JE MUNGU ANAWEZA KUMUACHA MTOTO/MWANA WAKE??


Bro Jackobo

Utakuwa nami mtumishi katika kristo Yesu
Name:Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu?? Karibu tujifunze kwa pamoja kidogo kuhusu hili swali...

Tutaliangalia somo hili katika mtiririko huu ili kuturahishia kuelewa
✍️Utangulizi: Mtoto/mwana wa Mungu ni yupi?
✍️Mungu anasema nini kuhusu kumuacha Mtoto wake katika agano la kale na agano jipya?
✍️Nini hitimisho juu ya swali hili
✍️ Nini matokeo endapo mtu atamuacha Mungu
✍️ Hitimisho juu ya mtu baada ya kumuacha Mungu inakuwaje sasa kuhusu ushirika wake na Mungu
✍️Hitimisho la mwisho kamili la swali {Jibu kamili la swali}

Kumekuwa na mjadala mkubwa sana kwamba je Mungu anaweza kumuacha mtu/mwana/mtoto wake??...

Jibu rahisi kabisa: MUNGU hawezi kumuacha mtoto wake hata siku moja na hajawahi kufikiri hata siku moja kukaa naye mbali ila mwanadamu anaweza kumuacha Mungu.

Kupitia hilo jibu hapo tutaenda kudadavua vizuri sasa kupitia maandiko na baada ya hapo tutaona matokeo ya mwana au mtoto kumuacha Mungu.

UTANGULIZI WA SOMO

Je mwana wa Mungu ni yupi?
Mtoto au mwana ninayetaka kuzungumzia hapa ni yule mtu ambaye amekwisha kuamini na kufanyika ushirika na Mungu ambaye Mungu amekuwa Baba na yeye mwana. Sasa ili mtu ufanyike mwana wa Mungu lazima ukubali kumpa Yesu kristo maisha yako yaani uokoke.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Yohana 1:12-13
"Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu."

Unapompokea Yesu ndipo unafanyika mwana wake na kumpokea Yesu kunakuja kwa wewe kuamini na kumkiri Yesu kristo ambapo huo ukiri unatakiwa kuenenda pamoja na Matendo yako ya kila siku unapokuwa unaishi.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Warumi 10:9-10,13
"Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka."

Baada ya kuamini na kuokoka ndipo unafanyika kuwa mwana/mtoto wa Mungu na kama ukaamini ukawa bado unaishi maisha ya Dhambi wewe bado hujatambua vyema kufanywa kwako upya na hapo unakuwa sio mwana wa Mungu bali unakuwa mtu wa Mungu maana ikiwa unalitaja jina lake inakupasa uache dhambi zako zoteπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

2 Timotheo 2:19
"Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. 
Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu."
Msingi wa mwanadamu kuwa mwana wa Mungu lazima akubali kuuacha uovu wake wote yaani asiendelee kuishi katika dhambi.

1 Yohana 1:6
"Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;"

Yohana 14:21
"Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake."
Ukisoma hayo mafungu mawili yanakuonyesha wazi kwamba anayekubalika ni yule ambaye anaishi sheria za Mungu na sio kunena katika kinywa tu halafu huku anaishi tofauti na sheria ya Mungu.

Kiufupi nitaenda kueleza juu ya Mtu aliyeokoka, Mungu pamoja na kuacha.

Baada ya kuona mwana/mtoto ninayemzungumzia ni yupi basi tuende kwenye kiini cha neno/somo letu lililo katika mfumo wa swali. "Je Mungu anaweza kumuacha mtoto wake?"

KIINI CHA SOMO:

Kama nilivyokwisha kuwaambia ya kwamba Mungu hawezi kumuacha mtu yeyote tena hana hata mpango wa kumuacha mtu yule ambaye yuko kwakwe na anaishi katika kweli yake. Naomba nianze katika agano la kale namna Mungu alivyolithibitisha hili neno kwamba hawezi kukuacha hata siku moja.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Isaya 49:14-16
"Bali Sayuni alisema, YEHOVA ameniacha, Bwana amenisahau. Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe. Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima."

Hapo Mungu alikuwa akizungumza na wana wa Israel walipokuwa wanafikiri kwamba Mungu amewaacha lakini Mungu anakuja kuwajibu kwamba hawezi kuwaacha maana wako kwenye vitanga vya mkono wake kiasi kwamba anawatazama mda wote wakiwa hata kama wakiwa kwenye kipindi kigumu. Ndio maana hata Suleiman Mungu alimwambia aende katika njia ya Mungu ndipo atakuwa na yeye na kuzithibitisha zile ahadi aliahidiana na Daudi baba yake.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

2 Mambo ya Nyakati 7:17-18
"Nawe, ukienda mbele yangu kama alivyokwenda Daudi baba yako, ufanye sawasawa na yote niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu; ndipo nitakithibitisha kiti cha enzi cha ufalme wako, kama nilivyoagana na Daudi baba yako, nikisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kutawala katika Israeli."

Sio Suleiman aliambiwa peke yake pia hata Yakobo aliahidiwa kwamba Mungu atakuwa naye wakati woteπŸ‘‡πŸ‘‡
Mwanzo 28:15
"Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia."
N.B: unaweza kusoma kwa wakati wako {Yoshua1:5, Yeremia30:11, 46:28}

Tumeona namna agano la kale ambavyo Mungu aliwaahidi watumishi wake kwamba hatawaacha naomba tuone pia katika agano jipya Mungu alisemaje piaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Yohana 6:37-39
"Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe. Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka. Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho."

Kama nilivyokwisha kukueleza kwamba Mungu hana mpango wa kumuacha Mtoto wake, unaona hapo Yesu anasema mwenyewe wote ambao wamekuja kwake hatamtupa hata mmoja na ndio maana nakuambia Mungu hawezi kumuacha mtoto wake hata siku moja maana yeye anatamani tukae katika pendo lake siku zote. Na ndio maana Yesu alijitahidi kuwalinda wanafunzi wake wote ili asiwepo hata mmoja wa kupotea πŸ‘‡πŸ‘‡
Yohana 17:12
"Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie."

Hitimisho 1: Kulingana na namna tulivyoenda na kuona maandiko hayo hapo juu ni dhahiri kwamba Mungu hawezi kumuacha mwana/mtoto wake hata siku moja na huwa anachokiangalia ni kuhakikisha mtu huyu anakaa kwenye neno lake la kweli tu.

Je inakuwaje sasa ikiwa mtoto amefanya dhambi??
Dhambi ni uasi yaani kwenda kinyume na maagizo ya Mungu aliyokuamuru kuishi kwa hayo. πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
1 Yohana 3:4
"Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi."
Mungu wetu ni mwaminifu ambapo amempa mtu nafasi ya kuchagua mema au mabaya sasa yeye mwenyewe anaweza kuamua kuishi katika dhambi au kuishi kwa namna Vile Mungu anataka. Sasa ikiwa huyu mtu ambaye Mungu amesema hatamuacha akaenda kufuata tamaa na mambo ya kidunia biblia inasemaje hapo??

Yohana 14:21
"Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake."

2 Mambo ya Nyakati 7:19-20
"Lakini mkigeuka, na kuziacha sheria zangu na amri zangu nilizoweka mbele yenu, mkienda, na kuitumikia miungu mingine, na kuiabudu; ndipo nitawang’oa katika nchi yangu niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaiondosha itoke mbele zangu, nami nitaifanya kuwa mithali na tukano katikati ya watu wote."

Katika maandiko hayo anaonyesha ya kwamba yeye atakuwa pamoja na wale ambao wanaishi kwa sheria yake na hao ndio atakuwa anajidhihirisha kwao lakini ukiwa unafanya dhambi basi uwe na uhakika atakuwa mbali na wewe ila kwasababu ya wewe kutokumheshimu yeye.

MATOKEO YA DHAMBI KATIKA USHIRIKA NA MUNGU

1. Kuharibika kwa uhusiano wako na Mungu.
Isaya 59:2
"lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia."
Matokeo ya kufanya uovu yanakufanya uhusiano wako na mungu uharibike.

2. Roho wa Mungu anahuzunishwa ndani
Waefeso 4:30
"Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi."
Ukianza mistari ya nyuma utaona anawaeleza habari ya dhmbi ndio anakuja kuwaambia msije kumhudhunisha roho wa Mungu.

3. Roho mtakatifu kuondoka ndani ya mwamini
Zaburi 51:11
"Usinitenge na uso wako, 
Wala roho yako mtakatifu usiniondolee."
Daudi alipofanya dhambi na akaamua kutubu anakuja kusema Roho wa Mungu asiondolewa hiyo inatupa picha kwamba utendapo dhambi Roho mtakatifu anaondoka.

4. Kuacha Mungu kujidhihirisha kwako katika mambo mbalimbali
(Yohana14:21, 2Nyakati19-20)

Yapo matokeo Mengi ya dhambi ila nimeyaweka haya ili niweze kukamilisha somo.

Sasa ukiangalia hapo kwenye hayo maandiko na hizo tokeo za dhambi ni zahiri kwamba kwasababu ya dhambi huwa ushirika unaharibika maana kama Roho mtakatifu atakuwa anahuzunika, akaondoka kwako na akaacha kujidhirisha kwako utakuwa na usalama gani na utakuwa unahusiana na Mungu kwa namna gani?? Kwahiyo baada ya wewe kumuacha Mungu na yeye pia anakuacha uende unakotaka maana yeye amekupa maamuzi ya kuchukuaπŸ‘‡πŸ‘‡

Kumbukumbu la Torati 30:19
"Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;"
Japo anakushauri bado uchague mema ili aende na wewe.

Mwingine atasema hatuhesabiwi haki kwa matendo yetu sasa inakuwaje? Na tena tuko kwa kipindi cha Neema... Sawa nakubaliana na wewe ila naomba tuoneπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Warumi 6:1-2
"Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?"
Tito 2:11-12
"Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;"
Ili uelewe neema imefunuliwa kwako lazima uwe hauishi maisha ya dhambi ndipo ambapo utakuwa katika neema, kama wewe unaishi maisha ya dhambi bado hauko katika neema na ukiwa katika kristo Yesu lazima uache dhambi na hautakiwi kuishi huko kwenye dhambi.
Mwingine atasema kwamba sitahesabiwa haki kwa matendo yangu... Sawa nakubali lakini biblia imesema tujitahidi kuishi namna Mungu anataka ndipo atajionyesha kwetu, haki yako iko ndani ya kristo na ukiwa katika kristo lazima uyafanye ya kristo aliyokuwa anayafanyaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

1 Yohana 1:6
"Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;"
Kwahiyo ukiri, imani lazima iendane na matendo.

Pia kumbuka biblia inavyosemaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Warumi 8:9
"Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake."
Sasa ukiwa Roho wa Mungu hayupo pamoja na wewe inakuwaje? wewe unakuwa sio mwana wa Mungu bali unakuwa ni mtu wa Mungu ambapo anakuwa anakusubiri utubu ili aweze kukusamehe na aendelee kuwa pamoja na wewe.

Hitimisho2: kutokana na maandiko hapo juu ikiwa mtu amefanya dhambi basi anafungua mlango wa Mungu kumuacha maana Mungu hana ushirika na giza maana huyo mtu atakuwa hayuko na Mungu mpaka pale atakapokuwa ametubu na kuungama dhambi zake.

