuipiga ndipo utakuwa na usalama lasivyo utajikuta unakosea wakati wote. 
Mfano kwa vija sio kitu cha ajabu huyu mtu ni mtumishi lakini anaangalia picha za ngono, na kuwaka tamaa kila amtazamapo binti yeyote sasa hii ni changamoto kubwa na ndio maana biblia inasemaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 Mathayo 5:27-28
 "Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake."

Hapa inaeleza kwamba ukimtazama kwa kumtamani  tayari umekwisha kuzini naye. Kwahiyo lazima uangalie vile ambavyo unaishi na unavyochagua kuvitazama kwenye maisha yako ya kila siku. Watumishi wengi wameishia njiani kwasababu ya tamaa ya macho.

 3. KIBURI CHA UZIMA 
Hapa ukizungumzia kiburi cha uzima unamaanisha jumla ya dhambi au makosa ambayo mtu anakuwa anayafanya kwasababu yeye ni mzima au amepewa kufanya vyema zaidi na Mungu.
Watumishi wengi wamekuwa mda mwingine wakikataa kufanya huduma kwasababu wao wanapofanya huduma wengi huwa wanabarikiwa kwahiyo wanajikuta wakihitaji wapewe fedha nyingi ndipo wahudumu na hicho ndio kiburi cha uzima chenyewe sasa.

Mfano kuna baadhi ya waimbaji huwa hawawezi kuja kwa mialiko mpaka wapewe fedha nyingi sasa hiyo ni sehemu moja wapo ya vitu vitakavyo wafanya washindwe kuurithi ufalme wa Mungu maana wanafanya mambo ambayo ni machukizo mbele za Mungu. Na kwa mfumo huo hawawezi kwenda pamoja na Mungu.

Mungu akubariki kwa kuwa pamoja nami tangu tumeanza mpaka hapa.
Tutamalizia kipengele cha mwisho kwa wakati mwingine 

Ulikuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu 
Jina: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

KWENDA MWENDO MPAKA MWISHO PAMOJA NA MUNGU {SEHEMU YA KWANZA}


Bro Jackobo

UTANGULIZI
Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu?? Karibu kwenye somo letu zuri tutakalojifunza kwa vipindi kama vitatu juu ya "Kwenda mwendo pamoja na Mungu"

Utakuwa nami mpendwa katika Kristo Yesu
Name: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

Nini maana ya kwenda pamoja na Mungu

✍️✍️ hii ni hali ya kuishi maisha matakatifu na ya  utauwa yenye ushuhuda mwema mbele za Mungu na mbele za wanadamu wanaokuzunguka.

✍️✍️hii ni hali ya mwamini au mtu aliyemkubali kristo Yesu kuweza kuishi maisha ya unyoofu kwa kuangalia maelekezo aliyoyatoa Mungu mwenyewe mpaka pale kifo kitamkuta {Mwili na Roho kutengana}. 

hapa huyu mwamini anakuwa anazishika sheria za Mungu sio kwa kuzinena au kuzitamka kwa watu tu bali ni pamoja na maisha yake kiujumla yanakuwa yanaenda namna vile anakuwa anasema na kuwaonyesha wengine namna ambavyo anaamini.

Katika maana hizo mbili zote zimekuja na kutengana kwa mwili na Roho kwasababu baada ya kufa kinachofuata ni hukumu na huo ndio mwisho mwenyewe na siku zote mwisho wa jambo ndio mwanzo wa jambo lingine.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Waebrania 9:27 "Nakama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;"

Kwahiyo lazima utambue kwamba mwisho ninaouzungumzia kwenye somo letu ni kifo kitakapo kukuta.

Kwahiyo tutaangalia mwendo mzima wa lwamini tangu anapokuwa ameamini mpaka anapata u mauti wake.


MAANDIKO YA MSINGI
{2TIMOTHEO 4:5-7; KUTOKA 33:14-17(14-15)}

2 Timotheo 4:5-7
"Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako. Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;"

ukisoma misitari hapo juu utaona namna ambavyo Paulo anasema na Timotheo akimuelekeza kustahimili yote ila atimilize huduma yake. Tena anakuja kuonyesha namna ambavyo alikuwa ameshafanya tathmini yake mwenyewe ya namna alivyofanya kazi ya Mungu na Roho wa Mungu akamshuhudia ya kwamba ameilinda imani na mwendo ameumaliza akiwa anaona siku zake za kufa ziko karibu kutimia.

