KUUTUNZA WOKOVU (SEHEMU YA PILI)


Bro Jackobo

Utakuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
+255766944441
jackobombwaga@gmail.com 

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu? Mungu akubariki kwa kuwa pamoja tena kwenye sehemu ya pili ya somo letu juu ya KUUTUNZA WOKOVU. 

Kama haukufanikiwa kuipata au kusoma sehemu ya kwanza unaweza kubonyeza hapa ukasoma SEHEMU YA KWANZA. Ukisoma hiyo sehemu ya kwanza itakurahisishia kuelewa mtiririko wa Somo namna linaenda.

Sehemu ya kwanza tuliona utangulizi wa Somo letu na kuangalia namna unavyoelezewa huu wokovu kwamba ni kitu gani kwa msingi wa maandiko. Kwa kadri ambapo kiufupi tuliona kwamba Wokovu unaletwa na Mungu mwenyewe pasina ushawishi wa mwanadamu na mwanadamu yeye anafanya kuupokea huu wokovu. Basi embu tuendelee kipengele cha Tatu cha mfululizo wa Somo letu.

3. MAMBO YA MSINGI KATIKA KUUPATA WOKOVU
Tunapoendelea kujifunza naomba turudi kwenye andiko hili kwanza hapa

Yohana 3:16-17 (KJV) Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.

Ukisoma hapo andiko linaonyesha kwamba Mungu kwasababu ya Upendo ndio aliamua kumtoa mtoto wake wa pekee ambapo sasa huyo mtoto wake wa pekee kazi yake ilikuwa ni kuuleta wokovu kwa kila anaye amini maana yeye ulikuwa ndio wokovu pekee maana Damu za kondoo na wanyama wengine hazikuweza kuondoa dhambi ya mwanadamu bali zilizifunika Dhambi ambapo kila mwaka ilimpasa kuhani kupaingia patakatifu pa patakatifu afukize uvumba ili kufunika dhambi za wana wa Israel.

Waebrania 10:1-4 (KJV) Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.
 Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi?
 Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka.
 Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.

Ukisoma hapo juu unaona ambavyo dhabihu zote zilikuwa bado zina kumbukumbu la dhambi ndio maana sasa Mungu kwa Upendo wake aliona kwamba sio vyema sasa huyu mtu abaki kuwa na kumbukumbu la dhambi akataka sasa kumfanya huyu mtu aweze kuwa huru mbali na dhambi zote akiwa na lengo la kumfanya mwanadamu kuwa mtakatifu asiyekuwa na mawaa ya aina yeyote kama ambavyo alikuwa amemuumba hapo mwanzo akiwa ni mtakatifj kamili kama ambavyo yuko Mungu mwenyewe.

Sasa ukiwa umeambatana na mimi toka sehemu ya kwanza mpaka hapa utaona ya kwamba kuna mambo makuu mawili yanayoleta wokovu na kuwa kamili kwa mwanadamu ambayo ni
  1. Neno la Mungu
  2. Imani
A. NENO LA MUNGU
Neno la Mungu ni mbegu ambayo hiyo hupandwa kwa mwamini na kumpatia ufahamu na uelewa juu ya kile ambacho Mungu anakuwa amekikusudia kwa ajili yake.

Luka 8:11 (KJV) Na huo mfano, maana yake ni hii; Mbegu ni neno la Mungu. (Soma kuanzia msitari wa 4-15) 

Ukiangalia huo mfano utaona namna Yesu anajaribu kuwaelekeza wanafunzi wake namna ya uwezo wa mbegu kuweza kuleta matokeo ambapo ili kuleta matokeo kunategemea na mpokeaji namna ambavyo yeye yuko ambapo nitaidadavua vizuri kwenye kipengele cha Imani. Kwamba mbegu inakuwa haina shida kuleta matokeo isipokuwa huyu mtu ambaye anatakiwa kupata mabadiliko ndio itabaki kwenye utashi wake kuweza kuamua kukubali mabadiliko au la.

Sasa ukisoma kiundani zaidi utaona unapolizungumzia Neno la Mungu unakuwa moja kwa moja unamzungumzia Yesu kristo.

Yohana 1:1-5 (KJV) 
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.


Yohana 1:14 (KJV) Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

Ukisoma vifungu hivyo viwili unaona mojaa kwa moja kwamba huyo neno alikuwa kwa Mungu na alikuwa Mungu na alifanyika mwili ambapo hapo unakuwa unamzungumzia Mungu katika nafsi mwana katika utendaji wake kwenye utatu mtakatifu wake. Sasa Huyu neno ndiye ambaye analeta Nuru au mwangaza kiasi kwamba huyu mwanadamu anaweza kujua uhalisia wa Mungu katika uzuri wake wote maana humfunua Mungu. Pale anapokuwa anafunuliwa Mungu tunakuja kuuona Upendo wa Baba namna anafanya kujitoa mwenyewe ili sisi tuweze sasa kuokolewa. Kama Mungu asingejitoa kwetu na tukaona namna ambavyo Neno la Mungu linaweza kuleta matokeo kwenye maisha Yetu ambapo tokeo kubwa ni kutupatia wokovu.

Sasa pasipokuwa na neno la Mungu (Yesu kristo) hakuna mtu yeyote anaweza kuokoka maana tena Jina la yesu ndilo ambalo sisi wanadamj tunapaswa kuokolewa kwalo na hakuna jina lingine lenye uwezo wa kutupatia wokovu.

Matendo ya Mitume 4:12 (KJV) Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.

Ukisoma toka msitari wa kwanza wa sura hii ya nne utaona namna ambavyo mafarisayo walikuwa wakilalamika kwamba wasieleze habari zozote kupitia jina la Yesu na baadaye Petro akiwa amejaa Roho mtakatifu anakuja kuwaambia kwamba hakuna wokovu unaweza kupatikana nje ya Yesu na hakuna Jjna zaidi ya Yesu ambalo mwanadamu anaweza kuokolewa kwalo. Kwahiyo pasina kuwa na neno la Mungu hakuna wokovu wa aina yeyote unaoweza kupatikana.


B. IMANI
Ukirejea andiko letu tuliloanza nalo kwenye kipengele hiki cha pili (Yohana 3:16) utaona kuna jambo linaelezewa kwamba  aaminiye ataokoka (Tendo hili ndilo linaleta IMANI). Kwahiyo moja wapo ya vitu vya msingi katika kuupata wokovu ni kupitia Imani ambayo hii inatoka kwa mwanadamu. Basi kabla hatujaenda mbali naomba tuangalie Imani ni kitu gani sasa.

Maana ya Imani kulingana na maandiko yanavyosema

■  IMANI ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana(Waebrania 11:1)

Ukisoma hilo fungu linakuletea moja kwa moja maana ya Imani ambayo hiyo tumekuwa tunaambiwa kila inapoitwa leo. Kwahiyo Imani lazima ijengwe katika uhakika ambapo mtu anakuwa haoni katika mazingira ya kawaida bali anajua hii itakuwa kama hivi. Kiufupi ni kuwa na taraja la uhakika. Kwahiyo mtu inatakiwa awe na uhakika kwamba pale anapomkiri Yesu anapata moja kwa moja wokovu pasipo hivyo haiwezekani kuwa na huo wokovu.

■ IMANI ni hali ya ndani kwenye eneo la nafsi ya mtu au mwamini kuweza kupokea kile ambacho Mungu amekileta kwa ajili ya usalama wa Roho yake.

Warumi 10:17 (KJV) Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

Kwahiyo Hakuna kuamini pasipokuwa na taarifa mwanzo ndio maana Sehemu ya akili kwenye Nafsi ya mtu lazima ipokee taarifa juu ya wokovu ambao huo unakuja kupitia neno la Mungu. 

Kwahiyo Imani huwa inakuwa ni mwitikio wa mwanadamu juu ya kile Mungu anataka kufanya kwenye maisha yake mwenyewe. Kwahiyo sisi lazima nafsi zetu ziitikie kuwa kuna jambo la kupewa wokovu pasina kulazimishwa na mtu yeyote. 

Hapa lazima utashi wa mwanadamu(Sehemu ya nafsi) uamue kukubaliana na taarifa za kukombolewa. Moja wapo ya kitu cha thamani na kitu hatari Mungu kampatia mwanadamu ni UTASHI. Ni kitu cha thamani kwakuwa kinampa mwanadamu kuamua atakavyo kama  Mungu anavyoweza kuamua lakini ni hatari kwakuwa pia unaweza kuamua kufuata mapenzi yako nje na mapenzi ya Mungu yaani unaweza kuamua kinyume na Mungu.

Kwahiyo Suala la kuamini ni suala liko kwenye uwezo wa mwanadamu kuweza kukubali au kukataa ila Roho mtakatifu anakuwa anatoa ushauri tu wa vitu unapaswa kufanya kwa wakati fulani. 

■ IMANI ni kuwa na tumaini kamili liletalo uaminifu na kujitolea


Tumaini ni taraja analokuwa nalo mtu juu ya jambo fulani kwamba litakuja kutokea. Sasa hili taraja lazima lisiwe na shaka ya aina yeyote ndipo linakuja kuwa imani ambalo hili linakuja kumjenga mtu katika kufanya kwa uadilifu kamili (Utakatifu usiokuwa na mawaa ya aina yeyote) na huyu mtu anakuwa yuko tayari kufanya kwa ajili ya Mungu (kujitoa).

Habakuki 2:4 (KJV) Tazama, roho yake hujivuna, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake.

Waebrania 10:38-39 (KJV) Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.
 Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.


Habakuki alikuwa analia akiwa anaona maovu yanaongezeka na Mungu bado haonyeshi kufanya lolote na Mungu anakuja kumjibu kuwa mwenye haki anaishi kwa Imani hata kama haoni kwa nje maana akisitasuta Mungu anakuwa hana furaha naye tena.

 Pia ukiangalia mwandishi wa Waebrania (Inasemekana ni Paulo japo haijawa wazi moja kwa moja) anajaribu kuonyesha na kuongea na kanisa kwamba lilipokuwa limempokea kristo kwanza lilistahimili sana baadaye anaona kama kuna namna hawaendi kama wenye haki anakuja wakumbusha sasa kuwa wataishi kwa Taraja kamili sasa maana wao wako miongoni mwa walio na imani ya kuokolewa Roho zao. Ndivyo ambavyo iko kwamba huwezi kuokolewa pasina kuwa na Imani hata siku moja kwahiyo lazima sasa nawewe nafsi yako ikubaliana na wokovu unaoletewa na Mungu.