HITIMISHO KAMILI
Mungu hawezi kumuacha mtu hata siku moja na wakati wote atakuwa anatafuta namna ya kumfanya mtu aendelee kukaa kwenye pendo lake wakati wote ila endapo huyo mtu atachagua kutokuenda na Mungu basi yeye hamlazimishi anamuacha atoke kwenye utawala wake na milki yake.

Mpendwa katika kristo jitahidi kufanya mapenzi ya Mungu ili usije ukafarakana na Mungu na kujikuta umebaki mwenyewe.

Ulikuwa nami mpendwa katika kristo yesu
Name: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

KUJIKANA NDANI YA KRISTO


Bro Jackobo
Utakuwa nami mpendwa katika kristo yesu
Name: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email; jackobombwaga@gmail.com

Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu??

Karibu tujifunze kwa pamoja somo hili "kujikana ndani ya kristo Yesu"

Maana:
Kujikana katika kristo ni hali ya kuacha mambo yako yaliyokuwa na heshima, ufahari na kukupatia faida kwa ajili ya kufanya mapenzi ya  Mungu kristo/ Bwana wako.

Luka 9:23-24
"Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha."

Ukiangalia hapo Yesu alipokuwa akisema na wanafunzi wake alikuwa anawaandaa katika hali ya kumuishia Mungu katika mantiki ya kwamba wayahesabu mambo yao sio ya maana bali waone kwamba mambo ya Kristo Yesu ndio ya maana zaidi.

Hii ilimfanya ufike wakati sasa awaambie wajikatae/kujikana ili kwamba wamfuate Yesu na huku wamebeba mizigo/msalaba/mateso yao.

Hapa alikuwa akiwaonyesha kwamba katika kristo sio kwamba watapata kufurahi tu bali hata mateso yangewakuta.

Nani alikuwa mwanzilishi wa kujikana??
Note: Mwanzilishi mkuuu wa kujikana alikuwa ni Yesu mwenyewe kwa namna ambavyo aliacha Enzi na utukufu wake akaja kutuokoa sisi. Na aliona kwamba ile heshima na utukufu wa ki-Mungu sio kitu cha maana ila kukamilisha ule wito au kule kukubali kwake kujitoa kwa ajili ya maisha yetu hata ukafika hatua akawa yuko tayari kunyenyekea hata mauti ili aweze kutupata sisi ambao tulikuwa tumepotea.

Wafilipi 2:5-7
"Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;"

Pia Yesu aliweza kutuchagua sisi licha ya kwamba tulikuwa na dhambi ili kwamba atufanye sisi tuwe wana wa Pendo lake na sio sisi tuliomchagua yeye. Sasa huku kwa yeye kutuchagua kunaonyesha kujikana kwake mbele ya Mungu baba ambako pia ndio mfano tunatakiwa kuufuata.

Yohana 15:16
"Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni."

Katika kujitoa/kujikana kwa Yesu kristo ndiko ambako mwamini inatakiwa afuate mfano wake na sio mfano wa mwanadamu awaye yeyote. Hii ilimfanya mpaka atupe uhakika wa kuweza kufanya mambo ambayo ameyafanya na zaidi ya yale aliyokuwa ameyafanya. Ona hapa ambapo alituthibitishia ili kwamba tukiwa na hekima na maarifa ya Ki-Mungu tuweze kufuata njia yakeπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Yohana 14:12
"Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba."

MAENEO MUHIMU AMBAYO MWAMINI ANATAKIWA KUJIKANA NDANI YA KRISTO
1. Utumishi
2. Maisha ya utakatifu na utauwa.

1. UTUMISHI
hii ni hali ya kuwa na utayari wa ndani na kutekeleza majukumu/maagizo ambayo Bwana wako amekupa  ili uweze kuyatekeleza.

Wafilipi 3:7-8
"Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;"

Paulo kwa ajili ya kristo aliamua kupata hasara ili aweze kumpendeza kristo ambaye alimuita ili aweze kumtumikia yeye na huku ndiko kujikana ambapo Kristo alitamani wanafunzi wake wawe kama namna ambavyo paulo alikuwa tayari kuingia gharama. Paulo aliacha mshahara na marupurupu mbalimbali kutoka kwenye dini ya kiyahudi ili aweze kumpendeza Mungu.

Kuna wakati kama mwamini lazima ufike hatua uwe tayari kuacha yote ili uweze kuitimiza ile kazi ambayo Mungu amekupa wewe kuifanya kama vile ambavyo paulo alifanya.
Ndio maana Yesu alipokuwa anaondoka aliwaambia wanafunzi juu ya utumishi katika kuieneza injili yake na sio vinginevyo. Na alitamani wanafunzi wake wawe hivyo onaπŸ‘‡πŸ‘‡
Marko 16:15
"Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe."

Sasa wewe uliye tayari kuwa na Mungu lazima ukubari kuihubiri injili kwa mazingira yawayo yoyote ili kuonyesha utayari wako kumtumikia Mungu katika eneo ambalo amekupa uweze kutumika.

Usikubali kukaa tu ndani ya nyumba ya Mungu pasina kuwa na kazi yeyote lazima uwe tayari kuifanya ile huduma ambayo Mungu amekupa wewe.

Watu wamejikuta wanakumbana na vikwazo vingi sana vinavyowafanya washindi kujidhabihu vizuri katika eneo la utumishi. Tutaviangalia hivyo vizuizi kiufupi sana ambapo nimevuweka katika makundi makuu mawili.

VIKWAZO KWENYE UTUMISHI
A). Upinzani wa ndani ya nyumba ya Mungu/kanisa
B).  Upinzani wa nje ya nyumba ya Mungu/kanisa

A. UPINZANI WA NDANI YA NYUMBA YA MUNGU/KANISA
Hivi vizuizi vinakuwa vinatokana na mazingira ya ndani kwenye nyumba ya Mungu ambayo yanamfanya huyu mtumishi wa Mungu ashindwe kuishi ule utayari wake wa kumtumikia Mungu ambapo ndio kujikana halisi kwa mwamini.

Mathayo 16:21-23
"Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu."

Ukiangalia hapo juu utaona Yesu alikuwa akikemewa na petro kwamba hata pitia mateso lakini Yesu hakumsikiliza Petro bali aliangalia mbele ili kutimiza kusudi lake lililomleta.

Tulitegemea kwamba Petro asiwe kikwazo au kumvunja moyo Yesu kutimiza kusudi japo kwa akili ya kibinadamu ilikuwa ni ngumu sana kuelewa ule utumishi ambao ilitakiwa Yesu kuupitia. Hii ndio inatufanya hata nasi kama waamini lazima uelewe vizuri ni kwa namna gani Mungu amekuita ile uweze kumtumikia na kama usipoelewa ndio unajikuta sasa unaishia kuvunjwa moyo na watu wako wa karibu au ndani ya nyumba ya Mungu.

Unaweza ukavunjwa moyo na watumishi wa Mungu mfano Mwalimu, mchungaji, mzee n.k lakini usiache kufanya kazi ya Mungu. Wewe hakikisha unamtazama kristo tu kama kielelezo chako katika kumtumikia Yeye.

Kwa namna gani upinzani wa ndani unaweza kuwafanya waamini wakate tamaa??
1. Kuzuiliwa katika huduma na kiongozi wako wa kiroho; usiaangalie ni kwa namna gani kiongozi wako kakuambia au kukukataza kutumika kikubwa jihakikishe  uhusiano wako na Mungu halafu uendelee kumuomba Mungu ili akupe namna ya kutumika.
2. Maisha ya dhambi kwa viongozi wa kiroho wanaosimama mbele ya madhabahu; watu wengi wanaosimama mbele ya madhabahu wamekuwa wakiwavunja moyo watumishi wengine kutumika kwa kuwa na maisha mabovu sana. Japo usimfanye mwanadamu akawa ni kielelezo chako kwenye kumtumikia Mungu maana wanadamu watakukatisha tamaa lakini wewe mtazame Yesu na umfuate na sio vinginevyo.

B). UPINZANI WA NJE YA NYUMBA YA MUNGU/KANISA

Yohana 16:1-3
"Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa. Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi."

Yesu aliamua kuwaambia wanafunzi wake juu ya changamoto na upinzani watakao upata kutoka kwa watu wa dini ya kiyaudi ili kwamba wasihe vunjika moyo hata siku moja. Na aliwaambia hivyo maana alijua wapo watakao fanya kama kuwaua kabisa wakijua ya kwamba wanamtumikia Mungu lakini kiuhalisia hawako kumtumikia Mungu bali wanafanya kazi ya shetani.
Pale ambapo ukikutana na watu wanakupiga vita juu ya kumtumikia Mungu huko nje usije ukaacha kumtumikia Mungu hata siku moja wewe fanya kazi ya Mungu tu hata kama mazingira ni magumu sana.

Watu wamekuwa na urafiki usiokuwa na mipaka kiasi kwamba hawawezi tena hata kuwaambia watu wengine juu ya utumishi wao walio nao. Kwahiyo watu wako wa nje na nyumba ya Mungu lazima uishi nao kwa kwa akili sana ili usije ukapoteza lengo la kuishi.
Hakikisha maisha yako mwenyewe ni ushuhuda tosha kwa ajili ya kukurahisisha kuweza kuwahudumia wale walioko nje waujilie ule upendo wa Kristo Yesu.

2. MAISHA YA UTAKATIFU NA UTAUWA
Hili ni eneo la pili la muhimu ambalo mwamini inampasa kuishi katika namna ya kujikana kama kukubali ule wito aliotupa yesu katika "Luka9:23-24" 

Neno "utakatifu" na neno "utauwa" ni maneno ambayo yamekuwa yakitumika kama neno lenye maana moja lakini yana utofauti kidogo ila yanafika kuwa na shabaha moja.

Maana ya "Utakatifu"
Utakatifu ni "hali ya usafi wa kiroho, nafsi na kimwili". 

Asili ya neno "utakatifu"
Neno "utakatifu" linaweza kuelezewa kutoka kwa maneno mawili, neno la kiebrania na neno la kigiriki
✍️Neno "utakatifu" limetokana na neno la kiebrania "Qadash"  likiwa na maana "kujitenga au kutengwa kwa usafi"
✍️Neno  "utakatifu"  linaweza elezewa na neno la kigiriki "Hagios" likimaanisha "kutokuwa na makosa au udhaifu au uchafu"

Mungu anatamani watu wote waliokubali kumuishia waishi maisha ya utakatifu haijarishi mazingira yake yako magumu vipi hata kama pia yanamshawishi yeye kuingia katika dhambi ila kwa ajili ya Mungu anatuyaka kuwa na maisha ya utakatifu na sio kitu kingine chochote.

Mambo ya Walawi 19:2
"Nena na mkutano wote wa wana wa Israeli, uwaambie, Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wenu, ni mtakatifu." 

Mungu alimwambia Musa awakumbushe wana wa Israel kwamba inatakiwa waishi maisha ya utakatifu maana yeye ni mtakatifu ndio vivyo hivyo hata kwetu kwamba tukijikana kwa ajili ya kristo Yesu basi tutakuwa tayari kuyaishi maisha ya utakatifu siku zote maana Yesu mwenyewe ni mtakatifu na sisi inatakiwa tuwe hivyo maana Yeye katika kuishi kwake hakufanya dhambi. Ona hapo chiniπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
1 Petro 2:22
"Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake."
Kama yeye hakufanya dhambi basi nasi lazima tuufuate mfano wake ili tuwe tumejikana kikamilifu na kumfuata namna ambavyo alikuwa amesema tumuishie.