Paulo alifika hivyo kugundua ni kwasababu allliishi neno la Mungu na Roho alikuwa akishuhudia ndani yake juu ya utendaji wa kazi ya Mungu. Roh wa Mungu ndiye huwa anazungumza na kutuhakikishia usalama wa safari yetu kila inapoitwa leoπŸ‘‡πŸ‘‡

Warumi 8:16-17
"Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.".

Kutoka 33:14-15
"Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha. Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa."

ukifuatilia sura nzima ha 33 na 32 hapo kutoka utaona wana wa Israel walikuwa wamejichanganya yaani hawamfuati Mungu namna ambavyo anataka waishi mpaka ukafika wakati Mungu akawa amewachoka akawaambia ya kwamba wana shingo ngumu kwahiyo hawezi kuvumiliana nao kwahiyo akamuambia Musa kwamba Yeye hatakwenda pamoja nao katika hiyo safari bali Malika wake ndiye atawatangulia lakini Musa kwa kuelewa umuhimu wa kuenda pamoja na Mungu aliona ni vyema basi amuambie Mungu kwamba hawezi kuendelea mbele bila yeye kuenda pamoja naye.

Sasa kanisa la leo limekuwa na changamoto liko tayari kuendelea mbele angali liko mbali kabisa na Mungu yani utaona Mhubiri, Mwimbaji, nabiii, mwalimu, mtume anafanya huduma lakini mahusiano yake na Mungu hayajakaa sawa. inakuwa sawa na malaika kukuongoza kwenye safari ili mradi ile ahadi aliyoitoa iweze kutimia kama kwa wana wa Israel. Watu wanaendelea kujisifu kwakuwa huduma zao ni kubwa na Mungu anajidhihirisha japo hawaendi pamoja na Mungu kwenye maisha yao.

Watu wamesahau namna biblia inasema hapaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Mathayo 7:21
"Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni."

unaweza ukatumika vizuri na ukaona matokeo lakini baada ya hapo ukaonekana ulikuwa unafanya kwasababu ya faida zako binafsi ulizonazo na sio utumishi wa Ki Mungu kabisa na ndio maana utakuwa miongoni mwa wale walitajao jina la Bwana lakini hawatakiwa na sehemu katika ufalme wa Mungu kabisa.

sasa tukiwa tunajua ya kwamba siku moja kuna wakati tutapo lala yaani Roho na mwili vitatengana {KIFO} lazima tujichunguze na kuangalia ni kwa namna gani tutaweza kufikia hapo hali tukiwa na usalama katika Roho zetu na uhakika wa maisha ya umilele pamoja na kristo na sio katika ziwa la moto.

NOTE: Usije jaribu kulinganisha matokeo ya huduma yako na mahusiano yako na Mungu hata siku moja maana kuna wakati unaweza ukawa unafanya huduma lakini Ukawa uko mbali sana na Mungu.⚠️⚠️⚠️

KWANINI KWENDA PAMOJA NA MUNGU MPAKA MWISHO?
Lengo kuu la kuenda pamoja na Mungu kwenye safari hii ya wokovu pamoja na Mungu ni KUURITHI UFALME WA MUNGU WA MILELE. Katika hayo yote pia kuna sababu ndogo ndogo zinazo weza kumuwezesha Muumini kufikia vigezo vya kuurithi ufalme wa Mungu. sasa embu tuangalie sababu zinazofanya tuende pamoja na Mungu 

✍️✍️1. Mungu ndiye anajua mambo yote yaliyokuwapo, yaliyopo na yatakayokuwepo

Ufunuo wa Yohana 1:8
"Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi." 

katika kipindi kanisa linapita kwenye wakati mgumu mateso na dhiki kali kutoka kwa wakuu wa dini ya Kiyahudi na serikali ya kirumi Mungu alijifunua kwa Yohana akiwa katika kisiwa cha Patimo akimpa maelekezo juu ya makanisa Saba. Lakini Yesu anaanza kujifunua kwanza kwa kujitambulisha Yeye ni nani na anajitambulisha kwamba yeye alikuwepo, yupo na atakuwepo. 
kwa hiyo yeye anaelewa hata ya kesho itakuwaje sasa kama ukiwa unasafiri maisha ya wokovu bila Mungu hutaweza kujua yatakayokuja maana mengine ni magumu yanayokutaka kuwa na uvumilivu ili uweze kushinda lasivyo itakuwa ngumu kuweza kushinda. kwahiyo lazima ujipange ndani ya pendo lake na ujifiche humo ndipo utaweza kuurithi ufalme wa Mungu.