Kwahiyo NENO LA MUNGU huleta wokovu huku IMANI ni mkono wa kuupokelea huu wokovu ambao unaletewa na Mungu ambapo ukikiacha kimoja wapo kati ya hivi viwili haviwezi kuwa na ukamilifu wa aina yeyote kwahiyo na wewe uwe na utayari hata kama umepewa bure haina maana hakuna utayari unaotakiwa kuwa nao.

Note 1: Wokovu ni mkono wa Mungu wa kuleta usalama kwa mwanadamu ikiwa ni 
  1. Kusamehewa dhambi, 
  2. Kuhesabiwa haki na 
  3. kupewa utakatifu

Note 2: Imani huu ni mkono wa mwanadamu wa kupokelea mambo makuu matatu ya usalama kutoks kwa Mungu ambayo ni
  1. Kusamehewa Dhambi 
  2. Kuhesabiwa haki
  3.  Kupokea haki

4. MWANADAMU ANAWEZA KUOKOKA TU PINDI AKIWA YUKO HAI NA SIO BAADA YA KUFA.
Kumekuwa na dhana ambapo watu hawaamini kuwa kuna uwezo wa watu kuokoka akiwa yuko hapa Duniani wakiwa wanaamini tu kwamba mtu huwa anaongoka tu na anakuja kuokoka baada ya kufa.

Kabla ya yote labda tuangalie maana ya KUONGOKA na tutaangalia uhusiano wa KUONGOKA na KUOKOKA.

KUONGOKA hii ni hali ya mtu kugeuka kuelekea kwenye uthabiti kwenye Imani pasipo kupeperushwa na Upepo mbalimbali au mafundisho yanayokuja kwenye kipindi cha maisha.

Luka 22:31-32 (KJV) 
 Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano;
 lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako.
Ukisoma andiko hapo juu linajaribu kutupa mwongozo wa kuongoka ukoje ambapo sasa ukiangalia Yesu anamuambia petro kuwa atapitia nyakati ngumu lakini akisha kugeuka na kuwa kwenye Imani aliyowaachia basi awarejesha na wenzake. Kwahiyo kuongoka ni kugeuka katika uthabiti au uimara unaopaswa kuwa kama msingi wa neno.

Mathayo 18:3 (KJV) akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Yesu alikuwa anajaribu kuonyesha kwamba lazima mtu ageuke kama watoto maana hawa watoto wakiamua kukufuata huwa wanafanya katika kweli pasina kinyongo maana mioyo yao inakuwa haijatiwa sana na giza. Kwahiyo ukiongoka unakuwa umemgeukia Mungu wako.

1 Timotheo 3:6 (KJV) Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.
 Ukiangslia hapo Paulo anampa waraka Timotheo kuonyesha sifa za Askofu kwamba hapaswi kuwa mtu ambaye ameongoka hivi karibu yani hajageuka kuishi imani katika uthabiti akaja kunasa kwa mtego wa kujisifu maana bado atakuwa hajapata baadhi ya mambo ya msingi kuweza kuwa thabiti kwenye Imani.

Tumekwisha kuona sasa maana ya kuongoka ambapo hapo inakupa mwongozo kuwa ni suala la kuimarika katika uthabiti wa imani kwahiyo sisi tunaendelea kuongoka tukiwa katika Imani kwasababu kristo huwa anajifunua kwa kadri anavyotaka kiasi kwamba huwezi kujisifu kwamba nimeshakufika ndio maana hata paulo alisema kwamba

Wafilipi 3:12-14 (KJV) Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.
 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;
 nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.

Hili la kusema Duniani hakuna kuokoka huwa watu wanajenga msingi wao kwenye kifungu hiki hapa chini, ngoja tukichambue kidogo

Mathayo 10:22 (KJV) Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
(Soma pia Marko13:13, Mathayo 24:13)

Ukisoma hilo fungu hapo juu unaweza hitimisha kwamba kumbe wokovu au kuokoka ni pale mwisho wa safari ya mwanadamu lakini ukisoma kiundani utaweza kuelewa vizuri kabisa.

Hapo Yesu alikuwa akiwaambia wanafunzi wake juu ya nyakati ambazo zinawajia kwamba watapita katika moto lakini inawapasa kuvumilia isije ikatokea mtu kwasababu ya magumu anakuja kuikana Imani, hapa ndipo anakuja kueleza sasa matokeo ya kuikani Imani ndio hayo unakuwa umepoteza wokovu au usalama wako hapa ndipo pana msingi wa kwamba sasa hizi nyakati ukishakuwa thabiti (Ongoka) ndipo penye usalama wako. Sasa hili neno linazungumzia kuto kuikana Imani na kama wewe utaikana imani ni moja kwa moja wewe huwezi kumpendeza Mungu.

Waebrania 11:6 (KJV) Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

Sasa ukiona pasipokuwa na Imani haiwekani kumpendeza Mungu ina maana kwamba wewe una farakakanisha mahusiano yako wewe na Mungu wako

Kama ndiyo hivyo, kwanini sasa haiwezekani mtu kuokoka baada ya kufa??
Mtu anapokuwa amekufa kinachotokea ni kwamba Mwili na Roho vinatengana maana Roho inapomtoka mtu huwa inaondoka na Uzima wake ndio maana maandiko yanasema kwamba

Yohana 6:63 (KJV) Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
Kwahiyo pasina Roho hakuna uzima wa aina yeyote na kama hakuna uzima wa aina yeyote thamani ya mwanadamu inakuwa sasa haiko katika Mwili ule. Na mtu ili aweze kuokoka huanzia kwenye kuamini kwake pindi anapokuwa yuko katika mwili sasa akiwa amekufa atawezaje kuamini? Au atawezaje kulisikia neno la Mungu ili liweze kumbadilisha ingali hayupo katika mwili?? Sasa kama umefuatana nami vizuri utakuja kugundua kwamba huyu mtu aliyekufa anakuwa ameshapoteza sifa za kuweza kuokoka maana huyu mtu anakuwa hana hata uwezo wa kutubu. Ndio maana biblia inasema kwamba

Waebrania 9:27 (KJV) Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;

Ukisoma hapo unaona kwamba mtu anapokuwa ameshakufa kinachotokea mara moja ni kuhukumiwa na hapa kuhukumiwa ni kupewa haki yako kjlingana na namna ambavyo ulikuwa umeishi hapa duniani na sio vinginevyo  maana kila mtu atalipwa sawa sawa na matendo yake. Kwahiyo hakuna nafasi ya kuweza kutubu pindi mtu anapokuwa amekwisha kufa.

Pia hakuna mabadiliko yanaweza kutokea ikiwa hata mtu ataombewa Dua za kutosha ili Mungu amsamehe Dhambi zake alizofanya baada ya kufa. Mpendwa katika kristo Yesu usidanganyike kwamba eti mtu akifa anaweza kuombewa akabadilishiwa hatima ya kule alikokuwa anapaswa kwenda kwa kuombewa basi ingekuwa hivyo ilimpasa na kristo Yesu kuteswa mara mbili, mtu alishapewa msamaha wa dhambi tayari kazi yake ni kukubaliana na hilo pindi akiwa bado yu ngali ni mwenye uzima baada ya hapo utapewa kulinganisha na matendo yako.

Kwahiyo kuokoka ni hapahapa Duniani  na sio mbinguni kama wengine wanavyofikilia. Fanya uwezalo usikubali kufa kabla hujampokea Yesu kristo. Yesu yuko kazini bado anatafuta mtu aliyeko tayari aweze kumsamehe dhambi zake na kumpatia wokovu ulio jaa thamani isiyokuwa na mawaaa ya aina yeyote.

Note; Kwahiyo kuokoka ni suala la mwanzo kabisa ambalo mtu anapaswa kuwa nalo huku kila anapoendelea kuishi anaendelea kuongoka (kuwa thabiti katika Imani).

Neema ya wokovu bado imefunuliwa kwako kama hujampokea Yesu krusto kuwa Bwana na mwokozi wako wakati ni huu sasa wa kuweza kutengeneza maisha yako na Mungu ili aweze kukupatia usalama ulio jaa msamaha wa dhambi, kuhesabiwa haki pamoja na utakatifu. Unaweza kuwasiliana nami kwa njia ya mawasiliano yangu hapa chini kwa msaada na maswali na kujengana xaidi.

Naomba tukutane sehemu ya tatu ya mwendelezo wa somo letu pindi Mungu akitupatia kibali.

Ulikuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo 
+255766944441
jackobombwaga@gmail.com 


KUUTUNZA WOKOVU (SEHEMU YA KWANZA)


Bro Jackobo



Utakuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo 
+255766944441
jackobombwaga@gmail.com 

Bwana Yesu asifiwe watumishi wa Mungu?? Karibu tena katika Darasa ambalo Mungu kanipa neema ya kuweza kushiriki nanyi sehemu ya Mambo Mungu kanipa kuelewa kwa kiasi ili niweze kushiriki nanyi baraka hizi za Rohoni. Tutajifunza Juu ya kuutunza wokovu ambao Mungu ametupatia kupitia Yesu kristo.

Vipengele muhimu vya somo vitakuwa kama ifuatavyo
1. Utangulizi wa Somo
2. Maana ya wokovu katika mitazamo mbalimbali namna biblia imeeleza
3. Mambo ya msingi katika kupata wokovu
4. Kujibu dhana ya mwanadamu kuweza kuokoka akiwa bado yupo Duniani na sio baada ya kufa
5. Kweli kuu juu ya uhusiano wa matendo na wokovu
6. Mambo yanayo imarisha wokovu
7. Mambo yanayo dhohofisha wokovu

1. UTANGULIZI
Ashukuriwe Mungu ambaye siku zote anatufanyia mambo mengi kwenye maisha hata kama hatukusitahili ila anatustahilisha kuwa nayo na kuwa na uhalali kamili wa kuyamiliki hayo.
Mungu alipo muumba mwanadamu alimuweka bustani ya edeni kwa kupenda mwenyewe lakini hakuacha mwanadamu aweze kukaa peke yake bali alimpa na kampa aitunze kitu ambacho kinatupa ufunguo kwamba lolote Mungu anakupa kuna sehemu ya wewe kufanya hata kama umepewa bure.

Mwanzo 2:15
"BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza."

Pia ukiangalia hata maisha na uhai wetu Mungu ametupa hatuna sehemu ya kujiongezea uhai wetu ila Mungu ametupa maarifa ya namna nzuri ya kuhakikisha tunatunza afya zetu ndio maana kawapa wengine neema ya kuwa madakitari, wauguzi, wataalamu wa maabara n.k ili kuhakikisha kwamba afya zetu zinakuwa imara. Pia katoa baadhi ya mambo mtu anaweza akafanya ili asijikute afya yake ikawa inatahayarika mfano kufanya mazoezi, kula mlo kamili n.k. lakini mambo yote haya lazima yafanyike huku Mungu anakuongoza na kukutangulia maana kwa akili zako wewe huwezi ndio maana maandiko yanasema..