✍️✍️✍️Usije ukajiachia hata siku moja maana utakatifu huwa unatafutwa na sio suala la dakika moja bali linaitaji kujengwa kuanzia msingi wa wewe kumjua na kumuelewa Mungu.
Waebrania 12:14
"Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;"
✍️✍️✍️ Lazima ujizoeze kuuishi utakatifu siku zote hata kama unaona mazingira yanakuwa magumu kwako huko ndiko kutakufanya kujikana kikamilifu wakati wote.
✍️✍️✍️Pia lazima ufike hatua ujue ya kwamba utakatifu unahusisha mwili, nafsi pamoja na Roho. Sasa kama wewe uko tayari kwenda na Mungu lazima ujue kuishi utakatifu  katika maeneo yote hayo matatu.
1 Wathesalonike 5:23
"Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo."
✍️✍️✍️ Jifunze kuwa mtu wa kusoma neno na kulitafakari neno la Mungu, kuwa mtu wa maombi n.k ndipo utaweza kuyaishi maisha ya utakatifu. Unaweza soma vifungu hivi (Yoshua1:9, Mithali4:20)

Maana ya UTAUWA
Utauwa ni hali ya kujitoa ki-Mungu ambayo huambatana na kuongezeka kwa uchaji mbele za Mungu.

1 Timotheo 3:16
"Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, 
Akahubiriwa katika mataifa, 
Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu."

Ukisoma maandiko hapo juu unaona namna Paulo anavyomwaambia Timotheo kwamba utauwa una siri kubwa halafu anaanza kueleza namna ambavyo Yesu alijitoa na kufanya kazi ambapo inatujengea msingi mkuu katika kuelewa kwamba Utauwa unaambatana na kujitoa katika kristo Yesu.

1 Timotheo 6:5
"na majadiliano ya watu walioharibika akili zao, walioikosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida."
 
Katika kujitoa ndiko kunawafanya watu waweze kupata faida, sasa ukimuangalia Paulo anazungumza na Timotheo kwamba watu ambao hawako vizuri na Mungu wanahisi kwamba utauwa unawapa wengine faida sasa hii pia inatupa maana ya namna kuuelewa Utauwa.

Katika hayo yote Yesu pia alitamani tuweze tuongezeke katika kumcha Mungu kwa kujitoa kwetu siku zote za Maisha yetu tunapokuwa chini ya Jua hapa.

Kaa chini angalia ni kwa namna gani ambavyo umejikana kwa ajili ya kristo na uishi kwa namna gani ili uwe sahihi mbele za Mungu.

Ulikuwa nami mpendwa wako katika kristo
Name: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email; jackobombwaga@gmail.com

HATA KESHO IPO


Bro Jackobo


Utakuwa nami mpendwa katika kristo Yesu
Name: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com


Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu?? Ninakusalimu kwa jina la Yesu kristo aliye haiπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ

 "Hata kesho ipo" imekuwa ni kauli ya kawaida sana kwa waamini katika kanisa siku za leo katika utendaji wa kazi ya Mungu pamoja na kuyaishi maisha matakatifu katika ukristo... karibu tuione jinsi hii kauli "hata kesho ipo" ilivyokuwa na matokeo yake ndani ya Muamini kwa habari ya UTENDAJI WA KAZI YA MUNGU pamoja na KUYAISHI MAISHA MATAKATIFU...

Mithali 27:1
"Usijisifu kwa ajili ya kesho; 
Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja."

Biblia inajaribu kuweka wazi kwamba hautakiwi kufika hatua ukajisifia kuhusu kesho maana siku za mtu zimefungwa katika mamlaka ya Mungu na yeye ndiye anajua jambo gani litakuwepo na litatokea. Sio andiko hilo tu pia unaweza ukaona katika fungu lifuataloπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Yakobo 4:13-15
"Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka. Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi."

Usiitegemee faida ijayo hata siku moja nje ya kusudi, mpango na tumaini la Mungu maana yeye ajua yote yanayokuja. Embu tuone sasa ni kwa namna gani kanisa limeutumia huu usemi "Hata kesho ipo"

1. KUYAISHI MAISHA MATAKATIFU.

Mambo ya Walawi 11:45
"Kwa kuwa mimi ni BWANA niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu."

1 Petro 1:16
"kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu."

Ukiyasoma hayo mafungu mawili utaona mpango wa Mungu kwa mwamini ni kuyaishi maisha matakatifu siku zote na wakati wote.

Katika kanisa na kizazi cha leo sio kitu cha kushangaza mtu kumuona yuko kanisani lakini maisha anayoyaishi ni tofauti sana na neno la la Mungu kisa kwamba anajua hata kesho ipo na anaweza akatubu... 

Mbona kujipalia moto wa adhabu mwenyewe kwa kuyadharau maneno ya Mungu?? Unafikiri YESU alipokuokoa alitazamie uishi maisha ya dhambi?? Kwanini unaingia kwa nyumba ya Mungu na Bado mambo unayoyafanya yanafanana na watu wa mataifa??

Watu mmefika kuitumia neema ya Mungu vibaya sana aise.. ni kweli kabisa Mungu anasamehe lakini kwanini uruhusu kufanya dhambi kwa sababu utatubu?? Kumbuka paulo alivyosemaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Warumi 6:15
"Ni nini basi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali chini ya neema? Hasha!"
Paulo alifika wakati akaona kanisa la Rumi linaitumia vibaya neema ya Mungu kwa kuendelea kuishi katika dhambi kwasababu wanajua kuna nafasi ya kutubu. Ndivyo ilivyo kanisa la leo mana limekuwa linaitumia kauli "Hata kesho ipo" kuishi namna watakavyo maana watatubu eti..

Hasira ya Bwana iko juu yako wewe ambaye unafanya dhambi kwa makusudi ukisema utatubu, hivi wewe ushawahi kuelewa hili fungu???πŸ‘‡πŸ‘‡

Mathayo 5:13
"Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu."
Hili andiko hapa juu linatuambia kwamba mwamini ni chumvi na ikiwa ameharibika hafai tena. Sasa ukikaa chini ukajiuliza vizuri utaelewa. Wewe umeokolewa ili uwafae wengine kwa ajili ya kazi yake na utumishi wake kwa hiyo ukishatambua hivyo lazima utunze kila kitu ambacho Mungu amekupa mwana wa Mungu. Jitahidi sana uishi utakatifu utakuwa na usalama. Usiwe na maisha ya sirini ya Michanganyo ili Mungu ajivunie wewe✍️✍️ 

Note: UTAKATIFU WA MTU unapimwa kwa maisha yako ya sirini na sio ambavyo unajionyesha kwa watu maana mtu wa kwanza kuyashuhudia maisha yako ya utakatifu ni wewe na Mungu pekee.

ACHA KUIFURAHIA DHAMBI UKISEMA UTATUBU KWA SIKU NYINGINE.πŸ‘‡πŸ‘‡

Mithali 27:12
"Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; 
Bali wajinga huendelea mbele wakaumia."

Tafuta kuwa Miongoni mwa watu wenye busara ukayaache mabaya yako yote ya sirini na umtumikie Mungu kwa moyo mnyoofu.

2.UTENDAJI WA KAZI YA MUNGU.
Pia watumishi wa Mungu wengi wamefika hatua ya kuchukulia ni kitu cha kawaida kuamua kufanya kazi ya Mungu pale wanapopata nafasi.

Yakobo4:17
"Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi."
Biblia inakuambia ukiwa unajua kufanya mambo mema usiyafanye ni dhambi. Unajua kwamba wewe unatakiwa kumtumikia Mungu katika eneo fulani usifanye kwako ni dhambi.

Wapo waimbaji, walimu, wainjilisti n.k ambao wanaipuuzia sana nafasi ambayo Mungu amewapa ya utumishi na kufanya huduma wanavyojisikia wakijifariji na kusema kwamba watafanya hata siku nyingine kitu ambacho ni machukizo mbele za Mungu.

Yeremia 20:9
"Nami nikisema, Sitamtaja, wala sitasema tena kwa jina lake; basi, ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia."

Moja ya kitu ambacho nilijifunza hapa kwa nabii Yeremia ni hiki richa ya upinzani na ugumu ambao alikutana nao kwenye huduma yake alipojaribu kuacha ule wito ndani ulimpa kutokutulia  sasa wewe Mungu kakupa huduma ya kufanya unawezaje kutulia ukasema nitafanya siku nyingine wakati unao muda wa kufanya. Hicho ni moja ya kipimo cha wewe kwamba umepungua kiroho na una hatihati ya kufa na kupotea katika msitari wa Mungu.

Zaburi 86:12
"Nitakusifu Wewe, Bwana, Mungu wangu, 
Kwa moyo wangu wote, 
Nitalitukuza jina lako milele."

Daudi alidhamiria toka ndani kumtumikia Mungu katika eneo la Sifa kwa moyo wake wote na sio nusu nusu kwamba leo kidogo na kesho itakuwepo nitafanya. Mungu anatamani umtumikie kana kwamba hautatumika tena. Pale unapopata nafasi jifunze kufanya kama hutafanya tena achana na mawazo ya kwamba kesho ipo.

Mungu akubariki kwa kuambatana nami katika hili somo fupi

Ulikuwa nami mpendwa katika kristo Yesu
Name: Bro Jackobo
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

MADHARA YA TENDO LA NDOA KABLA YA NDOA


Bro Jackobo


Utakuwa ndugu mpendwa 
Bro Jackobo (JAM295)
Phone: +255766944441 and +255621036471
Email: jackobombwaga@gmail.com

Naomba twende wote kwa pamoja

Mara nyingi tumekuwa tukichukulia kawaida  suala la Mahusiano ya kirafiki na kiuchumba na kuona ni kama kipindi cha Kujiachia,au cha Kujaribu jaribu kama kuna bahati yako au la, kumbe nikipindi Muhimu ambacho ni msingi wa ndoa ya mtu.

Ndoa nyingi zina machafuko yasiyokoma,ambayo masuluhisho mengi ya kwa wazazi, wasimamizi,wachungaji,mpaka na mahakama yamegonga mwamba hakuna kutulia, Machafuko yametokea kwasababu mbalimbali lakini nitazungumza juu ya jambo moja tu ambalo ni kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa au Msingi Mbovu wa Mahusiano unaoambatana na Tendo la Ndoa. 

Miongoni mwa vitu ambavyo wengi wa wanaofunga ndoa upuuzia nakuona ni kitu kidogo,ni Ni wao kuanguka katika zinaa(Kushiriki ngono)kabla ya ndoa halafu wakaoana wakiamini wanaendeleza Upendo,kumbe ndo wamefuta upendo.

πŸ‘‰πŸ‘‰Labda nikupe siri hii ya Kisaikolojia na kiroho sex ina pande mbili za shilingi ni TAMU na INAUNGANISHA NAFSI ZA WATU na kuwafanya wawe na Sura moja (Kama imefanyika katika muda muafaka kwa watu sahihi bila hatia)πŸ‘‡πŸ‘‡

1 SAMWELI 1:19
"Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za Bwana, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye Bwana akamkumbuka."