✍️✍️2.  Mungu ndiye anayetoa Nguvu za kuishi maisha matakatifu
Nguvu ni uwezo wa kufanya jambo fulani. Sasa Mungu kupitia Roho mtakatifu huwa anaachilia huo uwezo wa kuweza kustahimili maisha ya kumpendeza  na kuyaishi yale ambayo alikuwa anayataka wayaishiπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Matendo ya Mitume 1:8
"Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi."

sasa huo uwezesho ndio ambao utamfanya mtu aweze kufika mpaka mwisho hali akiwa na wokovu ndani yake. ndio maana hata Daudi akaonyesha kwamba Mungu ndiye nguvu zake, na ngao yake. πŸ‘‡πŸ‘‡

Zaburi 28:7-9
"BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru. BWANA ni nguvu za watu wake, Naye ni ngome ya wokovu kwa masihi wake.Uwaokoe watu wako, uubariki urithi wako, Uwachunge, uwachukue milele."

Pia Paulo anaonyesha namna ambavyo kapita nyakati ngumu na nyakati za raha lakini katika nyakati hizo zote Mungu alikuwa akimuwezesha maana alimpa nguvu. unaweza ukaonaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Wafilipi 4:12-13
"Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu."

sasa ukiangalia hapo iko wazi kabisa kwamba Mungu ndiye alikuwa akimuwezesha ko alijua ya kwamba yeye mwenyewe asingeweza mwenyewe kuweza kustahimili ndio maaana katika kusafiri lazima awepo Mungu ili aweze kutusaidia maaana kwa asili mwanadamu hawezi kujisaidia mwenyewe.


✍️✍️3. Asili ya Mwanadamu Ni Mungu na yuko kwa mfano wa Mungu.

Mungu alimfanya mwanadamu kwa mfano wake kwa sababu alikuwa anataka mwanadamuaishi kama yeyeπŸ‘‡πŸ‘‡ 

 Mwanzo 1:26 
 "Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi."

Mungu Alimuumba mwanadamu kwa mfano wake katika vigezo hiviπŸ‘‡πŸ‘‡
➡️Utashi 
⏩utakatifu
⏩Ufanano katika Roho

 UTASHI
Mungu alimpa mwanadamu utashi wa kuweza kuamua jambo analolitaka Na Mungu hakumfungia kama vile ambavyo mnyama alivyo kwamba hawezi kuamua.
Sasa Mungu kumpa uhuru wa kuamua hakutamani kwamba huyu mwanadamu aamue vibaya na ndio maana anakulekeza kwamba kuna njia mbili ila anakupa chaguo uchague uzima maaana yeye anatamani tuwe na uzima siku zoteπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 Kumbukumbu la Torati 30:19
 "Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;"

Sasa haya huu utashi ndio ambao lazima utambue kwamba usipoenda kama Mungu anavyotaka hutaweza kuwa salama hata kidogo.

 UTAKATIFU
Hii ni hali ya Kuwa na haki kuu mbele za Mungu pasina kuwa na mawaa wala uchafu wa nmna yeyote.
Adamu alipoulbwa alikuwa mtakatifu kabisa hakuwa na dhambi yeyote na hayo ndiyo maisha Mungu aliyataka wayaishi milele maana yeye ni mtakatifu siku zoteπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 Mambo ya Walawi 19:1-2
 "BWANA akanena na Musa, akamwambia, Nena na mkutano wote wa wana wa Israeli, uwaambie, Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wenu, ni mtakatifu."

 Sasa mwingine anaweza sema kwani mwanadamu anaweza kuwa mtakatifu???πŸ€”πŸ€”πŸ€” 

Jibu ni Ndio ila sasa huo utakatiu tunapewa haki kupitia kumuamini Kristo YesuπŸ‘‡πŸ‘‡

 Warumi 3:23-24 
"kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; 

Wewe kumuamini kristo Yesu kumekufanya uhesabiwe haki pamoja na utakatifu. Kwahiyo hayo maisha ya utakatifu huyawezi mwenyewe bila yeye kuwa pamoja na wewe.