Zaburi 127:1
"BWANA asipoijenga nyumba waijengao wafanya kazi bure Bwana asipoulinda mji yeye aulindaye akesha bure"

Pia ukisoma hapa

Yuda 1:3
"Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu."

Ukisoma andiko la hapo Juu utaona Yuda alivyoandika waraka wake maana aliona kwamba wamepewa wokovu bure lakini haina maana kwamba ndio wakae hivi hivi akaamua kuwaandikia waweze kuelewa kwamba imewapasa kuishindania imani maana hata wokovu ni Tendo linalo kuja kwa imani. Pia aliandika hivyo kwasababu alijua kuwa kuna mafundisho mabaya ya kuwaharibu kama hawatasimama imara kuishindania imani. Kwahiyo hapo anatuonyesha umuhimu wa kutunza kile ambacho umepewa na Mungu.

Nimeandika haya yote kwasababu kuna watu wanao amini ya kwamba mtu akisha kuokoka hana jambo la kufanya kwakuwa Yesu kristo amekwisha kumaliza yote wanasahau kwamba Mungu anasema hivi..


Mathayo 11:28-30
"[28]Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. [29]Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; [30]kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi."

Yesu anaeleza kuwatua watu mizigo (Kuondoa tabia zisizostahiki kwa kumpa uwezo wa kuacha), tena anatoa wito wa mtu kwa utayari wake kujifunza kwake mwenyewe na sio kumlazimisha mtu (Hapa inaonyesha wazi kuna jambo la mwitikio kwa mwamini juu ya mambo ambayo Mungu anataka kukupea wewe kama mwamini, tena anamaliza kwamba kuna kazi ya kuubeba mzigo wake ulio mwepesi(Hapa anaonyesha tabia za haki ambazo mwamini anatakiwa kuwa nazo ambazo zinabaki katika uwezo wa mwanadamu yeye mwenyewe kuamua kumfuata au kuishi wema pasipo kulazimishwa). Kwahiyo Mungu anapofanya kwako kuna sehemu ya wewe kulinda kile Mungu amekupa.

2. MAANA YA WOKOVU KATIKA NAMNA MBALIMBALI AMBAZO BILBLIA IMEELEZEA.
Kumekuwa na dhana na Imani ambazo haziamini kwamba kuna kuokoka hapa Duniani zikiamini hakuna mwanadamu anaweza kuokoka akiwa Yupo hapa Duniani mpaka atakapokufa lakini katika msingi wa maandiko haijakaa sawa kwasababu biblia inaeleza wazi kwamba kuna uwezekano wa mtu kuokoka hata anapokuwa hapa Duniani.

Naomba tuangalie maana mbalimbali zenye mlengo mmoja katika kuelezea wokovu ni nini.

  • WOKOVU ni mpango wa Mungu kumtafuta mwanadamu ili kumrejesha huyu mwanadamu katika sehemu ambayo alikuwa amemuweka aweze kukaa katika asili yake.
Mwanzo 2:7-8
"[7]BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. [8]BWANA Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya."

Mungu alituumba tuweze kukaa bustani ya Edeni ambapo kulikuwa hakuna magonjwa wala tabu za aina yeyote yaani ilikuwa ni sehemu ya amani ya kujitosheleza. Sasa baada ya anguko la mwanadamu Mungu alimuondoa mahali pale kwakuwa tayari alikuwa ashaleta tabia ambazo hazikupaswa kuwepo pale.
Sasa Mungu alianza kumtafuta mwanadamu tangu pale alipoanguka ili amrejeshee utakatifu aliokuwa ameupoteza ns ndio maana huu mpango ulianza kwa kusurubisha Dhambi yaani kiufupi palipo na na dhambi kuna adhabu itokanayo na hiyo dhambi. Sasa Mungu kwa kumpenda mwanadamu ili amuokoe na ile adhabu aliamua kumuua mnyama ili ampe mwanadamu sitara yake kwakuwa alikuwa alishapoteza utukufu wa Mungu.

Mwanzo 3:21
["21]BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.

Hapa Mungu alifanya ili kumpa mwanadamu heshima kwasababu ya Upendo wake ambapo ni utabiri wa wokovu kwa mwanadamu na ndio maana aliwavisha mavazi ya ngozi ikiwa na maana kwamba kuna mnyama alikufa ili Adamu na Eva wapate sitara.

Waefeso 2:10 (KJV) Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.

Mungu alimuumba mwanadamu aweze kuishi maisha yaliyo jaa matendo mema ambapo hapo Mungu alipomuweka Adamu Edeni alikuwa amemuelekeza kuishi maisha yaliyo mema peke yakena sio vinginevyo. Sasa huu mpango wa kumuokoa unamfanya mtu aweze kurudi katika lile kusudi la Mungu la asili kuishi katika matendo mema peke yake.

Sasa uwezo wa kuishi matendo mema ulipotea pale mwanadamu alipokosea pale edeni

Mwanzo 2:16-17 (KJV) Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,
walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Sasa ukiona hilo neno hakika utakufa ndio hilo linaonyesha kuvunjika kwa ushirika uliojaa uwezesho wa kuweza kufanya mapenzi ya Mungu ndio maana sasa Mungu alimtuma sasa Yesu kristo ili aweze kuturudishia huo uwezo wa kuweza kuishi tukiwa tuko hai yani tukiwa tunafanya mapenzi ya Mungu.

  • Wokovu ni hali ya kuwekwa mbali na hatia na adhabu itokanayo na makosa ambayo mwanadamu ameyafanya na kupewa haki kwa kumuamini Yesu kristo.
Mahali popote panapokuwa na makosa lazima kuwepo na adhabu stahiki kwa kukosea  huko. Sasa ukija katika suala la wokovu ni kwamba Mungu anakuweka mbali kabisa na makosa  kwakuwa umemuamini Yesu kristo.

Warumi 3:23-25 (KJV) kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;
 ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake,ili aonyeshe haki yake ,kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilzotangulia kufanywa.

Ukiangalia andiko hapo juu linaonyesha kiuhalisia mwanadamu hana haki mbele za Mungu maana kafanya dhambi ila haiishii hapo inakuja kutoa maelekezo kwamba kuna kuhesabiwa haki kupitia kuamini ukombozi wake unaopatikana kupitia Yesu kristo maana yeye anatukomboa kutoka kwa shetani kwa kutupatanisha na Mungu kupitia Damu yake mwenyewe iliyo mwagika pale msalabani. Sasa pale ambapo wewe unapo kuja kuamini kazi ya msalaba ndipo sasa unakuwa una haki mbele zake ndio maana ukisoma hapa...

Warumi 10:9-10 (KJV) Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.

Kwahiyo unaona kazI ya mwanadamu ni kumkiri Yesu, kumuamini Yesu ndipo anapata kuokolewa na hapo ndipo ambapo sasa moyo (Sub-Concious mind) huamini kiukweli kulinganisha na taarifa ambayo huyu mwanadamu anapaswa kuwa nayo kwanza na kukiri kwa kinywa chake na kuupata wokovu. 


Warumi 8:1-2 (KJV) Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.

Ukisoma hapo pia juu unaona kwamba mtu aliye ndani ya kristo hakuna hukumu ya aina yeyote anayoweza kuipata maana yeye anaye Roho mtakatifu ambaye huyo humuweka na kumpa nguvu ya kuishi nje ya dhambi. Kwahiyo ile hukumu ilipaswa kupatikana kupitia dhambi Yesu aliishaiondoa na kutufunza sisi sasa kumuishia Yeye kwenye maisha Yetu ya kila Siku.

  • Wokovu ni kipawa cha Mungu ambacho kimefunuliwa kwa mwamini na kumpa uwezo wa kuishi mbali na dhambi
Waefeso 2:8 (KJV) Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;

Sasa huu wokovu ni zawadi ambayo Mungu amempatia mwanadamu ambayo yeye mwanadamu hana namna yeyote ya kufanya ili apate bali Mungu mwenyewe ndiye ameachilia kwa mwanadamu kwa kupenda kwake yeye mwenyewe.

Sasa hiki kipawa ndicho ambacho humpa mwamini kuweza kuishi sasa nje ya dhambi na ndio maana hakuna mtu anaweza sema nimeokoka akawa bado katika matendo yasiyo katika njia ya Mungu maana katika kufunuliwa kwa kipawa hiki ndiko ambako sasa kunaleta uwezo wa kuyaishi mapenzi ya Mungu maana hiki kipawa kinapofunuliwa kina mpa mwanadamu shule au Elimu ya namna ya kuishi akiwa yuko hapa Duniani.

Tito 2:11-12 (KJV) Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;

Kwahiyo unapopewa wokovu ni kwamba umepewa uwezo wa kuishinda dhambi kiufupi.

Hitimisho:  Kutokana na maana hizo hapo juu tumejifunza tunaweza kueleza kiufupi kwamba WOKOVU ni usalama ambao mwanadamu anakuwa anaupata pindi anapokuwa ameshamkubali, kumuamini na kuamua kufuatana naye kwenye maisha yake huyu mtu anakuwa amekwisha kuokoka na kuwa na haki zote za urithi kwakuwa mwana wa Mungu kwelikweli. Hii inaonyesha hapa

Yohana 1:12 (KJV) Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;

Mungu akubariki kwa kufuatana na mimi kwa sehemu hiii ya kwanza  ambapo ni kama msingi unaotupa kuelewa vizuri tunako elekea. Niombe basi ufuatilie sehemu ya pili itakuwa na package nyingine inayoendelea. Nkngeweza kuendelea lakini  ukiweka mambo mengi sana wengine hawawezi kusoma ndio maana nimejaribu kuligawa somo hili.

Lakini kama hujaokoka na unatamani kuingia kwenye ushirika huu wa Kuwa na Yesu kristo kristo kwenye maisha yako unaweza kuwasiliana nami kupitia mawasiliano hapo chini.

Ulikuwa nami mtumishi katika Kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo 
+255766944441
jackobombwaga@gmail.com 

KUFUNGIWA NIRA PAMOJA NA KRISTO/ USHIRIKA NA KRISTO (Sehemu ya Kwanza)


Bro Jackobo


Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu?? Karibu tujifunze kidogo neno la Mungu juu kufungiwa Nira pamoja na Kristo.

Utakuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

Maana ya Nira
Nira ni mti ambao unawaunganisha kwa pamoja ng'ombe (Maksai) wawili wanapokuwa wanalima.

Kwahiyo kufungiwa nira pamoja na Kristo ni hali ya kujijenga kimahusiano au kiushirika baina ya mwanadamu/Mwamini na Mungu wake kupitia Kristo Yesu.

2 Wakorintho 6:14
"Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?"

Ukisoma vizuri maandiko hapo juu utaona ya kwamba mtumishi wa Mungu Paulo alipokuwa anazungumza na wakorintho anazungumzia suala la kufungiwa nira na wasio amini kwa namna isiyo sahihi, kumbe Katika kufanya ushirika Kuna masharti na vigezo vya ushirika.

Hakuna ushirika wowote usio kuwa na vigezo na masharti lazima viwepo vitu ambavyo ndio kipimo cha kuweza kushirikiana baina ya watu hawa wakiwa kwenye kuhusiana. Kwahiyo Tunapokuja kuzungumzia suala la Kufungiwa nira pamoja na Kristo lazima viwepo vigezo vinavyotakiwa kuwepo ili huyu mwamini aweze kushirikiana na Mungu wake katika Utumishi ambao kaitiwa na Sio kwenda pasipo kuwa na utaratibu.

Sasa ukiangalia mwanzilishi wa kwanza wa Ushirika alikuwa ni Mungu mwenyewe ambaye yeye ndiye alitaka kuwa na uhusiano na mwanadamu ndio maana baada ya anguko la mwanadamu pale Bustani ya Edeni Mungu yeye ndiye alikuwa wa kwanza kutangaza kutaka ushirika๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Mwanzo 3:21 (KJV)
"Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika."

Kitendo cha Mungu kuwafanyia Adamu na eva mavazi ilikuwa ni kurudisha uhusiano waliokuwa wameshauharibu kwa kukosa utii kwenye maisha yao. Mavavi huwa ni Sitara na tena aliwatengenezea mavazi ya ngozi ikimaanisha kwamba kuna mnyama ambaye aliuawa ili yeye azichukue dhambi za Adamu na Eva, kwahiyo hatia ya makosa ya Adamu na Eva ilikuwa juu ya mnyama aliye uawa ili watengenezewe mavazi hawa watu. Huu ni upendo wa Ajabu sana Ambao Mungu ana muonyesha mwanadamu kwamba licha ya kuwa kakosea ila bado anatamani huyu mwanadamu awe na mahusiano na yeye, Hii ndio maana halisi ya kwamba Mungu katupenda kwa upendo wa milele๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Yeremia 31:3 (KJV)
"Bwana alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu."

ukiangalia maandiko hapo utaona Mungu anamuambia Yeremia ili asije akajidharau bali ajichukulie katika heshima ambayo Mungu amempatia. Ndivyo ambavyo Mungu ametupenda na sisi na anataka tuishi na kujiona ni wenye thamani ili tusije tusikajidharau na ndio maana ametuita kwa fadhili zake ili tuweze kuwa karibu na yeye.

Sasa Mungu alikuwa ameona kikwazo kilichopo ambacho huwa kinawafarakanisha wanadamu na Mungu ambapo ni maovu au dhambi tunazozifanya. Maana Mungu huwa hawezi kuwa na Ushirika na mtu ambaye anazo Dhambi maana huwa dhambi zina mtenga mtu na Mungu wake๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Isaya 59:1-4 (KJV)
"Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong'ona ubaya. Hapana adaiye kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu."

Sasa baada ya kuona hilo kuwa mwanadamu akiwa na Dhambi hawezi kushirikiana na yeye ili mlazimu amtume mwanawe Yesu kristo aje kuwa ondoleo la dhambi zetu tulizokuwa nazo wakati huo๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Yohana 3:16 (KJV)
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

kwasababu ya Upendo wake Mungu aliona ni vyema sasa akamtoa Mwanawake yeye azichukue dhambi zetu pale kalivari ili aweze kushirikiana na Sisi

Yohana 1:29 (KJV)
"Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!"

Waebrania 9:26 (KJV)
"kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake."

1 Timotheo 1:15 (KJV)
"Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi."

Ukisoma vifungu vyote hapo juu utaona Yesu kumbe ndiye alikuwa ondoleo la Dhambi kwa mwanadamu kwahiyo mimi ili niweze kushirikiana na Mungu lazima nikubali kazi ya msalaba ambapo yeye alizibeba Dhambi zetu pale kalivari.

Isaya 53:12 (KJV)
" Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji"

Isaya alipewa maono juu ya Yesu kuchukua dhambi zetu ndio maana hata pale msalabani Yesu alikuwa akilia Kwamba Mungu mbona kamuacha kwakuwa dhambi za ulimwengu zilikuwa juu yake na Mungu haambatani na dhambi hata siku moja๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Mathayo 27:46 (KJV) 
"Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?."

Kwahiyo kwasababu hiyo lazima sisi kama waamini tuwe na ushirika na Yesu Kristo wakati wote maana bila yeye hatuwezi kuwa na mahusiano mazuri na Mungu.

KAZI YA YESU KWENYE USHIRIKA WAKE NA MWAMINI ANAVYOIFANYA
Kuna mambo mengi Yesu huwa anayafanya kwenye maisha yetu ili tuweze kuwa na ushirika naye embu tuangalie๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Mathayo 11: 20-30 (28-30) (KJV)
"Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi."

✍️✍️ Yesu alifanya miujiza lengo kuwafanya watu wa miji hiyo wamuamini kwa ajili ya kazi alizokuwa anazifanya
✍️✍️ Tena miujiza huwa inadhihirisha utendaji wa Mungu katika eneo japo hapa lazima kuwa makini maana hata shetani huwa anafanya miujiza ili aweze kuwateka watu waweze kumuendea yeye kwenye maisha yao.
N.B: Huo utendaji na udhihirisho wa Mungu kamili unatosha kabisa kumfanya huyu mtu aweze kuamini na kuingia kwenye pendo la Mungu yaani katika NIRA.
✍️✍️Yesu sasa anawaita watu wote wenye mizigo/Dhambi waje kwake ili aweze kuwatua hapo ndipo tunapo pata nafasi ya kuwa na ushirika na Yeye.

Mathayo 8:4 (KJV)  
" Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao."

Marko 1:44 (KJV)  
"akamwambia, Angalia, usimwambie mtu neno lolote, ila enenda zako ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe alivyoamuru Musa kwa kutakasika kwako, iwe ushuhuda kwao."

✍️✍️✍️ Yesu alimuambia mtu yule mwenye ukoma akajionyeshe kwa makuhani kama sehemu ya kuwafanya na wao waelewe na  waamini kazi ya Mungu ili na wao pia waingie kwenye ushirika wake wakati wote.

Embu turudi kwenye andiko letu la msingi la kwanza๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

2 Wakorintho 6:14-18 (KJV)   
"Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.  Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,"

Paulo alikuwa anazungumza na watu wakorintho kujiepusha na mambo yafuatayo
1. Ibada ya sanamu
2. Kulichafua hekalu la Mungu
3. Kufanya uasi yaani kwenda kinyume na sheria ya Mungu
 4. Kuacha kumtazama Yesu kama mwanadamu yaani asiringanishwe.

Sasa ikiwa tunayaishi hayo hapo juu ndio kufungiwa Nira pamoja na wasio amini maana hayo ndiyo asili yao kwenye mambo kama hayo. Kwahiyo lazima kujitenga na kila namna inayoleta shida kwenye ushirika na Mungu wetu maana tunapo yaepuka hayo ndipo yeye anakuwa Baba kwetu nasi tunakuwa wana (Shirika au uhusiano au Nira inawekwa baina yetu na Baba).

hii ndiyo maana yesu alipokuwa akiwafundisha wanafunzi wake aliwajenga zaidi katika mahusiano mazuri zaidi na Mungu (Mathayo 6:9-15).

Paulo anawaambia watu wa Korintho kuweka mbali kila namna ya Uovu kwenye maisha yao akitamani Dhambi isitamkwe kwao yaani maisha yawe ya ushuda wa kristo maana kuishi maisha ya ushuhuda huwafanya wengine ambao walikuwa hawaamini kuvutwa kuja kwa kristo Yesu. Kwahiyo kama kanisa lazima tuishi kwa ushuhuda  mzuri ili tuwe na ushirika na Mungu ili hata wengine wavutwe kwenye huu ushirika na Mungu.

Mungu akubariki kwa kuambatana na mimi tangu tumeanza sehemu hii ya kwanza ya somo tutaendelea sehemu ya pili pale Mungu atatupa kibali. Unaweza ukamshirikisha na mwenzako juu ya neno hili ambalo Kristo ameliweka ndani yangu kwa ajili ya Kanisa lake la wakati huu


Ulikuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com


KIU YA KUMTAFUTA MUNGU (sehemu ya pili)


BRO JACKOBO

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu??
Utakuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com


Kutokana na baadhi ya maswali na michango nimekuwa nikiipokea nimeona ni vema niongezee kipengele cha pili kwenye somo juu ya KIU YA KUMTAFUTA MUNGU kwa upande wa Umuhimu wake

Kama haujasoma sehemu ya kwenza unaweza kubonyeza hapa๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰SEHEMU YA KWANZA

Basi Nikianzia na maana niliyokuwa nimetoa mwanzoni๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

 KIU hii ni hali ya ndani anayokuwa nayo mtu ili aweze kupata au kufanikisha jambo fulani alilokuwa na uhitaji nalo. 

 Kiu ya kumtafuta Mungu hiii ni hali ya ndani inayojengeka kwenye Nafsi ya mwamini kuhitaji ushirika na Mungu katika nyanja zote za maisha yake yani kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiroho.


UMUHIMU WA KUWA NA KIU YA KUMTAFUTA MUNGU KWA MWAMINI 
Sasa umuhimu wa kuwa na kiu uko hivi ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

1. Kumruhusu Mungu achukue hatamu ya maisha kwa kila jambo ambalo utakuwa unalifanya

 1 Wakorintho 10:31
 "Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu."

Ukisoma hilo Fungu unaona Paulo ana wausia watu wa Korintho kwamba kila kitu kinapofanyika kwa mwamini inatakiwa kufanyika kwa utukufu wa Mungu. Kwahiyo ukiwa na kiu utafanya mambo yako yote chini ya maongozi ya Mungu na papo hapo itakuwa Mungu anatukuzwa kwa kuwa mambo au mafanikio yako yatakuwa yamejengwa kwa Mungu mwenyewe ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ


2. Inasaidia kujijengea heshima ya kibinafsi juu ya mambo yako [SELF DISCIPLINE]

๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰Kwakuwa ndani ya nafsi yako imejengeka hali ya kumuhitaji Mungu hautafanya mambo kwa pupa maana nafsi yako itakuwa iko kwenye hitaji la kumtukuza Mungu kwahiyo maamuzi yako yatakuwa sahihi yaliyokuwa balanced..