πŸ‘‰πŸ‘†Sex ikifanyika kwa watu waliosahihi yaani mke na mme ina MKONO WA BWANA WA BARAKA.

πŸ‘‰Pili  SEX inakawida ya Kuwaachanisha watu nafsi, kufuta upendo, Amani, furaha kati ya watu Walioifanya Kinyume, nje ya muda na si watu sahihiπŸ‘‡πŸ‘‡

2SAMWELI 13:10-17
" Amnoni akamwambia Tamari, Kilete chakula chumbani, nipate kula mkononi mwako. Basi Tamari akaitwaa mikate aliyoifanyiza, akamletea Amnoni nduguye mle chumbani. Naye alipokwisha kuileta karibu naye, ili ale, Amnoni akamkamata, akamwambia, Njoo ulale nami, ndugu yangu.  Naye akamjibu, La, sivyo, ndugu yangu, usinitenze nguvu; kwani haifai kutendeka hivi katika Israeli; usitende upumbavu huu.  Nami nichukue wapi aibu yangu? Wewe nawe utakuwa kama mmoja wa wapumbavu wa Israeli. Basi, sasa, nakusihi, useme na mfalme; kwa maana hatakukataza kunioa.
 Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye. akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako. Naye akamwambia, Sivyo, kwa kuwa mabaya haya ya kunitoa ni makuu kuliko yale uliyonitendea. Lakini alikataa kumsikiliza. Ndipo akamwita mtumishi wake aliyemtumikia, akasema, Mtoe sasa mwanamke huyu kwangu, ukafunge mlango nyuma yake."

πŸ‘‰πŸ‘† Wakati sex isiyo halali inakuwa ina vutia na inapofusha macho nikama unajituliza ila matokeo yake baadaye INAFUTA KILA AINA YA FURAHA NA AMANI KATIKA NAFSI ZA WAWILI

MADHARA YA TENDO LA NDOA KABLA YA NDOA
Naandika haya sio kukupa hofu bali kukufanya uweze kutambua madhara na matokeo ya jambo utakalo kulifanya

1. Madhara ya kiujumla wa maisha ya mtu
2. Madhara wakati mkiwa kwenye mahusiano
3. Madhara mkishaingia kwenye ndoa


 1. MADHARA YA KIUJUMLA YA MAISHA YA MTU

πŸ‘‰πŸ‘‰ DHAMBI
Kiasili toka mwanzo tendo la ndoa sio dhambi kabisa ila likifanyika kwa wanandoa tu na kama wanandoa wakiwa pamoja basi hata Roho wa MUNGU anakuwepo akiwafurahia na ndio maana toka asili alimuumba mtu mume na mke (MWANZO 1;27) lakini kwa wasiokuwa wanandoa ni dhambi.
Hapa sipendi nipazungumzie sana ila inafahamika kwamba afanyaye tendo la ndoa kabla ya ndoa huyo kwake ni dhambi

πŸ‘‰πŸ‘‰ KUVAMIWA NA MAROHO MACHAFU.
 Katika kufanya ngono, wengine wanaenda hadi kwa waganga wa kienyeji na wachawi na huko wengine  wanapewa madawa ya ajabu ambayo yanapelekea kuwamiwa na mapepo ya ajabu, na wengine kwa kupenda ngono wamefanya ngono na majini bila wao kujua na tayari yamesha wamiliki na hawajui watatokaje kwenye kifungo hicho. Lakini Mungu wetu ni wa Rehema anao msaada kwako kupitia Yesu kristo yaani msamaha wa Dhambi kama ukikubali na kumuamini Yeye utapata ondoleo la dhambi na kuwekwa huru kabisa

πŸ‘‰πŸ‘‰ KUWAPA WENGINE MIAKA YAKO.
 Uchunguzi unaonyesha kwa mtu anayependelea kufanya ngono mara kwa mara hasa anapoanza kabla ya ndoa mara nyingi hawezi kuishi kwa muda mrefu si hivyo tu lakini pia tumeona mara nyingi vijana wakijiua/wakiuana /wakifa kwa ajili ya mapenzi, wengine wanaugua hadi wanakufa wadogo na kupatwa na magonjwa mabaya, na hivyo muda waliostahili waishi hapa duniani na hivyo wanakuwa wamewapa wengine miaka yao.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

MITHALI 5:9 
"Usije ukawapa wengine heshima yako na wakorofi miaka yako"

Ukitaka kuelewa vizuri fungu hili soma sura nzima ya mithali 5 utaelewa kwanini nimesema hivyo

 2.MADHARA MKIWA KWENYE MAHUSIANO 
Hapa tutaona mkiwa bado hamjaoana nini huwa kinatokea

πŸ‘‰πŸ‘‰ Kupoteza Uaminigu baina yenu
kisaikolojia watu wakikutana na kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa huwa inakuwa ngumu kuaminiiana maana kuna kuwa na hisia za kwamba atakuwa anafanya hivyohivyo kwa wengine so kuaminiana kunakuwa kugumu

πŸ‘‰πŸ‘‰Kupungua au kufa kwa Upendo 
ukisoma kwenye fungu la juu utaona namna ambavyo Amnoni baada ya kufanya tendo la ndoa na tamari alimchukia sana tena sana na ndivyo iko kwa watu ambao wanafanya hivyo kabla ya ndoa
Baada ya kufanya mapenzi mara nyingi upendo hupungua hasa kwa vijana wa kiume na kwa mabinti upendo huongezeka na hii imewafanya Mabinti wengi wamejikuta wakipoteza THAMANI yao baada ya kuruhusu ku'sex na vijana wa kiume wakidhani kuwa kwa kufanya hivyo upendo utaongezeka kwa mwanaume kumbe wanajitengenezea misiba yao wenyewe.
Note: Upendo wa mtu huwa haupimwi kwa njia ya sex kwahiyo uwe makini.

πŸ‘‰πŸ‘‰ kuwashibisha wengine nguvu zako.

Mithali 5:10
"Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni"
Tendo la ndoa ni tendo linalohitaji mtu atumie nguvu, hivyo kadri mtu (hasa mwanume) anapofanya  mara kwa mara anajipotezea nguvu zake anawashibisha wengine nguvu zake na hivyo dhoruba itamkuta katika ndoa yake pindi atakapooa kwa sababu hatakua na nguvu tena kama awali.

πŸ‘‰πŸ‘‰ utavunjiwa heshima.
 Siku zote yule unayefanya naye tendo la ndoa kwanza atakuona wewe ni mpumpavu kwa sababu anajua afanyaye tendo hilo hana akili kabisaπŸ‘‡πŸ‘‡

 mithali 6:32 
 "Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake"

kwa hivyo atakudharau, zaidi atakutangaza kwa wengine na wewe mwenyewe pindi utapooa au kuolewa kwa kuwa nguvu zako uliwashibisha wengine basi utavunjiwa heshima na huyo mwenzi wako.

πŸ‘‰πŸ‘‰ Kufanya jambo liangamizalo nafsi yako

Mithali 6:32
"Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake."

Nafsi kwa kiyunani inaitwa Psuche, ndani yake kuna hisia, akili na maamuzi ya mtu. Hivyo kuiangamiza nafsi yako ni kuangamiza future yako na mipango yako uliyokuwa umejiwekea ya mbele na ndio maana mtu huyu akishazoea kufanya tendo la ndoa atajikuta mda mwingi akili yake inamsukuma akafanye tendo la ndoa maana nafsi yake haina uwezo wa kuamua vyema. Kuna mengi ya kueleza hapa lakini ngoja niweke tu kiufupi sana hivyo.

πŸ‘‰πŸ‘‰ Kujitengenezea Majeraha na Fedheha
Sikiliza katika ngono unaweza ukapata kilema cha maisha, na magonjwa ya hatari kama vile kaswende, ukimwi n.k. Haya magonjwa yatapelekea nyama na mwili wako kuangamia utashindwa kufikia malengo uliyojipagia, utabakia kujuta tu na watu watakufanyia fedheha na wakati huo upo kitandani hujiwezi.
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

MITHALI 6:33
" atapata jeraha na kuvunjiwa heshima wala fedheha yake haitafutika"

 3. MADHARA WAKATI WA NDOA
Sasa hapa tutaona matokeo yanayoweza kutokea kipindi mko katika ndoa.

πŸ‘‰πŸ‘‰ uaminifu kati yenu inakuwa changamoto
 Kuna uwezekano mkubwa Hakuna atakaye kuja kumwamini mwenzake kwamba atakuwa mwaminifu kwasababu ulikuwa na Ujasiri wa kuvunja uaminifu wako mbele zake katika ujana wako.
kwa sasa ndo anaona huwezi shindwa vunja tena huo uaminigu wako. Yani kiufupi msingi wenu wa ndoa ulikuwa umeharibika maana mlianza vibaya na itakuchukua hatua nyingine kuujenga

Zaburi 11:3
Kama misingi ikiharibika, 
Mwenye haki atafanya nini? 

Mtaishi maisha ya kuwindana, kulaumiana sana. Kawaulize wote walioangukia Kona hii hata kama ni watumishi wa Madhabahuni, wengi wao wanalazimisha kuaminiana mdomoni ila Moyoni na Akilini wanashitukiana

πŸ‘‰πŸ‘‰ Kushuka kwa Heshima baina yenu wawili 
Ukiona umevua au umevuliwa nguo kabla ya ndoa na huyo huyo mkaoana, Respect kati yenu inashuka chini ya nusu kwasababu Usiri wamiili yenu unabeba Heshima ya mioyo na utu wenu. 

Mkisha vuana nguo Usitegemee, Baba mwenye nyumba kupata full respect,au mama kupendwa full love utakuwa na Partial.... Maana respect na love vilivuliwa moyoni mwako nje ya ndoa, hukuja navyo ndani ya ndoa.

πŸ‘‰πŸ‘‰ Kuna uwezekano mkubwa wa kuachana kimwili  
kwanini hii hutokea?? Simply ni kwamba  vitu muhimu vinavyo shikilia Ndoa hamkuingia navyo ndani mliviacha pale mlipovuana nguo ( Vitu kama, Usiri, Aibu, heshima, shahuku kwa mwenzako,) kwa hiyo mgogoro ukianza ndani Hauzimwi unatafuta Kuachana.

Huna haja ya kujiuliza sana yani fikilia tu kwamba mtu hamjaoana ila kila unachokita unakipata kwake yani unaweza kutimiza matakwa yako ya mwili (sex) hata unapotaka kumuoa huwezi kuwa na shauku kuu ya kumuhitaji maana wewe tayari kwake huna geni lolote.

Kilicho thamani huwa kinasitiriwa mpaka wakati ulio sahihi ufike ndugu yangu, please usijipotezee thamani mbele za Mungu na kwa mwenzi wako embu tunza utakatifu kwanza 

πŸ‘‰πŸ‘‰ Fujo, magomvi Kunyimana tendo la ndoa haviwezi kukoma baina yenu.