Kwahiyo kwakuwa wewe ni mfano wa Mungu na asili yako ni Mungu ndio maana lazima tunapaswa kwenda na Mungu mpaka mwisho ili tuwe na usalama.

Mungu Akubariki kwakuwa pamoja nami katika sehemu hii ya kwanzaπŸ™πŸ™ 

Tutaendelea kwa wakati mwingine na sehemu ya piliπŸ™ŒπŸ™Œ

Ulikuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu
Name: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

JE MUNGU ANAWEZA KUMUACHA MTOTO/MWANA WAKE??


Bro Jackobo

Utakuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Name:Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu?? Karibu tujifunze kwa pamoja kidogo kuhusu hili swali...

Tutaliangalia somo hili katika mtiririko huu ili kuturahishia kuelewa
✍️Utangulizi: Mtoto/mwana wa Mungu ni yupi?
✍️Mungu anasema nini kuhusu kumuacha Mtoto wake katika agano la kale na agano jipya?
✍️Nini hitimisho juu ya swali hili
✍️ Nini matokeo endapo mtu atamuacha Mungu
✍️ Hitimisho juu ya mtu baada ya kumuacha Mungu inakuwaje sasa kuhusu ushirika wake na Mungu
✍️Hitimisho la mwisho kamili la swali {Jibu kamili la swali}

Kumekuwa na mjadala mkubwa sana kwamba je Mungu anaweza kumuacha mtu/mwana/mtoto wake??...

Jibu rahisi kabisa: MUNGU hawezi kumuacha mtoto wake hata siku moja na hajawahi kufikiri hata siku moja kukaa naye mbali ila mwanadamu anaweza kumuacha Mungu.

Kupitia hilo jibu hapo tutaenda kudadavua vizuri sasa kupitia maandiko na baada ya hapo tutaona matokeo ya mwana au mtoto kumuacha Mungu.

UTANGULIZI WA SOMO

Je mwana wa Mungu ni yupi?
Mtoto au mwana ninayetaka kuzungumzia hapa ni yule mtu ambaye amekwisha kuamini na kufanyika ushirika na Mungu ambaye Mungu amekuwa Baba na yeye mwana. Sasa ili mtu ufanyike mwana wa Mungu lazima ukubali kumpa Yesu kristo maisha yako yaani uokoke.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Yohana 1:12-13
"Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu."

Unapompokea Yesu ndipo unafanyika mwana wake na kumpokea Yesu kunakuja kwa wewe kuamini na kumkiri Yesu kristo ambapo huo ukiri unatakiwa kuenenda pamoja na Matendo yako ya kila siku unapokuwa unaishi.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Warumi 10:9-10,13
"Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka."

Baada ya kuamini na kuokoka ndipo unafanyika kuwa mwana/mtoto wa Mungu na kama ukaamini ukawa bado unaishi maisha ya Dhambi wewe bado hujatambua vyema kufanywa kwako upya na hapo unakuwa sio mwana wa Mungu bali unakuwa mtu wa Mungu maana ikiwa unalitaja jina lake inakupasa uache dhambi zako zoteπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

2 Timotheo 2:19
"Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. 
Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu."
Msingi wa mwanadamu kuwa mwana wa Mungu lazima akubali kuuacha uovu wake wote yaani asiendelee kuishi katika dhambi.

1 Yohana 1:6
"Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;"

Yohana 14:21
"Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake."
Ukisoma hayo mafungu mawili yanakuonyesha wazi kwamba anayekubalika ni yule ambaye anaishi sheria za Mungu na sio kunena katika kinywa tu halafu huku anaishi tofauti na sheria ya Mungu.

Kiufupi nitaenda kueleza juu ya Mtu aliyeokoka, Mungu pamoja na kuacha.

Baada ya kuona mwana/mtoto ninayemzungumzia ni yupi basi tuende kwenye kiini cha neno/somo letu lililo katika mfumo wa swali. "Je Mungu anaweza kumuacha mtoto wake?"