Pia inabidi ujue kuwa kwenye nafsi ndiko kuliko UTASHI, UELEWA, MAAMUZI, AKILI NA MOYO(HIFADHI/KUMBUKUMBU).  Kwahiyo ukiwa na Kiu mambo yako na maamuzi yako yatajikiti kwenye kuhakikisha unampendeza Mungu si utajizuia kwa mambo mengi.

N.B hapo kwenye NAFSI ni somo linajitegemea ambapo inahitaji pia mda wa kutosha kuelewa ila kama Mungu atatupa kibali nitaliweka pia kwenye hii website yangu.

Ndio maana Suleiman anasema kwamba ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

 Mithali 29:18
 "Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria."

Nia pia inakuonyesha jambo la kufanya ndio maana hukupa ile self discipline for anything you will be intending and interesting to do in future.

3. Kumfanya mtu awe na ushirika {FELLOWSHIP} bora na Mungu.

๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰ Maisha ya ukristo sio tu kwenda kanisani bali ni uhusiano binafsi wa mtu na Mungu wake katika mazingira na nyanja mbalimbali za maisha. Kwahiyo mtu mwenye kiu huwa inamfanya atamani sana kukaa na Mungu kwa karibu kitu kinachomjengea msingi mkuu wa ushirika wake na Mungu.

 1 Petro 2:2
 "Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;"

Unapokuwa na kiu utakuwa mtu wa kujifunza maneno ya Mungu na kujikuta unaukulia wokovu ambako huko hufanya kuimarisha ushirika na Mungu wako.

4. Kuondoa hali ya mazoea kwenye utumishi wako 

๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰Watu wengi wanafanya mambo kwa mazoea yaani bila kufwata maelekezo ya Mungu anavyotaka kwakuwa ndani ya maisha yao haiko Shauku au Kiu ya kumtaka Mungu bali wanafanya kama taratibu za kila siku.

Huduma yeyote ambayo umepewa na Mungu unahitaji unyenyekevu wa hali ya juu na sio kwakuwa unaweza au ulimuona mtu fulani anafanya basi na wewe unafanya. Embu ona hawa watu๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Matendo ya Mitume 19:13-16
 "Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa."

Hawa wapunga pepo kwakuwa kiu yao ilikuwa kujipatia faida na sio kuwa na Yesu walijikuta wanaingia pabaya na kutendewa yasiyo faa na yule pepo mchafu.

Kwahiyo ukiwa na kiu hutafanya kwa mazoea kama hawa watu walivyofanya ili wajipatie heshima mbele za watu wa mji ule. Sasa wewe kwenye utumishi wako utatenda ili Mungu atukuzwe ndani yako na kukufanya hali ya mazoea kuto kuwepo ndani yako.


5. Kuruhusu Tunda la Roho kuleta matokeo ndani yako.

๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰Mtu anapokuwa ameokoka huwa Roho mtakatifu anakuja ndani yake ila madhihirisho ya kujazwa na Nguvu au uwezo wa Roho mtakatifu hufuatia baadaye pale anapokuwa anaendelea  kuukulia wokovu japo kuna wengine pia hupata madhihirisho wakati huohuo baada ya kumuamini Yesu na kazi yake ya msalaba na umuhimu wake. (๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰Mfano wanafunzi wa Yesu walipata madhihirisho baada ya Yesu kuondoka.. Soma Matendo 2:1-4 wakati wengine ka Kornelio walipokea papo hapo pindi anaipata injili.. soma Matendo 10:44-46 ila soma sura nzima ya 10 hiyo)

Sasa Roho mtakatifu huwa analeta yale matunda ya Roho kwenye MATENDO 5:22-24  Kuwa dhahiri kwa mwa mwamini. Kwahiyo kwa mtu aliyekuwa na kiu ndani ndio huruhusu hayo mambo kufanyika kwake na hii ndio huja kuleta utofauti baina ya mwamini na mwamini mwingine.

6. UNYENYEKEVU kuwa ni sehemu ya maisha yako.

Mtu ambaye bado hajajikita kumtaka Mungu ni rahisi sana kutaka yeye aonekane kwenye jambo lolote na sio Mungu. Ila huyu mtu akiwa na kiu anakuwa na hali ya uhitaji kiasi kwamba anakuwa ana unyenyekevu na kuwekelea mbali kila namna ya kiburi ndani yake kitu ambacho humfanya apate kibali mbele za Bwana. Embu ona watu hawa๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

 Mwanzo 11:3-4
 "Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote."

Ukiwaangalia hawa watu utagundua walitamani wajipatie sifa na kuacha kufuata agizo la Mungu la kutakiwa kutawanyika juu ya uso wa nchi yote kama alivyosema๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

 Mwanzo 1:28
 "Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi."

Hapo unaona kiburi kiliinuka lakini kama wangekuwa wanamtaka Mungu basi wangefuata maelekezo yake ambayo ingeleta unyenyekevu ndani yao.

Pia siku zote mtu anayemtaka Mungu lazima awe na unyenyekevu ndani yake maana Kwake maelekezo ya Mungu kwake ni Lulu na uhai maana sisi katika kristo huwa๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Matendo ya Mitume 17:28
"Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake."

Mungu akubariki kwa kusoma sehemu hii ya pili. Unaweza kuwashirikisha na wengine pia

Ulikuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Phone; +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

KIU YA KUMTAFUTA MUNGU (Sehemu ya kwanza)


Bro Jackobo


Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu? Karibu tujifunze kwa pamoja hili somo ambalo Mungu amenipa

Utakuwa nami mtumishi katika Bwana wetu Yesu kristo
Name: Bro Jackobo
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441


KIU hii ni hali ya ndani anayokuwa nayo mtu ili aweze kupata au kufanikisha jambo fulani alilokuwa na uhitaji nalo.

Kiu ya kumtafuta Mungu hiii ni hali ya ndani inayojengeka kwenye Nafsi ya mwamini kuhitaji ushirika na Mungu katika nyanja zote za maisha yake yani kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiroho.

Zaburi 42:1-2
"Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? "

Daudi anajaribu kuonyesha uhitaji wake wa ndani kwenye nafsi yake namna ambavyo anatamani kuwa na ushirika na Mungu, anaonyesha kuwa na njaa kwenye nafsi yake ili aweze kufanya maamuzi sahihi ya kuweza kuamua vyema kwenye maisha yake ya kila siku. Daudi alihisi kama vile Mungu yuko mbali na yeye kwahiyo alitamani sana awe karibu na Mungu kwenye ushirika.

Daudi alipopita nyakati za Giza aliona kama machozi yake yamekuwa ndio chakula chake (Utoshelevu wake) lakini yeye akaona Utoshelevu zaidi ni kuwa na Ushirika na Mungu ndio maana akawa anahitaji nafsi yake ishikamane na Mungu.

NB: Mwanadamu kaumbwa na vitu vikuu vitatu yaani Mwili, Roho na Nafsi, Ambapo nafsi ndio kama daraja lililopo kati ya mwili na Roho lenye kubeba maamuzi ndani ya mtu.

Mungu alipomuumba mwanadamu alimfanya awe chombo cha mahusiano (Relational being) na ndio maana kila wakati aliwatembelea kipindi cha jioni katika ile bustani ya Edeni.

Mwanzo 3:8
"Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone."

Kwahiyo Mungu anatamani kuona ushirika mzuri baina ya mwanadamu na yeye wakati wote na ndio maana baada ya uhusiano na mwanadamu kuharibika pale bustani ya edeni alimleta Bwana Yesu ili afanye uimara wa ushirika huu.

Mwamini anayo kila sababu ya yeye kujenga uhitaji mkuu wa ndani mwenyewe kutaka kukaa na Mungu kwa karibu kimazungumzo zaidi.

MAMBO YANAYO DHOHOFISHA KIU YA KUMTAFUTA MUNGU.

1. Dhambi/Uovu
Mtu afanyapo maovu au Dhambi Upendo ndani yake huwa unashuka kiasi kwamba anashindwa kuona uzuri wa Mungu kwenye maisha yake na kumfanya asiwe na uhitaji wa kuwa na ushirika naye. Hii ndiyo maana yesu alisema maneno yafuatayo ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Mathayo 24:12
"Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa."

Pia Dhambi ina tabia ya kumfukuzisha mtu kuwa karibu na Mungu, kwahiyo huyu mtu anakuwa na haja ya kutoka na kukaa mbali na Mungu. Mfano Adamu na Eva baada ya kula Tunda waliamua kwenda kujificha maana ile Dhambi yao iliwaondolea ujasiri wa kukaa kwenye utukufu wa Mungu kiasi kwamba hawakuweza kustahimili kusikia sauti yake.

Mwanzo 3:10
"Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha."

Pia uovu wa mwanadamu una tabia ya kumfanya yeye akae mbali na Mungu maana huleta faraka baina ya huyu mwamini na Mungu wake.๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Isaya 59:2
"lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia."

Kwahiyo kama utaruhusu dhambi na Maovu kuwa sehemu ya maisha yako yatakuwa yanakufanya wewe usimpende Mungu, pia kukufanya uwe na faraka na Mungu na pia kumruhusu Shetani akupige upofu katika macho ya moyo wako hali ambayo huleta ugumu wa wewe kuwa na shauku ya kuwa na ushirika na Mungu.


2. Roho ya Mazoea
hii ni hali ambayo huwapata watu waliokuwa na ushirika mzuri na Mungu pale wanapoacha kuisikiliza sauti ya Mungu na kuishi kwa namna wanataka bila ushirika wa mzee wa siku mwenyewe.

Mungu anataka kila jambo tulifanyalo tulifanye kwa utukufu wake na chini ya maongozi yake.

Waamuzi 16:20
"Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa Bwana amemwacha."

Samsoni alijizoeza kwamba yeye ni mwenye nguvu wakati wote hakujua kwamba ili yeye awe na nguvu lazima patano la agano liwepo yaani vishungi saba vya nywele na ndio maana baada ya kuviondoa aliishiwa Nguvu.

N.B Lazima ukae na kujua kila Agano linalofanyika huwa linakuwa na vigezo na masharti pindi vigezo na masharti yanapopuuzwa basi uhalali wa agano huwa unaondoka kabisa kwenye maisha ya mtu.