(Maana moyo wa Upendo uliisha chukuliwa na adui) mtasuluhisha ila muafaka haupo,wanacho laumiana ni kidogo sana ila kinakuzwa na mbegu ya zinaa iliyofanyika. Mwaweza ishi ila si kwa Amani na upendo, mtakuwa na vipindi vifupi vya furaha na kipindi kirefu cha dhoruba.

HITIMISHO: KWA KIJANA AMBAYE BADO HAUJAOA AU BINTI AMBAYE HAUJAOLEWA USIKUBALI MTU AKAKUJUA MAPEMA KABLA YA NDOA KWA AJILI YA USALAMA WA MAISHA YAKO YA SASA NA YA BAADAYE NA KAMA ULISHAHARIBU KAZI BASI KUMBUKA KUINGIA KWA TOBA MBELE ZA MUNGU NA UWEZE KUSAIDIWA NAMNA YA KUWEZA KUTOKA HUKO

kuna watu wameshafika hatua wamepata addiction yani wanaona hawawezi kuishi bila kufanya tendo la Ndoa lakini nikuambie inawezekana na ukihitaji unaweza kutoka huko neema Ya Mungu imefunuliwa kwa ajili yako.

Ulikuwa nami mpendwa wako
Bro Jackobo 
Phone: +255766944441 na +255621036471
Email:jackobombwaga@gmail.com

ROHO MTAKATIFU NDANI YA MWAMINI


Bro Jackobo {JAM295}


Nini maana ya kujazwa Roho mtakatifu?

Kabla sijaendelea naomba nianze na utangulizi kidogo juu ya Roho  mtakatifu kabla sijaeleza kujazwa Roho mtakatifu ni nini

ROHOMTAKATIFU NI NANI??? 
NOTE. Kwanza jua ya kwamba huwezi kumtenganisha ROHO MTAKATIFU pekee yake akawa anajitosheleza palipo yeye lazima hata mwana na Baba wote wapo na hapa si watatu bali ni mmoja 

1.ROHO MTAKATIFU NI MUNGU Hizi ni sifa zake zinazoonyesha uungu wake
✓Anajua yote
1 Wakorintho 2:14
"Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni."

✓Yupo mahali pote
Zaburi 139:7-9
"Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko. Ningezitwaa mbawa za asubuhi, 
Na kukaa pande za mwisho za bahari;"

✓Ana nguvu zote
 Matendo ya Mitume 1:8
"Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi."

Ni wa milele yote
Waebrania 9:14
"basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?"

✓Ana uwezo wa kufufua 
Warumi 8:11
"Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu."

2.ROHO MTAKATIFUNI NAFSI YA TATU YA MUNGU 
sifa zake kama nafsi 
Roho mtakatifu anasema
 MDO10:19-20 
Roho mtakatifu anakataza
 Matendo ya Mitume 16:6-7
"Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa"

Kwanini tujawe na Roho mtakatifu?

kujawa Roho mtakatifu ni kukipokea kipawa cha Mungu alichokiahidi{Matendo 1:8} 

Huu ujazo wa Roho mtakatifu huwa unadhihirika kwa ishara ya kunena kwa Lugha na mambo mengne mengi yaliyo elezwa katika utendaji wa kazi ya Mungu  pamoja na mwamini

Matendo ya Mitume 2:1-4
"Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka."

Kujazwa ROHOMTAKATIFU sio swala la siku moja ni la kila siku kwa kila Mwamini. 

Note: kuna uwezekano mkubwa mtu akawa ameokoka lakini bado hajajazwa ROHOMTAKATIFU bali anaye ROHOMTAKATIFU 

tofauti kati ya mtu aliyejazwa na ambaye ana Roho Mtakatifu iko hapaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡ 

1️⃣Mtu aliyejazwa anaye ROHO MTAKATIFU pamoja na nguvu za Mungu na huyu mtu anaweza kusimama kama mwakilishi wa MUNGU {Matendo 1:8}  wakati aliye na Roho mtakatifu pekee hana ile nguvu na hawezi kuwa mwakilishi wa Mungu vizuri na hata kama akiwa mwakilishi atakuwa mtu wa kuanguka na kusima siku zote. Hii ina maana kwambaπŸ‘‡πŸ‘‡
Huyo aliyejazwa Roho mtakatifu anaweza akasimama akawashahidi wa MUNGU lakini huyu aliye na Roho wa Mungu lakini hajajaa hawezi akasimama kama shahidi maana hataweza kusimama kwa ujasiri kueleza siri za MUNGU na huyu yuko hatiani sana kuanguka wakati wowote

Kumbuka petro kabla hajajazwa Roho mtakatifu alimkana yesu lakini baada yakujaa alieleza siri za MUNGU kwa ujasiri Mbele ya kadamnasi bila woga Soma {Matendo 2:14-42} 

2️⃣Pia mtu ambaye amejazwa Roho mtakatifu huwa anashuhudiwa ndani yake kwamba yeye ni mwana wa Mungu na Mungu anafanya kazi pamoja naye lakini mtu ambaye hajajazwa huwa hana wa kumshuhudia pia ni ngumu kujitambua nafasi yake vizuri kama kweli kaokoka au bado na ndio maana anakuwa mtu wa kuanguka ovyoovyo.

Warumi 8:16-17
"Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye."


KWANINI KUJAZWA ROHO MTAKATIFU NI MUHIMU KWA MWAMINI

Note: Kila aliye mwami Yesu ni lazima ajazwe na ROHO MTAKATIFU 

Kujazwa na Roho mtakatifu ni agizo la Yesu kwa wafuasi wake
MDO1:2-4; YOH15:16 

✓Ahadi yetu kutoka kwa baba
LUKA24:49; MDO2:38-39 

kwasababu ya wajibu/majukumu tuliopewa na Baba
tumepewa wajibu/Majukumu  muhim sana kama yafuatayo 
Kujengana ndani ya kanisa, kumwabudu Mungu yoh 4:23-24, math15:8
•kuufikiaulimwengu Rumi8:1 

Mpendwa katika Kristo Yesu imekupasa kupokea nguvu ya Roho mtakatifu ili kuwa na usalama wa safari yako ya mbinguni. 

Kwa hiyo ni lazima ujae na kunena kwa Lugha mpya, kuweka mikono juu ya wagonjwa waka pata afya japo hiyo sio tiketi ya kwamba umejawa na yeye maana yeye huwa anajisimamia mwenyewe katika utendaji wa kaziyake kwahiyo lazima uhakikishwe na yeye mwenyewe kwamba wewe ni wake kabisa.

 NJIA ZA KUJILIWA/KUJAZWA NA ROHO MTAKATIFU 

✓ Kusikia neno laMUNGU MDO10:44-46 
✓ Kusifu na kabudu katika utakatifu 
LUKA24:50-53 MDO16:24 
✓ Kumuomba MUNGU juu ya ujazowa NGUVUzake LUKA11:13 
✓ Kuwekewa mikono na watumishi wa Mungu
MDO 8:14-17 MDO 19:6-7 

SIFAZAMTU MWENYEKUJILIWA NA ROHOMTAKATIFU 

1.lazima awe AMEOKOKA
MDO2:37-39 MATH5:8 
2.Lazima huyuMTU awe na kiu ya Kumpokea ROHO MTAKATIFU yoh7:37-39 MATH5:6 
3.Lazima awe na imani ya kumpokea Roho wa Mungu EBR11:6 

MATOKEOYA KUJILIWANAROHO MTAKATIFU 
1.Kunena kwa LUGHA MPYA MDO2:4 
2.kupoke nguvu Za Mungu MDO 1:8 na mengine mengisana 

Ulikuwa nami mpendwa katika kristo Yesu 
Bro Jackobo
jackobombwag@gmai.com 
jackobombwaga.blogspot.com
+255766944441 +255621036471 

JE UNAYO NAFASI YA KRISTO YESU NDANI YA MOYO WAKO?


Bro Jackobo

Utakuwa namimi mpendwa wako katika kristo Yesu

Name:Bro Jackobo email: jackobombwaga@gmail.com 
Phone; +255766944441

Bwana Yesu apewe sifa Wana wa Mungu? napenda tushirikiane jambo hili kidogo

Kanisa la Leo limekuwa ni waaminifu sana kuhudhuria Ibada na vikundi mbalimbali vilivyo ndani ya kanisa lakini nafasi ya Yesu ndani ya maisha yao imekuwa ni shida sana tena sana mpaka inaleta huruma kuona watu hawana msimamo kamili wa Ki-Mungu ila wanaishi kimazoea tu kama walivyoishi Jana.

Ndipo nakumbuka kuna wakati Yesu aliwahi kuzungumza neno lifuatalo

 MATHAYO 15:8-9
 "Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami Nao waniabudu bure Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu."

Wakuu wa dini walikuwa wakiishi kwa  mapokeo lakini waliacha msingi wa kweli wa kumfanyia Mungu Ibada ya kweli kwahiyo katika vinywa vyao walikuwa wakitamka kumpenda Mungu lakini kiuhalisi hawakuwa na Mungu ndani yao na hili ndilo kanisa ambalo tuko nalo kizazi cha leo watu wanaeleza wema wa Mungu lakini hawawahi kupata Raha iliyoko ndani ya kristo. Ni kawaida Ukaona mtu anafundisha Ubatizo wa Roho mtakatifu lakini hajawahi kushuhudia Radha ya Roho mtakatifu hata siku moja..

Nampenda sana paulo maana alitamani kanisa liishi kwa mfano pia hata wake. Embu ona hayo mafunguπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 1 WAKORINTHO 11:1
 "Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo."

 WAFILIPI 3:17
 "Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi."

Mafungu yote hapo juu yanaonyesha namna paulo alivyojiweka kipaumbele mwenyewe ili kwamba watu waige mfano wao lakini kanisa la leo halina watu wanao weza kunena kwa ujasiri kwamba mnifuate mimi kama nilivyo mfuata kristo Yesu kwasababu maisha yao hayana ushuhuda hata kidogo maana wamejichanganya kupita kiasi tena kiasi. Mungu akukumbuke ndugu yangu badilika.

 LUKA9:57
"Yesu akamwambia, Mbweha wana pango,na ndege wa angani wanaviota, lakini Mwana wa Adamu hana pa kujilaza kichwa chake."

Ukianza kusoma mistari ya nyuma utaona huyu mtu alitaka kumfuata lakini Yesu anakuja kumpa majibu magumu sana yule mtu kwamba hana nafasi ya kuweza kukaa kwake. 

Yule mtu alikuwa na nia yakumfuata kristo lakini ndani yake alikuwa hajampa kristo nafasi hata kidogo maana Imani bila matendo imekufa πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 YAKOBO 2:17
 "Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake."

Wengi wetu tuna nia ya kumfuata kristo lakini hatujaambatanisha nia zetu pamoja na matendo yetu. Na ndio maana biblia inasisitiza kujikana mwenyewe lasivyo utakuwa unaingia kwenye nyumba ya Mungu lakini hutakuwa una nafasi ya Yesu kristo.

 MATHAYO 16:24 
 "Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate." 

Nikuulize swali na wewe je umempa nafasi gani kristo Yesu kwenye maisha yako?
 
Au umekuwa na wewe unaingia kwenye nyumba ya Mungu huku umemuweka mbali sana Yesu kristo?  