KIINI CHA SOMO:

Kama nilivyokwisha kuwaambia ya kwamba Mungu hawezi kumuacha mtu yeyote tena hana hata mpango wa kumuacha mtu yule ambaye yuko kwakwe na anaishi katika kweli yake. Naomba nianze katika agano la kale namna Mungu alivyolithibitisha hili neno kwamba hawezi kukuacha hata siku moja.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Isaya 49:14-16
"Bali Sayuni alisema, YEHOVA ameniacha, Bwana amenisahau. Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe. Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima."

Hapo Mungu alikuwa akizungumza na wana wa Israel walipokuwa wanafikiri kwamba Mungu amewaacha lakini Mungu anakuja kuwajibu kwamba hawezi kuwaacha maana wako kwenye vitanga vya mkono wake kiasi kwamba anawatazama mda wote wakiwa hata kama wakiwa kwenye kipindi kigumu. Ndio maana hata Suleiman Mungu alimwambia aende katika njia ya Mungu ndipo atakuwa na yeye na kuzithibitisha zile ahadi aliahidiana na Daudi baba yake.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

2 Mambo ya Nyakati 7:17-18
"Nawe, ukienda mbele yangu kama alivyokwenda Daudi baba yako, ufanye sawasawa na yote niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu; ndipo nitakithibitisha kiti cha enzi cha ufalme wako, kama nilivyoagana na Daudi baba yako, nikisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kutawala katika Israeli."

Sio Suleiman aliambiwa peke yake pia hata Yakobo aliahidiwa kwamba Mungu atakuwa naye wakati woteπŸ‘‡πŸ‘‡
Mwanzo 28:15
"Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia."
N.B: unaweza kusoma kwa wakati wako {Yoshua1:5, Yeremia30:11, 46:28}

Tumeona namna agano la kale ambavyo Mungu aliwaahidi watumishi wake kwamba hatawaacha naomba tuone pia katika agano jipya Mungu alisemaje piaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Yohana 6:37-39
"Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe. Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka. Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho."

Kama nilivyokwisha kukueleza kwamba Mungu hana mpango wa kumuacha Mtoto wake, unaona hapo Yesu anasema mwenyewe wote ambao wamekuja kwake hatamtupa hata mmoja na ndio maana nakuambia Mungu hawezi kumuacha mtoto wake hata siku moja maana yeye anatamani tukae katika pendo lake siku zote. Na ndio maana Yesu alijitahidi kuwalinda wanafunzi wake wote ili asiwepo hata mmoja wa kupotea πŸ‘‡πŸ‘‡
Yohana 17:12
"Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie."

Hitimisho 1: Kulingana na namna tulivyoenda na kuona maandiko hayo hapo juu ni dhahiri kwamba Mungu hawezi kumuacha mwana/mtoto wake hata siku moja na huwa anachokiangalia ni kuhakikisha mtu huyu anakaa kwenye neno lake la kweli tu.

Je inakuwaje sasa ikiwa mtoto amefanya dhambi??
Dhambi ni uasi yaani kwenda kinyume na maagizo ya Mungu aliyokuamuru kuishi kwa hayo. πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
1 Yohana 3:4
"Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi."
Mungu wetu ni mwaminifu ambapo amempa mtu nafasi ya kuchagua mema au mabaya sasa yeye mwenyewe anaweza kuamua kuishi katika dhambi au kuishi kwa namna Vile Mungu anataka. Sasa ikiwa huyu mtu ambaye Mungu amesema hatamuacha akaenda kufuata tamaa na mambo ya kidunia biblia inasemaje hapo??

Yohana 14:21
"Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake."

2 Mambo ya Nyakati 7:19-20
"Lakini mkigeuka, na kuziacha sheria zangu na amri zangu nilizoweka mbele yenu, mkienda, na kuitumikia miungu mingine, na kuiabudu; ndipo nitawang’oa katika nchi yangu niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaiondosha itoke mbele zangu, nami nitaifanya kuwa mithali na tukano katikati ya watu wote."

Katika maandiko hayo anaonyesha ya kwamba yeye atakuwa pamoja na wale ambao wanaishi kwa sheria yake na hao ndio atakuwa anajidhihirisha kwao lakini ukiwa unafanya dhambi basi uwe na uhakika atakuwa mbali na wewe ila kwasababu ya wewe kutokumheshimu yeye.

MATOKEO YA DHAMBI KATIKA USHIRIKA NA MUNGU

1. Kuharibika kwa uhusiano wako na Mungu.
Isaya 59:2
"lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia."
Matokeo ya kufanya uovu yanakufanya uhusiano wako na mungu uharibike.