Hali ya mazoea huwa inafanya mtu asiwe na haja ya kuhitaji kuwa na maelekezo kutoka kwa Mungu kitu ambacho hupelekea yeye huyo mtu asiwe na shauku ya kuwa na ushirika na Mungu wake kwakuwa anakuwa ana hali ya kujiona yeye ana utoshelevu wake mwenyewe.

3. Roho ya Kiburi

Kiburi ni hamu isiyoratibiwa ya kujipatia ukuu dhidi ya wengine pengine hata dhidi ya Mungu.

Au

Kiburi ni hisia na fikra zilizopotoka kuhusu ukweli na uhalisia wa mambo namna yanapaswa kuwa .

Mwanadamu ukifika hatua anatamani kujitengenezea nafasi kubwa mbele za watu humfanya yeye asiwe mtu wa kujishusha. Embu tuangalie hiki kisa๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Mwanzo 11:3-4
"Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote."

Sasa ukisoma hicho kisa utaona namna ambavyo watu walipotaka wao wajitengenezee jina na sifa nyingi na sio kumpa Mungu utukufu.
Hao watu wa kwanza baada ya ile gharika walikuwa na lugha na usemi mmoja kiasi kwamba wakakubaliana kufanya jambo kwa ajili ya wao wajipatie utukufu.

Watu hawa waliutamani ukubwa kiasi kwamba wakaacha mpango wa Mungu aliokuwa amewaagiza kuijaza nchi wao wakataka kukaa sehemu moja kwa matakwa yao binafsi. Ona hapa๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Mwanzo 1:27-28
"Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi."

Ukisoma hapo Mungu alipokuwa amekwisha kuwaumba adamu na Eva basi lengo lake ilikuwa ni kuwa waijaza dunia yote lakini Kiburi cha hawa watu kikawafanya watu hawa wapingane na mpango wa Mungu.

Kwahiyo kiburi kitakufanya ukatae mpango na utaratibu ambao Mungu amekuwekea uufatwe kitu ambacho kitakufanya usitake ushirika kuwa na Mungu.

Sasa tumeona namna ambavyo baadhi ya vitu hudhohofisha watu kuwa na ushirika na Mungu basi ngoja tuone namna gani tunafanya ili tuweze kuwa na kiu ya ushirika pamoja na Mungu.

MAMBO YA MSINGI ILI MTU AWE NA KIU YA KUMTAFUTA MUNGU

1. Kuacha kuishi maisha Ya Dhambi
hili ndilo jambo la kwanza kwa mwamini ambapo yeye kama yeye hawezi kuacha dhambi ila kuacha kwake dhambi ni kupitia kumuamini Kristo Yesu ndiye atampa uwezo wa kuishinda dhambi.๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Mathayo 11:28-30
" Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi."

Kwahiyo kwa Yesu huwa hatuendi angali tumekuwa watakatifu bali yeye hutuondoa mizigo ya Dhambi zetu na ndio maana hata kama mtu kakosea hatakiwi kumkimbia Mungu bali amuendee ili yeye amtue zile shehena za Dhambi.

Pia kama mtu atakosea lazima akumbuke kutubu mbele za Mungu kwa kosa lolote ambalo kalifanya maana Mungu wetu ni mwaminifu huwa anasamehe๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Ufunuo wa Yohana 2:5
"Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu."

Kwahiyo kupitia kuacha dhambi kutasaidia wewe kumuhitaji sana Mungu pia upendo wako kwa Mungu utaimarika sana maana Dhambi hudhohofisha upendo (hii tumekwisha kuiona mapema).

2. Kuacha kuishi kwa mazoea
Hii itakufanya uwe mnyenyekevu sana mbele za Mungu na kujikuta wakati wote unamsikiliza Mungu na nafsi yako inajengeka katika ibada ya kuhitaji ushirika na yeye

Wafilipi 2:5-8
" Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; "

Lazima ujifunze kuwa na hali ya unyenyekevu kama Kristo Yesu namna alivyo kuwa mnnyenyekevu ndipo utaweza kuimarika ndani na kujikuta hali yako ya ndani inahitaji kuwasiliana na Mungu wakati wote.

Hali ya unyenyekevu ilimfanya Yesu kuwa mtu wa kumfanyia Mungu Baba Ibada na hii ikiwepo kwetu tutajikuta ni watu tunaopondeka na kuwa watu tutakao kumfanyia Mungu Ibada.

3. Kuwa na Roho Mtakatifu pamoja na kujazwa
Roho mtakatifu ni nguvu yaani uwezesho wa mwamini katika kutenda kazi ya Mungu. Sasa mtu anakuwa na Huyu Roho mtakatifu anakuwa anatiwamoyo wa kuendelea kumtafuta Mungu na kujikuta ile hamu ya kuwa na Mungu inakuwa kubwa.

Matendo Ya Mitume 1:8
"Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi."

4. Kuwa na Neno la Mungu ndani yako
Neno la Mungu huwa linatuonyesha namna maisha yetu yalivyo mbele za Mungu kiasi kwamba unaweza kujitambua wewe uko vipi mahusiano yako na Mungu pia linakuonyesha kinachokupasa kukifanya kwa wakati.๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡


Zaburi 119:105
"Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu."

Hii ndio maana Paulo pia alisema kwamba neno lake Kristo Likae kwa wingi katika mioyo yenu

Wakolosai 3:16  
"Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu."

Pale neno la Mungu linapokuwa limeujaza moyo wako basi huwa linakufanya ujitambue wewe ni nani na jambo gani unatakiwa kuwa nalo. Kwahiyo linakuongoza unakotakiwa kwenda.

Hii itakufanya wewe ujitambue wewe ni kiumbe umeumbwa kuwa kiumbe cha mahusiano (Relational being)  na Mungu ko utajikuta kila wakati unatamani kushirikiana na Mungu wako.

5. Kuwa mtu wa maombi
Maombi ni mawasiliano baina ya pande mbili yani Mungu na mwamini yaliyojengeka katika mfumo wa mahusiano na sio swala la kupeleka tu shida zako mbele za Mungu.

Watu wengi hawapati matokeo ya kile wanachokiomba kwakuwa wameyafanya maombi ni sehemu ya kupeleka tu shida zao mbele za Mungu pasina kujua kwamba kuwa ni sehemu ya kimahusiano na Mungu wako. Hii ndio maana uliambiwa hivi๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

1Wathesalonike 5:17
"ombeni bila kukoma"

Ingekuwa suala kuomba ni wakati wa shida basi isingekuwa kuomba bila kukoma. (Kama Mungu atatupa neema nitaandaa somi juu ya Maombi kiundani zaidi).

Sasa unapokuwa kwenye maombi huwa watu wanatiwa Moyo pia wanapokea nguvu ya uwezesho kuendelea kukaa kwenye ushirika na Mungu kitu ambacho hukusaidia wewe kuwa na hamu na furaha ya kuendelea kuwa na ushirika na Mungu.

Mungu akubariki kwa kufuatana nami kwenye somi hili unaweza ukawa shirikisha na wengine pia๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™


Unaweza kusoma sehemu ya pili ๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰๐Ÿ‘‰SEHEMU YA PILI hii nimei update baada ya wengi kuhitaji kujua umuhimu wake

Ulikuwa nami mtumishi katika Bwana wetu Yesu kristo 
Name: Bro Jackobo
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441

KIPI KITUMIKE KATIKA KUOA AU KUOLEWA??? LOVE♥️♥️


Bro Jackobo


Bwana Yesu asifiwe mtu wa Mungu???
Nilikutana na hili swali na mimi nikawa na jibu lake... Karibu tulione

Swali: Je inakaaje hapa maana tunasikia kwamba๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

"Mwanaume unatakiwa kuoa mwanamke anayekupenda sana kuliko wewe unavyompenda au Mwanamke unatakiwa kuelewa na Mwanaume anayekupenda sana kuliko wewe unavyompenda"

Utakuwa nami mchambuzi wako
Name: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

anajibu๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡...

Tunashukuru Mungu kwakuwa tunapata changamoto na mawazo mbalimbali yanayotupa akili na ufahamu wa kutafuta kujua kweli.๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™


Tatizo sio hiyo statement ila hiyo statement iko na a lot of pains behind...

Niliwahi kusikia wakisema "There is unspoken truth within the song that someone loves the most"
sasa๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

People have faced with a lot of "Psychological tortures and disappointments" following true love they had before, sasa baada ya kuumia wameshikwa na kitu kinaitwa๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡ "Post Traumatic stress Disorder {PTSD}" sasa hii inawagharimu maana wanahisi wakiwa na mtu wanampenda sana wanaweza kuumizwa tena mara ya Pili. Sasa ego zao ndio zinawafanya wawe na little faith kwamba watampata mtu ambaye ni mwaminifu siku zote ili kuepuka kuumia mara ya pili๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ.

So watu wanakuwa na Denial kwenye kuwa na mtu anayempenda maana kiuhalisia hakuna ambaye hataki kuoa au kuole na mtu ampendaye sana. Kuna mengi ya kusema but acha niishie hapo hope utakuwa umenipata kidogo......

labda kimsingi inatakiwa iwe namna gani kimsingi??๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

What will make people bounded together firmly is True love only kwahiyo lazima umpende mtu unayetaka kumuoa au kuolewa naye.

Mwingine atasema mwanamke anaheshimu ila Mwanaume anapenda๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ sawa sikukatalii ngoja nikuonyeshe kitu hapa ndugu yangu๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Waefeso 5:24-25 (KJV)
"Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;"

Msingi wa Ndoa ni Yesu Kristo na kanisa. Mwanaume akitaka kuoa lazima ajipime kwa kigezo cha Kristo Yesu katika kumpenda mtu huyo anataka kumuoa ukiona huwezi kuwa kama Yesu alivyo na anavyolipenda kanisa basi wewe hutakiwi kumuoa huyo mtu maana kuna wakati mambo yanaweza yakaenda kombo na itatakiwa hivi๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

๐Ÿ‘‰Ujitoe sadaka kwa ajili yake na uwe radhi hata kufa kwa ajili ya mkeo_
๐Ÿ‘‰uwe tayari kumsamehe katika kila kosa atakalokufanyia ndio maana biblia inazungumza masuala ya kutokuwa na uchungu na wake zenu_
๐Ÿ‘‰Kuwa tayari kudharilishwa kwa ajili ya huyo mke wako au mtu wako ili apate heshima mf Soma Hosea kwa Gomeri ilikuwaje {kitabu cha Hosea} pia Yesu mwenyewe kwa ajili yetu sisi. N.k

Hapo nimekuonyesha nafasi kidogo ya namna mwanaume anatakiwa kumpenda mkewe. Sasa ukiona kwa namna hiyo huwezi kumpenda mkeo au mtu huyo uko naye kwa mpango wa ndoa basi wewe hauko tayari kwenda na huyo..........