Au umekuwa ni mtu unaye mfuata Yesu wakati wa kustarehe na ukifika wakati wa magumu ulekuwa ukimuacha?
πŸ‘‰lazima uwe mtu wa kuvumilia kutenda mema siku zote ndipo utapata nafasi ya kuurithi ufalme wa MUNGU lasivyo unajidanganya.

 MATHAYO 24:13 
"Lakinimwenye kuvumiliahata mwisho, ndiyeatakayeokoka."

Mwisho wa safari yako ya hapa duniani ndiyo taswira kamili ya kile unachotakiwa kukipata baada ya yote hayo maana baada ya kifo ni hukumu.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 WAEBRANIA 9:27
 "Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;"

Kuna mafundisho yapo ambayo yanawaambia watu kwamba eti mtu anaweza kuombewa baada ya kufa akaenda peponi hayo ni mafundisho potofu yenye lengo la kuwafanya watu wasiogope kufanya dhambi wakiamini wataombewa na Mungu atawasamehe {wajidanganya bure} basi haikuwa na maana ya kuwaambia watu waishi maisha ya kumfuata Yesu na pia kwamba Ajikane mwenyewe basi Yesu angeseme mtu asiponifuata na ndugu zake watamuolbea akifa aende kwenye haki. Kwahiyo ukifa ni hukumu tu hakuna cha nafasi tena ya toba yani matendo yako yataambatana nawe.

Nikuambie tu ukweli kwamba kama umebadili mwili wako na moyo wako kuwa sehemuya uovu jua hukumu inakungoja haijarishi unaingia kanisani au hauingii

 MATHAYO 21;12
 "Yesu akaingiandani yahekalu,akawafukuzawote waliokuwa wakiuza na kununua hekaluni,akazipindua meza za wabadili fedha, na viti vyao waliokuwawakiuza njiwa"

kristo hataki michanganyo hata siku moja ndio maana alipoona wamegeuza sehemu ya ibada kuwa kama gulio ilimkasirisha sana YESU. ndivyo vivyohivyo anavyochukia pale unapoacha njia ya MUNGU na kufanya Mambo unayoyataka yaliyo tofauti na neno lake. 
Tambua ya kwamba wewe ni hekalu tena u sehemu ya ibada ya MUNGU ndani ya moyo wako. 
maana siku ile Mwana wa Mungu atakapokuwa kwenye kiti cha enzi atawabagua kama Mbuzi na kondoo kwa kadri ya mtu na matendo yake. (soma Mathayo 25:31-46)

usikae kwa hasara Mahali ulipo maana hukumu inakuja wala usije kuwa una mheshimu Mungu kwa kinywa tu bali na matendo yako yaambatane na namna kinywa chako kinavyozungumza.

nipende kukusihi ndugu yangu badirisha njia zako na kama bado hujatengeneza na MUNGU Yeyeb ado anatoa mwito yoyote aliye na mzigo wa aina yeyote yeye atakupumzisha.πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

 MATHAYO 11:28 
 "Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha."

Usiridhike na kuingia kwako ibadani tu ridhika ikiwa unashuhudiwa na Roho mtakatifu kwamba umekaa sawa.

 WARUMI 10;10 
 "Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu."

kazi yako ni kuamini na kumpa kristo maisha yako na sio kwenda kanisani tu na huku unafanyavitu visivyofaa

Saa ya hukumu iko karibu badili njia zako ndugu yangu.

Mungu alibariki kwa kuusoma ujumbe huu na Mungu akupe hatua ya kutoka katika kifungo chako kinachokutesa kinachokufanya unakuwa na maisha ya kifafa.
Unaweza ukapata masomo yanu mengine ukatafuta kwenye browser yako kwa kuandika
(Jackobombwaga.blogspot.com)

 Ulikuwa nami mpendwa katika kristo Yesu
Name:Bro Jackobo
Email: jackobombwaga@gmail.com
Phone: +255766944441

JIFUNZE KUWA MWAMINIFU MPAKA MWISHO HATA KAMA UNAONA UGUMU


Bro Jackobo {JAM295}

Utakuwa nami mpendwa katika kristo Yesu.
Name: Bro Jackobo
Phone; +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu?? Karibu tushiriki pamoja neno hili kwa kifupi sana katika siku hii ya leo.

Kumekuwa na ugumu sana wa watu kuutunza uaminifu pindi pale mazingira kwao yanapokuwa magumu na mazingira ya kweli yao yanawaumiza wao wenyewe.

Mwanzo 39:9-12
"Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?
Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye. Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani; huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje."

Yusufu alipita wakati mgumu ambao huo wakati ulikuwa mgumu maana yake alipata nafasi kabisa ya kuweza kulala na mke wa potifa lakini yeye aligoma kabisa kulala na mke wa potifa maana alikuwa akitafuta kuwa mwaminifu mbele za MUNGU hakujali hata kukimbia na kuacha mavazi yake ambayo aliona kwamba yangemletea shida hata kwa baadae kwenye maisha yake.

Jiulize mara ngapi wewe umeacha sheria ya MUNGU kwa sababu ya magumu yaliyokuzunguka?? Ni mara ngapi umevunja uaminifu wako kwa sababu ya vitisho kwenye maisha yako ya kila siku??

Mathayo 15:8-9
"Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure,
Wakifundisha mafundisho
Yaliyo maagizo ya wanadamu."

Mbona umekuwa ni Mtu wa kumuheshimu Mungu tu kwenye maisha yako kwa kinywa lakini matendo yako yamekuwa yakimkana Mungu siku zote.

Au hujui ya kwamba kuna laana ipo pale ambapo mtu akifanya mambo ya ajabu lakini asiwe tayari kuishi katika kweli ya Mungu? πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Mithali 28:13
"Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema."
Ukiwa mtu wa kumheshimu MUNGU kwa kinywa tu na matendo yako yanamkana MUNGU inamaanisha huwa unauficha ubaya wako wa kila siku baada ya kwamba uutubie huo ubaya wako wewe unaendelea kujificha jua ya kwamba unajiletea laana mbele za Mungu kwenye maisha yako.

Ndio maana nakushauri ndugu yangu kwamba uamue kuwa mwaminifu siku zote za maisha yako hata kama unaona magumu kwenye maisha yako.

Ndio maana YESU anakushauri hivi
πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Ufunuo wa Yohana 3:15
"Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto."

Katika maandiko hayo hapo juu yako wazi kabisa na yanakutaka uamue kuchagua upande mmoja wa kuwa mwaminifu ukiamua kuwa wa kristo basi uishi kama Kristo na kama ni kwa shetani uishi kama kwa shetani tu. Usiwe mtu wa kumega huku na kule.

MAENEO AMBAYO YAMEKUWA NA KUKOSEKANA KWA UAMINIFU NDANI YA KANISA
Kuna maeneo mbalimbali na mengi sana ambayo yamekuwa na changamoto kuwa na uaminifu lakini nitakuelezea maeneo machache tu
{A} Mahusiano, uchumba na ndoa
{B} Biashara
{C}Ibada na maombi
{D} Matoleo pamoja na ahadi

{A} MAHUSIANO, UCHUMBA NA NDOA
mahusiano na uchumba
Vijana wengi wamekuwa wanaingia kwenye mahusiano na uchumba kwa siri na hata kufanya mambo yasiyotakiwa kwa siri(kukosa uaminifu) huku wanafanya ibada kila inapoitwa leo
Mbona umekuwa unafanya tendo la ndoa, unafanya Romance wakati hauko kwenye ndoa ndugu yangu? Mungu akupe neema utoke huko kwa jina la Yesu kristo.
Kuna watu wanadai kwamba miili inawasukuma kufanya hivyo lakini nawaambia kuna mambo mawili hapa ya msingi ukiyajua yatakusaidiaπŸ‘‡πŸ‘‡

πŸ‘‰πŸ‘‰Moja: Mwili kuhitaji tendo la ndoa kwa mwanadamu ambaye yuko vizuri kibiolojia ni kitu cha kawaida lakini umepewa namna ya kuweza kushinda


Wagalatia 5:16
"Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili."

Hapo juu biblia inakuambia uenende kwa Roho ili usitimize tamaa za mwili kiufupi ni kwamba tamaa za mwili zitakuja isipokuwa ili usizitimize/usiziishi lazima uwe katika Roho yaani ukubali kuwa chini ya maongozi ya Roho mtakatifu lasivyo utakuwa unajidanganya tu. Wengi wanajikuta kuingia kutenda dhambi ni kwasababu hawajakaa katika Roho mtakatifu.

1 Wathesalonike 4:3-5
"Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu."
Maandiko hapo juu yanakukukataza uasherati lakini yanakuambia ujue kuuweza mwili wako katika utakatifu na heshima kwahiyo hata kama ikitokea wewe nenda mbele za Mungu kwa moyo wa Toba na yeye atakusamehe na kukusafisha kabisa.
Mwingine anaweza sema nawaambia watu waendelee katika tamaa lakini sio hivyo ila hiyo inatokea na ndio maana paulo alisema

1 Wakorintho 7:1-2
"Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke.
Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe."
Hapo anaeleza habari ya zinaa ndio inamfanya mtu basi awe na ile ya kumgusa na kuwa na mke au mume ambapo zinaa ni matokeo ya tamaa. Kwahiyo usiogope ikitokea hivyo ila mtafute Mungu atakusaidia.

Note: mtu asije akakudanganya kwamba eti ukiwa katika kristo kama ni kijana uliye okoka kushituka hakupo. Kushituka kupo ila Mungu anatutunza na kutupa uwezo wa kustahimili. Aliposema kila mtu ajue kuuweza mwili inamaana mwili kuna namna utahitaji hakusema mkiwa katika kristo mwili utakuwa hauna chochote. Na anaposema kwamba hatutatimiza tamaa za mwili maana yake yapo matamanio ya mwili ila tukiwa katika Roho hatutayaishi.

πŸ‘‰πŸ‘‰Pili, Tendo la ndoa sio dhambi kabisa ila likifanyika kwa wakati sahihi na kwa watu sahihi

Kwahiyo ukiona huwezi kukaa bila tendo la ndoa basi jitahidi kuoa au kuolewa na kuepukana na hatia ya dhambi itakayokuwa kwako kwa kuqhindwa kujizuia kwako.

Ndoa
Pia hapa kuna changamoto kubwa sana ndani ya kanisa unaweza kukuta mwalimu wa kwaya au kiongozi yeyote anatembea na mshirika ndani ya kanisa mahali palepale kitu ambacho kinaleta shida kubwa sana ndani ya kanisa.

Mpendwa usiendelee kujifariji tu kwamba uko na Mungu kumbe Mungu amekuacha  tubu dhambi yako biblia imejieleza kabisa katika
Kutoka 20:14 "Usizini." Jitahidi utoke huko bado Mungu anakupenda.