2. Roho wa Mungu anahuzunishwa ndani
Waefeso 4:30
"Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi."
Ukianza mistari ya nyuma utaona anawaeleza habari ya dhmbi ndio anakuja kuwaambia msije kumhudhunisha roho wa Mungu.

3. Roho mtakatifu kuondoka ndani ya mwamini
Zaburi 51:11
"Usinitenge na uso wako, 
Wala roho yako mtakatifu usiniondolee."
Daudi alipofanya dhambi na akaamua kutubu anakuja kusema Roho wa Mungu asiondolewa hiyo inatupa picha kwamba utendapo dhambi Roho mtakatifu anaondoka.

4. Kuacha Mungu kujidhihirisha kwako katika mambo mbalimbali
(Yohana14:21, 2Nyakati19-20)

Yapo matokeo Mengi ya dhambi ila nimeyaweka haya ili niweze kukamilisha somo.

Sasa ukiangalia hapo kwenye hayo maandiko na hizo tokeo za dhambi ni zahiri kwamba kwasababu ya dhambi huwa ushirika unaharibika maana kama Roho mtakatifu atakuwa anahuzunika, akaondoka kwako na akaacha kujidhirisha kwako utakuwa na usalama gani na utakuwa unahusiana na Mungu kwa namna gani?? Kwahiyo baada ya wewe kumuacha Mungu na yeye pia anakuacha uende unakotaka maana yeye amekupa maamuzi ya kuchukuaπŸ‘‡πŸ‘‡

Kumbukumbu la Torati 30:19
"Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;"
Japo anakushauri bado uchague mema ili aende na wewe.

Mwingine atasema hatuhesabiwi haki kwa matendo yetu sasa inakuwaje? Na tena tuko kwa kipindi cha Neema... Sawa nakubaliana na wewe ila naomba tuoneπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Warumi 6:1-2
"Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?"
Tito 2:11-12
"Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;"
Ili uelewe neema imefunuliwa kwako lazima uwe hauishi maisha ya dhambi ndipo ambapo utakuwa katika neema, kama wewe unaishi maisha ya dhambi bado hauko katika neema na ukiwa katika kristo Yesu lazima uache dhambi na hautakiwi kuishi huko kwenye dhambi.
Mwingine atasema kwamba sitahesabiwa haki kwa matendo yangu... Sawa nakubali lakini biblia imesema tujitahidi kuishi namna Mungu anataka ndipo atajionyesha kwetu, haki yako iko ndani ya kristo na ukiwa katika kristo lazima uyafanye ya kristo aliyokuwa anayafanyaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

1 Yohana 1:6
"Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;"
Kwahiyo ukiri, imani lazima iendane na matendo.

Pia kumbuka biblia inavyosemaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Warumi 8:9
"Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake."
Sasa ukiwa Roho wa Mungu hayupo pamoja na wewe inakuwaje? wewe unakuwa sio mwana wa Mungu bali unakuwa ni mtu wa Mungu ambapo anakuwa anakusubiri utubu ili aweze kukusamehe na aendelee kuwa pamoja na wewe.

Hitimisho2: kutokana na maandiko hapo juu ikiwa mtu amefanya dhambi basi anafungua mlango wa Mungu kumuacha maana Mungu hana ushirika na giza maana huyo mtu atakuwa hayuko na Mungu mpaka pale atakapokuwa ametubu na kuungama dhambi zake.

HITIMISHO KAMILI
Mungu hawezi kumuacha mtu hata siku moja na wakati wote atakuwa anatafuta namna ya kumfanya mtu aendelee kukaa kwenye pendo lake wakati wote ila endapo huyo mtu atachagua kutokuenda na Mungu basi yeye hamlazimishi anamuacha atoke kwenye utawala wake na milki yake.

Mpendwa katika kristo jitahidi kufanya mapenzi ya Mungu ili usije ukafarakana na Mungu na kujikuta umebaki mwenyewe.

Ulikuwa nami mpendwa katika kristo yesu
Name: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

KUJIKANA NDANI YA KRISTO YESU (sehemu ya tatu- Final)

Bro Jackobo Utakuwa nami mpendwa katika kristo yesu Name: Bro Jackobo Phone: +255766944441 Email; jackobombwaga@gmail.com Bwana Yesu asifiwe...