Sasa twende kwa upande wa mwanamke๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Tumekwisha kuona msingi wa Ndoa ni Yesu Kristo na Kanisa๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ

Yaani YESU=Mume na KANISA=MKE. Ukitaka kuelewa kwanini wanasema mwanamke amtii mume basi jifunze kwa kanisa๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Yohana 15:16 (KJV)
"Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni."

Ukisoma hapo ni kwamba Yesu ndiye anachagua halafu kanisa linatii wito ndipo imekuja hii concept bro๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ kwamba Mwanaume atamchagua mwanamke anayemtaka kwa maongozi ya Mungu mwenyewe then mwanamke atapima na kumkubali au kumkataa sasa ikiwa amemkubali inabidi afuate yale maagizo ya mumewe yaani atii๐Ÿ™Œ sijui umenipata concept ilipokuja kuanzia eehh๐Ÿค”๐Ÿค”๐Ÿค”

sasa kwanini nimesema lazima kuwe na True love between them from both side yani Kijana wa kiume na Binti๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Ona hapo mtumishi
Yohana 14:15-16 (KJV)
"Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;"

Yesu anawaambia wanafunzi/Kanisa wakimpenda watashika amri zake ni sawa niseme hivi..๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

"Mke akimpenda mume atamtii yaani atashika sheria za mumewe"

Sasa kinachoweza kumfanya Mke aweze kumtii mumewe ni Yeye kumpenda mumewe bila kumpenda hawezi kumtii yaani mimi kanisa nisipompenda Yesu piga ua galagaza siwezi shika sheria zake.

Kwahiyo mke sio kwamba alipoambiwa amtii mumewe basi hatakiwi kupenda ila nikujaribu kuonyesha msisitizo wa kiuongozi ndani ya Familia na mgawanyiko wa kimajukumu ili kwamba kusije tokea migogoro isiyo ya lazima๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ

Kama ni binti lazima uwe na mtu ambaye unampenda.

Hilo wazo la kwamba "Umuoe mtu anayekupenda sana au uolewe na anayekupenda sana" litaleta shida kubwa katika ndoa kikubwa lazima kuwepo kwa upendo baina ya watu hao ndipo wataweza kuwa pamoja na Roho wa Mungu atawafunika katika kila kitu wakifanyacho. Huwa ninasema hivi siku zote๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

"Love is life, out of Love there is no life"

So without Love no marriage that will exist.

So Mwanamke hajawa excluded kupenda.

Moja ya dhara kubwa ya kuishi ma mtu usiyempenda ni kwamba๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

"Ukiwa na mtu usiyempenda huwezi kuwa committed kwake na kuna uwezekano mkubwa mkaachana maana bado haujampenda huyo mtu vizuri."

Yaani kuna watu wanafikiri kwamba zile sifa za upendo kwenye wakorintho๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

1 Wakorintho 13:4-8(KJV)
"Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika."

Hufikiri kwamba hizi sifa hazitumiki katika ndoa kitu ambacho ni wazo potofu. Sasa huu upendo unatumika katika ndoa bila hivyo hamtaweza kudumu pamoja.

LET LOVE LEAD❤️❤️

Ulikuwa na mchambuzi wako
Name: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

KWENDA MPAKA MWISHO PAMOJA NA MUNGU {SEHEMU YA TATU_FINAL)


Bro Jackobo


Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu?? Karibu tumalizie sehemu ya tatu na ya mwisho ya somo Letu.

Utakuwa nami mpendwa katika Kristo Yesu
Jina: Bro Jackobo
Phone: j255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

Baada Ya kuona sehemu ya kwanza juu ya maana ya kwenda mpaka mwisho pamoja na Mungu na kuangalia kwanini watumishi wengi wamekuwa wakianza vema lakini wakiishia njiani.

Sasa tutaenda kuangalia mambo yanayoweza kufanyika kumsaidia huyu mwaminini kuweza kufika mwisho pamoja na Mungu. 

Kama haujaona sehemu ya kwanza unaweza bonyeza hapa➡️SEHEMU YA KWANZA. Pia unaweza angalia sehemeya pili hapa➡️SEHEMU YA PILI

 MAMBO YA KUFANYA ILI KUMUWEZESHA MTU KUWEZA KUFIKA MPAKA MWISHO PAMOJA NA MUNGU.

 1⃣. KUMJUA MUNGU
Mwamini anapaswa kumjua Mungu kwa kila nyanja ya maisha mfano kiuchumi, kijamiii n.k ili apate kujua ule utendaji wa ki-Mungu namna ulivyo kwa kila sehemu ambayo atakuwa yupo. 

Kiukweli kufika hatua ukasema unamjua Mungu ni ngumu maana hauwezi kumchunguza Mungu lakini inatakiwa ujibidishe umuelewe MUNGU na ndio maana Ayubu anazungumza kwamba inakupasa umjue Mungu ili uwe nayo Amani.

 AYUBU 22:21
 "Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia."

Kwahiyo kupitia kumjua Mungu itakuepusha na WOKOVU WA KIFAFA (yaani maisha ya kuanguka na kusimama) kwahiyo utakuwa ni mtu ambaye hauwezi kutikiswa na jambo lolote kwenye maisha yako ya kila siku kwahiyo utaweza kutembea na Mungu kwenye nyakati zote ambazo ziko kwenye maisha yako ya kila siku hata kama zinakupa huzuni.

 Sasa ni kwa namna gani mtu anaweza akamjua Mungu??

 a)  Kuwa watu wa Kumfanyia Mungu Ibada
Unapozungumzia swala la ibada unaweza ukachukulia ni kitu cha kawaida lakini ili tuseme kwanza kunayo ibada lazima kuwe na vitu vikuu vitatu MTOA IBADA (mwanadamu), MTOLEWA IBADA (MUNGU) pamoja na MADHABAHU (Sehemu ya kumfanyia Mungu ibada ambayo huwa inaambatana pamoja na utoaji wa Sadaka na Dhabihu mbalimbali) unaweza ukasoma habari za ELIYA katika kitabu cha 1WAFALME 18 sura yote utaelewa.

Kwahiyo kutoa kwetu ibada kutatufanya tuachane na maisha ya kuanguka na kusimama kila siku bali yatatupa kukaa na Mungu mda wote ambao tutakuwa tu wazima.

 WAEBRANIA 10:25
"wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia."

Kwahiyo kukusanyika kwetu katika ibada kila siku kutatusaidia sana kuweza kuelekezana mambo mbalimbali juu ya kweli ya Mungu na namna ya kuweza kuishi maisha ya utaua/ utakatifu. Kuna baadhi ya watu ambao huamini kwamba hata wasipokusanyika kwenye nyumba za ibada wako salama lakini kiuhalisia hawako salama hiyo ni kanuni ya kiMungu ambayo kaiweka mwenyewe sasa kwanini uachane na utaratibu wake??

Mungu atusaidie sana tuwe watu wa ibada. Lazima utafute  kuwa na Ibada za pamoja lakini kama ukikosa pia kuwa na Ibada za binafsi ujue bado kuna vitu utavikosa sana kwenye maisha yako. Mungu akufungue sana kama unafanya ibada za pamoja tu na haufanyi ibada ya kwako binafsi uelewe umuhimu wake.

 b) Kuwa watu wa Maombi

Maombi ni mawasiliano baina ya muhitaji na mtoa majawabu ya mahitaji. Kwahiyo Maombi ni mawasiliano kati ya mwanadamu (ambao hawa ndio wahitaji) pamoja na Mungu( mtoa majibu ambaye huyu huwa anajitosheleza).

Kwahiyo lazima tuwe waombaji ili tuwe karibu na Mungu na itatusaidia kwa kiwango kikubwa kutokata tamaa na safari yetu ya wokovu tuliyo nayo

 LUKA 10:22
 "Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni."

YESU alipokuwa anawaambia wasijewakiingia majaribuni sio kwamba alimaanisha wasingekutana na majaribu ila ni kwamba hawatayatii yale majaribu ya shetani kwenye maisha yao yani wakaenda kwa namna majaribu yanataka wawe.

 1 WAKORINTHO 5:17.
 "ombeni bila kukoma".

Kwahiyo inatupasa siku zote tuwe watu wa kutaka kuwa na Maombi na kumtafuta Mungu ndipo tutapata usalama lasivyo tunajipotezea nafasi mbele za Mungu

2⃣.KUONGEZA SHAUKU YA KIU YA HAKI
Shauku ni nia ya ndani ya kufanya jambo fulani kwa viwango vikubwa.
Endapo mwamini ataluwa anahitaji kwa kiwango kikubwa kuwa na haki mbele za Mungu itamfanya Mungu amjibu matamanio yake ambayo yuko nayo.. ona hapa ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

 Mathayo 5:6 
 "Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa."

Ukiangalia hapo Yesu alikuwa akizungumza na wanafunzi wake kwamba yeye ambaye akiwa na njaa na kiu ya haki yeye atashibishwa na Bwana, kwahiyo endapo kama ukiwa na shauku ya haki itakufanya ukawa unaishi maisha ya kumpendeza Mungu wakati mwingi maana wakati wote utakuwa ukitaka kumfanyia Mungu yale yanayompendeza na kujikuta unaishi maishi ya kuwa karibu na Mungu. Hii itakupa uwezo wa mda wote kuwa karibu na Mungu.

3⃣. KUENENDA KATIKA ROHO MTAKATIFU

Hii ni hali ya mwamini kuweza kuenda au kuishi kulingana na maelekezo ya Roho mtakatifu.
Maelekezo ya Roho mtakatifu huwa yanamfanya mwamini kuishi maisha ambayo yanamtukuza Mungu๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

 Wagalatia 5:16-17
 "Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka."

Ukisoma hapo utaona paulo alivyokuwa akiwaambia wagalatia ambao walikuwa wameanza kwa Roho lakini baadae wakaanza kuishi kwa namna mwili unataka na sio kama Mungu alivyokuwa anataka maana matendo maovu yalikuwa sehemu yao.
Sasa mpendwa kama ukikubali kuwa chini ya maongozi ya Roho mtakatifu utaweza kabisa kuwa na nguvu za kuishi utakatifu mpaka pale utakuwa ukiondoka Duniani.