{B} BIASHARA
Katika eneo hili Mungu atusaidie kanisa tutoke hapo maana wafanyao biashara wamekuwa ni watu wa kuwaibia wale watu wanaowauzia wakitaka kupata faida kubwa katika vile vitu wanavyovuza mfano
πŸ‘‰Watu hutengeneza vifaa vya kuuzia vidogo chini ya kipimo sahihi na namna inatakiwa n1 kujikuta wakifanya mambo yasiyofaa na kuangukia katika Dhambi

Mambo ya Walawi 19:35
"Msifanye yasiyo haki katika hukumu, wala katika kupima, wala katika mizani, wala katika cheo."
Mithali 11:1
"Mizani  ya hadaa ni chukizo kwa BWANA; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza."
Ezekieli 45:10
"Mtakuwa  na mizani ya haki, na efa ya haki, na bathi ya haki."
Maandiko hayo yamejieleza kufanya katika mizani ya haki kwahiyo jitahidi kuwa mwaminifu katika eneo hilo 
πŸ‘‰pia watu walioajiliwa huwa wanaiba katika faida zile wanapata na kupeleka pungufu kwa waajiri wao.
Kwahiyo Mungu akusaidie ufanye kama inavyotakiwa usiwe mtu wa kuvunja uaminifu bado Mungu anakupenda.

{C} IBADA NA MAOMBI
Watu wengi wamekosa kuwa waaminifu kwenye maisha yao binafsi maana wamekuwa ni watu kufanya ibada ili waonekane lakini unakuta ndani yao hakuna ibada ya kweli jifunze kuwa mtu wa ibada ya kweli inayoanzia ndani mwako hata unapokusanyika na wenzio basi iwe kama hitimisho la ibada na Mungu atakufanikisha sana na utanawili sana kwenye maisha yako ya kila siku.
Katika eneo la maombi inakubidi kufanya kama maandiko yanavyotaka kufanyika basi Mungu akupe neema nmejaribu kukuelezea kifupi tu ili upate mwanga.
 
Kwahiyo jitahidi kuwa mwaminifu katika eneo lolote ambalo utakuwa umekaa na ndio maana na ndio maana huwa nina msemo mmoja huuπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡ 

UKIWA MWAMINIFU TU MBELE ZA WATU WAKATI UKIWA MWENYEWE HUWEZI KUUTUNZA UAMINIFU BASI UJUE WEWE SIO MWAMINIFU BALI NI MIONGONI MWA WANAFIKI WALIOPO

Nina Mengi ya kusema katika hili lakini naomba nieleze tu hiyo kifupi maana kuna baadhi ya mambo hapo unaweza ongezea mfano
πŸ‘‰Mambo yatakayoniwezesha kuwa na uaminifu
πŸ‘‰Namna gani baadhi ya watumishi waliomfano wa maaandiko walivyotunza uaminifu wao kila siku
πŸ‘‰Faida za uaminifu 
πŸ‘‰Madhara yatokanayo na kukosa uaminifu

Yote hayo ningeyazungumzia lakini kwakuwa nimepewa kwa leo kuandika hayo naomba niishie hapo ila kama itatokea neema nitaandika sehemu ya pili ya hili

Ulikuwa nami mpendwa katika kristo Yesu.
Name: Bro Jackobo
Phone; +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

SAFARI YA JANGWA KWA MWAMINI {sehemu ya pili Final}


Bro Jackobo

Utakuwa nami mpendwa wako katika kristo Yesu
Name: Bro Jackobo {JAM295}
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

Bwana Yesu asifiwe mtumishi wa Mungu? Na tumaini utakuwa unaendelea vizuri na kama hauko vizuri basi Mungu akutokee kwa jina la Yesu kristo. Naomba nimalizie kipengele cha pili kwenye somo letu hili na kama hukufanikiwa kusoma sehemu ya kwanza ningekuomba ukipitia ili tuende pamoja. Kama hukuona basi bonyeza hapaπŸ‘‰SEHEMU YA KWANZA kuisoma


BAADHI YA MAENEO AMBAYO MTU ANAWEZA AKAPITA WAKATI WA JANGWA 
Kuna maeneo mengi sana watu wanapita katika jangwa lakini nitayaorodhesha machache tu na wewe utatafakari utaelewa.
1. Mahusiano na ndoa
Katika eneo hili watu hupitia magumu kama yafuatayo
A)Ndoa
   ✓Kukosekana kwa amani baina ya wanandoa
   ✓Kukosa watoto katika ndoa
   ✓ Usaliti katika ndoa yaani kuchepuka kwa mwezi wako
   ✓kuvunjika kwa ndoa baina ya wanandoa
{Soma 1samweli 1:1-16}

B) Mahusiano
   ✓ Kukataliwa na watu pindi unapotaka kuanza safari ya ndoa
   ✓Kuvunjika kwa uchumba pasipokuwa na sababu ya msingi
   ✓kusalitiana wakati bado mko kwa mahusiano 

2. Uchumi
Katika eneo hili watu hupitia magumu kama yafuatayo
   ✓Kukosa mafanikio wakati unafanya kazi kwa bidii
   ✓kupotea kwa mali zako pasina kuelewa huku unafuata sheria zote za Mungu
   ✓kuwa na madeni ambayo mda mwingine inakuwa ngumu kuyaeleza
 {Soma 2wafalme 4:1-2}

3. Elimu
Katika eneo hili watu hupitia magumu kama yafuatayo
     ✓ Kuwa na matokeo mabaya wakati unafanya bidii katika kusoma kwako
     ✓kukosa vufaa vya kukuwezesha kuweza kupata elimu mfano Ada n.k
     ✓Kukosa watu watakao kutia moyo katika kusoma kwako

Pia yapo maeneo mbalimbali unaweza ukapita katika jangwa lakini natamani tuende moja kwa moja katika msingi mkuu wa somoo tunalo jifunza. Nakuombea upate neema ya kuelewa vizuri mahali hapa na Roho mtakatifu akufunulie upate kujua siri hii kwa jina la Yesu kristo mnazareti.


MAMBO YA KUKUSAIDIA KUISHI KIPINDI CHA JANGWA KAMA MWAMINI

✍️ KUMJUA MUNGU KIUNDANI
Ayubu 22:21
"Mjue sana Mungu, ili uwe na amani Ndivyo mema yatakavyokujia."

Katika kumjua Mungu ndio kutakuletea amani kwenye maisha yako kwahiyo msingi wa kuona amani kwa maisha ya mwamini ni kumjua Mungu maana panapo jangwa hakuna amani wala kutulia bali ni machafuko tu.

NAMNA GANI NAWEZA KUMJUA MUNGU WANGU
N.B Suala la kumjua Mungu ni la kila siku sio suala la siku moja wala wiki moja na ndio maana inahitajika jitihada sana ili uweze kumjua Mungu

πŸ‘‰πŸ‘‰Kuwa na neno la Mungu ndani yako
Ayubu 32:18
"Kwa kuwa nimejaa maneno; 
Roho iliyo ndani yangu hunihimiza"
Yohana 6:63
"Roho  ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima"
Wakolosai 3:16
"Neno  la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu."

Maandiko ya hapo juu yanatuhitaji kwamba tuwe na nzno la  Mungu ndani yetu tena yanatuambia kabisa juu ya umuhimu wa kuwa na neno la Mungu ndani yetu maana linatufunulia kwamba kukiwepo na neno kuna uwezo wa kuimizwa n1 unapokuwa unahimizwa ndio unamuelewa Mungu anataka kitu gani kwenye maisha yako. Tena biblia iko wazi kabisa kwamba maneno ni Roho kwahiyo kama ni R'oho ukiwa na Neno la Mungu ndani yako ujue utakuwa na uwezo wa kuwa na Roho wa Mungu ndani yako ambaye huyo atakufariji na kukupa namna ya kuendelea mbele hata kama mambo yako vibaya kwenye maisha yako.

Sasa kwanini tuhitaji neno la Mungu ndani Yetu wakati wa jangwa??
      ✓Neno la Mungu linatuhimiza katika mambo mema
Kwahiyo utaweza kuhimizwa zaidi kuendelea kusimama na Mungu wako hata kama mambo ni magumu ndio maana unasisitizwa kuwa na neno la Mungu ndani yako.
     ✓Neno la Mungu humfunua Mungu katika uhalisia wake.
Kinachotokea katika kanisa la leo ni kwamba Watu wengi Mungu hajajifunua kwao na ndio maana ni rahisi sana mtu akawa mtu wa kusimama n1 kuanguka lakini ukiwa na neno lake Mungu atajifunua dhahiri kwako utajua juu ya nguvu za Mungu, utendaji wake ulivyo, mamlaka yake ilivyo, namna Mungu anaruhusu baadhi ya mambo kuja kwetu huku akiwa bado ana mawazo mema na sisi katika yote tunayapitia. Katika gumu sasa linapokupata utakuwa una uelewa kamili namna Mungu anafanya kwahiyo utaweza kuvumilia ukijua yeye bado yupo na atakuwepo.
        ✓Neno ni mwanga katika maisha ya mwanadamu
Mwanga huwa unaondoa giza mahali kwahiyo kupitia nzno la Mungu unakuwa una taa ndani yako ambayo kwahiyo unaweza kupata muelekeo mzuri wa jinsi ya kuenda pindi uko katika wakati mgumu yaani hata kama unapigwa vita katika huduma bado Mungu atakuwa anakupa maelekezo kwamba ufanye nini ili uweze kufika salama katika safari yako.
         ✓Neno la Mungu hutuongoza wokovuni
Tunapokuwa na uwezo wa kusimama katika wokovu ndipo tunapoweza kuendelea kumtumaini Mungu katika yote ambayo yanatukumba hata kama yanatuvunja moyo.

πŸ‘‰πŸ‘‰Kuwa mtu wa Maombi siku zote za maisha yako kila inapoitwa leo

Luka 22:40-42
"Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni. Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba, akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke."

Yesu alikuwa katika kipindi kigumu cha jangwa maana alikuwa anajua wale aliowafanyia mema wanaenda kumtenda hiana ndio maana aliingia kwa maombi.
Pia yule ambaye alikula naye meza moja anaenda kumsaliti (Luka 22:47-53)
Pia ndio maana unashauliwa usizimie wakati wa tabu zako (Mithali 24:10) 

  πŸ‘‰πŸ‘‰Kuwa watu wa Kumfanyia Mungu Ibada
Unapozungumzia suala la ibada unaweza ukachukulia ni kitu cha kawaida lakini ili tuseme kwanza kunayo ibada lazima kuwe na vitu vikuu vitatu MTOA IBADA (mwanadamu), MTOLEWA IBADA (MUNGU) pamoja na MADHABAHU (Sehemu ya kumfanyia Mungu ibada ambayo huwa inaambatana pamoja na utoaji wa Sadaka na Dhabihu mbalimbali) unaweza ukasoma habari za ELIYA katika kitabu cha 1wafalme 18 sura yote utaelewa

Waebrania10:25
"wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia."
Kwahiyo kukusanyika kwetu katika ibada kila siku kutatusaidia sana kuweza kuelekezana mambo mbalimbali juu ya kweli ya Mungu na namna ya kuweza kuishi maisha ya utaua(uchaji)/ utakatifu. Kuna baadhi ya watu ambao huamini kwamba hata wasipokusanyika kwenye nyumba za ibada wako salama lakini kiuhalisia hawako salama hiyo ni principle ya kiMungu ambayo kaiweka mwenyewe sasa kwanini uachane na utaratibu wake??
Mungu atusaidie sana tuwe watu wa ibada.
Pia kuwa na Ibada za pamoja ni jambo jema sana lakini kama ukikosa kuwa na Ibada za binafsi ujue bado kuna vitu utavikosa sana kwenye maisha yako. Mungu akufungue sana kama unafanya ibada za pamoja tu na haufanyi ibada ya kwako binafsi uelewe umuhimu wake.