 Kwanini sasa kama mwamini unatakiwa kuongozwa na Roho mtakatifu??
✍️ Kuongozwa na Roho mtakatifu utaweza kujulishwa mambo yale yaliyopo, yaliyopita na  yanayokuja
✍️ Roho mtakatifu tukiongozwa naye ataondoa kwetu Roho ya mazoea maana yeye ndiye atakuwa anatuongoza
✍️Roho mtakatifu ni Mungu mwenye nguvu ya uwezesho katika nafsi ya tatu ya Mungu. Kwa hiyo bila yeye hata ujitahidi vipi huwezi kufanya lolote.
✍️Roho mtakatifu atakuwa anatufundisha namna ya kuishi kwa utakatifu wote
✍️ Kukubali kuongozwa na Roho ni sehemu mojawapo ya kuonyesha itiifu wako mbele za Mungu.

4⃣. KUICHUKIA DUNIA
Hii ni hali ya kukataa kuyaishi mambo ya kidunia ambayo yanakufarakanisha na Mungu. Kwenye sehemu ya pili kuna mambo tuliyaona ukiyafanya hayo anakuwa anaupenda ulimwengu. Sasa katika kuichukia Dunia lazima uyakatae hayo mambo makuu matatu 

 A. Kukataa tamaa ya macho
Lazima kama mwamini ajue namna ya kuushinda huo ubaya utokanao na macho lasivyo utakuwa unaishi lakini kiroho umekufa lazima macho yako yatiwe Nuru ya Kristo ili uweze kumpendeza Mungu wakati wote.

 B. Kuishi nje ya tamaa ya mwili
Kama tulivyoona matendo dhahiri ya mwili yalivyo kwenye wagalatia sura ya tano. Sasa kama mwamini lazima ujue kuuweza mwili wako lasivyo utakuwa unajidanya hata kama unafanya huduma na kuhubiri kwenye maisha yako ya kila siku.๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

 1 Wathesalonike 4:3-5
 "Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu."

Paulo anaandika kwa  watu wa kanisa la Thesalonike kwamba wafanywe safi na waepukane na tamaa za mwili mfano uasherati. Pia paulo anawaambia watu wote waweza kuuweza mwili wao katika Utakatifu na heshima. Huku ndiko kutawafanya waepukana na tamaa za mwili. Hii itawafanya waishi na Mungu vizuri bila mawaa wakati wote mpaka kifo chake.

 C. Lazima kuachana kiburi cha uzima ndipo pia utaweza kuwa na usalama mpaka unaiacha Dunia

MUNGU akubariki kwa kuwa pamoja nami sehemu hizi tatu za somo letu. 

Lakini ngoja nikuongezee Swali moja niliulizwa na mtumishi wa Mungu yawezekana ukawa upo miongoni mwao ila unaogopa kuuliza.๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

SWALI
  A. Hivi Kama mtu ameshaanguka na kiukweli yuko hatua nyingi nyuma ya alivyokuwa mwanzo afanye nini?  
B. Labda hata hawezi kuomba tena, hawezi kusoma Neno tena, hawezi kumsifu Mungu na kumuabudu Mungu tena katika Roho na kweli kama mwanzo, Hawezi hata kukemea Dhambi hata ile nguvu ya injili imeisha kabisa yani kiufupi amekata tamaa, Moyo wa toba umeisha afanyeje???. 

 JIBU๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Ohhh ikiwa imemkuta nampa pole lakini bado tunalo tumaini katika kristo Yesu.....

Huyu mtu kwanza tatizo lake kuu liko katika "Ufahamu wa Pendo la kristo Yesu kwake" maana kama akielewa Upendo wa Kristo Yesu hawezi kufikia viwango vya kukata tamaa kiasi hicho. 

Japo wengi wao ambao wanakumbwa na hali hiii wanakuwa walikuwa wamemshuhudia Mungu kwa viwango vikubwa kwenye maisha yao na baada hapo wanakuja kuanguka sasa hatia ya dhambi inakuwa inawatesa ndio maana wanafika hatua wanapoteza kila kitu yaani Shauku, nguvu ya kuomba na kila kitu.

 Sasa haya ni baadhi ya mambo ambayo anatakiwa kuyafanya huyu mtu wa namna hiii๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡ 

 1. Jambo la kwanza kabisa auelewe Upendo wa Mungu 
Upendo wa Mungu unajidhihirisha kwa namna tofautitofauti kwa mwamini yeyote. Sasa inabidi huyu mtu apate uelewa juu ya namna ambavyo Mungu  anampenda ili kuweza kumpa mtu uwezo wa kusonga mbele .
Watu wengi wanapotea kabisa kwasababu ya mafundisho๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
 Hosea 4:6a
 "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;"
Hapo unaona mtu akikosa uelewa tu ni rahis sana akafungwa ufahamu na adui kiasi kwamba akajikuta hawezi kusonga mbele zaidi hata hatua moja.

 Kwenye pendo la Mungu akielewa haya yanaweza kumsaidia๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

 ➡️ Mungu ametupenda sisi tukiwa na dhambi na sio kwa matendo yetu mema.
 
Yohana 3:16 
 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Mungu kitendo cha kumtuma mwanawe haikuwa kwasababu tulikuwa watakatifu bali wenye dhambi ili tupate uzima sasa ukifika hatua ukajua ulipendwa angali una dhambi basi hutakwama kuendelea mbele zaidi hata kidogo.

 Warumi 3:23-24
"kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;"
Hili fungu nililielezea. Ukishajua ya kwamba watu wanakosea ila kupitia kristo yesu tunahesabiwa haki ko kazi yake sio kujikinai mwenyewe bali ajishushe kwa Yesu pekee.

 ➡️ Mungu anasamehe dhambi zote na alikuja kwa ajili ya hilo

Isaya 1:18
 "Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu"

Hapo anaonyesha ukifanya dhambi ya namna gani bado Mungu anaweza akakusamehe haijarishi umefanya kosa gani.

1 Petro 2:24
 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.

Pia hapo juu unaona kwamba yeye ndiye aliyechukua dhambi zetu so ukiwa umekosea lazima uende kwake tu na ndio maana alisema kwamba๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

 Mathayo 11:28 
 "Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha".

Ukisoma hapo Mungu anataka watu wamuendee na mizigo yani dhambi zao yeye ndiye atawapumnzisha na sio waache dhambi zao ndio wamfuate bali ukiwa na makosa umuendee yeye akupe haki.

Sasa kuna namna nyingi upendo wa Mungu unajidhihirisha kwa mtu ambako huko kuna mfanya mtu akikosea aweze kurudi kwake na kusamehewa.

Kwanini nimeelezea hiki kipengele๐Ÿค”๐Ÿค” ni kwasababu watu wanafundishwa mafundisho yanayowafanya wajihisi kuwa na hatia wakati wote na sio upendo wa Mungu kwa kanisa kinachowafanya wengi sasa wakikosea kukumbana na hizi hali๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

✍️✍️Asione haja ya kwenda kwa ibada maana akienda anakuwa anahisi hatia tu ndani
✍️✍️ Anakosa ujasiri wa kuomba. Japo ukifanya dhambi usipoitu ia lazima ikutee hii hali
✍️✍️ Hawezi tena kusema Habari za Mungu kwa ujasiri.
N.k

Na hii ndio sababu nimekuelekeza kwamba lazima apate uelewa vizuri wa upendo wa Mungu kwenye maisha yake. Ndio hatua yake ya kwanza kuweza kutoka maana bila hapo atakuwa mtumwa tu kwenye fikira zake.

 Note: kuelewa kwamba Mungu anakupenda usije ukatenda dhambi kwasababu atakusamehe hata utakapokosea 

2. UKISHAJUA UPENDO WA MUNGU HAYA MAMBO YANAWEZA KUKUSAIDIA SASA KUTOKA HAPO
 A. Kuweka peupe kosa lililokufanya ukaanguka
Hapa inatakiwa mtu huyu amuelekeze kiongozi wake wa kiroho juu ya jambo hili alilolifanya lengo ni kulifanya lisiwe na nguvu ya hatia ndani yake.
Kufanya hivyo unakuwa unaiaibisha dhambi hiyo kwenye maisha yako na hapo sio kwamba unakuwa unaenda kutubu kwa mchungaji wako bali unakuwa unauaibisha ubaya ulioufanya hii itakupa ujasiri wa kuendelea kumtafuta Mungu. Lazima ulikiri kosa lako peupe.

B. Kuwa na watu watakaokufanya uendelee mbele zaidi
Lazima utafute mtu/watu ambaye anaweza kushirikiana naye katika maswala ya kiroho ili pale unakosa nguvu akutie joto la kuendelea mbele๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

 Mhubiri 4:9-11
"Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao. Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua! Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto?"

C. Tafuta kwanza kuwa kwenye maombi ya ushirika sana kuliko wewe mwenyewe binafsi

D. Kumtaka bwana na Nguvu zake

yaani kuongeza shauku ya kuwa na nguvu za Roho mtakatifu maaana shauku ya kuabudu ni suala ambalo linakuja kulingana na ufahamu na hiyo nguvu ya Roho mtakatifu ndiyo itampa bubujiko na shauku kuu ndani ya ibada๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ

E. Lazima abadilishe vitu anavyoviangalia mara kwa mara ndipo ataweza kutoka huko.

Mfano mwingine unakuta mda wote anasikiliza nyimbo za bongo fleva, picha za ngono, na kufanya mambo mengi yafananayo na hayo huku anataka shauku ya ibada iongezeke kiasi kwamba anakuwa anajidanganya tu.

Hiyo inaweza kumsaidia huyo mtu kama atakuwa yuko tayari kutoka hapo alipo. Hatua ya kwanza siku zote ni kujua kwamba hauko sehemu sahihi na ukishajua ndipo unaweza kupiga hatua nyingine mbele. Zaidi itakayokufanya ufanye maamuzi sahihi.

Yuko kwenye wakati mzuri wa kuweza kutoka huko maana ameshatambua ya kwamba huko aliko sio salama na ndio maaana anataka aweze kutoka huko.

Mungu akubariki mtumishi kwa kuwa namimi tangu tumeanza mpaka hapa tulipofikia. Kulikuwa na mambo mengi ya kuweza kujadiliana lakini kwa sababu ya Muda nafikiri tuishie hapa. Ukiwa na swali maoni unaweza kuyaweka chini au kwa njia za mawasiliano hizo hapo.

Ulikuwa nami mtumishi katika kristo Yesu 
Name: Bro Jackobo
Phone; +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

KUJIKANA NDANI YA KRISTO YESU (sehemu ya tatu- Final)

Bro Jackobo Utakuwa nami mpendwa katika kristo yesu Name: Bro Jackobo Phone: +255766944441 Email; jackobombwaga@gmail.com Bwana Yesu asifiwe...