Note: Kuna namna nyingi sana unaweza kumjua Mungu ila kikubwa sana ni kutaka kuelewa makusudi ya MUNGU. Naomba niendeleee na point ya pili ya namna ya kuweza kuishi kipindi cha Jangwa.

✍️UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU

Matendo ya Mitume 1:8
"Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi."
Nguvu ni uwezo wa kufanya kazi. Watu wengi wapo kanisani wana Roho wa Mungu lakini bado hawana Ujazo wa Roho mtakatifu na hao ni wana wa Mungu kabisa maana 
Warumi 8:14 
"Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu
Lakini hata kabla ya hapo Yesu aliwaambia wanafunzi wake majina yao yameandikwa mbinguni (Luka 10:17-20) na ilikuwa kabla ya kushuka katika ubatizo siku ya pentecoste kwahiyo walikuwa na Roho wa Mungu ila hawakuwa na ujazo ambayo ndio hutoa uwezo wa kushinda maana baada ya hapo ndio anapotoa kwamba mtakuwa mashahidi wangu n. K
Kwahiyo kupitia nguvu ya Roho mtakatifu utaweza kuwa mwaminifu mbele za Mungu katika moments/Nyakati mambo yanapokuwa magumu na wakati hakuna wa kukuambia kwamba mshike Mungu, Roho yeye atakukumbusha yote kwahiyo tafuta nguvu kwanza ndipo utaweza kuwa salama.

✍️ KUKUMBUKA NAMNA MUNGU AMEFANYA JUUU YAKO
MWANZO 39:8-11
"Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu. Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu? Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye. Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani;"

✓Yusuph aliingia wakati wa jangwa pindi pale ambapo mke wa yule potifa alimtaka kingono maana alitegemea asingeweza kumwambia hivyo ila ashukuriwe Mungu alikumbuka namna Mungu alivyokuwa naye kwahiyo ukikumbuka namna Mungu amekutendea hutayahesabu magumu yale kuwa kitu cha maana zaidi utaishi kwa kusudi la Mungu na sio kuishi kwa matatizo. 
✓Jifunze kuwa mtu wa tafakari siku zote usiwe mwepesi wa kuamua jambo lolote fikiri kwa kina ndipo uchukue uamuzi wa kufuata jambo fulani na kweli ya Mungu itakuongoza katika maamuzi.

✍️ KUAMINI JUU YA UTENDAJI WA MUNGU KWENYE MAISHA YAKO NA KUKUMBUKA ALIKOKUTOA MPAKA ULIPOFIKA.
1Wakorintho 10:10-12
"Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu. Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke."

Kuamini ni kuwa na uhakika kwamba Itatokea hata kama huoni namna ya kuweza kufanikiwa. Ukiona kuna namna ya kwamba nitafanikisha na unamazingira yote ya kukufanikisha hiyo sio Imani.
Wana wa Israeli walishindwa kuamini juu ya utendaji wa Mungu walipokuwa wanatolewa katika nchi ya utumwa wakawa wanamnung'unikia Mussa pamoja na Mungu na ndio maana waliangamizwa lakini wewe usiwe mtu wa kumnung'unikia Mungu hata kama mambo yamekuwa magumu wewe amini tu ya kwamba atafanya na utauona mkono wa Mungu kwenye maisha yako.

✍️KUYAHESABU MAMBO YALIYOKUWA FAIDA KUWA SI FAIDA TENA KWAKO
Wafilipi 1:12-14
"Lakini, ndugu zangu, nataka mjue ya kuwa mambo yote yaliyonipata yametokea zaidi kwa kuieneza Injili; hata vifungo vyangu vimekuwa dhahiri katika Kristo, miongoni mwa askari, na kwa wengine wote pia. Na wengi wa hao ndugu walio katika Bwana, hali wakapata kuthibitika kwa ajili ya kufungwa kwangu, wamezidi sana kuthubutu kunena neno la Mungu pasipo hofu."

Wafilipi 3:7-8
"Lakini  mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;"

Mafungu hayo yameonyesha namna paulo alikuwa katika wakati mgumu kwa ajili ya kristo hata kapata vifungo mbalimbali kwa ajili ya kristo lakini bado mbele anakuambia mengi aliyaona  kuwa mavi yaliyokuwa thamani kwake kwahiyo alikubali kuchukua mzigo utakao kuja kwake kwa ajili ya Kristo Yesu.
Kama ukiweka mambo yako chini kuna namna Mungu atakusaidia kuweza kushinda kwahiyo magumu, changamoto, pale ambapo hakuna mtu wa kukuambia acha dhambi, kukufariji katika huduma yeye atakusaidia na kukupa mwangaza wa mafanikio.
Kama kuna mambo yanakupa faida lakini yanakupelekea wakati mgumu kwenye utumishi wako inakupasa kuyahesabu kama sio kitu cha maana yahesabu hayoo mambo kuwa si kitu cha thamani bali kristo ndani yako ndiye wa thamani utapata neema ya kushinda.

Mungu akubariki kwa kuungana nami tangu mwanzo mpaka mwisho toka sehemu ya kwanza mpaka hii ya pili.
Unaweza ukawashirikisha na wengine pia mwana wa Mungu. 

Lakini katika yote nakuombea ufanikiwe katika magumu yako yote Mungu akufanyie mlango kwa jina la Yesu kristo Amen...

Ulikuwa nami mpendwa wako katika kristo Yesu
Name: Bro Jackobo {JAM295}
Phone: +255766944441
Email: jackobombwaga@gmail.com

SAFARI YA JANGWA KWA MWAMINI{sehemu ya kwanza}.


BRO JACKOBO

Jina: Bro Jackobo (JAM295)
Phone: +255766944441 na +255621036471
Email: jackobombwaga@gmail.com

UTANGULIZI WA KUELEWA JANGWA KWA MWAMINI

Maana ya Jangwa

JANGWA ni mahali pa ukame ambapo hakuna mvua ya kutosha na kupelekea mazao pamoja na wanyama kuwa na mazingira magumu katika ukuaji.

JANGWA kwa mwamini inaweza kuwa
✍️✍️Kukosa msaada katika mazingira ya ROHONI na MWILINI

A. MAZINGIRA YA KIMWILI
•kutelekezwa
• kuumizwa,
• kutukanwa
•kudharaulika hata kushushwa chini kuliko vile ulikuwa unategemea kuwaiwe kulinganisha na namna ulivyo
•Jaribu katika maisha yako ya kila siku n.k

B. MAZINGIRA YA ROHONI
unakosa msaada wa kiroho yaani namna ya kuweza kukutana na Mungu
•Hapa unakuwa umekosa mtu wa kukusaidia au mazingira yanakuzuia kuweza kumtafuta Mungu wako
•kutembea katika wakati ambapo huoni bubujiko la Roho mtakatifu ndani yako wakati hakuna dhambi ambayo umeifanya
• Kupigwa vita katika Huduma

UFUNUO WA YOHANA 1:9-11
"Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu, ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiat ira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia."

Yohana alikuwa katika Mazingira ambayo kiuhalisia ilikuwa changamoto sana maana alitengwa katika kisiwa cha patimo na hakuwepo mtu wa kumkumbusha namna gani amtazamie Bwana katika maisha yake alipokuwa mahali pale ila Maisha yake yalimfanya Mungu aonekane kwake nakumpa ufunuo. Pia mazingira yale aliyokuwa yupo yalikuwa ni mazingira yasiyokuwa na usalama pia hapakuwa na faraja yeyote ya mwanadamu mahari pale. Ukiangalia hapo utajua kwamba kweli ilikuwa ni wakati mgumu kwake sana maana alikuwa ametengwa na haoni msaada wowote wa kumpa tumaini la usalama pale kisiwa cha PATIMO. Inawezekana na wewe upo kwenye wakati ambapo hakuna mtu hata mmoja anaye kutia Moyo kila ukitazama unaona hakuna mlango wa Kupita lakini usiogope hata kidogo endelea nami kunalo tumaini.

Yohana hakuyahesabu mazingira yale kuwa kikwazo cha yeye kuwasiliana na Mungu. Ila ilikuwa ni kipindi cha Jangwa kwake maana
✍️Hapakuwa na faraja ya mwanadamu
✍️Hapakuwa na mazingira mazuri yakumfanya awe na usalama maana alikuwa sehemu yenye uwezekano wa samaki hatarishi kama nyangumi n.k
✍️hakuhimizwa kumtafuta Mungu

MWANZO 37:23-28
"Ikawa Yusufu alipofika kwa ndugu zake, wakamvua Yusufu kanzu yake, kanzu ile ndefu aliyoivaa, wakamtwaa wakamtupa katika birika; na hiyo birika ilikuwa tupu, hamna maji. Nao wakakaa kitako kula chakula; wakainua macho yao, wakaona, msafara wa Waishmaeli wanakuja wakitoka Gileadi na ngamia zao, wakichukua ubani na zeri na manemane, wakisafiri kuvichukua mpaka Misri. Yuda akawaambia ndugu zake, Kwafaa nini kumwua ndugu yetu, na kuificha damu yake? Haya, na tumwuze kwa hawa Waishmaeli, wala mikono yetu isimdhuru, maana yeye ni ndugu yetu, na damu yetu. Ndugu zake wakakubali. Wakapita wafanya biashara Wamidiani; basi wakamtoa Yusufu, wakampandisha kumtoa katika birika, wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande vya fedha ishirini; nao wakamchukua Yusufu mpaka Misri."

Kwahiyo pia hata ukimuangalia Yusufu utagundua kwamba wale watu waliokuwa ni ndugu zake ndio waliomtendea hiana kwenye maisha yake maana walikuja kumtoa kuwa kama bidhaa ya kuuza na kununuliwa. Kwahiyo hiyo ilikuwa jangwa kwa namna ifuatayo
✍️Ndugu zake ilitakiwa wampe ulinzi lakini waliondoa ulinzi kwake.
✍️Ndugu zake walikuwa wakimuwazia mabaya maana walikuwa wanatamani hata kumuua..
✍️Yusuph alitupwa kwenye birika(shimo) ambapo mle hakuwa na msaada wowote

Kwa mazingira kama hayo unaweza ukagundua namna Jangwa linakuwa kwa mwanadamu awaye yeyote haijarishi kwamba ni ndugu au ni watu toka mbali wanamfanya awe katika hilo jangwa

Tutaendelea sehemu ya pili kwa wakati Mwingine kama MUNGU atatupa kibali cha kuendelea naamini umepata jambo hapo namna mwamini anavyoweza kuwa anapita wakati wa Jangwa.

Mungu akubariki kwa kusoma kipengele hiki cha kwanza cha UTANGULIZI juu ya Namna ya kuishi wakati wa jangwa kwa mwamini

Ulikuwa nami mpendwa katika kristo YESU

Jina: Bro Jackobo (JAM295)
Phone: +255766944441 na +255621036471
Email: jackobombwaga@gmail.com

KUJIKANA NDANI YA KRISTO YESU (sehemu ya tatu- Final)

Bro Jackobo Utakuwa nami mpendwa katika kristo yesu Name: Bro Jackobo Phone: +255766944441 Email; jackobombwaga@gmail.com Bwana Yesu asifiwe...